Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 29 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 372 2023-05-19

Name

Godwin Emmanuel Kunambi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlimba

Primary Question

MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa majengo yaliyobaki ya Kituo cha Afya Mlimba utakamilika?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Godwin Emmanuel Kunambi, Mbunge wa Jimbo la Mlimba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2016/2017, Serikali ilitenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili; jengo la upasuaji na nyumba ya mtumishi katika Kituo cha Afya Mlimba. Ujenzi wa majengo hayo umekamilika na kwa sasa kituo kinatoa huduma katika ngazi ya kituo cha afya ikiwemo huduma za upasuaji wa dharura wa akina mama wajawazito.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itakamilisha ujenzi wa majengo yaliyobaki ya Kituo cha Afya Mlimba, kadiri ya upatikanaji wa fedha.