Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 27 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 361 2023-05-17

Name

Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: -

Je, lini Serikali itawahamisha wataalam wa maendeleo ya jamii kuwa chini ya Wizara?

Name

Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali inatekeleza Tamko la Sera ya Ugatuaji wa Madaraka kutoka Serikali Kuu kwenda kwa wananchi kwa kushusha madaraka kutoka Serikali Kuu kwenda Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kusogeza huduma na utalaam karibu na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kufuatia kuundwa kwa Wizara hii ya Maendeleleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ambapo kada za msingi za kitaalam ni Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii, Serikali inaendelea na hatua za kuimarisha mifumo ya uratibu ngazi ya Sekratarieti ya Mikoa na Halmashauri ili kujibu mahitaji ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara hii mpya.