Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 27 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 349 2023-05-17

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaipandisha hadhi Zahanati ya Solwa kuwa Kituo cha Afya?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christina Christopher Mnzava, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutumia fursa hii mbele ya Bunge lako Tukufu kumwelekeza Mganga Mkuu wa Mkoa kufanya ukaguzi na kutoa ushauri wa kitaalamu katika Zahanati ya Solwa ili kuona kama inakidhi vigezo vya kupandishwa hadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pindi Mkoa utakapojiridhisha na miundombinu iliyopo, watawasilisha ombi hilo Ofisi ya Rais, TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya kwa ajili ya hatua za kuipandisha hadhi Zahanati ya Solwa na kuwa Kituo cha Afya.