Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 25 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 330 2023-05-15

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Primary Question

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza: -

Je, lini Mahakama ya Wilaya ya Nyasa itaanza kujengwa?

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, nikushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria naomba sasa nijibu swali la Mheshimiwa Engineer Stella Martin Manyanya, Mbunge wa Nyasa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kujenga Mahakama ya Wilaya ya Nyasa katika mwaka huu wa fedha wa 2022/2023, ambapo taratibu zote za awali za kupitia michoro na makadirio ya gharama zimekamilika, na hatua za kupata mkandarasi wa ujenzi ipo katika hatua za mwisho.

Mheshimiwa Spika, Tunategemea muda wowote jengo hili litaanza kujengwa, na kukamilika katika mwaka ujao wa fedha wa 2023/2024.