Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 25 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 323 2023-05-15

Name

Kabula Enock Shitobela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FURAHA N. MATONDO K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELO aliuliza: -

Je, lini Serikali itaongeza wauguzi katika Hospitali ya Bugando kwani kwa sasa ina upungufu wa wauguzi 1,200?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Bugando ina watumishi jumla 1,930, wauguzi wakiwa 667. Katika watumishi hawa wote, Serikali inawalipa mishahara watumishi 1,120. Hopsitali ya Bugando kwa mapato yake ya ndani inawalipa watumishi 2,205 mishahara kamili pia inawalipa watumishi 605 nusu mshahara.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.