Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 18 Works, Transport and Communication Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 232 2023-05-04

Name

Bahati Khamis Kombo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. BAHATI KHAMIS KOMBO aliuliza: -

Je, ni lini Kituo cha Posta kilichopo Kengeja kitafanyiwa ukarabati na kutumika?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA NA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Bahati Khamis Kombo, Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Shirika la Posta Tanzania linaendelea kufanya ukarabati wa majengo yake nchi nzima kwa kutumia fedha zake za ndani kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 – 2025/2026. Kutokana na mpango huu, ofisi ya Kengeja imepangwa kufanyiwa ukarabati kwa mwaka wa fedha 2024/2025.