Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 5 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 56 2023-04-12

Name

Martha Festo Mariki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto ya upungufu wa Watumishi katika Mkoa wa Katavi?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Martha Mariki, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Katavi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi wa Mkoa wa Katavi kila mwaka kwa kuendelea kutenga Ikama na Bajeti kama inavyopitishwa na Bunge lako. Katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, Serikali ilitenga nafasi 522 za kada mbalimbali kwa Mkoa wa Katavi na katika mwaka wa fedha ujao (2023/2024) tunakusudia kutenga Ikama ya ajira mpya 914 kwa Mkoa wa Katavi iwapo Bunge lako likiridhia na kuipitisha Bajeti ya Serikali iliyopendekezwa.