Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 3 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 37 2023-04-06

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itakamilisha Ujenzi wa Barabara ya Njombe – Ludewa – Itoni hadi Manda kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ujenzi kwa kiwango cha zege wa Barabara ya Itoni - Ludewa hadi Manda yenye urefu wa kilomita 211.42. Ujenzi kwa kiwango cha zege wa sehemu ya Lusitu – Mawengi kilomita 50 umekamilika na ujenzi wa sehemu ya Itoni – Lusitu kilomita 50 unaendelea.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa sehemu zilizobaki utaendelea kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.