Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 2 2024-01-30

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: -

Je, mpango wa kuugawa Mkoa wa Morogoro umefikia wapi hasa baada ya kuonekana kuwa na sifa ya kugawanywa.

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga, Mbunge wa Jimbo la Kilombero kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali imeweka kipaumbele katika kuimarisha utoaji wa huduma za kiutawala, kiuchumi, kijamii kupitia ujenzi wa miundombinu na upatikanaji wa vifaa katika maeneo ya utawala yaliyopo ya Mikoa, Wilaya, Halmashauri, Tarafa, Kata na Vijiji, endapo kuna ulazima wa kuanzisha maeneo mapya, Serikali itatoa maelekezo muda muafaka utakapofika.