Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 49 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 436 2022-06-22

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Meatu?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Leah Jeremiah Komanya, Mbunge wa Jimbo la Meatu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Ujenzi wa Vyuo vya VETA kwa awamu katika mikoa na wilaya mbalimbali kulingana na upatikanaji wa fedha. Katika kipindi ambacho Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA katika Wilaya ya Meatu, wananchi wa Meatu wanashauriwa kutumia Vyuo vingine vya VETA na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilivyopo kwa ajili ya kupata elimu ya mafunzo ya ufundi, nakushukuru sana.