Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 2 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 17 2023-11-01

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kutumia Televisheni ya Taifa na Redio katika kutoa elimu ya kilimo salama na chenye tija?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Felister Deogratius Njau, Mbunge wa Viti Maalum kama kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Kilimo inaendelea kutoa elimu katika mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa mazao nchini kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo matumizi ya vyombo vya habari kupitia televisheni na redio; mikutano; mafunzo rejea kwa nadharia na vitendo; na mifumo ya kidijitali.