Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 49 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 434 2022-06-22

Name

Mohammed Said Issa

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Konde

Primary Question

MHE. MOHAMED SAID ISSA aliuliza:-

Je, Serikali inaisaidiaje Zanzibar kupata faida ambazo TFF inazipata katika kuendeleza soka la Tanzania?

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia TFF imeendelea kuhakikisha kuwa Zanzibar inanufaika na fedha za misaada kutoka FIFA ambapo hadi sasa miradi kadhaa ya kuendeleza soka imetekelezwa ikiwa ni pamoja na kusaidia timu za Taifa, mashindano ya ndani, mawasiliano na mafunzo kwa wadau wa michezo. Hata hivyo, Serikali inatambua changamoto zilizopo baina ya TFF na ZFF katika uendeshaji soka katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kutatua changamoto hizi, Wizara yetu pamoja na Wizara ya Michezo na Vijana Zanzibar zimeitisha kikao maalumu baina ya ZFF na TFF kwa lengo la kutatua changamoto hizo.