Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 49 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 433 2022-06-22

Name

Antipas Zeno Mgungusi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Malinyi

Primary Question

MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza:-

Je, kwa nini Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania hawafundishi nje ya nchi hata katika Ukanda wa Afrika Mashariki au Nchi za SADC?

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Tanzania ina makocha 19 wenye viwango vya CAF A Diploma ambao wanakidhi viwango vya kufundisha nje ya nchi. Hata hivyo, makocha hawa hawafanikiwi kupata fursa za kufundisha nje ya nchi kutokana na historia ya elimu walizonazo. Hivyo basi, Wizara kwa kushirikiana na TFF wanaratibu mpango wa kutoa mafunzo ya Ukocha kwa wanafunzi wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya michezo ikiwemo Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, Butimba na Vyuo Vikuu nchini ili kupata Makocha wenye sifa.