Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 49 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 429 2022-06-22

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa fedha za kujenga mabweni katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Bulamata?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Moshi Selemani Kakoso, Mbunge wa Mpanda Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua changamoto ya mahitaji ya mabweni, hasa kwenye maeneo yenye changamoto ya umbali kwa wanafunzi. Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imetenga kiasi cha shilingi milioni 50 katika bajeti ya Mwaka 2022/2023 kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya ukamilishaji wa bweni moja Shule ya Sekondari Bulamata ambapo bweni hilo lilijengwa kwa nguvu za wananchi mpaka hatua ya msingi.