Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 11 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 175 2024-02-13

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza: -

Je, Serikali inatoa tamko gani kwa waajiri wanaowanyima safari watumishi wanaonyonyesha kwa kigezo cha kutumia fedha nyingi kujikimu?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Fatma Hassan Toufiq, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2008 aya ya 5(1) ikisomwa pamoja na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za Mwaka 2009 zinaelekeza watumishi wanaosafiri safari za kikazi wakiwemo wanaonyonyesha kupewe posho ya kujikimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia maelezo hayo, Serikali inaelekeza tena na kusisitiza kwa waajiri wote wa watumishi wa umma kuwa watumishi wa umma wahudumiwe kwa usawa na haki kwa kuzingatia sera na kanuni zilizopo. (Makofi)