Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 2 2023-10-31

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Zahanati katika Kata ya Binza – Maswa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Minza Simon Mjika, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Mwongozo wa Ujenzi wa Zahanati katika Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) wa mwaka 2007 wananchi wanatakiwa kuanza ujenzi wa boma mpaka hatua ya lenta.

Mheshimiwa Spika, baada ya kufikia hatua ya lenta Serikali hupeleka fedha kwa ajili ya umaliziaji wa jengo. Hivyo wananchi wa Kata ya Binza wanashauriwa kuanza kwa utaratibu huo, ahsante.