Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 3 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 40 2023-11-02

Name

Michael Constantino Mwakamo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Vijijini

Primary Question

MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza:-

Je, lini Serikali itawasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Wazee?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM, alijibu:-

Mheshmiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Michael Costantino, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, napenda kulithibitishia Bunge lako tukufu kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa wazee nchini. Sera ya Wazee ya mwaka 2003 iko katika hatua za mwisho za mapitio ili kujumuisha masuala mapya yanayojitokeza tangu kupitishwa kwa Sera hiyo iliyopo.

Mheshimiwa Spika, kukamilika kwa mapitio ya Sera ya Wazee kutatoa fursa ya kutungwa Sheria ya Wazee na Serikali kuwakilisha Muswada huo wa Sheria ya Wazee Bungeni kwa hatua za sheria hiyo iliyotungwa, ahsante. (Makofi)