Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 3 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 39 2023-11-02

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y. MHE. JULIANA D. MASABURI aliuliza:-

Je, lini Serikali itakipandisha hadhi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Musoma ili kiweze kutoa shahada?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Didas Masaburi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ili chuo kiweze kufikia hatua ya kutoa elimu kwa ngazi ya shahada, kinatakiwa kiwe na ithibati kamili na kiwe na vigezo stahiki ikiwemo miundombinu ya kutosha kutoa kozi husika, rasilimaliwatu ya kutosha na yenye sifa stahiki na Bodi ya Uendeshaji.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hatua zinazoendelea ili kuboresha mazingira ya chuo kwa ujumla wake, Wizara itaendelea kushirikiana na wadau wa kisekta kufanya tathmini ya kina kuhusu lini kozi hiyo ianze hasa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya soko la ajira kwa wahitimu wa shahada, ahsante. (Makofi)