Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 3 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 34 2023-11-02

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza:-

Je, lini Wilaya ya Rungwe italetewa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi?

Name

Jerry William Silaa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukonga

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendelea kuajiri Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi ili kuongeza kasi ya kusikiliza na kuamua mashauri ya ardhi. Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya ya Rungwe ameteuliwa na kupangiwa kituo tarehe 18 Septemba, 2023 na tayari ameanza kazi. Nakushukuru.