Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 38 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 339 2022-06-06

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga mabweni pamoja na miundombinu mingine katika Chuo cha VETA Kitangali?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna Salum Mtanda, Mbunge wa Newala Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimwa Naibu Spika, Serikali inatambua mahitaji ya miundombinu ya kufundishia na kujifunzia ikiwemo mabweni katika Chuo cha VETA Kitangali ambapo mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali ilitoa Sh.299,267,002.00 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, jengo la utawala na vyoo na ukarabati wa karakana ya ushonaji, umeme pamoja na uwekaji wa samani na vifaa.

Mheshimwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na jitihada za kutafuta fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya miundombinu ikiwemo mabweni, bwalo, nyumba za Walimu na uzio katika Chuo cha VETA Kitangali.

Mheshimwa Naibu Spika, nakushukuru sana.