Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Edward Olelekaita Kisau (39 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. EDWARD K. OLELEKAITA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii, lakini kabla ya yote nimshukuru sana Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kunipa afya hii njema hadi leo niko Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili niwashukuru wananchi wangu wa Jimbo la Kiteto kwa imani kubwa na wamenichagua kwa kura nyingi sana. Nawaahidi kabisa kwamba nitawajengea heshima kubwa hapa Bungeni haijawahi kutokea. Vilevile nikishukuru Chama changu Cha Mapinduzi kwa kuniteua na nikapeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nijielekeze kutoa maoni yangu kwa Mpango huu wa Maendeleo. Mpango wa Maendeleo ni mzuri sana na kwa kweli katika kupitia zipo taarifa kama tatu hivi ambazo ni kubwa kweli. Kwa hiyo, maoni yangu ya kwanza nafikiri kama hatutayatendea haki sana mapendekezo haya kwa siku zilizopangwa kama nne hivi. Document ya kwanza ina kurasa karibu 164; ya pili 51; nyingine 107. Sasa ukichanganya zote na dakika tano hizi utajua kabisa kwamba pengine tungehitaji wiki mbili hivi za namna ya kuzungumza ili tuweze kuishauri Serikali vizuri sana katika mpango huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na muda kuwa mchache, nijielekeze kwenye kilimo. Kilimo hapa tumeambiwa kwamba pato la Taifa ni 27% na kinawaajiri Watanzania zaidi ya 65%. Nimshukuru sana Rais kwamba mapendekezo ya maendeleo mwaka huu ni kuwekeza nguvu kwenye kilimo. Tukiwekeza nguvu kwenye kilimo na hususan mbegu zipatikane kwa wakati na kuwaondoa wakulima kwenye jembe la mkono na ku-mechanize, tutaweza kulikwamua Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mahusiano katika kuendeleza kilimo siyo tu yana tija kwenye uchumi, lakini vilevile na mahusiano makubwa sana ya kupunguza umaskini kwa Watanzania walio wengi. Kwa hivyo kwa kweli naomba Wizara ya Kilimo isilale katika hii miaka mitano, tuwekeze nguvu kubwa sana kwenye kilimo na kwenye mbegu, unajua nchi zile zilizoendelea sasa wana-patent hizi mbegu, kwa hiyo tusiwekeze tu kwenye kufanya utafiti, lakini pia tu-patent mbegu zetu ili tuweze kulinda masoko yetu huko mbele ya safari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiwekeza kwenye kilimo, kwenye mifugo, kwenye uvuvi na tukaweka nguvu zetu zote huko tutakuwa tumeshughulika na vitu wanavyoita watu wengine the really economies kwa sababu ndiyo Watanzania wengi wako huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni umeme na ningemwomba sana Waziri wa Nishati anisikilize vizuri hapa, Hotuba ya Mheshimiwa Rais ukurasa wa nane na nimeshamwandikia Mheshimiwa Waziri memo nyingi sana kuhusu suala la umeme. Nafurahi sana tumewekeza kwenye umeme na nawapongeza sana na Wizara wakati wanajibu maswali hapa walisema hivi, kwamba wamejiwekea miezi 18 kumaliza tatizo la umeme kwa vijiji vyote vilivyobaki. Hii ni ishara nzuri sana, lakini ni lazima sasa tuangalie umeme tulionao, Mheshimiwa Rais alisema hivi na naomba ninukuu, ukurasa wa nane wa hotuba ya 2015; “Mheshimiwa Spika eneo lingine ni TANESCO, TANESCO pamekuwa ni suala la kukatikakatika kwa umeme mara kwa mara na kuwepo na umeme wa mgao na hilo limelalamikiwa sana na wananchi wetu.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiteto kwa miezi mitatu sasa umeme ni kukatikakatika halafu hatupati taarifa yoyote ile. Sasa wakati tunawekeza huko kutengeneza umeme, lazima sasa tuwe na uhakika wa umeme tulionao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda naunga mkono hoja lakini…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa ahsante kengele imeshalia

MHE. EDWARD K. OLELEKAITA: Ahsante sana.
Hoja Kuhusu Bei ya Kuuza na Kununulia Mahindi
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi ya kuzungumzia habari ya suala la mahindi.

Mheshimiwa Spika, Kiteto ni hub na ndio bread basket ya ukanda huu. Tangazo la Serikali la kufunga kupeleka mahindi nje tunaamini ilikuwa ni nia njema sana. Lakini kwa mfano Kiteto, mahindi kwa gunia ilishafika elfu tisini lakini baada ya zuio hilo, na nimetoka jana Kiteto imekuwa shilingi 55,000.

Mheshimiwa Spika, tunachosema, wazo la Serikali kununua mahindi hapa limepokelewa vizuri sana na wakulima. Tunachoomba Serikali inunue kwa bei ambayo wakulima walikuwa wauze huko. Tukitoa tangazo na likashusha bei itaumiza wakulima. Kwa hiyo tunachoomba ni rahisi sana, Mheshimiwa Waziri wa Kilimo mahindi yalishafika bei elfu tisini kama mnatoa na kwingine naambiwa imefika laki na ishrini.

Mheshimiwa Spika, kama mnataka kununua mahindi yote na fedha zipo, tengenezeni vituo na tuwe na navyo Kiteto na kila Kanda ya nchi hii na tukubaliane bei hapa na Mheshimiwa Waziri, tangaza bei hiyo, tena chukua ile ambayo ni the highest kama ni laki na ishirini ndio imekuwa the highest Serikali inunue kwa hiyo laki na ishirini. Mkifanya hivyo wakulima mtakuwa mmewatendea haki sana.

Mheshimiwa Spika, mwaka huu mvua ilikuwa kidogo, upatikanaji wa mahindi umekuwa ni mgumu sana…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa, kengele imeshagonga.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, ahsante na naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Kwa sababu ya muda niruhusu nimpongeze Rais peke yake. Tunampongeza Rais kwa kuleta mapendekezo ya Mpango huu na mpango huu kwa mara ya kwanza unakuja wakati tuna Tume mpya ya Mipango na sheria mpya na Wizara maalumu inayoshughulikia mipango ya Serikali. Kwa hiyo, tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa ukweli kwa direction hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile nampongeza Rais kwa hatua ambazo zina maana kubwa sana, maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga upya. Nilivyokuwa nasoma Hotuba ya Profesa Kitila Mkumbo, kwanza is very radical, hotuba Fulani, imechukua angle fulani hivi ambayo ndiyo tunataka. Tunataka mipango ambayo inaelekezwa kwenye vijiji vyetu. Watanzania walio wengi wako vijijini, hivyo, tunataka focus ya mpango huu iende kweney rural development. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia data za Serikali hapa, mikopo ya biashara shilingi trilioni 22 halafu second percent peke yake ndiyo imeelekezwa kwenye kilimo, wafugaji na wavuvi. Hii haiwezekani, hapana. Kama ni kweli tunataka twende kwenye rural development, lazima tuweke pesa nyingi sana kuelekeza kwenye kilimo, mifugo na uvuvi. Kwa sababu, ndiyo Watanzania wengi wako huko. Tukiwa na mipango ambayo ina-move na watu walio wengi, hapo ndiyo tunazungumzia habari ya maendeleo. Maendeleo ni watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani kila wakati tunakuja hapa halafu tunasema tunawekeza kwenye kilimo, kwenye ufugaji na uvuvi lakini hatuoni, haiwezekani. Kwa hiyo, Mheshimiwa Profesa Kitila assignment yako ya kwanza sasa, tunataka hii rural economic development tuione, huko vijijini siyo kwenye vitabu. Tunataka tutoke kwenye vitabu sasa. Hii nchi ina documents nyingi, nzuri sana, lakini tukienda kule kwenye vijiji vyetu hatuoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati naangalia hii, ni kweli wafugaji wametajwa, wakulima wametajwa na wavuvi, lakini ukisoma hii huoni tangible, vitu ambavyo vinamhusu mtu anaitwa mfugaji. Waziri amezungumzia habari ya kuwa na viwanda na kuziongezea thamani products zinazotokana na mifugo. Honestly hivi ipi ya kwanza, ni mahali pa kuhifadhia hii mifugo au wanataka viwanda? I think Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi ukurasa wa 52 tuliweka commitment kwamba, kuhakikisha tunatenga maeneo ya ufugaji yapimwe na infact tumeweka mpaka statistics, mpaka zifike hekta milioni sita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani kabla hatujazungumza habari ya viwanda, lazima tuwe na maeneo ambayo yamelindwa kisheria. Tukishakuwa na maeneo hayo ndiyo tuzungumze habari ya viwanda. Kwa hiyo, tunataka bajeti zijazo na Mpango wake tuone bajeti kubwa ikienda kwenye maeneo haya. We are not interested in reading nice documents, tunataka kuona tangible results. Nilikuwa nasoma hapa mpango wetu huko kwa wakulima; “kuendeleza juhudi za kujitosheleza kwa mahitaji ya chakula nchini na kuendelea kuongeza matumizi ya mbolea, mbegu bora na kilimo na umwagiliaji”. That’s fine, lakini trekta ziko wapi hapa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Serikali inataka wakulima hawa na wakulima wa nchi hii wanafanya kazi kubwa sana, pamoja na kwamba wakati mwingine wanapata statements za ajabu ajabu. Wanaambiwa wanalima kienyeji, wanafuga kienyeji, lakini hizi hizi documents ndizo zinazosema the reason we have fought self-sufficient zaidi ya asilimia 120, ni kwa sababu ya wakulima hawa. Wanalima hivyo hivyo mnavyoita kienyeji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbona hapa tunaona hifadhi ziko nyingi sana, karibu sijui ishirini na ngapi na mapori tengefu. Ukiangalia size ya hiyo, lakini uki-compare na nchi kama Namibia, ina National Parks saba tu. Halafu ukiangalia tunapata nini kutokana na mapori haya au na sisi tuseme mnahifadhi kienyeji kienyeji hivi? I think it is high time twende kwenye quality. Alizungumza Mheshimiwa Mbunge wa Mbarali jana hapa, “Development must be people centered. There is no question of development where by human beings in individuality is being destroyed for the sake of wildlife,” haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima watu kwanza. Hata hili lililotokea hapa leo tusipoweka emphasis kwenye kutetea watu, maendeleo hayana maana. Lazima, a true definion ya maendeleo must start from a human perspective. Mheshimiwa Profesa Kitila, hapa tunazungumzia habari ya utawala wa sheria, kama nguzo ya maendeleo yetu kama Taifa, nakubaliana, as a lawyer I agree. But what is the rule of law kama sheria zetu na hapa naongelea msingi huo wa reforms. Mheshimiwa Rais anataka reforms, lakini tuna sheria za kikoloni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eti mfugaji ng’ombe wameingia shambani halafu we are not interested with a fine, eti una-forfeit. Una wa-impoverish watu halafu tunazungumza habari ya mipango, wakati sisi na mpango huu tulitaka Watanzania watajirike. Sasa, lazima tuamua, tuendelee kuwa na sheria ambazo zinawa-impoverish watu ama tuwe na sheria ambazo nia yake ni kukataza matatizo yasitokee. Unapo-forfeit ng’ombe leo unam-impoverish huyo mtu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inatokea kwa sababu ya kuwa na sheria tu ya kikoloni. Mheshimiwa Attorney General, sijui kama yuko hapa. Hii forfeiture, hii section ipo, tangu Sheria ya mwaka 1958 na tumepata uhuru. We cannot question … (Makofi)

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Edward Olelekaita kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Ester Bulaya.

TAARIFA

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampa taarifa kaka yangu Mwanasheria kwa mchango mzuri sana kuhusiana na masuala ya utekelezaji wa sheria. Hivi tunavyoongea Jimbo la Bunda Mjini, Kata ya Kunzugu, familia 16, ng’ombe 500 wameshikiliwa na TANAPA na wana mpango wa kuwataifisha, lakini Mahakama imetoa ruling walipe faini. Wananchi wanataka kulipa faini ili waokoe ng’ombe wao, lakini TANAPA wanakataa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nampa hiyo taarifa. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Olelekaita, unaipokea taarifa?

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea sana.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, …

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Naomba Mheshimiwa Bulaya atupe uthibitisho wa hiyo hukumu inaelekeza nini ili na sisi tuweze kuthibitisha kwa upande wa TANAPA na kuweza kuchukua hatua kama ni kweli Mahakama imeruhusu waweze kulipa faini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Edward Olelekaita, malizia mchango wako.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Sasa, sijui hata nisemeje. Siji nipokee ile ama nifanye nini, anyhow. Niseme hivi, in fact kama Mheshimiwa Waziri, anataka tulete hizo kesi ziko nyingi sana, lakini iko hivi, kwa sababu lazima sasa twende a step further. Tukileta atafanya nini? (Makofi)

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilindie muda wangu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Lulida.

TAARIFA

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nakushukuru kunipa hii nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna sheria na kuna mipaka ilishatengenezwa, corridor za wanyamapori na binadamu, lakini vile vile hao wafugaji. Leo wako katika Mkoa wa Lindi. Vurugu za wafugaji kuvamia maeneo na mashamba ya wananchi zimekuwa kubwa, mpaka wananchi wameuawa na wafugaji. Tusiendelee kukubali vitu ambavyo havitaki kufuata sheria. [Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Mwenyekiti, twende na sheria, Serikali ina sheria yake na wafugaji watii sheria ya nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kumpa taarifa hiyo. Sasa hivi twendeni Lindi mkaone migogoro ya wafugaji kuvamia maeneo ya wakulima na kuleta kero kubwa katika mazingira haya, ahsante sana.

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Ngoja, Mheshimiwa Riziki, tunashukuru kwa taarifa yako. Hii taarifa ulikuwa hunipi mimi, ulikuwa unampa Mbunge anayechangia. Mheshimiwa Olelekaita, endelea na mchango.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na namheshimu sana mama yangu Mheshimiwa Lulida. Nilikuwa naongelea kitu tofauti kidogo. Nilikuwa nasema hivi, hapa tunaongea na Waziri wa Mipango ya Nchi hii by the way. Kwa hiyo, wengine watulie kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachosema hapa mipango ya nchi na Mheshimiwa Profesa Kitila amesema vizuri sana hapa, amezungumza jambo sawa. Amesema, Mpango wa Maendeleo wa Taifa siyo mpango wa Serikali and it is true. Tutatarajia sasa kabla ya ule mpango mkubwa kuja, sasa waje watwambie wamewa-consult watu akina nani. Pengine this time, hebu waanzishe mjadala wa Kitaifa tuzungumze habari ya Mpango huu wa Taifa, kwa sababu nakubali, siyo mpango wa Serikali, ni mpango wa Taifa letu. Kwa hiyo, hiyo statement ni nzuri sana, tunataka tuone. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa wameongelea kuhusu watumishi wa umma na ni kweli, engine ya mipango ya yote ya Serikali ni watumishi wa umma and I agree with you, amem-quote mpaka Waziri Mkuu wa Singapore. Kama tunataka kufuata njia ya Singapore unajua lazima tuwe na discipline sasa. It is not enough kusema twende kama Singapore, no! Lazima tujue Singapore wamefanya nini ili tutembee kwenye hiyo barabara. Hapa Waziri ametengeneza quotation nzuri sana na watu wengine huwa wanafikiri, kuna wakati Singapore pia walianza kufikiri mfumo wa elimu yao pengine sio mzuri kama tulivyo leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wengine wanasema hivi, unajua kwa nini Marekani watu wao ni innovators na ukiangalia wale watu wakubwa, sio kwamba walikuwa na distinctions kwenye universities, no! tofauti ya vyuo vyetu na nchi nyingine, kwa mfano kama Marekani, wao wanachoangalia they are interested in who you are as person rather than the test ulizopata kwenye distinction yako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, they appreciate those who take bold decisions, those who do nothing, do things differently, those who overcome problems, those who are street smart, those who see the world for what they can do, not what they cannot do. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiwa na sheria ambazo zinaleta barriers leo, badala ya ku-support hizo innovation na watu wa umma, sisi tumeletewa Ripoti ya CAG hapa. That is a very good test, kama tunataka nidhamu kwa sababu Waziri amesema ndio nguzo ya mpango huu, ni kutekeleza ripoti kama za CAG, lakini tutakwenda a step further na kusema what is wrong with recruitment? Halafu tubadilishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza kwa sababu ya muda nichukue muda huu kupongeza Kamati ya Ardhi, Maliasili, Mazingira na Utalii kwa kazi nzuri ambayo wameifanya hapa, nipongeze pia Serikali Wizara ya Ardhi na Maliasili kwa kazi wanazojaribu kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaongelea kidogo kuhusu migogoro. Tumeona data hapa kwamba vijiji viko 12,318 hivi, halafu vijiji vilivyopimwa na kuwa na matumizi bora ya ardhi ni 3,681, halafu ambazo bado ni karibu 8,638 hivi, sasa hii inatisha kidogo, kwamba migogoro ambayo imekuwepo kwa muda mrefu baina ya vijiji na hifadhi, Wilaya - Wilaya, Kijiji kwa Kijiji, lakini kubwa zaidi migogoro inaondoa raha sana kutoka kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vyema Wizara na specifically Tume hii Taifa matumizi bora ya ardhi kama walivyosema Kamati wapewe pesa nyingi sana ili tukiondokana na migogoro haya mengine yote tunayapanga itawezekana, bila kupima vijiji kwanza, mipaka ikafahamika na matumizi ya ardhi yakawekwa vizuri migogoro inaweza ikaendelea kwa miaka na miaka. Kwa hiyo ni vema pesa zikatengwa za kutosha kwa ajili ya Tume hii ya Taifa ya Mipango na Matumizi bora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukifanya hivyo itaondoa migogoro na migogoro nadhani ndiyo easiest kuliko kutafuta pesa za barabara. Hilo ni rahisi kuliko yote, tuliambiwa hapa kwamba Kijiji sijui milioni 15, kama ndiyo Tume inasema hivyo, sasa tutashindwaje kutafuta bilioni 300 kweli ili tumalizane na migogoro ili haya mengine yote tunayoyapanga iwezekane, hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulibadilisha sheria hapa ya kuondoa mamlaka kwa Mabaraza yale ya Kata, sasa tunataka ije kwenye Mabaraza ya Wilaya na nadhani thinking ni kwa sababu sheria hawa wanafahamu zaidi. Tunatarajia Wizara ya Ardhi sasa muanze kuajiri hawa ili sasa migogoro isirundikane bure. Kwa mfano, Kiteto Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ardhi nakumbuka na nawapongeza sana kwa kuja Kiteto na timu yenu mnahangaika sana, mnakwenda kila mahala na Waziri wako, ndio maana Waziri wako karibu nywele kichwa chote kinakuwa nyeupe na wewe kila siku mnapishana, lakini Jimbo la Kiteto ambalo kila siku nazungumza hapa migogoro ni mingi mikubwa kuliko Mkoa halafu bado mnatuletea Mwenyekiti anayetembelea sijui anatoka wapi? Mheshimiwa Waziri mtuletee Mwenyekiti wa Balaza la Ardhi Kiteto awe pale full time ili migogoro ishughulikiwe na kwingine kote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine Wizara ya Ardhi kuna clip ya Mheshimiwa Rais Mstaafu ilikuwa inatembea hapa siku za hivi karibuni kusema hii Wizara yenu bwana kuna watu wagumu kwelikweli, sasa sijui ni changamoto na hiyo imegeuka kuwa nayo ni changamoto ama ni confusion iliyopo kwamba wale Maafisa Ardhi waliopo Wilayani hawajulikani kama wako Halmashauri ama wako kwenu ni kama wana-hang tu hivi, ni vyema mkaweka hili sawa ili na wale waanze kufanya kazi huko Wilayani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nirudi Maliasili na Utalii, kwanza nimpongeze Waziri na Naibu Waziri kwa kuja na huu mpango wa kukutana na Wabunge Mikoa, nadhani itawajengea fursa ya kufahamu changamoto nyingi kutoka kwa watu wanowakilisha wananchi hapa ambao ndiyo wanatupa kura hapa. Sasa mkichanganya na ripoti zile za wataalam wenu na nyinyi mkapata na picha huku nadhani mtatengeneza majawabu ambayo ni mazuri kwa watu na uhifadhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nitajikita kwenye WMA zaidi na WMA nchini kuna WMA karibu 38 hivi, lakini 22 ndio ziko active kidogo na Kiteto tuna WMA, Mahakama ya WMA lakini kuna Waheshimiwa Wabunge wengi sana hapa wana WMA, Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Baran Sillo ana WMA ya Bunge Mheshimiwa Mpakate ana WMA, Mheshimiwa Kuchauka, kuna Wabunge zaidi kama 30 hivi, Dkt. Steven Kiruswa kule Longido.

Mheshimiwa Mwenyekiti, WMAs zilianzishwa na Sera ya Wanyamapori ya mwaka 1998 na nia ilikuwa ni kwamba pamoja na kwamba tuna maeneo ya hifadhi (core protected areas); maeneo mengine ya kufanya uhifadhi bila kubugudhana na watu ni kushawishi watu washiriki kwenye suala la uhifadhi. Kwa hiyo, wananchi wanatenga ardhi zao, halafu wanapewa mamlaka ya kuingia mikataba na wawekezaji. Kwa hiyo, nimependa sana Kamati walivyoweka hapa kwamba WMA siyo Hifadhi za Taifa wala siyo extension ya National Parks, siyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama walivyosema Kamati, WMA siyo Hifadhi ya Taifa wala siyo mwendelezo wa Hifadhi za Taifa, hizi ni ardhi za vijiji, ambacho wanachofanya ni wanafanya mnachofanya ninyi, kuhifadhi. Sasa nadhani ingekuwa ni jambo jema kama Hifadhi za Taifa za hizi za kijamii zikafanya kazi pamoja na mkashindana kibiashara bila kusumbuana, kwa sababu lengo ni lile lile. Data hapa zinatuambia pamoja na mbuga zote ishirini na ngapi sijui, asilimia 65 mpaka 70 ya wanyamapori wako nje ya hizi tunazoziita core protected areas na logic ni simple tu, mnyama wala hajui kwamba eti ndio na cross Serengeti sasa kwa hiyo anaanza ku-vibrate kwamba navuka mpaka wa Serengeti, no these are free agents, wanakwenda kila mahali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo unless tu-improve mahusiano zaidi na watu ndio itafanya uhifadhi uwe complete. Itakuwa ni kujidanganya sana kama mnafikiri mtafanya uhifadhi bila ku-involve watu, hiyo haitowezekana. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri task kubwa ni kuangalia mahusiano, mahusiano ya wananchi na hifadhi na wanyamapori. Siku mkitengeneza balance nzuri sana uhifadhi utakuwa umekamilika vizuri sana na utakuwa na manufaa makubwa zaidi kwa nchi na kwa wananchi wenyewe. Tutaongea mengi zaidi tukikutana kwenye Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kilichonifurahisha sana leo ni Maazimio ya Bunge kuhusu pesa za WMA; WMA wamepewa Madaraka, wanasaini mikataba na wawekezaji, mwekezaji kalipa hela halafu hela haziji. Hawa wanashindwa kulipa mishahara, wanashindwa kufanya kazi za uhifadhi, wanashindwa ku-control majangili kwa sababu pesa zimekwama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hii kwa kweli Kamati kwa kweli shikamoo Kamati, kama ndio Mwenyekiti ndio anapokea kwa niaba yenu. Mmefanya jambo ambalo limetusumbua kwa muda mrefu kidogo. Azimio lenyewe; Serikali ihakikishe inarejesha kiasi chote cha fedha kinachostahili kwenda WMA na naambiwa na watu wa WMA wanadai kama four point something billion sasa. Kwa hiyo, mlete hiyo haraka kama lilivyosema azimio hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine zuri sana mtengeneze mpango wa kuhakikisha kwa sababu tumeshakubaliana kikanuni, kila mtu anapata nini hapa, WMA percent ngapi, Serikali, wilaya na wawekezaji na wao wako tayari, kwani akiandika cheque tatu kila mtu akapata kwa wakati kuna shida gani? Kwa hiyo, kama azimio hili lilivyoweka vizuri tunataka hela za WMA ziende directly, hizi za kwenu zinazokwenda Hazina kwanza ziende huku, hiyo vita ni yenu wenyewe kwa wenyewe lakini hizi za wananchi angalau ziende straight ili mambo ya uhifadhi na pia isilete migogoro kati ya WMAs na wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu leo you can imagine an investor ana-sign mkataba na WMA hela haziji, halafu anaye-hold hela siyo sehemu ya mkataba, anaye-hold hela ana-frustrate ile agreement kwa sababu ya ku-hold hela. Kwa hiyo, sheria kama ilivyokuwa inasema hizi hela ziende, kwa kweli hapa Kamati mmetufanya sisi ambao tunatoka maeneo haya, tumefurahi sana na WMA nchi nzima leo nadhani zinafuatilia sana hili na wamefarijika sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la mwisho, narudi kwenye mahusiano, mimi nawaambia wananchi wangu wa Kiteto, hizi fidia hizi tunazozungumza hapa, kanuni hizi ambazo mmesema kifuta jasho, sijui ni kifuta nini, halafu haziji na zinachelewa. Mimi Kiteto pekee yake wananchi wameleta forms zaidi ya 223 lakini kesi za mifugo 21, majeruhi wanne, vifo vinavyotokana na wanyamapori.

Mheshimiwa Mwenyekiti, is very unfair, leo tembo anavuruga shamba lote na wananchi wale hawalali kila siku wako mashambani. Halafu tembo au wanyamapori anakuja anavuruga, halafu mnaniambia shilingi 500,000 na shamba lote eka mia, mia mbili lote limevurugwa.

Kwa hiyo, kati ya vitu ambavyo kwa kweli ningetamani hii kanuni mmelete haraka sana ili turekebishe ili wananchi hawa wasivunjike moyo ambao hawalali usiku na mchana wakijaribu kulima ili wanufaishe nchi na Taifa kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nafurahi na nashukuru sana, ahsanteni sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Tume ya Mipango wa Mwaka 2023.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi na kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa afya njema leo na pili nimpongeze Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sheria zetu; tatu nimpongeze Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakili msomi Simbachawene, Naibu Waziri Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete wakili, Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Ndumbaro wakili, Mheshimiwa Attorney General Jaji Eliezer Feleshi na watumishi wote ambao wamehusika kuleta maboresho ya Miswada hii mitatu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa Tume ya Mipango na nianze kwa kusoma Ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 63(3)(c) inasema hivi na ninaomba ninukuu. “kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo.”

Mheshimiwa Spika, Mpango wa Taifa ni jukumu la msingi la Bunge hili na ndiyo maana Muswada huu ambao unafufua tena Sheria ya Tume ya Mipango ni jukumu zuri sana na tunampongeza Mheshimiwa Rais lakini Wabunge wengi wamezungumza hapa kwenye mjadala huu wa bajeti wakati fulani fulani wakisema wakielezea umuhimu wa kuwa na Tume ya Mipango ya Taifa. Kwa hivyo Muswada huu leo utaleta tena Tume hii ya Mipango ya Taifa kwa hiyo, kwa kweli tunawapongeza Serikali kwa kuleta mpango huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninakumubuka Mheshimiwa Askofu Josephat Gwajima alizungumza hapa sana kuhusu uzuri wa Taifa kuwa na mpango wa muda mrefu na wa muda wa kati kwa sababu ndiyo itaongoza Taifa letu. Sasa muswada huu leo utafanya hayo yawezekane lakini mtakumbuka vile vile kwamba Sheria ya Fedha ya 2018 ilifuta iliyokuwa Sheria ya Tume ya Taifa sura ya 314 na kwa hivyo sasa tumerudisha tena lakini imerudi namna gani sasa?

Mheshimiwa Spika, kwanza tunampongeza Mheshimiwa Rais siyo tu kwamba imerudi lakini imerudi kwa sura mpya zaidi. Ukilinganisha sheria iliyofutwa majukumu ya tume yalikuwa ni 13 lakini kwa mujibu wa sheria hii sasa Muswada huu majukumu yameongezeka kutoka 13 hadi majukumu 19 na hii inaonyesha tu dhahiri kwamba kuna imerudi kwa sura na nguvu mpya zaidi na mategemeo yetu kwamba baada ya sheria hii kupitishwa na Bunge hii tume itafanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sheria hii vilevile imetengeneza kwa mara ya kwanza na niseme tu kwa historia ya nchi yetu hii Tume ya Mipango imekuwa inapewa majina tofauti tofauti lakini ipo tangu mwaka 1961. Kwa hivyo kila wakati tumekuwa tunabadilisha majina na kubadilisha kwamba safari hii iwe Ofisi ya Makamu wa Rais, iwe chini ya Wizara ya Fedha lakini tafiti zinaonyesha kwamba nchi ambazo zinachukulia kwa usahihi na kwa lugha ambayo ni kubwa zaidi ni kwamba tume hii ikiwa chini ya Mheshimiwa Rais kama Mwenyekiti itafanya itaongezea nguvu na hadhi kubwa tume hii na utafiti duniani inaonyesha nchi zinazofanya vizuri zaidi kwa mfano Ghana, Indonesia, Afrika Kusini na India zote zina tume hii na Mwenyekiti wa tume hii ni Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, uzuri wa sheria hii safari hii kwa sasa bado ni Muswada kwa mara ya kwanza na haijawahi kutokea hii imeona jukumu la kupanga na jukumu la fedha kwamba ni vitu viwili tofauti. Imeleta wazo la kuwa na Mawaziri wawili ambao ni wajumbe kwenye tume hii ambaye ni Waziri anayeshughulika na masuala ya fedha na Waziri atakayeshughulika na Mipango ya Maendeleo ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii kwa kweli ni innovation mpya sana kwa hiyo kwa mara ya kwanza baada ya Muswada huu kupita kuwa sheria tutategemea hata muundo wa Serikali utabadilika. Tutakuwa na Waziri ambaye ana deal na maendeleo ya Taifa peke yake halafu kutakuwa na Waziri wa Fedha ambao wote sasa ni Wajumbe kwenye tume hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukisoma kifungu cha tano utaona Wajumbe wengine ambao wanaongezwa wakiwemo Katibu Mkuu. Kwa hivyo tume hii kwa mara ya kwanza itakuwa na nguvu kubwa zaidi ya kuongoza Taifa kwa mambo yote yanayohusiana na maendeleo ya Taifa. Kwa hiyo, kwa kweli ni jambo jema sana.

Mheshimiwa Spika, vilevile Sheria ya, kuna utafiti fulani umefanywa 2022 na kuonyesha kwamba Wizara ya Fedha sasa kwa majukumu yake yaliyo mengi na kwa sababu tayari yalikuwa ni mengi tu ukiongezea jukumu la kupanga mipango ya maendeleo ya Taifa ni kazi kubwa zaidi. Hawataweza kuweka nguvu kubwa zaidi kwenye kutunga au kutengeneza Sera za Taifa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kwa kweli niwaombe Waheshimiwa Wabunge, kwamba kwa mara ya kwanza sasa hii sheria ikipita tutatarajia sasa mipango ya Taifa hili itakuwa ni ya muda mrefu, itaongoza Taifa letu na itaratibu mipango ya Wizara zingine na kutoa dira ya kimaendeleo kwa Taifa letu. Kwa hiyo nawaombeni sana tuunge mkono hii ipite kwa nguvu kubwa kidogo ili tutume ujumbe kwamba kwa kweli yale mawazo yenu kuhusu Tume hii kurudishwa tena na siyo tu kurudi lakini imeboreshwa zaidi kwa mara ya kwanza italeta manufaa makubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini sheria nyingine ni hii ya TISS (Tanzania Intelligence and Security Services bill) ambayo vilevile kamati yetu iliweza kuchambua na kwa kweli tulikubaliana kwamba kutokana na maendeleo ya intelijensia inavyoenda Duniani yapo maboresho ambayo ni ya lazima kisheria.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano Muswada huu sasa wa sheria hii inapunguza kazi za Waziri ambaye atakuwa anahusika ili kazi yake iwe ni mambo ya bajeti na mambo ya sera; na tumejaribu kuangalia sera na sheria zingine dunia, ziko hivyo. Kwa hivyo kwa kweli madhumuni ya kubadilisha muundo na kubadilisha kazi za TISS ili kazi yao iwe zaidi katika kuangalia mambo ya intelligence; na kwa kwakweli badala ya kwenda kwa Waziri waende kwa Mheshimiwa Rais; Kamati yetu iliona kwamba ina tija kubwa sana. Na hata baada ya kuwauliza wale ambao ni Mawaziri, ni Wizara hiyo wakakubali, kwamba kwa kweli in fact hata kwa fact tu peke yake huwa inafanyika hivyo kwa hiyo hakukuwa na hoja kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, lakini nyingine kubwa ambayo ni nzuri kwa sheria hii ni kwamba kwa kuwa TISS ni chombo cha Muungano. Sheria kuweka muundo sasa ambao ni wakimuungano ilikuwa ni wazo ambalo ni zuri sana, tuwe na ma-directors ambao mmoja anatoka upande mwingine wa muungano na mwingine anatoka upande mwingine wa muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini siyo hii tu, ni pamoja na kuwa na sifa za hawa ambao watakuwa wanaongoza vyombo hivi na kwa kweli tuliona kwamba ni innovation kubwa nzuri sana kwa kisheria hatuwezi kuwachagua watu ambao sifa zao haziko kisheria. Kwa hiyo hiyo pia inaonyesha kwamba tuko serious kuangalia zile credentials na kujua kwamba hawa wawe na sifa hizi, na kwa kweli sheria kwa mara ya kwanza imeweka vizuri sana hili jukumu na kwa kweli ni jambo zuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini sheria nyingine ni hii ya revision laws amendment bill, na yenyewe ukiangalia baadhi ya marekebisho yaliyoletwa kwa mfano Kifungu cha 14. Mtakumbuka mwaka mmoja, miwili iliyopita tulitunga sheria hapa tukasema sheria zetu zibadilishwe ziende kwa lugha ya Kiswahili, na sasa kuna zoezi linaendelea la kufanya sheria zote ambazo ziko kwa kingereza zifanywe kwa kiswahili. Lakini kwa kutambua jukumu vilevile kwamba sheria zetu zinatumika vyuoni na wanakuja Watanzania kutoka kila mahala na wanakuja watu kutoka nje ya Tanzania ni vyema tuwe na sheria za kiswahili lakini vilevile tuwe na sheria zimeandikwa kwa lugha ya Kingereza.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu hata Mahakama zetu siyo Watanzania pekee wanaenda wanaoenda huko lakini tulivyobadilisha ile sheria hatukuweka vizuri muda maalumu wa kufanya sheria hizi zote ziwe zinapatikana kwa lugha zote mbili. Kwa hiyo kati ya marekebisho haya ambayo yameletwa sheria hii sasa inaweka vizuri, kwamba sasa Serikali watakuwa na siku 90 baada ya sheria kupitishwa kwa lugha ya Kiswahili halafu na wao baada ya siku 90 wawe wamebadilisha iwe kwa lugha ya kingereza.

Mheshimiwa Spika, hii itasaidia itaondoa ombwe fulani la kuwa na sheria kwa lugha moja halafu kesho wanafunzi, vyuo vikuu ama mtu anakwenda Mahakamani halafu sheria bado haijatafsriwa ipo kwa lugha moja. Kwa hiyo mimi nadhani hii kwa Mheshimiwa Waziri wa Sheria hii kwakweli ni innovation kubwa na tumegundua haraka sana.

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo liko jambo lingine hapa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa, kengele ya pili imeishagonga.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, ahaa baada ya kusema hayo naomba niwashawishi tuunge mkono, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Yatokanayo na Urekebu wa Sheria wa Mwaka 2023 .
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi na kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa afya njema leo na pili nimpongeze Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sheria zetu; tatu nimpongeze Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakili msomi Simbachawene, Naibu Waziri Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete wakili, Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Ndumbaro wakili, Mheshimiwa Attorney General Jaji Eliezer Feleshi na watumishi wote ambao wamehusika kuleta maboresho ya Miswada hii mitatu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa Tume ya Mipango na nianze kwa kusoma Ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 63(3)(c) inasema hivi na ninaomba ninukuu. “kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo.”

Mheshimiwa Spika, Mpango wa Taifa ni jukumu la msingi la Bunge hili na ndiyo maana Muswada huu ambao unafufua tena Sheria ya Tume ya Mipango ni jukumu zuri sana na tunampongeza Mheshimiwa Rais lakini Wabunge wengi wamezungumza hapa kwenye mjadala huu wa bajeti wakati fulani fulani wakisema wakielezea umuhimu wa kuwa na Tume ya Mipango ya Taifa. Kwa hivyo Muswada huu leo utaleta tena Tume hii ya Mipango ya Taifa kwa hiyo, kwa kweli tunawapongeza Serikali kwa kuleta mpango huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninakumubuka Mheshimiwa Askofu Josephat Gwajima alizungumza hapa sana kuhusu uzuri wa Taifa kuwa na mpango wa muda mrefu na wa muda wa kati kwa sababu ndiyo itaongoza Taifa letu. Sasa muswada huu leo utafanya hayo yawezekane lakini mtakumbuka vile vile kwamba Sheria ya Fedha ya 2018 ilifuta iliyokuwa Sheria ya Tume ya Taifa sura ya 314 na kwa hivyo sasa tumerudisha tena lakini imerudi namna gani sasa?

Mheshimiwa Spika, kwanza tunampongeza Mheshimiwa Rais siyo tu kwamba imerudi lakini imerudi kwa sura mpya zaidi. Ukilinganisha sheria iliyofutwa majukumu ya tume yalikuwa ni 13 lakini kwa mujibu wa sheria hii sasa Muswada huu majukumu yameongezeka kutoka 13 hadi majukumu 19 na hii inaonyesha tu dhahiri kwamba kuna imerudi kwa sura na nguvu mpya zaidi na mategemeo yetu kwamba baada ya sheria hii kupitishwa na Bunge hii tume itafanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sheria hii vilevile imetengeneza kwa mara ya kwanza na niseme tu kwa historia ya nchi yetu hii Tume ya Mipango imekuwa inapewa majina tofauti tofauti lakini ipo tangu mwaka 1961. Kwa hivyo kila wakati tumekuwa tunabadilisha majina na kubadilisha kwamba safari hii iwe Ofisi ya Makamu wa Rais, iwe chini ya Wizara ya Fedha lakini tafiti zinaonyesha kwamba nchi ambazo zinachukulia kwa usahihi na kwa lugha ambayo ni kubwa zaidi ni kwamba tume hii ikiwa chini ya Mheshimiwa Rais kama Mwenyekiti itafanya itaongezea nguvu na hadhi kubwa tume hii na utafiti duniani inaonyesha nchi zinazofanya vizuri zaidi kwa mfano Ghana, Indonesia, Afrika Kusini na India zote zina tume hii na Mwenyekiti wa tume hii ni Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, uzuri wa sheria hii safari hii kwa sasa bado ni Muswada kwa mara ya kwanza na haijawahi kutokea hii imeona jukumu la kupanga na jukumu la fedha kwamba ni vitu viwili tofauti. Imeleta wazo la kuwa na Mawaziri wawili ambao ni wajumbe kwenye tume hii ambaye ni Waziri anayeshughulika na masuala ya fedha na Waziri atakayeshughulika na Mipango ya Maendeleo ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii kwa kweli ni innovation mpya sana kwa hiyo kwa mara ya kwanza baada ya Muswada huu kupita kuwa sheria tutategemea hata muundo wa Serikali utabadilika. Tutakuwa na Waziri ambaye ana deal na maendeleo ya Taifa peke yake halafu kutakuwa na Waziri wa Fedha ambao wote sasa ni Wajumbe kwenye tume hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukisoma kifungu cha tano utaona Wajumbe wengine ambao wanaongezwa wakiwemo Katibu Mkuu. Kwa hivyo tume hii kwa mara ya kwanza itakuwa na nguvu kubwa zaidi ya kuongoza Taifa kwa mambo yote yanayohusiana na maendeleo ya Taifa. Kwa hiyo, kwa kweli ni jambo jema sana.

Mheshimiwa Spika, vilevile Sheria ya, kuna utafiti fulani umefanywa 2022 na kuonyesha kwamba Wizara ya Fedha sasa kwa majukumu yake yaliyo mengi na kwa sababu tayari yalikuwa ni mengi tu ukiongezea jukumu la kupanga mipango ya maendeleo ya Taifa ni kazi kubwa zaidi. Hawataweza kuweka nguvu kubwa zaidi kwenye kutunga au kutengeneza Sera za Taifa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kwa kweli niwaombe Waheshimiwa Wabunge, kwamba kwa mara ya kwanza sasa hii sheria ikipita tutatarajia sasa mipango ya Taifa hili itakuwa ni ya muda mrefu, itaongoza Taifa letu na itaratibu mipango ya Wizara zingine na kutoa dira ya kimaendeleo kwa Taifa letu. Kwa hiyo nawaombeni sana tuunge mkono hii ipite kwa nguvu kubwa kidogo ili tutume ujumbe kwamba kwa kweli yale mawazo yenu kuhusu Tume hii kurudishwa tena na siyo tu kurudi lakini imeboreshwa zaidi kwa mara ya kwanza italeta manufaa makubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini sheria nyingine ni hii ya TISS (Tanzania Intelligence and Security Services bill) ambayo vilevile kamati yetu iliweza kuchambua na kwa kweli tulikubaliana kwamba kutokana na maendeleo ya intelijensia inavyoenda Duniani yapo maboresho ambayo ni ya lazima kisheria.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano Muswada huu sasa wa sheria hii inapunguza kazi za Waziri ambaye atakuwa anahusika ili kazi yake iwe ni mambo ya bajeti na mambo ya sera; na tumejaribu kuangalia sera na sheria zingine dunia, ziko hivyo. Kwa hivyo kwa kweli madhumuni ya kubadilisha muundo na kubadilisha kazi za TISS ili kazi yao iwe zaidi katika kuangalia mambo ya intelligence; na kwa kwakweli badala ya kwenda kwa Waziri waende kwa Mheshimiwa Rais; Kamati yetu iliona kwamba ina tija kubwa sana. Na hata baada ya kuwauliza wale ambao ni Mawaziri, ni Wizara hiyo wakakubali, kwamba kwa kweli in fact hata kwa fact tu peke yake huwa inafanyika hivyo kwa hiyo hakukuwa na hoja kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, lakini nyingine kubwa ambayo ni nzuri kwa sheria hii ni kwamba kwa kuwa TISS ni chombo cha Muungano. Sheria kuweka muundo sasa ambao ni wakimuungano ilikuwa ni wazo ambalo ni zuri sana, tuwe na ma-directors ambao mmoja anatoka upande mwingine wa muungano na mwingine anatoka upande mwingine wa muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini siyo hii tu, ni pamoja na kuwa na sifa za hawa ambao watakuwa wanaongoza vyombo hivi na kwa kweli tuliona kwamba ni innovation kubwa nzuri sana kwa kisheria hatuwezi kuwachagua watu ambao sifa zao haziko kisheria. Kwa hiyo hiyo pia inaonyesha kwamba tuko serious kuangalia zile credentials na kujua kwamba hawa wawe na sifa hizi, na kwa kweli sheria kwa mara ya kwanza imeweka vizuri sana hili jukumu na kwa kweli ni jambo zuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini sheria nyingine ni hii ya revision laws amendment bill, na yenyewe ukiangalia baadhi ya marekebisho yaliyoletwa kwa mfano Kifungu cha 14. Mtakumbuka mwaka mmoja, miwili iliyopita tulitunga sheria hapa tukasema sheria zetu zibadilishwe ziende kwa lugha ya Kiswahili, na sasa kuna zoezi linaendelea la kufanya sheria zote ambazo ziko kwa kingereza zifanywe kwa kiswahili. Lakini kwa kutambua jukumu vilevile kwamba sheria zetu zinatumika vyuoni na wanakuja Watanzania kutoka kila mahala na wanakuja watu kutoka nje ya Tanzania ni vyema tuwe na sheria za kiswahili lakini vilevile tuwe na sheria zimeandikwa kwa lugha ya Kingereza.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu hata Mahakama zetu siyo Watanzania pekee wanaenda wanaoenda huko lakini tulivyobadilisha ile sheria hatukuweka vizuri muda maalumu wa kufanya sheria hizi zote ziwe zinapatikana kwa lugha zote mbili. Kwa hiyo kati ya marekebisho haya ambayo yameletwa sheria hii sasa inaweka vizuri, kwamba sasa Serikali watakuwa na siku 90 baada ya sheria kupitishwa kwa lugha ya Kiswahili halafu na wao baada ya siku 90 wawe wamebadilisha iwe kwa lugha ya kingereza.

Mheshimiwa Spika, hii itasaidia itaondoa ombwe fulani la kuwa na sheria kwa lugha moja halafu kesho wanafunzi, vyuo vikuu ama mtu anakwenda Mahakamani halafu sheria bado haijatafsriwa ipo kwa lugha moja. Kwa hiyo mimi nadhani hii kwa Mheshimiwa Waziri wa Sheria hii kwakweli ni innovation kubwa na tumegundua haraka sana.

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo liko jambo lingine hapa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa, kengele ya pili imeishagonga.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, ahaa baada ya kusema hayo naomba niwashawishi tuunge mkono, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa fursa hii nichangie mpango huu. Kwanza nimpongeze sana Waziri wa Fedha kwa umahiri wa ku-present mpango huu. Katika kusoma mpango huu ziko baadhi ya taarifa ambazo ndiyo zinaongoza mpango huu. Moja ni Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, nyingine ni Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, nyingine ni hotuba mbili za Mheshimiwa Rais, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, na Mungu amlaze mahali pema peponi; nyingine ni Dira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2020 na nyingine ni Agenda 2063. Lakini muhimu kuliko yote ni Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025, hii hapa.

Mheshimiwa Spika, kama kuna ilani bora ambayo imewahi kuandikwa kwa utaalam mwingi sana na kwa lugha nyepesi sana ambayo Watanzania wanaifahamu ni Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2025. Na kama kuna zawadi ametuachia Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ni Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Bunge hili mkitaka heshima kwa Watanzania, na legacy ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ni kuleta mpango unaotekeleza ilani ya miaka mitano ijayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati tunatafuta kura, nimenunua ilani hizi na nimewapa wananchi wangu, nimewaambia wasome; Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji. Kwasababu miradi ya kimaendeleo ipo. Kama Bunge hili linataka heshima kwa Watanzania tuisaidie Serikali kutekeleza ilani hii kwa asilimia 100. Na sisi tutakuwa tumejenga heshima kubwa sana kwa Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na kwa wale ambao walikuwa Chato, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema hivi; mwanasiasa kwa level ya Urais ukichaguliwa miaka mitano ya kwanza unafanya bidii ile miaka mitano ili uchaguliwe tena, lakini miaka mitano ile mingine ya mwisho unaacha legacy.

Mheshimiwa Spika, ilani hii ina tafsiri zote mbili. Ni legacy ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kama tutakuwa tumetekeleza kwa asilimia 100. Lakini vilevile kwa lugha ya kisheria, ni fast turn ya Rais mama Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kama tutawekeza nguvu kutekeleza ilani hii kwa maana ya fast turn ya Mheshimiwa Rais wetu na legacy ya Dkt. John Pombe Magufuli, maana yake mpango huu tunatakiwa tu-double katika kuleta utekelezaji wa namna ya kutekeleza ilani hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukizungumza mambo ya kilimo, mimi nilikuwa naongea na wataalam wangu wa Wilaya ya Kiteto hapo. Kati ya hekta 1,000 walizowekeza kwa ajili ya umwagiliaji, ni hekta 15 tu ndiyo zinatumika. Na nilizungumza na Mheshimiwa Bashe hapa, excellent, alinishauri tulete andiko la mradi ili tuweze kuongeza hekta zile kwa ajili ya umwagiliaji, na tumeshaandika Mheshimiwa Naibu Waziri, the ball is on you.

Mheshimiwa Spika, sisi tunachotaka baada ya miaka mitano wananchi wale, Watanzania wale waliokuwa wanalia siku ile waweze kufuatilia ilani yao na kila kitu kilichosemwa kiwe kimetekelezwa kwa asilimia 100.

Mheshimiwa Spika, ilani hii inazungumzia barabara mbili kuu nzuri sana; Barabara ya kutoka Kongwa – Kiteto – Simanjiro mpaka Arusha, kilometa 430, ni mikoa karibu minne; Dodoma, Manyara, Arusha na Kilimanjaro. Unaunganisha mikoa minne, ni uchumi. Najua barabara hii iko kwenye ilani hii, lakini sasa tuweke vipaumbele.

Mheshimiwa Spika, barabara ya kutoka Tanga – Kilindi – Kiteto mpaka Singida, karibu mikoa mingine mitatu. Tulete sasa mkakati wa namna ya kutekeleza ilani hii ili wananchi hawa, Watanzania hawa waweze kusema legacy ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli imetekelezwa kwa imani kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namalizia na kitu kimoja alichosema Mheshimiwa Rais wetu juzi. Kuna concept inaitwa ya Serikali moja, ambayo sasa naomba Mawaziri wasikilize vizuri sana; sisi Halmashauri yetu ya Kiteto kwa mara ya kwanza baada ya mvua za miaka miwili hii tumepata maji mengi sana na tuna Samaki sasa na wafugaji wameanza kula Samaki sasa. Na wilaya yangu imetengeneza kama source ya mapato kwamba ni pato jipya, wameanza kutoa leseni. Anakuja Wizara ya Maliasili na Utalii anasema ninyi mmepewa leseni lakini hamruhusiwi kuvuna; concept ya Serikali moja.

Mheshimiwa Spika, naomba sana Ofisi ya Waziri Mkuu ishughulike na hii concept ya Serikali moja. Kitu ambacho wananchi hawataki kusumbuliwa kabisa ni Wizara moja inakupa leseni moja halafu mwingine anatoka anasema haiwezekani, hiyo confusion tuondoe. Tukiondoa hiyo wananchi wetu watakuwa wamenufaika.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru na ahsante sana. (Makofi)
Makadirio na Mapato ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi na kuwa mchangiaji wa mwisho nakushukuru sana. Kwanza kabisa nimshukuru sana Mheshimiwa Rais Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na timu nzima ya Wizara hii. Nimshukuru vile vile Mkurugenzi wa UCSAF kwa kweli kati ya wakinamama wanaofanyakazi vizuri sana Wakurugenzi wenye customer care inayotisha kwa kweli, kwa kweli anatisha sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiteto tulikuwa na changamoto kubwa sana ya mawasiliano watanzania wa Kiteto kwa miaka karibu 60 ya uhuru walikuwa hawawezi kufuatilia Redio Tanzania na mitandao ni tabu sana alikuja Mheshimiwa Naibu Waziri Eng. Kundo tarehe 21 Januari kwa kweli tume-drive kilomita 240 siku moja kuanzia saa mbili ya asubuhi mpaka karibu saa mbili usiku nafarijika sana kwamba kwenye bajeti hii ukurasa wa 145 vijiji 25 Kiteto ipo kwenye mipango ya mwaka wa fedha 2022/2023 nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri nawashukuruni sana kati ya vijiji ambavyo vilikuwa vinasumbuliwa na mtandao Esuguta, Ndotoi, Laiseri, Nsolosidan, Morokitikiti, Engangware, Amey, Lembampuli, Lolera, Emarti, Nati, Magungu, Kinua, Ndirigish, Taigo, Krash, Ndaleta, Orpopog, Mwitikira, Kiperesa, Asamato, Kimana na Songambele na Loltebes zote ziko kwenye bajeti ya Serikali nawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Redio Tanzania ilikuwa haisikiki kati ya wilaya saba ambazo imepangwa kwamba wataenda ku-revolutionize ili na sisi tupate Redio Tanzania kwa mara ya kwanza Kiteto imo nakushukuru sana Wizara hii kwa kweli tuipitishe hii bajeti kwa haraka sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na suala lingine moja tu dogo Mheshimiwa Waziri kumekuwa na mtandao watu wanatupigia simu wanajifanya ni customer care wa makampuni ya simu anajifanya anakupigia anakutapeli watanzania tumekuwa tuki-volunteer kuripoti hizi namba kwa makampuni hayo hatupati taarifa kwamba ile namba uliyoripoti tumefanya hivi tukifanya hivyo take them to task na sisi tutaendelea kuripoti hizi crimes ili watanzania wasitapeliwe nakushukuru sana ahsanteni sana na Mwenyezi Mungu awabariki sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Kwanza kabisa, nimpongeze Waziri na timu yake kwa hotuba nzuri sana. Niseme tu nilifarijika sana kuwaona Machifu wale kutoka Iringa na nguo zao za asili. Tujue tu nchi yetu ina tamaduni nyingi sana na style ziko nyingi sana za namna ya kutambua tamaduni hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, TAMISEMI ni hati ya kila kitu kinachoendelea nchi hii. Kama nilivyokwishasema siku nyingi tu Mwenyezi Mungu awabariki sana watu walioandika ilani hii. Niwatambue Mheshimiwa Dkt. Bashiru na Mheshimiwa Polepole wako hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati tunatafuta kura safari hii hatujatoa ahadi zile nyingi za wanasiasa kwa sababu Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeweka kila kitu. Kwa hiyo, kazi yetu iliyobaki sasa ni kuhakikisha Ilani hii inatekelezwa kwa asilimia 100. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wameongea Wabunge wengi hapa kuhusu TARURA. Nimshukuru, nilikuwa na jirani yangu hapa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hii ameniambia imeongezwa karibu bilioni mia moja na kitu kwa TARURA; kama ni kweli tuwapongeze sana, lakini bado Kamati imeendelea kusisitiza nia ya kuiongezea pesa TARURA. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wilaya yangu ya Kiteto tunatengewa shilingi bilioni moja, milioni 400 na…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Taarifa Mheshimiwa Tabasam.

T A A R I F A

MHE. TABASAM H. MWAGAO Mheshimiwa Spika, nampa Taarifa mzungumzaji, anasema TARURA imeongezewa bilioni 100 ni pesa ndogo sana hizo, hazitoshi kabisa. Naomba uendelee. (Makofi)

SPIKA: Unapokea Taarifa hiyo Mheshimiwa Mbunge wa Kiteto?

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakubali na ninapokea Taarifa hiyo, lakini lazima tuseme kwamba wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu anafunga Bunge la mwezi wa pili, alisema hivi, naomba nimnukuu: “Mheshimiwa Spika kumejitokeza mjadala unaohitaji uboreshwaji wa miundombinu ya barabara za mijini na hasa vijijini. Vyombo vya TARURA na TANROADS vinafanyia kazi na sasa tutakusudia kuongeza uwezo wa vyombo hivi na hivyo Waheshimiwa Wabunge tumepokea ushauri wenu.” Kwa hiyo, waliyofanya tuwashukuru, lakini kama walivyosema Kamati na kama alivyosema Mbunge aliyenipa taarifa, tuendelee kuongeza pesa kwa TARURA. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa natoa taarifa tu kuhusu Kiteto, mfano, tunapata karibu shilingi bilioni moja na mia nne na hamsini na nne na chenji kidogo, lakini uhalisia ni shilingi bilioni saba. Huo ni mfano tu kwamba tunahitaji pesa nyingi sana kwa TARURA.

Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mbunge wa Same, Mheshimiwa Mama Kilango, ni kweli Wilaya ya Kiteto ni kubwa unachukua Mkoa wa Kilimanjaro unachukua na Jimbo la Kongwa, combine, ndio Wilaya ya Kiteto, kubwa sana. Kwa hiyo, nakubaliana naye kwamba tunapotengeneza vipaumbele hapa tuangalie jiografia ya majimbo haya, ni kubwa sana. Mheshimiwa Spika alikuja kunitafutia kura, tumetembea kata nne tu, nakushukuru sana, lakini kila mkutano tulioufanya kero namba moja ni barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna Kata yangu moja inaitwa Dongo, yaani ni kubwa saba, kwa hivyo ndugu zangu tuangalie sana suala hili. kila mkutano niliofanya na nilikuwa naangalia notice zangu wakati natafuta kura, kila mahali nimekwenda changamoto naandika, barabara. Tukifanya hivyo Watanzania watakuwa wamefarijika sana. Barabara za Kata za Sunya, Asamatwa, Magungu, Dongo, Makame, Katikati, Robosoid, Mserengine, Olpopori, Kiberesa, Nigish, Mbeli na Kiteto ni bread basket, mahindi yote yanayokuja huku yanatoka Kiteto, kwa hivyo, tuongeze juhudi katika kutengeneza barabara hizi ili wananchi hawa waongezee bidii.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ambayo hata Kamati imesema, ni hizi asilimia 10 ambazo ziko kwenye Ilani yetu. Kwa hiyo, sisi ni kutembea na Ilani tu, ukurasa wa 30, tuwe wakali kwa halmashauri zile ambazo hazitengi asilimia kumi. Sio kwamba tu wana-violate takwa la kisheria, lakini hawasomi Ilani yetu. Kati ya vitu ambavyo Wabunge tunatakiwa tuwe wakali sana hapa ni tuhakikishe Ilani hii inatekelezwa kwa asilimia 100. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vituo vya afya. Ndio maana mimi nasema Ilani hii naipenda sana, inasema kila mahali tutajenga vituo vya afya, Wilaya ya Kiteto kati ya kata 23 tuna vituo vya afya viwili tu. Kwa hiyo, nafikiri tukija hapa mtuulize Bwana Olelekaita una kata ngapi ambazo hazina vituo vya afya, halafu tufanye mathematics simple, kila mwaka mnatakiwa mnipa ngapi ili baada ya miaka mitano tutekeleze, hivyo tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukisema tunapeleka computer kwenye sekondari kadhaa, mimi ninazo 18, kwa hiyo, ningekuja tu hapa nidai computer zangu 18. Labda kitu cha kufanya pia ni kujaribu ku-cost hii Ilani yetu ili tujue tunahitaji gharama ya shilingi ngapi miaka mitano ijayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wananchi sasa kwa muamko huu ambao umeoneshwa kupitia TAMISEMI wamechanga michango kwa ajili ya vituo vya afya; Dosidosi, Matui, Ndedo, kazi zinaendelea. Kwa hivyo, inatakiwa tu mkono wa Serikali kidogo ili tushirikiane kutekeleza Ilani hii. Kwa hiyo, tuangalie vipaumbele hivi na tutembelee maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, mimi nimekwenda kwenye kata moja katika mkutano wa hadhara, kumbe nikagundua wananchi wala hawataki hata ule mkutano wananiambia tu twende tukuoneshe kituo cha afya. Nilivyofika pale ikabidi niseme na mimi kwa Mfuko wa Jimbo nitaweka mkono hapa na nimeshafanya hivyo, lakini sasa pesa ya Serikali, mtuunge mkono ili wananchi wale wajue kwamba wakihangaika Serikali na yenyewe inaweka mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wizara hii ni hati. Walimu wapo wengi sana wanajitolea, wanaomba ajira hizo tena kwa miaka mingi tu. Mimi nilikuwa naongea na Afisa wangu hapa akaniletea karibu majina 100 tu kwa Kiteto na wako walimu wazuri wenye taaluma tena za Kiswahili, mabingwa. Tumepitisha sheria hapa ya kuruhusu Kiswahili sasa kianze kutumika na tuna wataalamu wamejaa wanasubiri.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa muda wako umeisha.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na ninaunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Kwanza kabisa nampongeze Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na timu yao wote.

Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru, juzi alituwekea foundation nzuri sana. Tunapozungumza habari ya kilimo au mifugo na uvuvi, kama asilimia 65 au 70 ya Watanzania wako huko; we have no option, lakini Bunge hili umenisaidia, kwamba baada ya miaka mitano Watanzania wanufaike na sekta hizi za mifugo, uvuvi na kilimo. Najua pengine tutakuwa tumechelewa mwaka huu, lakini tunaanza kutema cheche hapa ili sasa mwaka wa fedha ujao Serikali ijue kabisa, kama tunataka kuweka legacy kwenye kilimo, mifugo na uvuvi, ni lazima tu-commit pesa nyingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nasoma takwimu za Serikali hapa, tunaambiwa kuna mifugo karibu milioni 33.6. Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeainisha vitu vingi sana ambavyo tumeahidi kufanya kwa miaka mitano ijayo. Hekta za mifugo kutoka 2,788,000 hadi hekta 6,000,000. Kwa hiyo, maana yake tumeahidi kutenga hekta 3,211,000. Ili mifugo iweze kustawi ni lazima wawe na maeneo.

Mheshimiwa Spika, mzungumzaji aliyepita alikuwa anasema ng’ombe anazaliwa Kagera anaishia Lindi, there is absolutely nothing wrong. Ng’ombe kuhama ni coping mechanism ya magonjwa, wanatafuta maji na malisho. Wafanye nini sasa kama hifadhi zinachukuwa maeneo yao? Kuhama kubaya ni ile ya kusababisha migogoro na watumiaji wengine wa ardhi. Hiyo hapana, lakini kuhama ni coping strategy.

Mheshimiwa Spika, vile vile ilani inazungumza na nilikuwa nasoma hotuba ya Wizara hapa; inasema mtajenga majosho 129. Ni kidogo sana na hii inatokana na bajeti yenu kuwa ndogo sana. Kwa mfano, Kiteto peke yake majosho tunayohitaji ni 48, kwa sababu ilani inasema lazima katika kila kijiji chenye mifugo kiwe na josho. Sasa kama mnapewa bajeti ya kutengeneza majosho 129, Kiteto peke yake inahitaji 48, haiwezekani. It is a very big joke.

Mheshimiwa Spika, vile vile ilani imesema tutajenga mabwawa kama 400 hivi kwa miaka mitano. Kwa hiyo, in average ni mabwawa karibu 91 kila mwaka, lakini hapa ninyi mmepewa mabwawa manne tu. Kama siyo manne, Matano. It is a very big joke. Kwa Kiteto peke yake, pungufu ya malambo ni 44, halafu tunaweka kwenye bajeti manne.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tumedhamiria kwamba Bunge hili liwanyanyue Watanzania katika sekta hizi muhimu sana, nashauri; kwa sababu nilikuwa naangalia hapa, uvuvi na mifugo; na imetokea trend siku hizi ukichanganya mifugo na kilimo kuna sekta moja itapewa pesa nyingi kuliko nyingine. Ukichanganya maji na mifugo kuna sekta moja itapewa hela kutoka nyingine. Sasa maji tunafanya vizuri, kilimo tunaelekeaelekea hivi kidogo, sasa mmechanganya uvuvi na mifugo. Sasa uvuvi inachukua bajeti mmetenga hapa karibu shilingi bilioni 90 na kitu kwa uvuvi halafu mifugo shilingi bilioni 16.

Mheshimiwa Spika, tukitaka kufanya vizuri zaidi labda huko mbele tutenge kabisa, tuwe na Wizara maalum ya Mifugo, tuwe na Wizara maalum ya Uvuvi, tuwe na Wizara ya Kilimo. Tukitenga hivi tutaweza kuweka nguvu kubwa zaidi.

Mheshimiwa Spika, nami napendekeza tena, lazima tuji-commit, kuweka asilimia 10 ya mapato yetu kwenye uvuvi, kwenye mifugo na kilimo. Tukifanya hivyo tutaweka investment, lazima iwe serious. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mzungumzaji aliyepita alikuwa anatoa mifano ya nchi nyingine kama Ethiopia, Rwanda na Uganda; na Botswana by the way, ndiyo inafanya vizuri zaidi kuliko nchi yoyote Afrika kwa ku-export beef, lakini angalia investments zao, ni kubwa zaidi.

Mheshimiwa Spika, nami nakubaliana nawe. Kuna siku nimetembelea NARCO hapo, kwenda kuangalia ng’ombe pale. Ni kweli, yaani hata majani yaliyoko pale hayawezi kumalizwa na ng’ombe walioko NARCO. Ni afadhali mngewapa wafugaji tu. Kwa hiyo, ni lazima tuangalie tija kwa miradi tunayowekeza kwenye sekta hizi.

Mheshimiwa Spika, tulikuwa tunasoma ilani hapa; tani za kunenepesha mifugo nchi hii ni 900,000 peke yake na tuna ng’ombe milioni 33 na tumejiwekea malengo ya kutengeneza hizo tani milioni nane. Kwa hiyo, huo ni mfano tosha tu kwamba hatuja-invest heavily kwenye mifugo. Kwa hiyo, tusishangae sana.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, pato la Taifa asilimia 7.9 siyo kidogo. Wakati mwingine huwa nafikiri kwamba hatutengenezi mipango sahihi ya ku-capture contribution ya mifugo. Kama kuna wanywa bia hapa, hakuna mnywa bia hata mmoja asiyekula nyama. Nami sitaki kuvuruga Bunge lako, lakini ningesema leo wanyooshe mikono wanaokula nyama hapa, watasimama mpaka wale waandishi wa habari ambao wanapiga kamera hapa. Hiyo ni contribution ya mifugo. Kwa hiyo, I think hamjaweza ku-capture kabisa contribution ya mifugo.

Mheshimiwa Spika, kwa Jimbo la Kiteto peke yake tuna mifugo 500,000, mbuzi 500,000, siyo kidogo hiyo, ni contribution kubwa sana. Ripoti zeni zinasema kuna watu milioni nne wanategemea direct income kutoka kwenye mifugo katika nchi hii. Kwa hiyo, lazima tuwe serious katika ku-invest, tuweke pesa nyingi ili mifugo yetu iweze kuleta tija kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa naangalia ripoti zangu za Kiteto hapa wataalam wanaohitajika, ukiangalia wataalam wanaohitajika kwenye sekta hii ni 106 halafu waliopo ni 35, pungufu 40. Kwa hiyo lazima kweli tu-invest kwenye mifugo na uvuvi kama tunataka kwenda mbele huko. Miaka miwili iliyopita sisi tumepata mvua kubwa sana na Kiteto sasa tuna wafugaji wanakula Samaki sasa.

T A A R I F A

MHE. ESTHER MATIKO: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Taarifa Mheshimiwa Esther Matiko nimekuona.

MHE. ESTHER MATIKO: Mheshimiwa Spika, ahsante nataka tu nimpe taarifa ndogo mchangiaji wakati anachangia amesema tukiamua kuazimia nakuchukua walau asilimia kumi ya mapato, tungeweza kufika mbali upande wa mifugo, uvuvi hata kilimo. Nimkumbushe tu kwamba ni Azimio la Malabo ambalo tumelisaini ambalo linatutaka walau tutenge asilimia kumi ya bajeti ya Serikali kwenye eneo la kilimo, mifugo na uvuvi. Kwa hiyo, siyo kwamba tuhiari tu kama mapato ila ni Azimio ambalo tumelisaini. Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Taarifa hiyo unaipokea Mheshimiwa Edward.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakubali na napokea, lakini ninataka tu nimuambie kwamba hatuhitaji Malabo actually ili tuamue ku-invest ten percent. Malabo declaration ni kwamba tu wametusaidia, lakini kweli kama tungekuwa tunasubiri Malabo declaration na Malawi na hata hivyo pamoja na declaration hiyo investment inayoenda kwenye kilimo ni less than one percent, less than one percent. Kwa hiyo, kwa kweli lazima, lazima tutoke huku tu-invest every kwenye uvuvi, tu-invest every kwenye mifugo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hivi, siku hizi Kiteto tumepata kama mabwawa mawili ya samaki na tumeanza kujifunza kula samaki na wilaya yangu kwa mara ya kwanza kwa mwaka fedha wamesema tutapata kodi kama milioni nane hivi inatokana na Samaki na wafugaji wameanza kutengeneza leseni kutoka kwenye halmashauri.

Mheshimiwa Spika, halafu anakuja mtu wa maliasili eti anawaambia wale wafugaji wale brand new, watu ambao wanataka kula samaki for the first time, halafu unawaambia tena eti hairuhusiwi, sijui nini, yaani tunawaongezeeni watu wa kula samaki ili tuongeze tija zaidi halafu mtu anatwambia mambo ya leseni yametoka wapi ni confusion na ndio ile Mheshimiwa Rais wetu alikuwa anasema concept of one government. Kwa hiyo, kwa kweli lazima tuwatetee, lakini baada ya kusema haya lazima sasa na ninyi mifugo muwe serious nilikuwa nasoma ripoti zenu hapa.

Mheshimiwa Spika, wanasema eti ng’ombe milioni sita zimekamatwa kwenye mapori tengefu, ng’ombe milioni sita ipo kwenye ripoti hapa, na kwanza nashangaa kwa sababu hawajaandika jimbo langu na kila siku wanakamatwa hapo na pori hili Tengeru linaitwa Mkongoroyo, lazima muwatete wafugaji hawa, ipo kwenye ripoti zenu. Naona Waziri anamuuliza mwenzake hapo. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, ukisoma ukurasa wa 205 nendeni mkasome data za mifugo kukamatwa kwenye mapori haya, ni lazima kama nchi tusimame huu ni uchumi hatutaki ng’ombe hizi zikamatwekamatwe hovyo ni uchumi wa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi; na niungane na Wabunge wengine kukupongeza kwa unavyouendesha mjadala huu. Kwa kweli kama kuna mjadala ambao umefanyika kwa ufanisi sana. Ni mjadala huu wa ripoti ya CAG; na si kwa bahati mbaya, kwa sababu hii ndiyo imebeba kila kitu cha nchi hii, kwa hiyo nikupongeze sana, I am very proud, as your student, I am very proud. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwapongeze sana Wajumbe wa Kamati hizi zote tatu, LAAC, PIC na PAC, kwa kweli wamefanya kazi nzuri sana, na ni kazi ngumu kwelikweli. Mimi nadhani mwaka mmoja uliopita halmashauri yangu iliitwa kwa hiyo nilishuhudia mahojiano kati ya Kamati yetu ya LAAC na halmashauri; inafanana kabisa na process zile za cross-examination za mahakama, ni nzuri sana. Kwa hiyo kwa kweli tuwapongeze sana.

Mheshimiwa Spika, nimejaribu kuangalia zile ripoti zota za CAG, takriban repoti 17, kama zote tutazifuatilia, pages 3,632. Hii maana yake nini? Ni kwamba, huko mbele ili tuweze kupata muda mzuri wa kuchangia vizuri, labda pengine tuangalie pia muda ili Wabunge waweze kuchangia. Niwapongeze Wabunge wale wote ambao wamepitia ripoti hizi, kwa kweli kazi nzuri sana wamefanya.

Mheshimiwa Spika, mimi nazipongeza pia halmashauri zilizofanya vizuri. Wale ambao wamefanya vibaya tuweze kuwasema sana. Tusipo shughulika na wale wanaofanya vibaya inaondoa uzalenda wa wale wanaofanya vizuri, kama alivyokuwa anasema Mheshimiwa Shigongo. Lazima wanaofanya vibaya waadhibiwe.

Mheshimiwa Spika, Jaji mstaafu wa Kenya aliwahi kusema hivi, “the greatness of any nation lies in its fidelity to the its constitution and adherence to the rule of law but above all respect to God”.

Mheshimiwa Spika, CAG ameshafanya kazi yake ya kikatiba na ameonesha madudu ambayo yamefanyika kila mahala. Kazi iliyobaki ni ya Bunge. Bunge liko kwenye trial wanasubiri sasa kuona Bunge litachukua maamuzi gani. Kwa hiyo, kwa kweli tufanye maamuzi ambayo yatasaidia nchi hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama walivyosema Wajumbe wengine hapa, Mheshimiwa Rais anafanya kazi nyingi sana, anahangaika kila mahala kutafuta pesa kwaajili ya miradi ya Tanzania. Lakini ukisoma ripoti hizi, na ukaangalia mfano tu wa zile fedha alizotafuta kwaajili ya miradi ya UVIKO, ilivyoleta heshima kila mahala nchi hii, halafu unaambiwa ni TirionI 1.3 tu; lakini ukisoma ripoti hii unaambiwa kuna zaidi ya Tirioni 1.8 zimepotea. Maana yake kwamba, kama hizi fedha tungeweza kupeleka kwenye miradi mingine heshima yetu ingekuwa kubwa zaidi na zaidi.

Mheshimiwa Spika, hakuna kitu kimenisikitisha sana kama unakuta unaambiwa eti kuna halmashauri 47 wamenunua dawa zimeharibika. Fedha zimetumika na maisha ya Watanzania tunayaweka kwenye wakati mgumu wa kuwa na dawa ambazo zimeharibika, this is shame. Kwa hiyo si tu kwamba fedha zao zimepotea lakini wanaweza pia wakapata madhara ya afya kutokana na dawa ambazo zimeharibika.

Mheshimiwa Spika, nilitaka pia kupata clarification kwa ripoti hii ya CAG, ukurasa wa tano. Kwenye ku- summarize zile recommendation, wanazosema 10,824 kwenye jedwali namba mbili wanasema utekelezaji unaendelea kwa recommendation 10,864.Lakini paragraph iliyopo juu hapo, wanasema mapendekezo 1,864 sawa na asilimia 17 hayajatekelezwa, lakini ukiangalia kwenye chati ambayo hayajatekelezwa ni 3,637, nadhani hiyo confussion lazima iwe clarified ili tujue. Kwa sababu hapa ni kama ime swap kidogo.

Mheshimiwa Spika, habari za halmashauri zimezungumzwa hapa na sisi tunakutana hapa kama wawakilishi wa wananchi, na kila mahala tunakokwenda hakuna maji, hakuna barabara, hakuna zahanati hakuna vituo vya afya, madarasa, madawati halafu ukiambiwa kuna fedha zinapotea na watu wapo na Sheria zipo ni hatari kidogo.

Mheshimiwa Spika, ukisoma ripoti hii, Mheshimiwa Attorney General ambaye kwa kweli namheshimu sana, I think is the only man, amekuwa DPP amekwenda judicial na Sasa ni Attorney General na is the most qualified, by the way. Naomba ulisaidie Bunge hili, next ripoti tusipate ripoti inayo tokana na mikataba ambayo inafungwa fungwa kwa ajabu ajabu. Bunge hili lilifanya mapinduzi ya sheria kwa kufanya wanasheria wote kuwa chini yako, hata wale wa halmashauri, nadhani nia ilikuwa ni mfanye quality assurance ili walau basi yale yanayotokana na mikataba mmusaidie CAG ili ripoti ijayo isiwepo.

Mheshimiwa Spika, kuna suala la TAMISEMI, na ripoti imezungumzwa hapa, kwamba hamrejeshi fedha, na sijui kama Waziri wa TAMISEMI yuko hapa. Nakushukuru na nakupongeza sana, ulisema unataka kuweka misingi ili wanao kufuata wakutane na misingi hiyo. Sasa, kuna suala linatusumbua kila wakati, kutorejeshwa kutoka hazina pesa mnazochukua kwa kigezo kwamba mwaka umeisha. Tumeshazungumza hapa, mnapeleka fedha na hamrudishi. Kwa mfano Kiteto imechukuliwa fedha milioni nane ya mfuko wa jimbo ambayo ilitakuwa iwe imejenga darasa Zambia Kata ya Lengateu, hamtaki kuleta milioni 32 za Basket Fund. Mheshimiwa Waziri kama unanisikiliza hizi pesa Monday, Tuesday Wednesday or next week hizi fedha zije tena. Haiwezekani mnatutengenezea hoja, kesho ripoti za CAG zije halafu mnatuambia kwamba miradi imechelewa, kumbe ni ninyi. Tulishasema hapa mzipeleke hizo fedha. Mheshimiwa Waziri hiyo ndiyo test yako ya Kwanza.

Mheshimiwa Spika, yamezungumzwa mambo mengi hapa, wizi takriban kila mahala, eti mpaka kwenye Balozi zetu; that is how desperate we area, mpaka kwenye Balozi. Sasa ukiona madudu yanafanyika mpaka kwenye Ubalozi basi ujue kwamba tuko desperate sana.

Mheshimiwa Spika, ripoti ya CAG inatuambia, kati ya maagizo ya Bunge hili 619 kwa mamlaka 99 eti kuna maagizo 264 ya Bunge lako hili hayajatekelezwa. Sasa ndiyo tutashangaa zile za Waziri wa Elimu na Bodi ya Mikopo, honestly kama maagizo 264 ya Bunge hili hayatekelezwi!

Mheshimiwa Spika, nimesoma ripoti ya Bodi ya Mikopo inasikitisha sana, kwamba wananchi masikini hata wale wanaotokana na familia za TASAF ambao kimsingi walitakiwa kuwa na dirisha maalum, wanakosa mikopo. Watoto wa wakulima, watoto wa single parent eti wanakosa mikopo. Mwalimu Nyerere alishasema hapa, ukitaka kumsaidia mtoto wa masikini, mpe elimu. Elimu haizuii umasikini, lakini ni silaha ya kupambana na umasikini. Sasa tusipoweka fedha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wetu, watapambanaje na umasikini?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kweli hili la Bodi ya Mikopo, nashukuru sana kwa maazimio ya Bunge yaliyofanyika juzi. Wanafunzi wanahangaika kila mahali, wanatusumbua sisi Wabunge; “napiga simu hapa niangalie kama nitapata mkopo.” Wanafunzi ambao hali zao wanatoka kwenye familia ambayo ni masikini sana. Inasikitisha sana.

Mheshimiwa Spika, kwa maneno yangu ya mwisho kabisa, kwa sababu ni lazima tutengeneze majawabu. Nilikuwa nasoma kitabu fulani hapa. Institute inaitwa, Wajibu Institute of Public Accountability, wanasema hivi, naomba ninukuu, kwa sababu inaweza ikatusaidia mbele huko.

“Naombeni ushauri, Serikali kuiwezesha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa ndani kuwa na fungu au Vote ili kumjengea uwezo na kufanya kazi zake kwa uhuru zaidi. Aidha, wajibu wa kumshauri Mkaguzi Mkuu wa ndani awe anapeleka taarifa hizi kwa Katibu Mkuu Ikulu ili taarifa zake zimfikie kwenye Baraza la Mawaziri ambalo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mwenyekiti wake. Ripoti hii ikimfikia Rais kabla ya Septemba, tarehe 30, ambapo itakuwa ni miezi tisa baada ya mwaka wa fedha wa Serikali kumalizika, hii itampa fursa Mheshimiwa Rais kujua hali ya utendaji wa Serikali kabla ya ripoti ya CAG.”

Mheshimiwa Spika, nadhani hili likichuliwa pengine linaweza likasaidia ku-improve ripoti huko mbele. Nakubaliana na maagizo yote na ripoti zote mbili, naomba Bunge hili sasa lionyeshe kazi yake.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii na kwa wale ambao hawafahamu Mheshimiwa Naibu Spika ni Mwalimu wangu, alinifundisha Law School of Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa napenda nimpongeze sana Waziri wa Maji; Waziri wa Maji kati ya wageni wangu niliowatambulisha leo, nilitembelewa na waliogombea na mimi, aliyegombea kupitia ACT Wazalendo Ubunge na aliyegombea kupitia CUF, wa ACT Wazalendo Ndugu Kamota amekubaliana na kasi ya Chama cha Mapinduzi na kazi anazofanya Mbunge hapa na amekubali kuungana na Chama cha Mapinduzi. Namshukuru sana kwa uungwana wake mzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiteto nilishazungumza hapa ni takribani square kilometa 17,000 ni majimbo mengine kama matano hivi ni jimbo kubwa sana. Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi ambayo naongelea kila wakati kwasababu, ndio social contract ya kwetu na wananchi ukurasa wa saba na naomba ninukuu kabisa “Kuongeza kasi ya usambazaji maji safi na salama kwa asilimia 85 vijijini na 95 mijini”.

Mheshimiwa Waziri, kwanza kabisa naomba bajeti ya Kiteto msiipunguze hata nukta moja, tuanzie hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vile vile, kwanza Mkoa wa Manyara overall ni asilimia 58 tunapata maji below national average kwa hiyo, katika kutengeneza vipaumbele hivi tuangalie mikoa ambayo ipo nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ukiacha Manyara sasa, Wilaya ya Kiteto ni asilimia 52 na Mji wa Kibaya ambao ndio mji wetu kwa miaka 20 sasa, ni asilimia 44 maji na miundombinu pale mjini yamechakaa ni ya mwaka 1980. Mheshimiwa Waziri, ukitutengea milioni 100 tutaweza kufumua mifumo ya maji ile na kutengeneza vizuri sana, ili Mji wa Kibaya ambao ndio sura ya wilaya ipate maji ya kutosha. Kata kama za Njoro Mji wa Matui, Kijungu, Lengatei, Dongo hazina maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Hotuba ya Rais mama Samia Suluhu Hassan, ukurasa wa 29... (Makofi)

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Olelekaita kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani.

T A A R I F A

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni mdau wa Wilaya ya Kiteto nalima mashamba yangu kule, Mheshimiwa Mbunge ametaja kata ambazo zinakosa maji kwenye eneo hilo na nilikuwa namkumbusha tu kwamba asisahau Kata ya Dosidosi ambayo nimewekeza pia. Ahsante sana. (Makofi/Kicheko)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge alikuwa anaendelea kutaja kata zake. Haya unaipokea taarifa hiyo, unakumbushwa kwamba kuna kata inayohitaji.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea sana sana kabisa na nimkumbushe tu kwamba Katibu wa Mbunge anatoka Dosidosi. Na napokea sana na niseme tu kwa kuwa amenikumbusha, nilipata bahati ya kutembelewa na aliyekuwa Makamu wa Rais ambaye ni Rais wetu sasa Mama Samia Suluhu Hassan, kunitafutia kura na kituo cha kwanza kabisa ni Dosidosi. Dosidosi ni Kijiji cha kwanza tu ukitoka Kongwa na kutokana na ukame wa Jimbo la Kiteto, Mheshimiwa Rais aliahidi mabwawa Kiteto. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nakushukuru sana na ni kweli kama alivyosema naendelea kutaja kata zangu ambazo hazina maji; Kata ya Njoro, Kata ya Makame, Kata ya Lolera. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nasema hotuba ya Mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan ukurasa wa 29 naomba ninukuu. “Aidha, kwa maeneo yasiyokuwa na vyanzo vya maji tutajielekeza katika ujenzi wa mabwawa ya kuvuna maji ya mvua”. Kutokana na jiografia ya Jimbo la Kiteto mabwawa, na kuna ahadi ya muda mrefu ya Serikali ya bwawa la Dongo, Kata nzima ya Dongo. Bwawa hili likijengwa vijiji sita na kata mbili zitanufaika na mradi huu na wananchi walishatenga eneo kubwa tu. Kwa hiyo, namuahidi Waziri kati ya maeneo ambayo tutakwenda ni Dongo ukaone bwawa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, shida nyingine, kutokana na ukubwa wa Wilaya hii engineer ni mmoja tu na mafundi wako watatu, haiwezekani. Tunaomba engineers wawili tunaomba na mafundi sita, hatutaki wengi sana sisi sio selfish sana hao tu Mheshimiwa Waziri. Tukipata na magari mawili kutokana na jiografia ya jimbo hili utatusaidia sana na maji yatapatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la maji wanaoumia sana ni wakina mama kwa hiyo, kama tutaweza kutimiza takwa hili la Chama Cha Mapinduzi tutakuwa tunawasaidia wakinamama wengi sana nchini. Baada ya kusema hayo nakushukuru sana kwa nafasi hii, ahsante sana naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayofanya kwa wizara hii, tumeona bajeti imeongezeka; nimpongeze pia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Naibu Waziri, Katibu Mkuu na timu nzima ya wizara hii kwa kazi wanayofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka uliopita wafugaji walipata taabu kubwa sana kutokana na ukame; na Mheshimiwa Naibu Waziri alinitembelea tarehe 14 Januari, 2022 kuona athari za ukame kwenye Jimbo la Kiteto. Tulipata hasara karibu ya ng’ombe 25,000 kwa sababu ya ukame. Namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri alifika na aliona athari ambazo zimeletwa na ukame na nakushukuru kwa majosho Matano kwa vijiji vya Makame, Mwitikila, Lolela, Ngabolo na Katikati. Lakini kwa kuwa Kiteto ni Wilaya kubwa yenye mifugo wengi sana bado tuna upungufu wa majosho na tulitegemea bajeti hii mtatuongezea majosho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukame wa mwaka jana umetokana na kukosekana kwa mvua na malisho. Kwa hiyo, tunategemea wizara hii, kipindi hiki mje mlete bajeti ambayo inaleta solution kwa ajili ya mabwawa. Na mnafahamu nimeandika barua katika kuomba mabwawa. Natamani baadaye wakati mnahitimisha bajeti yenu mtupe majibu kwa sababu wafugaji hawa wanataka kusikia majibu yenu. Kwa kuwa tayari kuna dalili kwamba mwaka huu pia ni kama kidogo hivi; natarajia kabisa wizara ituambie baadaye mmejipangaje sasa ili madhara haya ambayo yanatokana na ukame isirudi kwa namna ambayo imefanyika mwaka jana, kwa kuandaa wafugaji na kuandaa maeneo kama ambavyo Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyosema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la Hereni ambalo limeendelea sasa. Ushauri wangu, elimu haipo sana ya kutosha kuhusu suala hili Mheshimiwa Waziri; tunawaombeni sana mtoe elimu kwa wafugaji wafahamu logic ya hii Hereni nini na pia tunaweza kusikia kelele kwamba bei hii ni kubwa kidogo kwa hiyo muangalie sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri ulifika Kiteto na ulitoa ahadi ya vitambaa vile vya magonjwa haya ya Ndorombo, tunatarajia baadaye wakati unahitimisha kwenye bajeti yako wananchi wa Kiteto wasikie majibu, tukipata vitambaa hivi tukaweka kwenye maeneo ya malisho itasaidia kupungu magonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa wizara hii inaangalia mifugo, siku hizi tumepata janga kubwa sana mahusiano siyo mazuri sana kati ya Wanyamapori, Hifadhi zetu na Wafugaji. Tunataka wizara kwa kuwa tulishazungumza hapa concept of one Government Wizara ya Maliasili na Utalii na Mifugo mzungumze ili kuondoa matatizo hayo kwa wafugaji.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa kwa mchango mzuri.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru; naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi na kwanza kabisa nimpongeze professor Waziri wa Kilimo, Naibu Waziri na timu yake na nawapongeza sana kwa sababu kwenye hotuba hii walau Kiteto imetajwa mara mbili tu, ukurasa wa 30 na ukurasa wa 127, lakini nawapongeza tena zaidi kwa sababu walau ninyi mmefuatilia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, na tunaka kila wizara tufuatilie Ilani hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukisoma Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ukurasa wa 42 tulijiwekea malengo ya kutengeneza tani laki 710 za alizeti, lakini kwenye hotuba hii nyinyi mmeweka tani milioni moja excellent tunataka tuwe na mwelekeo huu wa Ilani yetu. Lakini vilevile ukurasa wa 42 tulisema tutajenga maghala 14 kwenye mikoa hii ipo hapa excellent. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile tumesema kwenye ukurasa wa 43 tutawapatia vijana 400 kutoka mikoa tisa vifaa ipo kwenye hotuba yenu hapa safi sana. Lakini sasa nataka muongeze hivi vijana 400 mikoa tisa, kila mkoa tunataka mgawanye mlete mathematics ni vijana 44, na mkifika kwenye mikoa ile tunataka mtuambie mkoa ina wilaya ngapi na vijana wangapi watoke humo mimi nimeshapiga mahesabu nisipopata vijana sita kutoka Kiteto, Manyara mtakuja kutueleza mmefuata nini sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la umwagiliaji Kiteto ambayo nilikwisha kusema ni bread basket, kilimo cha mvua ni asilimia 99.9 kati ya hekta 1385 ambazo tumetenga kwa ajili ya umwagiliaji ni 0.00 percent ndio inatumika haiwezekani. Ni lazima tuwe wakweli kabisa tunaposema kilimo, kilimo inachangia pato la Taifa asilimia 29, 28 au 26 data zenu zote zinasema hivyo na inawaajiri watanzania asilimia 65 halafu tunapokuja kwenye bajeti tunawatengea bilioni 300, haifiki hata bilioni 300 honestly watafanya nini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Maputo declaration na Malaba declaration inasema nchi zime-commit kuongeza asilimia 10 kwenye agriculture, hii haifiki hata percent moja, hata hii program tunayosema tunafuatilia hii program ya kuendeleza kilimo ya pili ili-commit bilioni 13 kwa ajili ya kilimo we are not even one percent kwa hiyo, lazima tuwe serious tunapozungumzia agriculture. Imeajiriwa watanzania 65 pato la Taifa kubwa namna hiyo halafu tunawekeza sijui kwenye masekta gani huko tuwe serious kwa kweli tunapozungumzia agriculture. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na Ilani yetu imesema vilevile Chama Cha Mapinduzi tunataka kutoa wakulima kwenye jembe la mkono na kwenda kwenye matrekta, yamekuja matrekta hapa ya Urususi hapa wakulima wangu Kiteto wamechukua karibu matrekta 100, halafu mnawapeleka kwa Wizara ya Viwanda is a confusion yanatakiwa matrekta haya yawepo kwenye Wizara ya Kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili kwa sababu nyinyi mpo karibu na wakulima hawa halafu mnawaambia kwamba yale matrekta yale yalikuwa ya bei nafuu ni uongo mtupu, trekta bilioni 45, trekta milioni 55, sasa kuna unafuu gani hapo halafu mabovu kwanza, hebu tuwapatie wakulima matrekta haya wapate kuzalisha. Namshukuru sana waziri kwenye hotuba yako umewashukuru wakulima kwa sababu ni kweli, kilimo nchi hii ingekuwa wakulima wale hawalimi wala tusingekuwa na chakula. (Makofi)

SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa Edward.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika baada ya hayo nashukuru naunga mkono hoja ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwasababu ya muda nitatoa tu hongera ya jumla hivi, mnielewe. Nitawapongeza baadaye. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi, ukurasa wa 113 unasema hivi, naomba sana wataalam wetu waisome sana: “Kuimarisha mahusiano kati ya maeneo ya hifadhi na wananchi.” Mahusiano ya wananchi na hifadhi ni mabovu sana. Hilo moja. Ilani inaendelea kusema hivi, ili Sekta hii iwe endelevu, lazima mjali haki na maslahi ya wananchi. Hamwangalii sana maslahi ya wananchi wakati mwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nasoma vitu vingi tu hapa, nilichogundua ni kwamba, kama walivyosema wasemaji wengine, utalii tangu tumepata uhuru mambo yote bado yapo kikoloni zaidi; ni boots and guns, fences, fines, mnaanza kuua watu, mnachukua ng’ombe wa watu; hiyo siyo sustainable. Mwache! Uhifadhi ili uwe endelevu, ni lazima ushirikishe wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeambia kwenye data hapa kwamba sasa tunaongelea asilimia 32 mpaka 40 ya nchi hii, iko kwenye hifadhi, it may not be enough, lakini lazima mfahamu tumeongezeka. Ni dhana ya kikoloni ambayo ni exclusion, expansion, removable, nature, then people later, haiwezi kuwa sustainable. Nchi nyingine zimeshabadilika, wameanzisha model ambazo zina-accommodate watu na uhifadhi. WMA ni classic example, inawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo ya kukaa na kuanza ku-characterize ardhi za watu, eti corridor, eti buffer zone, eti wildlife or pastoral area, I mean! Mheshimiwa Waziri, kuna tangazo laki hapa nililisoma asubuhi hapa. Umewaelekeza watu wako wachaji ng’ombe 100,000 kwa kichwa cha ng’ombe. Miaka miwili iliyopita ilikuja sheria hapa ya kutaka kulishawishi Bunge lilete faini ya shilingi 100,000 kwa kichwa na Bunge lilikataa, hongereni sana. Sasa limeanza kurudi kwa mlango wa nyuma.

Mheshimiwa Waziri, this is illegal, haiendani na sheria zetu, nawe ni Mwanasheria, Wakili tena Dokta kabisa. Nakushauri sana, please rethink kuhusu hili, it is illegal, it is unlawful. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndiyo maana kuna wengine walikuwa wanasema hapa hatufuati sheria. Sheria haijasema hai-punish ng’ombe, inam-punish mwenye ng’ombe, ndiyo logic ya sheria. Sasa ninyi mkianza kuleta; na sheria iko hapa, haisemi hivyo. Fine kwa group minimum imetolewa na sheria na maximum. Kwa hiyo, mna-range pale. Hii idea ya kuleta sheria ya kichwa cha ng’ombe it is illegal, haipo! Kesho nataka nisikie hii inakuwa supported na sheria gani? Kama hamtasema, nitashika shilingi kwa mara ya kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuache. Nchi hii sasa tusipofikiria kuleta model zinazotuchanganya Pamoja, huu uhifadhi utafeli. Suala la mifugo, mimi nina mwananchi wangu Kijiji cha Warkyushi kuna pori linaitwa na Mkungunero. Pori la Mkungunero by GN liko Kondoa, Dodoma; lakini wanatuambia eti beacon ziko Kiteto, how? Kwanza kisheria ukishakuwa na GN ambayo ina-conflict na GPS points maana yake kisheria ni kwamba you can’t enforce, lakini wewe unakamata ng’ombe kila wakati. Mheshimiwa Hayati Rais Magufuli…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. EDWARD K. OLELEKAITA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Leo sauti yangu siyo nzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kama walivyosema Wabunge wengine, kweli bajeti hii ni ya wananchi. Kwa hiyo, pongezi za kwanza ziende kwa Mheshimiwa Rais wetu Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan na za pili ziende kwa Waziri wa Fedha, mzee wa wananchi. Unajua timu ya wananchi lazima pia upende wananchi, si ndiyo bwana! Hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza pia rafiki yangu Naibu Waziri. Hii timu imejipanga vizuri sana. Zaidi nampongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge na Makamu Mwenyekiti na timu yote ya bajeti. Hii bajeti tunayoisifia bila shaka imepita kwenye mikono mingi sana kuanzia kwa Kamati ya Bunge, wataalam na timu nzima ya Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu, mimi naichukulia Wizara ya Fedha kama ndiyo financiers, ni kama benki hivi. Kwa hiyo, lazima m-scrutinize miradi yote inayoletwa, halafu mwangalie ile ambayo ina tija. Wakati mwingine nikiangalia watafiti, ningefurahi sana kama Wizara hii ingekuwa na thinktanks wa nchi hii wote wawekwe kwenye Wizara ya Fedha. Kwa sababu kila kitu at the end kinakuja kwenu; ili kuangalia baadhi ya miradi mingine na kujua kwamba baada ya miaka mitano ijayo tutaweza kutekeleza ilani ambayo tumeinadi kwa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ya pili, pesa hizi za Watendaji Kata, Maafisa Tarafa, zimefurahisha sana wananchi kule majimboni, big up! Hata hivyo wakati niko kwenye shughuli za mwenge, akaninong’oneza Mtendaji wa Kata, akaniambia, waambie watukumbuke na pikipiki pia na sisi kama walivyofanya kwa Maafisa Tarafa. Hii itasaidia sana. Ni ujumbe tunawapa. Vile vile kupunguza faini kwa boda boda imewafurahisha sana wananchi, big up! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja nyingine nataka niweke sawa hapa. Kuna Waheshimiwa Wabunge wamekuwa kila wakisimama hapa, wanasema walipa kodi ni milioni mbili na nusu mpaka milioni tatu kati ya milioni 60, is not true. Shilingi milioni 60 unajua ni pamoja na Watoto! Sasa is a bit unfair kusema walipa kodi ni milioni mbili au milioni tatu eti kwa milioni 60 ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, data zetu zinasema, watu asilimia 68 ya population ya nchi hii hawalipi kodi kwa sababu ni below age na wengine ni wastaafu. Kwa hiyo, wakati mnasema wanaolipa kodi, I think is good to be fair; tunaongelea watu kama milioni 20 hivi, lakini ni kweli kama ni watu milioni mbili au milioni tatu wanalipa, tujitahidi.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Olelekaita taarifa.

Mheshimiwa Esther matiko.

T A A R I F A

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpa taarifa mzungumzaji kwamba ni juzi tu tulipewa semina na wataalam na hata akipitia zile power point walisema wanaolipa kodi ni chini ya 5% of the population. Sasa population ina-include na watoto wadogo hata waliozaliwa leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpa tu hiyo taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Olelekaita.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa taarifa nyingine za kuambiwa na wewe unaangalia. Si ndiyo bwana! Kwa sababu na sisi ni wataalam, watoto hawawezi kulipa kodi, wale waliostaafu hawawezi kulipa kodi. Sasa mimi nasema, kwa wale Waheshimiwa Wabunge wanaosema asilimia ya watu wanaolipa kodi ni milioni mbili kati ya milioni 60, this is what I want to correct. Mimi sizungumzii ile 5% waliyosema hawalipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu tena, hili Bunge tumeshazungumza hapa, tukasema hili Bunge baada ya miaka mitano, tunataka tujulikane kwamba ni Bunge la wakulima, wafugaji na wavuvi, kwa sababu asilimia 65 ya Watanzania wako huko. Mimi ninachoomba, kwa bajeti zijazo tujipange. Asilimia 10 ya mapato yetu tuwekeze kwenye kilimo. Natarajia huko mbele, tufanye hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine Ilani ya Chama cha Mapinduzi tunafurahi sana mmeongeza hela kwenye TARURA, big up! Nasi wengine tumeshafanya hata mikutano na tumeshakubaliana hiyo hela inaenda wapi? Kwa kweli tutasimamia ili hizi pesa zisipotee. Vile vile Ilani ya Chama cha Mapinduzi huko mbele huko tulishakubaliana, tukasema ukurasa wa 71 wa Ilani hii na naomba ninukuu: “kufanya mrejeo wa mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Barabara kati ya TANROAD na TARURA.” Ili tupate pesa nyingi kwa TARURA ni lazima tu-revisit hii formula ambayo tulikubaliana isiwe 30 kwa 70 tena, hapana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukubaliane kwa bajeti nyingine zijazo huko; na kwa kuwa ni commitment iko kwa kwenye ilani, tusema ni asilimia kama ni 50 kwa 50 ama 60 hata iende TARURA na TANROADS kwa sababu tulishakubaliana hivyo. Hii itaongeza chanzo kikubwa kwa barabara zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wamezungumza kuhusu tozo za utalii. Mheshimiwa Waziri, wenzetu jirani hapa baada ya Covid wao wametengeneza kitu kinaitwa Covid- 19 and Tourism in Kenya; Impact, Measures Taken, Recovery and Pathways. Yaani wanaangalia baada ya janga hili, tukakwama, kwa sababu ni kweli hii Covid-19 imepeleka hii sekta ya tourism down to its knees.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, walitakiwa – na ninyi sasa muangalie from that eye – na hiyo document nitakuletea, wataalam wetu waangalie ili na ninyi muweze kutengeneza a stimulus package, recovery package, ili huko mbeleni tuweze kunufaika. Kwa sababu ni kweli imepelekwa chini zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri mwingine; tumezungumza hapa sana kuhusu mambo ya umwagiliaji. Na tunajua ni kweli ardhi tunayo, mvua tunapata; tusipowekeza kwenye umwagiliaji hatutaweza kumkwamua mkulima. Tuwekeze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu bajeti hizi, nilikuwa naangalia Wizara ya Mifugo kwa mujibu wa ilani wanatakiwa wajenge mabwawa karibu 95, lakini kwa sababu ya uchache wa bajeti yao, wamepewa mabwawa matano tu. Sasa kwa miaka mitano tukiendelea na trend hii, baada ya miaka mitano tutakuwa tumetengeneza mabwawa 20, na tuli-commit kama 400 hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wakati mwingine tunapotengeneza plans hizi tujaribu kuangalia. In fact, nilishasema wakati mwingine, na ninarudia, labda Wizara ya Fedha iangalie ilani hii projects zote zilizoko kwenye ilani, tufanye tathmini tujue in terms of figures, how much projects zote ambazo tumesema tutafanya baada ya miaka mitano tuzungumze in terms of money ili kila mwaka tujue kabisa tukipata bajeti hii ikaenda kwenye barabara tutaweza baada ya miaka mitano kufanya vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano nilikuwa naangalia hapa kilometa za barabara kwa miaka mitano ni karibu 8,000. Sasa tusipotengeneza bajeti ya kujibu hizi 8,000 kila baada ya mwaka mmoja, tutajikuta baada ya miaka mitano tutashindwa kufanya barabara zote ambazo tumekubaliana. Lakini tuki-cost ilani yetu vizuri itatuongoza, itatoa mwongozo mzuri sana huko mbele tunakokwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii ni kweli ni ya wananchi. Na hotuba ya mama Samia Suluhu Hassan mimi nawashauri sana Mawaziri muisome vizuri sana ile. Kuna miradi kabisa anataja anasema huu ndio moyo wangu – iko kwenye hotuba yake. Ni vizuri tujielekeze huko ili kiu ya mama yetu kwa Watanzania ikapate kupata suluhu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja nyingine fupi sana nataka nizungumze. Imejitokeza huko mbele kuna mkanganyiko fulani; Wizara ya Ardhi wanawapa kijiji hati, TAMISEMI wanatambua, lakini anakuja bingwa mwingine kule kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii anaanza kuwavuruga wananchi wale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, concept ya Serikali moja anayozungumza mama yetu; msipeleke confusion kule kwa wananchi. Ninyi mkutane humu, mnyongane wenyewe kule maofisini halafu muelewane kabla hamjaenda kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya nakushukuru sana na ninaunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo Zilizowasilishwa katika Mkutano wa Pili wa Bunge
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii na mimi niweze kuchangia kwenye hotuba hii ya Kamati ya Sheria Ndogo na kwanza kabisa niwapongeze Wajumbe wote wa Kamati ya Sheria Ndogo, wakiongozwa na Dkt. Wakili Msomi Mheshimiwa Rweikiza; Makamu Mwenyekiti rafiki yangu Wakili Msomi Ridhiwani Kikwete, Wakili Msomi Ramadhani, Wakili Msomi Edwin na Wajumbe wote wa Kamati hii, kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana na wamefanya kazi kubwa ambayo kama walivyosema kwenye taarifa yao, kazi ya kutunga sheria ni ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, lakini kwa mujibu wa Ibara ya 97(5) ya Katiba imelipa Bunge mamlaka ya kukasimu madaraka haya kwa mamlaka zingine ndogo zinazotunga sheria.

Mheshimiwa Spika, lakini ni vyema tukafahamu kwamba ikitokea dosari kwenye sheria ndogo, anayepata lawama ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo kazi inayofanywa na hii Kamati ya Sheria Ndogo ni kazi kubwa sana wanafanya kwa niaba yetu wote kwa hiyo niwapoongeze sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na nilikuwa nasoma taarifa yao wanasema mpaka Februari, 2021 sheria ndogo zilizofanyiwa kazi na kuletwa ripoti hapa ni karibu sheria ndogo 915. Ni kazi kubwa sana na wamechambua vizuri sana wakaonyesha dosari mbalimbali zilizoko kwenye sheria nyingi ndogo zinazotungwa na mamlaka hizi za chini. Kwa mfano kwenye ukurasa wa 14 wanasema kuna sheria zaidi ya 15 ilikuwa na shida ya uandishi na ni kweli uandishi wa sheria sio kazi ndogo sana legal drafting ni soma kabisa linafundishwa na watu wengine wanachukua degree zao, kwa hiyo, sio kazi ndogo sana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ndio maana Bunge liendelee kufanya hiyo oversight, kuangalia sheria ndogo hizi, ili zisiwe na dosari ya aina yoyote. Lakini ukisoma pia taarifa yao wanasema kuna sheria zaidi ya 10 utekelezaji wake ni mgumu sana kwa jinsi ilivyotungwa na wakati mwingine zinaleta kero nyingi sana kwa wananchi, lakini nyingine hata kuna sheria ndogo baada ya wao kufanya uchambuzi, yanapingana na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo sio zile sheria mama tu, lakini hata zinakwenda mpaka zinakinzana na sheria mama, which is very....

Mheshimiwa Spika, nashukuru na Kamati nimesikia kuna sheria ndogo ya Halmashauri ya Kiteto hapa ambaye inatoza watu shilingi 20,000 kwa kweli ni sheria imepitishwa Disemba hapa kwa mujibu wa GN hiyo, hata mimi Mbunge wa Kiteto bado sihifahamu hii sheria vizuri, lakini nitaangalia hii kwa ukaribu zaidi kwa sababu sasa sijui…

SPIKA: Yaani Mheshimiwa hiyo sheria ni kwamba sasa mmegeuza majando yale kuwa ni chanzo cha mapato ya Halmashauri; yaani ndio mantiki yake. Kwa hiyo sasa matokeo yake watu wanakuja kuweka majando Kongwa. (Kicheko)

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika ahsante sana na jirani yangu unajua mimi na wewe vitu vingi tunashirikiana pamoja na wananchi wetu wa pande zote mbili wanafanya shughuli hizi, lakini lazima tuangalie ili isilete kero kwa wananchi kwa sababu inawezekana wale wanafanya shughuli hiyo labda wanatoza hela nyingi zaidi mpaka Halmashauri labda imefikiria labda ni chanzo cha mapato, lakini ni kweli nakubaliana na kamati tutaangalia vizuri sana ili isilete kero kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, lakini zipo sheria nyingi sana hapa mimi wakati nachangia kwenye bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ile kero ile ya kutoza ng’ombe shilingi 100,000 kwa kichwa, nilisema hapa inakinzana na Sheria ya Wanyamapori na nilishamwambia Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwanza hawafahamu kuna ng’ombe unaweza kununua kwa shilingi 100,000. Sasa kama faini inaweza kutozwa kwa shilingi 100,000 sasa si afadhali nikuachie huyo ng’ombe mimi nikanunue mwingine huko sokoni.

Mheshimiwa Spika, lakini kwa kuwa inakinzana na sheria mama tusikubali kabisa madaraka ya Bunge hili na mamlaka hizi za chini zituletee kero za namna hiyo na kutufanya watu waichukie Serikali kumbe mtu mmoja tu ndio ametunga sheria hizo, lakini sheria nyingine ya shoroba au marafiki zangu wa wanyamapori ilitungwa sheria na Bunge wakaambiwa wakatunge regulation kwa ajili ya shoroba hizi.

Mheshimiwa Spika, lakini Bunge likasema muoneshe haki za wananchi kwenye sheria hiyo yaani ndio obligation ya kwanza wao wakaweka masharti kwamba hawaruhusiwi kufanya moja, mbili, tatu wakati interest ya Bunge ilikuwa ni kuona haki gani wananchi wanazo kwenye sheria hizi.

Mheshimiwa Spika, mijadala ya sheria ndogo hizi na naendelea kupongeza Kamati hii na muendelee kutufanyia hii kazi wananchi wengi wanaumia kwa sababu ya sheria hizi ndogo ndogo ambazo zinatungwa na mamlaka za chini bila kuangalia sheria mama ama Katiba ama na sheria nyingine za nchi.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa naangalia hotuba hii na kama ulivyosema Sheria ya Tafsiri (The Interpretation Act) kifungu cha 36 kama alivyosema hapa inasema; “Subsidiary legislation shall not be inconsistent with the provisions of the written law under which it is made, or of any Act, and subsidiary legislation shall be void to the extent of any such inconsistency,” inapatikana kwenye sheria hiyo. Kwa hiyo, ni clear kwamba sheria ndogo hairuhusiwi hata kisheria tu infact haitakiwa iwe operational kama itakuwa inconsistency na sheria mama.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na huo ndio mchango wangu kwa leo, ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza nimpongeze Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria kwa hotuba yake nzuri sana, ametuwakilisha vizuri Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ni siku ya Katiba na Sheria ndogo; ni Sheria tu leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya vitu ambavyo nachangia leo, naanza na suala la ajira na kazi kwa sababu liko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, lakini ni jambo ambalo limekuwa na Changamoto nyingi sana. Vijana wetu wengi wako hapa wanahangaika wakitafuta ajira. Kila Mbunge hapa kila wakati analetewa majina, CV za vijana wengi wakitafuta kazi. Wakati interview zinafanyika, aidha nafasi ni 30 wanaletwa watu hapa 4000, 5000; si, sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi tumeona wameanza kubadilisha kidogo, sasa wameanza kugawa kwa zone, ili kuwaondolea vijana usumbufu kuhangaika k wenda sehemu moja wako 3000, 4000 halafu nafasi ni 50 tu. Kwa hiyo, ndilo jambo moja tu ambalo nilitaka nishauri Serikali mbadilishe na mje model ambayo itawasaidia kuwaondolea usumbufu vijana hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila Mbunge hapa, ukisikia ajira zimetoka 10,000 hesabu za haraka haraka ni kwamba unachukua idadi ya majimbo unagawa ili walau kila Mbunge kwake kule aone vijana wake kadhaa wamepata ajira. Hilo ndilo tegemeo la kila Mbunge hapa na tunataka hivyo. Hatutaki tusikie ajira ziko 10,000 lakini ajira zinavyoenda unashangaa humuoni mtoto wa Kiteto ama kutoka jimbo lolote la Mbunge hapa; mnatugombanisha na wananchi. Kwa hiyo, tengenezeni model nzuri sana itakayotusaidia. Kama mnavyogawa poesa za miradi, kwa mfano kama ilivyokuwa UVIKO; mbona imewezekana na miradi imekwenda kila mahala. Tunataka kwenye ajira pia Mlete Model ambayo itatusaidia wote tuone kwamba tumejumuishwa na suala la ajira na Kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala jingine muanzishe, anzisheni mijadala; mnajua hatusemi hili ni la kwenu peke yenu, tuanzishe nijadala ya mara kwa mara ya namna ya kuboresha suala la ajira nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ni ofisi au idara inayoitwa ya Mpigachapa wa Serikali (Government printer); sijui wabunge wangapi wanafahamu hii Government printer; hata sisi Kamati yetu kwa mara ya kwanza tumefahamu jana zaidi baada ya kuja kutuonesha na tukaona; lakini kazi kubwa inayofanywa na idara hii ni kubwa zaidi. Inasimamia Nembo na Bendera ya Taifa inasimamia kuchapisha nyaraka za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Mahakama na Bunge. Hata bendera tulizonazo; na mwaka jana hapa tulirumbanarumbana kidogo kujua ipi bendera sahihi ya Bunge; na siku hizi vipeperushi vingi sana vipo mtaani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ofisi hii haijawezeshwa ipasavyo Serikali imekuja na mkakati mzuri sana wa kuboresha ofisi hii ama idara ya Mpiga Chapa wa Serikali; ni Ofisi muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana kwa mfano walikuwa wanatuambia kwamba, kama wangeweza kupata pesa wangeweza kuchapisha nakala milioni sita ambayo ingeweza kupatia Serikali bilioni 20. Lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti sasa hivi wanapata nakala laki sita peke yake. Kwa hiyo ni muhimu wabunge wafahamu kwamba ofisi hii muhimu sana ya Serikali inayohifadhi nyaraka na alama za Taifa letu ni muhimu iwezeshwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) vilevile haipati pesa za kutosha ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. Mimi nilipata nafasi ya kumtembelea DPP siku moja, nilishangaa sana, ofisi yake ni ya ajabu sana. Najua sasa hivi wanajenga ofisi yao; lakini ni vyema Serikali ikatenga pesa ili watu hawa wanaofanya kazi kubwa wapate kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni Law School of Tanzania. Law school of Tanzania; na mimi ni mwanafunzi wa Law School of Tanzania, first cohort. Ukisikia mambo yanayoendelea huko wakati mwingine unasoma vijana wale wanenda kufungua kesi; mahakamani ni dhahiri kwamba kuna jambo la kufanywa na Serikali. Kwa mfano ripoti ya Dkt. Mwakyembe muilete bungeni tuangalie, tu-interrogate ili na sisi tuweze kushauri namna bora; na Mheshimiwa wakili msomi, Mavunde tulikuwa cohort moja first cohort; lazima, hata wewe unajua unamawazo mazuri ya namna ya kuboresha hiyo zaidi ili vijana wetu wasisumbuliwe lakini tuwatengeneze Wanasheria wazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na Kamati imesema hapa labda kuna haja ya kuanzisha ile entry exam. Lakini sheria ile iliyounda law school ni kama ilimlazimisha kila mtu kwenda Law School of Tanzania, ambayo si sawa. Waende wale ambao wanataka kuwa mawakili. Kwa hiyo kama kuna haja ya kufanya hivyo basi ni vizuri tuangalie mifumo ile. Na pengine baadhi ya courses, kwa mfano Mheshimiwa Mavunde wakati tunasoma accounting for lawyers; sawa ni important lakini kwa nini, but why do you examine me on accounting for lawyers inanisaidia nini? Halafu baadaye inanishushia tu grade zangu hainisaidii chochote. Kuna course nyingine ni muhimu lakini ukini-examine accounting for lawyers kweli? Na mengine mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu lugha ya uandishi wa sheria; Bunge hili lilipitisha sheria hapa ya kusema tutumie Kiswahili, jambo ambalo ni jema sana; Watanzania wengi lazima wafuatilie, waweze kusoma sheria tunazotunga na waweze kuelewa kwa lugha hiyo. Hta hivyo kwa sababu Tanzania si kisiwa peke yake, ni vyema kama walivyoshauri Kamati, tupate sheria hizi zote kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili, Kwa sababu si kwamba sheria zetu tunazotunga zina Mahakamani peke yake bali pia zinatumika kufundisha wanafunzi; na wanafunzi wanatoka kila mahali duniani kuja kwenye Mahakama zetu na kwenye vyuo vyetu. Kwa hiyo ni muhimu sana ili tuondokane na mambo kama hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho nitazungumzia habari za Mahakama. Hii program mliyoanzisha Mahakama ya-integrated justice, ile Mahakama Jumuisho, ni program nzuri sana. Siku hizi mahakama zetu unatembelea mahakama utafikiri ni hoteli kabisa. Hata ukitembelea judiciary square hapa naambiwa ni jingo sijui la sita ama la kumi Southern of Sahara, ni nzuri sana, program ile ni nzuri sana. Lakini sasa tunataka haki zitoke kwenye majengo yale. Sisi hatutaki kwa sababu ni jengo refu tu, no, challenge sasa ni kwamba we want justice kutoka kwenye Mahakama hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imezungumzwa hapa na sheria ndogo; wakati mwingine Bunge linashauri kuhusu jinsi tunavyotafsiri sheria zetu. Hakuna kitu kibaya sana kama Serikali msipofahamu bunge lilimaanisha nini kwenye sheria hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, liko suala la mifugo, ina-touch hii Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na vifungu vinavyotumika kila wakati ni Kifungu cha 116 cha Sheria ya Wanyamapori kwenye ku-compound offenses. Kama juna eneo ambalo tunafanya hovyo kuliko yote ni kwenye compounding of offenses. Sheria, na Bunge lilisema hivi, Section 116, na ninaomba kunukuu; “This section shall apply to offenses committed under the Act in relation to protected areas, the director may compound an offense by requiring a person to pay a sum of money provided that such money shall not be less than two hundred thousand shillings and not exceeding ten million shillings”

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo ndivyo Bunge lilivyosema; a person. Lakini wanakaa waswahili fulani tu kule wanaanza kuhesabu vichwa vya mifugo halafu wanasema lipa laki moja moja; that is not the intention of the law. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili likinyamazia vitu kama hivi; na si Bunge kabisa, ni mtu mmoja bingwa tu, alivyosema Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo hapa. Haya makosa yaliyogundulika takriban kanuni 31 zenye kasoro za kiuandishi zinakwenda kinyume na Katiba. Haya ni makosa tu yamegundulika kwa kusoma zile sheria, lakini wangekwenda field leo wakajua ni watu wangapi wameumia kwa sababu ya sheria hizo ni mbaya zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Sheria ya TANAPA Section 20A bado inazungumzia kwamba fine kama unataka ku-compound should not exceed one hundred thousand, should not exceed; lakini a person pays. Sasa, wakati Bunge linatunga sheria definition of livestock maana yake ni mbuzi kondoo nguruwe farasi kuku ndama hata mayai. Sasa laki moja leo ng’ombe ni wa laki moja na nusu ama laki moja halafu unataka kutoza fine ya shilingi laki moja utafanya Bunge hili lisiaminike hata kidogo. Lakini kumbe wala sio sisi, ni wale wanaosimamia sheria. Kwa hiyo Waheshimiwa Mawaziri muwe wakali sana. Bunge hili likisema na likishauri kanuni hii haifai ama hii compounded haifai ni vyema mkasimamia kwa nguvu zote ili Bunge liendelee kuheshimika…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa ahsante sana kengere ilishalia muda mrefu.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na ninaunga mko hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema ambayo ametujalia na ninampongeze Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya kwa nchi yetu. Kipekee kabisa kwa niaba ya wananchi wa Kiteto, Wizara ya Mifugo imetuletea majosho karibu Nane, bwawa kubwa la karibu Milioni 500. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais na tunaendelea kumuombea Mwenyezi Mungu aendelee kumpa afya njema aongoze Taifa letu vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili nampongeza Mheshimiwa Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Isdory Mpango kwa kuendelea kumsaidia Mheshimiwa Rais, nampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa kwa kuendelea kumsaidia Rais kutekeleza majukumu yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninampongeza Waziri wa Mifugo, rafiki yangu Mheshimiwa Ulega, kwanza ninampongeza kwa kuaminiwa na Mheshimiwa Rais kuongoza Wizara hii ya Mifugo na ninakupongeza kwa ziara mbili ulizofanya Kiteto. Umekwenda mpaka huko kabisa machungani, ulitutembelea wakati wa majanga ya ukame na uliona mifugo na ukatutembelea tena wakati tunatembelea Bwawa la Kawa, nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri. Pia ninampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri, Mheshimiwa Silinde, nampongeza Katibu Mkuu na timu nzima ya Wizara ya Mifugo kwa kuendelea kumshauri Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine niipongeze Timu ya Wananchi ya Yanga kwa kazi kubwa waliyoifanya na kuijengea heshima nchi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo sasa naomba nijadili changamoto zinazotokana na Wizara hii ya Mifugo. Moja ni mabwawa na majosho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Ilani ya Chama cha Mapinduzi ukurasa wa 50, 51 na 53 tuliahidi Watanzania kwamba tutajenga mabwawa karibu 454 maana yake mwaka ni mabwawa 92. Ninaomba sana Serikali iiongezee Wizara hii pesa nyingi sana ili tuweze kutimiza ahadi hizi kwa Watanzania. Nachelea kusema kwamba Wizara hii inapata pesa kidogo sana, ninamuomba sana Mheshimiwa Rais na Serikali waongeze bajeti kwenye Wizara hii, angalau hata Bilioni 500 itasaidia ili Wizara hii iweze kutimiza yale yote ambayo tuliyasema.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano majosho, tulisema kila kijiji chenye mifugo kiwe na josho. Kwa Wilaya ya Kiteto peke yake idadi ya mabwawa tuna upungufu wa mabwawa karibu 44, majosho 48. Pamoja na nguvu alizotusaidia Mheshimiwa Waziri hii inaonesha kwamba bado upungufu ni kubwa, mabwawa kama ya Dosidosi, Sunya, Njoro, Kinyungu, Matui, Sunya yote ni mabovu na kwa kweli Mheshimiwa Naibu Waziri tunaomba pesa kwa ajili ya mabwawa haya.

Mabwawa kama ya Dosi, dosi, ya Sunya, Njoro, kijungu, Matui. Sunya, yote ni mabovu na kwa kweli, Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaomba pesa kwa ajili ya mabwawa haya na Bwawa la Kaiwang Mheshimiwa Waziri endelea kufuatilia ili Watanzania wale wapate kunufaika na nguvu za Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, ni maeneo ya malisho. Salama ya wafugaji nchi hii ni kuwa na maeneo salama ambayo yamelindwa kisheria. Kwa hiyo, naipongeza Wizara kwa kuendelea kufanya hivyo, lakini tuendeleze kasi. Hii itaondoa migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wa ardhi wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, ni suala la umasikini kwa wafugaji. Mheshimiwa Waziri alikuja Kiteto. Ukame ule kwa Kiteto peke yake tulipoteza ng’ombe karibu 25,000 na sasa tafiti zinasema; kwa sababu kuna dhana fulani watu wanafikiri wafugaji ni matajiri tu, lakini tafiti zinasema, asilimia 20 ya watu wanaomiliki mifugo; asilimia 20 wanamiliki asilimia 80 ya mifugo iliyopo. Kwa hiyo, hii ni picha tu inayoonesha kwamba gap lililopo, na siyo kwa sekta ya mifugo peke yake, hata kilimo. Kwa hiyo, vizuri Mheshimiwa Waziri hebu mlifanyie utafiti ili dhana zinazojengeka kwamba wafugaji ni matajiri ifahamike kwamba siyo kweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, ufugaji wa kisasa unaozungumzwa kila wakati, kila Mtanzania angependa kufanya kitu chenye tija zaidi, lakini lazima tufahamu kwamba sekta ya mifugo tuna makundi matatu; kuna watu wanaofuga kiasili na kibiashara na ni sehemu ya maisha yao, ambao ndio Watanzania walio wengi, lakini kuna watu wanataka kujifunza biashara ya kufuga ng’ombe na kunenepesaha, na hapa wakiwemo Serikali. Serikali wanafanya biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapotengeneza mikakati lazima tufahamu kwamba haya makundi matatu yapo. Kufanya biashara ya kunenepesha siyo kitu kidogo. In fact nimewatembelea wafugaji wawili ambao wanajaribu kufanya ufugaji huu unaoitwa ni wa kisasa. Mmoja mwenye hekta 100 amepiga fence, na miundombinu ame-develop, na kuweka ng’ombe hawa mnaowaita wa kisasa, ni karibu Shilingi milioni 400 mpaka 500, investment.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikamtembelea mfugaji mwingine mdogo sana, ana hekta 20, anajaribu kutengeneza shamba. Hata hiyo, tunayosema ni kidogo ni Shilingi milioni 50.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, at times tukisema kwamba tufuge kisasa, mjue mkituletea hizo pesa, tuko tayari. Otherwise mfahamu kwamba mifugo ni sehemu ya maisha ya wananchi. Wakati mwingine tukisema tufuge kisasa bila kutuwezesha na tukapata nyenzo zinazohitajika, tunafikiri kama hamtufahamu vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kukamatwa kwa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi, imekuwa ni kero kubwa sana. Namshukuru hapa Mheshimiwa Waziri Mkuu, kauli aliyoitoa Mheshimiwa Waziri Mkuu hapa, hebu fuatilieni vizuri sana kwa sababu kukamatwa kwa mifugo katika maeneo haya, imeanza kuwa kero kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wanakamata tu ng’ombe, watu wanakwenda Mahakamani, wanashinda kesi, lakini hawapewi mifigo yao. Nina mwananchi wangu anaitwa Lenina, mpaka leo ni karibu miaka mitatu hajapata haki zake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni vizuri mwangalie, mzungumze na Waziri wa Maliasili na Utalii, make, mtengeneze. Kama anapenda kukamata ng’ombe zaidi, aambiwe kuna kanuni zilitengenezwa na Wizara ya Mifugo chini ya Sheria inaitwa The Animal Welfare Empowerment Animals Regulations of 2020. Kama anaweza ku-afford kwenda kuwatunza hao ng’ombe kwenye maeneo ya hifadhi, afanye hivyo, lakini kama hawezi, aachie ng’ombe, awakamate wafugaji. Kwa sababu tunawafanya wafugaji wanakuwa masikini unnecessarily. Ni jambo la kukaa na kuzungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mikopo na benki, Mheshimiwa Waziri amezungumza hapa kwamba twende kwenye benki. Kama kuna mradi ambao unafeli ni wa benki. Mfugaji anakwenda anataka mkopo, halafu unamwambia lete security, eti lete nyumba. Sasa kwani huyu mfugaji anafanya real estate? Kwa nini mifugo isiwe security? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mifugo ni mali kama mali nyingine. Kama kuna haja ya kutengeneza insurance ama bima kwa ajili ya mifugo ili tupate security tufanye hivyo, lakini hatupendi sana. Unakwenda una mifugo wazuri tu, eti mtu anakwambia nenda kalete hati ya nyumba au kalete shamba. Huyu hafanyi real estate, wala Halimi. Eeh, mtengeneze module ambayo inamfanya mfugaji aweze kukopesheka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la chanjo. Ilani imezungumza habari ya chanjo hizi za magonjwa 13, lakini wakati mwingine tunahisi kama haiji kwa wakati. Kwa hiyo, lazima Serikali iweke mkakati wa kuleta chanjo hizi kwa wakati ili wafugaji wapate huduma hizi kwa haraka zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho kabisa, nataka Mheshimiwa Waziri atengeneze wafugaji mabilionea. Wengine wametengeneza mipango mingi. Omba tu Mheshimiwa Rais akupe Shilingi bilioni 27,600,000,000/=, utapeleka katika majimbo yote 184. Karibu Shilingi milioni 150 watapewa vijana Hamsini Hamsini, watakuwa ni vijana 9,200 baada ya miaka miwili, utarudishiwa hizo pesa.

Mheshimiwa Naibu Spika, unajua lazima tuwe practical. Hii habari ya kufanya tafiti na kufanya workshop, sijui na kufanya ma-interview ambayo yanapoteza muda, tafuta hizo hela, ukipeleka hiyo milioni 150 kila jimbo, mtuachie kazi ya ku-recruit vijana ambao wanafanya hizi kazi za mifugo. Ukifanya hivyo, baada ya miaka miwili hiyo pesa itarudi, lazima tuwe practical. Hatutaki tena mambo ya kusoma mavitabu haya na matafiti. We have spent time, sixty years down the line, tunasoma tu ma-documents. Tunataka tuwe practical. Kwa hiyo, ifike mahali, nakuombea pesa nyingi zaidi, ukipata nadhani itatusaidia sana kutekeleza hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, kwa ahili ya interest ya muda, naunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsanteni sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema ambayo ametujalia.

Pili, nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kilimo, tumeona pesa nyingi zinaendelea kuongezeka kwenye kilimo. Nimpongeze pia kwa kuendelea kusukuma suala la Katiba Mpya. weekend hii tumeona vikao vinaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba sasa Serikali mlete zile Sheria ili tuweze kuweka miundombinu vizuri kwa ajili ya kujiandaa na zoezi hilo. Sheria ya Tume ya Uchaguzi na Sheria ya Usajili wa Vyama vya Siasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawapongeza Mawaziri hawa, timu nzuri sana hii, wanafanya vizuri sana na kwa sababu ya muda sitaendelea sana hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianzie hapo, kwanza, niwapongeze wakulima wa Tanzania. Wanafanya kazi kubwa sana na ndio maana leo tunakaa hapa tunazungumza habari ya sisi kuwa na utoshelevu wa chakula kwa asilimia zaidi ya 100. Hii ni kazi ya wakulima peke yao. Kwa hiyo, kwa kweli tuwapongeze wakulima.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuishauri Wizara, bei ya mazao. Bei ya mazao na hii ni kwa Tanzania nzima. Mkulima, mfugaji, mvuvi,yule ambae ni mzalishaji kabisa, wa katikati hapa anapata pesa nyingi zaidi kuliko mkulima. Kwa hiyo, ni lazima sekta hii ya kilimo kama kweli mnataka kuwalinda wakulima ni lazima tuwe na bei nzuri kwa wale wanaolima ambao hawalali.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, mbegu na mbolea, ripoti ya Kamati wamezungumza hapa na kwa kweli wameweka vizuri. Tumekuwa tukikutana mwisho wa mwaka ndio simu zinakuwa nyingi sana kuhusu mbolea iko wapi na mbegu iko wapi. Sasa, kwa sababu tunategemea mvua kwa asilimia kubwa sana kwenye kilimo chetu, ni vema Mheshimiwa Waziri mkaweka mipango tupate mbolea na mbegu mapema kabisa, hata kabla ya mwezi wa kumi. Kama tunajua mvua zinaanza mwezi kumi na wa kumi na moja, mna mwaka mzima wa kuanza kuweka mipango ili mbolea na mbegu zifike kwa wakulima kwa wakati tusisubiri mvua. Kwa sababu tukisubiri mvua, miundombinu, barabara zetu, magari mabovu, halafu technicality nyingi zinaongezeka hlafu zitatusumbua sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kimsingi wakulima wanavuna mwezi sita, mwezi wa saba wanapata pesa. Sasa, kwa nini msiwauzie mbolea na mbegu kipindi hicho ili wahifadhi lakini lazima tutoe elimu kwa sababu ni kweli wakulima wakati fulani fulani wanahitaji elimu ya mbolea hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la umwagiliaji, tunakupongeza sana Wizara hii imetengeneza a very ambitious plan ambayo ni nzuri kwamba tunataka twende kwenye umwagiliaji na ninashukuru sana hapa kwenye hotuba yenu ukurasa wa 235 nimeona Kiteto hapa Ngipa. Pia, jana nimepata simu kwamba timu zenu ziko huko sasa zinafanya upembuzi yakinifu, safi sana na hongera sana. Pia wananchi wa kiteto kwa kweli wanawasubirini kwa hamu kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiteto, nilishazungumza hapa mara nyingi, ukichukua ripoti za kilimo Kiteto ni karibu tani 400,000 za mazao mbalimbali na tunalima mazao karibu 28 tofauti tofauti. Kwa hiyo, kwa kweli ni bread basket. Mheshimiwa Waziri, ninachotaka kusema tunahitaji Soko kubwa la mazao Kiteto. Hawa wakulima wanalima sana na kama ni ardhi unataka njoo tutakupa bure.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

NAIBU SPIKA: Taarifa.

TAARIFA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba tu nimpe taarifa Mheshimiwa mzungumzaji, kwa sababu alipoanza kuzungumza ameihimiza Serikali kuhakikisha kwamba mchakato wa Katiba Mpya na Sheria zile zinazohusiana na Demokrasia ya Vyama Vingi ikiwemo Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Uchaguzi na Sheria ya Tume ya Uchaguzi vinakwenda haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa tamko la Mheshimiwa Rais la tarehe 6 mpaka sasa Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, tayari imeshajipanga kuitisha kikao cha wadau kupitia Baraza la Vyama vya Siasa kuhakikisha mchakato wa Katiba Mpya unaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sheria hizi ambazo zimezungumzwa na Mheshimiwa Mbunge naomba kulihakikishia Bunge lako tukufu kwamba tunataka kabla ya mwaka huu 2023, sheria hizi pia zitakuwa zimekwishafanyiwa kazi kusudi kila jambo liweze kwenda kwa wakati.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Edward, Taarifa hiyo.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, napokea na tuko tayari, tunasubiri kwa hamu kubwa sana.

NAIBU SPIKA: Tumpongeze Mheshimiwa Rais kwa hatua hiyo ya kuleta demokrasia nchini. (Makofi)

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, ndio kwa kweli tunampongeza sana Mheshimiwa Rais, pia namna bora ya kumpongeza ni kuleta hizo sheria tupitishe haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nazungumza habari ya masoko ya mazao. Kiteto ni bread basket. Mheshimiwa Waziri, specific kuhusu suala la alizeti, Kiteto tulihamasika sana kuhusu alizeti na tulihamasisha sana wananchi. Kwa sababu tumejifunza mambo mengi sana baada ya janga hili la UVIKO 19, kwamba tunaagiza mafuta kutoka nje. Kwa hivyo, ikitokea janga lingine maana yake tunaweza tukakosa mafuta. Pia, wakulima wa Kiteto waliahamasika sana na projection zetu za alizeti mwaka 2023, ni tani 171,000. Hata hivyo, Mheshimiwa Waziri, utakumbuka mwaka 2022, bei ya alizeti ilikuwa nzuri sana lakini sasa bei inaenda chini sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sasa ili wakulima hao wahamasike ni lazima Serikali ije na mpango wa kulinda bei hii. Kwa sababu ni zao la kimkakati na sisi tumejiwekea mpango tukasema kama tunataka kupunguza adha hii ya kutoa mafuta kutoka nje, ni lazima wakulima wetu wailme hasa. Sasa, lazima tunataka plan, unapokuja kuhitimisha bajeti yako please utwambie. Unawambie nini wakulima wa Kiteto ambao wameweka nguvu sana?

Mheshimiwa Naibu Spika, in fact nilikuwa nasoma statistic zenu kwenye taarifa yako iliyopita ya mwaka 2022 na mlisema tani milioni moja. Sasa kati ya tani milioni moja, kama Kiteto peke yake inatoa tani 171,000 lazima ufahamu kwamba wanachi wa Kiteto wamehamasika sana. Kwa hiyo, kwa kweli tunakusubiri utwambie baadae na wananchi wengi wa Kiteto wanakusikiliza wanataka kujua baadae unapohitimisha bajeti yako, nini suluhu ya bei ya zao la alizeti na mazao mengine?

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, ni suala la wanyamapori wanaoharibu mazao ya wakulima. Hii imekuwa ni adha kubwa sana, wakulima haa wanahangaika wanalima kila kukicha, wanakimbizana na mvua lakini wanyamapori wanaharibu mazao.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningetamani sana Wizara ya kilimo, itufanyie tathimini maalum kuhusu mazao hayo ambayo yanaharibiwa na wanyamapori. Tusipoweka ulinzi, wakulima hawa ambao wanahangaika usiku na mchana kulima halafu mazao yao yanaharibiwa na wanyamapori, lazima kama nchi tuwe na mkakati maalum ili kunusuru wakulima hawa ambao hawalali usiku na mchana wakilinda mazao yao. Tunataka kuona exactly cost ambayo inaletwa na wanyamapori kwa wakulima hawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu mitaji ya wakulima, tunajua wakulima wetu wengi sana wanahangaika na mitaji, wanakwenda wakati mwingine kwenye mabenki wanaomba kupata mitaji kwa ajili ya maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri, bajeti yako ya mwaka 2022 ukurasa wa 135 ulisema hivi, naomba ninukuu; “Wizara imeunda kamati maalumu inayohusisha viongozi mbalimbali katika Wizara ya Kilimo, taasisi na Mfuko wa Fedha na Maendeleo kwa ajili ya kupitia ushauri wa namna bora ya upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya Miradi ya maendeleo ya kilimo.”

Mheshimiwa Naibu Spika, tutapenda sana utuambie baadae hili mmefikia wapi? Wakulima wanahitaji hii mitaji kwa nguvu zote.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tulizungumza na ilani yetu iko wazi kwamba tunataka kupunguza jembe la Mkono kutoka asilimia 53 mpka asilimia 10 mwaka 2025. kwa mfano; Mradi wa matrekta umefikia wapi? Wakulima wangu wa Kiteto, tuliomba Serikali iweze kuweka pesa nyingi ili wakulima waweze kupata matekta mazuri ya bei nafuu na ya muda mrefu ili wakulima hawa kuendelea kulima.

NAIBU SPIKA: Ahsante.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo naomba kuunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi, na nimpongeze Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria na Wajumbe wote wa Kamati kwa kazi kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa sababu ya muda, niwapongeze Mawaziri wote ambao wanakuja kwenye Kamati yetu, wote, kuanzia Ofisi ya Waziri Mkuu, Chief Whip, Attorney General, Waziri wa Sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu mambo ya Ajira, Muungano – wote kwa ujumla wenu, kwa kazi kubwa ambazo kwa kweli mmefanya kwa utekelezaji wa kazi katika Wizara zenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Katiba na Sheria kwa muda wa mwaka mmoja imeweza kufanikiwa kurekebisha sheria karibu 58, siyo kazi ndogo sana; utungwaji wa sheria siyo kazi ndogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwenye sheria hizo, kati ya sheria maarufu sana ambazo tumebadilisha ni kuruhusu Kiswahili kitumike kwenye mahakama zetu na kutafsiri sheria zetu ziende kwa Kiswahili. Kwa kweli kati ya sheria ambazo nazikumbuka na mabadiliko mazuri sana kwa Watanzania ni kuruhusu Kiswahili kianze kutumika ili watu waanze kufuatilia mashtaka kwenye kesi za mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kinachonifurahisha zaidi ni kwamba Ilani ya Chama Cha Mapinduzi baada ya sisi kusema kwamba tubadilishe sasa sheria ziende kwa Kiswahili, Wizara ya Katiba na Sheria walitakiwa kwa mujibu wa ilani yetu wawe wametafsiri sheria 157. Lakini kwa kasi yao wamerekebisha na kutafsiri sheria 208; hongereni sana. kasi hii ikiendelea mtakipa Chama Cha Mapinduzi heshima kubwa sana kule. Kama ilivyo kwenye ilani, ukurasa wa 167. Na ninaomba ninukuu: -

“Kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu sheria mbalimbali kwa kutafsiri sheria 157 kutoka Lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili”

Mheshimiwa Mwenyekiti, big up. Ninyi mmevuka lengo. Najua mna kazi kubwa sana, kwa sababu hata mnatakiwa kutafsiri subsidiary legislation na zile nyingine karibu 39,000; mtakuwa na kazi kubwa sana. kwa hiyo, naamini Wabunge watawaelewa wakati wa bajeti, mkileta bajeti hapa mpewe pesa nyingi muendelee kuchapa kazi kubwa zaidi. Kwa hiyo kwa miaka mitano ninyi mmeshaturahisishia kazi. Sheria zile principal zipo karibu 449, ninyi meshavuka kabisa; hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Wizara ya Katiba na Sheria ilitakiwa, kwa mujibu wa Ilani yetu, kuboresha majengo ya mahakama. Wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria tulipata nafasi ya kutembelea mikoa mbalimbali kuona miradi ya mahakama; tumeanzia Kongwa, tumekwenda Morogoro, tumekwenda Njombe, tumekwenda Dar es Salaam, tumekwenda Arusha na leo tumekwenda Dodoma kuona jengo kubwa la mahakama, Judiciary Square ambayo inasadikiwa litakuwa jengo bora kuliko Central and Southern Africa, na Waheshimiwa Wabunge tunawakaribisha. Wizara ya Sheria wanatuambia mwaka huu Desemba, watafungua hili jengo. Jengo zuri halijawahi kutokea; hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mabadiliko mengine ambayo ni muhimu sana ni mabadiliko ya kuwaruhusu mawakili kwenda kwenda kwenye mahakama za mwanzo. Hii siyo tu inafungua fursa ya ajira lakini inawafanya wananchi wapate huduma za uwakilishi kwenye vijiji vyao; excellent.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kati ya sheria zilizobadilika ni kuweka break ile nolle prosequi na amicus curiae kwenye mambo ya sheria, itaongeza, na itapunguza mashtaka yale ambayo yanawasumbua wananchi sana. na vilevile kusema upelelezi ukamilike ndiyo tuendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa kusema hivi…

MWENYEKITI: Malizia sentensi ya mwisho Mheshimiwa Olekaita.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, sentensi moja. Na kwa kuwa Wizara ya Katiba na Sheria mna kazi maalum ya kufanya, naomba niseme Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 29, alipokuwa akihutubia UN, na mimi nasema he for she; alisema yafuatayo: -

“Aware that being passionate about gender equality is not sufficient, my government is reviewing policy, legal framework in order to come up with actionable, measurable plans to ensure economic empowerment for women but also aspects pertaining to gender equality and gender parity.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, mlete sheria hizi tuzibadilishe. Nakushukuru sana, naunga mkono hoja asilimia 100; ahsante sana. (Makofi)
Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Kuongeza Mamlaka ya Mahakama ya Afrika Mashariki
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi ili niweze kuchangia Itifaki hii ya kuongezea Mahakama ya Afrika ya Mashariki nguvu ya kisheria ya kuanza kusikiliza kesi za biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Waziri wa Katiba na Sheria na Mheshimiwa Naibu Waziri na timu yao yote kwa kazi ambayo wamefanya. Kazi ambayo Bunge imepewa ifanye sasa ni kwa mujibu wa Katiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema hivi na naomba ninukuu:

“Kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake ni lazima inahitaji kuridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, tunafanya kazi ya kikatiba kabisa ya Bunge na niwapongeze Mawakili Wasomi wale ambao wameanza mjadala, Mheshimiwa Mwinyi ambaye kwa kweli hili ndiyo eneo lake la kujidai Afrika Mashariki na Mheshimiwa Zainab Katimba, Mheshimiwa Jerry Silaa na Wakili maarufu sana hapa Bungeni Mheshimiwa Thadayo. Kwa kweli sasa napata wakati mgumu kusema baada ya hao wote kusema. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Afrika Mashariki sisi kama Taifa, kwanza ni faida kubwa kwetu kwa sababu Makao Makuu ya Mahakama hii ya Afrika Mashariki ipo Arusha Tanzania. Kwa hiyo, tayari kwa wenzetu wale Mahakama hii kuwepo kwetu ni faida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama walivyosema wengine hizi Itifaki za Common Markets, Monitoring Union na Customs Union tayari zimeshapitishwa lakini kwa integration ambayo inaenda vizuri sana, mkishaanza kuingia kwenye Itifaki hizi za Common Markets, Customs Union na Monitoring Union ni lazima mtarajie kwamba disputes zitatokea na kwa mujibu Treaty hii ukisoma article 5 and 6 imeeleza kabisa misingi ya Treaty hii kwamba ni lazima tumekubaliana tusuluhishe migogoro yetu kwa namna ya kisheria nzuri na hakuna namna bora zaidi, zaidi ya kwenda Mahakamani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ili Wanachama wa Afrika Mashariki waweze kufurahia protocols hizi za Monitory, Customs Union na Common Market lazima kuwe na Mahakama ambayo likitokea jambo, yeyote kati ya wale anaweza kwenda Mahakamani na akapata haki yake. Kwa hiyo, ni muhimu kabisa na hata nje ya dunia wakitaka kuangalia kama integration yetu ni nzuri sana, wataangalia kama kuna mechanism kwamba jambo likitokea unaweza kwenda Mahakamani na ukapata redress. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii jurisdiction kwa kweli wamefanya kazi nzuri sana. Labda nimtoe wasiwasi dada yangu aliyekuwa anazungumza hapa, nilikuwa naangalia hii protocol yenyewe article 3 kwamba hainyang’anyi haki za Mahakama zetu kusuluhisha migogoro hii. Ukisoma hiyo article 3(2) inasema hivi naomba ninukuu: “The extension of jurisdiction under paragraph 1 shall not preclude the exercise of jurisdiction conferred upon other bodies by the Treaty or the relevant laws of the Partner States”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hakuna confusion hapo. Hii ni option tu kwamba party anaweza kwenda Mahakama hii ya Afrika Mashariki kama ni jambo linalohusiana na mambo ya customs union, common market ama monitoring union. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata ukisoma Treaty yenyewe imeeleza kabisa kwamba, mtu anaweza kwenda kwenye Mahakama zetu na akaomba Mahakama zetu zitoe tafsiri ya Treaty hii ya Afrika Mashariki. Kwa hiyo hakuna confusion. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nagusia alichosema Mheshimiwa Tadayo. Unajua wakati wa Supreme Court of Kenya wakati kesi hizi zinaendelea, kati ya messages nyingi tulizozipata tunaulizwa hivi huku kwetu tuna wanasheria wazuri kama wale ambao tulikuwa tunawaona kwenye TV? Jibu ni ndiyo. Kabisa! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, lakini ni kweli, lazima tujiandae kwa sababu Afrika Mashariki ni competitiveness. Ukishakuwa competitive ni lazima soko sasa litafunguka. Kwa hiyo, niwatoe wasiwasi tu, wako Wanasheria wazuri sana, hapa kwetu tu ni minus TV ndiyo maana hamuwaoni, lakini kesi zikiwa live mtawaona, tena wako wazuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, lakini ni kweli, tuendeshe elimu nzuri sana ili watu wetu wajiandae kabisa namna ya kushirikiana na wenzetu wa Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nguzo kuu ya Afrika Mashariki ni kitu kinaitwa widening and deepening of integration. Kwa hiyo, hii ni stage moja wapo ya sisi kuendelea ku-widen scope ya Afrika Mashariki na kui-deepen. Kwa hiyo, kila wakati kumbuka to widen and deepen the integration kwa sababu tuliamua. Hii ni uchumi na kwa kweli kwa nchi zote za Afrika Mashariki na sasa nchi nyingine zinaongezeka, ziko Saba sasa, nchi yetu iko strategically positioned kuwa mnufaika mkubwa sana wa integration ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Kamati imefanya kazi nzuri sana. Ninaomba tulishawishi Bunge hili likubali kupitisha Itifaki hii bila kuchelewa ili Mheshimiwa Waziri na timu yake wakaendelee kufanya kazi nzuri sana. Na sisi kwa kweli we are Leaders in the region, lazima tuoneshe leading role kwenye vitu kama hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya, nakushukuru. Ahsante sana naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi hii na kabla ya yote kabisa nimpongeze sana Mama yetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa aliyofanya kwa mwaka mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru pia Makamu wa Rais, Dkt. Isdor Mpango na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa kuendelea kumsaidia Rais wetu kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nimshukuru sana Waziri wa TAMISEMI na timu yake yote kwa hotuba nzuri sana. Nimshukuru vilevile jirani yangu hapa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Makamu wake na timu yote na Kamati yote ile kwa kuendelea kuwakilisha Bunge vizuri kusimamia TAMISEMI.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiteto peke yake kwa mwaka huu uliopita, tumepata miradi ya zaidi ya shilingi bilioni saba hongereni sana. Wananchi wa Kiteto wamepanga na wameniomba nije niwashukuru sana kwa miradi na heshima kubwa mliyoijengea Kiteto. Madarasa ya shule shikizi peke yake ni shilingi 1,140,000,000 tumejenga madarasa 57; madarasa ya sekondari madarasa 44, shilingi milioni 880; vituo vya afya bilioni moja, vituo viwili vya afya vya tarafa zile na sisi tumepanga, nimeongea Mkurugenzi wangu asubuhi hii. Sisi tutamaliza hiyo kazi tarehe 20 Mei, mwezi mmoja kabla ambao mmetuwekea na nakukaribisha sana Mheshimiwa Waziri ututembelee ili vituo vile vingine vitatu vya tarafa tulivyokubaliana, hapa tulishakubaliana tujenge kwenye tarafa zote, Tarafa ya Makame, Dosidosi na Kibaya. Kwa hiyo, sisi sasa tunawadai tatu tu na kwa kweli kwa speed tunayokwenda nayo na nakualika Mheshimiwa Waziri uje uone ili mtupatie hizo fedha zingine tumalize biashara ya Tarafa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumepata fedha shilingi 1,500,000,000 kwa TARURA tunawashukuru sana. Na namshukuru sana kumuona Engineer Seif hapa, nimualike atembelee Kiteto. Kiteto ni jimbo kubwa sana ni kubwa kuliko Mkoa wa Kilimanjaro na tuna Meneja pale mzuri sana, shida yetu ni gari. Terrain ya Kiteto, jiografia na umbali wake, kwa kweli mtuletee Landcruiser moja nzuri sana ili kazi hii iendelee kufanyika vizuri zaidi. Namualika vilevile Mkurugenzi Mkuu wa TARURA atembelee Kiteto, karibu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tumepata shule za sekondari mbili mpya shilingi 1,200,000,000 na kazi zinaendelea. Bado sasa na kama kata nne hivi hazina sekondari na kwa kuwa tulishapanga tujenge sekondari kwa kata zote; tukiendelea na kasi hii Kata za Makame, Leseri, Lolela na Ndiligish na uzuri Mwenyekiti wangu wa Halmashauri yupo hapa juu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, ninaushauri sana ambao nilishakuutoa siku nyingi kidogo; ipo miradi, miradi ya wananchi ambayo imejengwa na nguvu za wananchi na niitumie nafasi hii kuwapongeza sana wananchi Kiteto. Mheshimiwa Waziri nipo na karatasi hapa miradi zaidi ya 119 ipo kwenye stage mbalimbali ambazo zimejengwa na nguvu za wananchi. Wakati tunapata fedha za UVIKO-19 tulitamani zile fedha zingemalizia miradi ile iliyojengwa na wananchi, lakini kutokana na masharti ya fedha za UVIKO tulimuelewa sana aliyekuwa Waziri wa TAMISEMI kwamba kwa sababu ya masharti tusingeweza kumalizia majengo yale. Lakini kwa kweli kwa juhudi hii iliyooneshwa na wananchi madarasa tu peke yake kwa mfano tu Kiteto tuna miradi 80 inaendelea kwenye vijiji 50 kati ya vijiji 63 vya Wilaya ya Kiteto. Lakini kwenye miradi ya shule shikizi bado tuna uhitaji wa madarasa 26. Lakini kwa zahanati 13 hizi nguvu za wananchi wa Kiteto kwa kweli zina-deserve Serikali iwaunge mkono, kwani tulishatoa ushauri Mheshimiwa Waziri I am sure kwa kweli m-consider hizi nguvu za wananchi ili wananchi waendelee kupata ari ya kuchangia miradi kwa kweli tutafarijika sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni la watumishi; ripoti ya CAG inaniambia Kiteto tuna upungufu wa watumishi 651. Sasa watumishi wakipungua kwa kweli ufanisi wa kazi utapungua nao zaidi. Kwa hiyo, naomba na ninafurahi sana kuona kwamba Waziri wa Utumishi ametoa ajira zile na ametoa breakdown kwamba walimu nafasi 12,000, afya 10,000, kilimo 814, mifugo 700, uvuvi 204, maji 261, sheria 53; tunachowaomba ajira hizi zinavyotoka mtumia formula mliyotumia wakati mnagawa fedha za Uviko, wote tupate. Heshima mliyowajengea Wabunge kwa fedha kwa hizi za UVIKO-19 mkifuata formula hii wallah nawaambia wale wanaotaka majimbo haya watapata taabu sana huko mbele kwa sababu mtakuwa mmewajengea heshima Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile maslahi ya watumishi, yakiangaliwa yanaongeza ufanisi zaidi. Na wameyazungumza Waheshimiwa Mabunge hapa kuhusu maslahi ya Madiwani kwa kweli Madiwani wetu wanafanya kazi nzuri zaidi. Tuwaangalie namna ya kuboresha maslahi yao. Lakini vilevile Wenyeviti wa Vijiji na Wenyeviti wa Mitaa wanafanya kazi kubwa sana tuwaangalie namna ya kuwasaidia ili kujenga ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini walikwisha kusema wengine hapa, tukiwapa uwezo, tukitengeneza zile semina za kuwajengea uwezo Madiwani na Wenyeviti, itaongeza ufanisi zaidi katika kusimamia miradi. Kwa hiyo, zile semina za kuongeza uwezo zitasaidia sana msiziache. Kwa kweli Madiwani wetu wangekuwa wanapata from time-to-time wapate semina kama hizo itaongeza ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni la TARURA; nawashukuru sana kwa kuongeza fedha kwa TARURA, lakini ni kweli Ilani ya Chama cha Mapinduzi tulishasema hivyo, tunataka tuongeze fedha nyingi zaidi najua mmeongeza fedha karibu bilioni 100 tena nawapongeza sana. Tunataka fedha za TARURA ziendelee kuwa nyingi zaidi ili barabara za vijijini na mijini zikapate kufunguka; barabara zitaongeza kasi ya uzalishaji. Kwa hiyo, kwa kweli endeleeni kuangalia TARURA kila wakati ikipatikana fedha muongeze fedha kwa ajili ya TARURA.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna majengo haya ya Halmashauri; Kiteto tuna jengo la Halmashauri ambalo sasa linaendelea kwa muda mrefu kidogo na kuna fedha karibu milioni kama 400 hivi bado; na mkandarasi anasema kwa kuwa malipo yamechukua muda mrefu kidogo tangu mwaka 2016 anaanza kufikiri kwamba zile fedha ni kidogo. Kwa hiyo, nawaombeni sana, hii miradi mkitoa fedha kwa utaratibu ili zisichelewe mtatuepusha sisi na matatizo ya huko ya kuanza kugombana na wakandarasi. Kwa hiyo, mkitugawia milioni 400 hiyo lile jengo tulimalizie kwa sababu mmeshatumia fedha nyingi sana na tunawashukuru sana. Kwa hiyo, nakukumbusha Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nyingine, kwenye ajira hizi hasa za walimu muangalie sana namna ya kuwajali walimu ambao wamekuwa wakijitolea kwa miaka mingi kidogo; hiyo iwe criteria kabisa namba moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vijana wetu ambao wamemaliza elimu zao na wakaona wasikae bure nyumbani waendelee kutusaidia wanafanya kazi kubwa sana. Mkiweka hiyo kama criteria wale wote ambao wana-volunteer na wanaendelea kutufundishia watoto wetu hiyo iwe criteria namba moja. Mheshimiwa Waziri usikubali kabisa kumuacha mwalimu ambaye ana record ya kuendelea ku-volunteer, mkifanya hivyo mtakuwa mmetenda kazi nzuri sana; na tuangalie wafanyakazi wetu wote wanao-volunteer kwenye sekta fulani fulani kila mtu anaye- volunteer nia yake ikitokea kanafasi basi apewe priority. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli baada ya kusema haya, mimi nakushukuru sana naunga mkono TAMISEMI mtakijengea heshima Chama cha Mapinduzi kwa sababu ukisoma ilani...

NAIBU SPIKA: Ahsante sana kwa mchango mzuri.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli nakushukuru sana naunga mkono hoja ahsanteni sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Utanisamehe sauti yangu leo si nzuri sana. Lakini kwanza kabla ya yote kabisa nimpongeze sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya kutatua kero za maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kiteto wakati tunachaguliwa Mkoa wa Manyara, nilishazungumza hapa mwaka jana, upatikanaji wa maji ni asilimia 58, way below national average. Lakini nafurahi sana kwamba kwa mwaka jana na mwaka huu bajeti ya mwaka huu, nilikuwa naongea na Engineer wananiambia kwamba mpaka Disemba tutakuwa tumefikisha asilimia 68 well done. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kumpongeza Mheshimiwa Rais nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri, Katibu Mkuu na timu yao wote kwakweli kwa kazi kubwa wanayofanya kumsaidia Rais. Tunaona kila mahala wanapokwenda kusimamia miradi ya maji big up. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mkurugenzi wa RUWASA na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara kwakweli kwa kazi kubwa wanayofanya. Ndiyo maana Mheshimiwa

Makamu wa Rais wakati alipotembelea Simanjiro aliahidi fedha kwa Meneja wa RUWASA wa Mkoa kwa kazi kubwa anayofanya, hii ni kutambua kazi yake kubwa anayofanya. Meneja wa RUWASA Kiteto anafanya kazi nzuri sana. Kwa kweli timu hii mmejipanga vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nilishazungumza hapa, kwamba Kiteto ni jimbo moja kubwa sana, zaidi ya Mkoa wa Kilimanjaro. Meneja wa RUWASA Kiteto hana gari. Alishalala siku moja mpaka saa nane kwenye mapori yale. Mheshimiwa Waziri tunaomba Landcruiser moja nzuri sana ili huyu meneja apate kufanyakazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais alituletea mradi mkubwa sana wa maji pale Mjini Kibaya Kata ya Kaloreni wenye thamani ya shilingi milioni 400; ni mradi mzuri sana. Lakini nilisema mwaka jana kwamba miundombinu ya mabomba pale mjini yamechakaa. Kwa hiyo, hata tukipata haya maji ya milioni 400 bila kufumua mabomba ya mjini pale, na nilikuomba milioni 100, hata huo mradi hatutafaidi sana itakuwa na linkage. Naomba milioni 100 ili tufumue mifumo ya maji pale ili wananchi wa-enjoy maji milioni yenye thamani ya Shilingi milioni 400 ambayo yameletwa na Mama Samia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu mabwawa. Kiteto ni kame. Nilishazungumza hapa tarehe 10 mwezi wa pili mwaka huu, kwenye swali namba 84, kuhusu Mabwawa ya Dongo, Dosidosi na Kijungu. Mliniahidi kwamba mtapata fedha na mtajenga mabwawa haya.

Naomba kwakweli Mheshimiwa Waziri nikufahamishe kuwa ilikuja timu ya Dosidosi hapa wakifuatilia Bwawa lao la Dosidosi; na nimeshazungumza mara nyingi sana hapa, kwamba wilaya hizi ambazo ni kame tusipopata mabwawa kwaajili ya wakulima na wafugaji kwakweli changamoto za ukame hata mifugo imekufa sana mwakajana kwasababu ya ukame huo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri mimi najua bajeti hii umetutengea karibu bilioni mbili tena, tunakushukuru sana. Tunayaomba sana Mabwawa haya ya Dongo, Dosidosi, Kijungu ili wananchi hawa wakapate kunufaika na maji.

Mheshimiwa Spika, napenda pia niwashukuru wadau wa maendeleo wanaosaidia miradi ya maji Kiteto kama vile OIKOS. Juzi tu siku mbili zilizopita tumekwenda kuzindua mradi wa vijiji 16 miradi ya maji ninawashukuru sana OIKOS. Kwakweli Mheshimwia Waziri hili Shirika la OIKOS mlisaidie na muwape support nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maabara ya maji naambiwa zilikuwa takriban 16 nchi hii lakini wameleta maabara ya maji Mkoa wa Manyara, Shirika hili la OIKOS.

Mheshimiwa Spika, mashirika mengine yanayojishughulisha na miradi ya maji kwenye Jimbo la Kiteto ni; Shirika la PINGOS, ELEWA AFRICA, KINAPA na PICODEO.
Mashirika haya yanahitaji support sana; na ninawashukuru sana kwa kazi kubwa wanayofanya. Juzi tu Kata karibu 10 zimenufaika na mradi huu Kata za Makame, Ndedo, Engusero, Lengateri, Loolera, Matui, Ndiringishi, Magungu na Bwawani kata 10 vijiji 16 kwakweli wanafanyakazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tulishazungumza mimi na Mheshimiwa Waziri na nilimualika aje Kiteto; na kati ya maeneo ambayo nilimuahidi tutatembelea ni kwenda Dongo kuangalia Bwawa la Dongo. Naomba sana, baada ya bajeti hii ambayo mimi najua itapita kwa speed kubwa sana kwa kazi unayofanya; tupange utembelee Kiteto. Vilevile nilimualika na Naibu Waziri pia twende Kiteto. Mheshimiwa Waziri tutampeleka Dongo huku huyu tutampeleka umasaini huko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Kiteto kwakweli kwa kasi ya maji, alikuwa ananiambia meneja wangu wa RUWASA, kwamba mpaka Juni mwaka huu tutakuwa tumetoka asilimia 52 ya maji mpaka asilimia 68, ambayo ni nzuri sana. Tukiendelea na kasi hii ile dream ya mama yetu yakuleta maji asilimia 95 vijijini na 85 tutafikia bila shida yoyote.

Mheshimiwa Spika, wakati Mheshimiwa Waziri, atakapohitimisha bajeti yake nitataka baadaye atuambie, zile mashine ambazo Mama Samia alisema ataleta kila mkoa hebu mtuambie imefikia wapi? Kwa sababu sasa tunataka kujishughulisha na mambo ya mabwawa yetu. Akifanya hivyo kwakweli Mwenyezi Mungu atambariki sana.

Mheshimiwa Spika, kwakweli Wizara Maji kwa kazi wanayofanya kwakweli tuwasaidie wapate pesa hizi za bajeti ili miradi hii ikatekelezwe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya naomba kuunga mkono hoja, ahsanteni sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi ya kuanza kuchangia TAMISEMI. Kwanza kabisa nimshukuru Mwenyenzi Mungu kwa afya njema aliyotujalia na nimpongeze Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa miradi mingi sana ambayo kwa kweli ameipeleka kwenye majimbo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jimbo la Kiteto pekee yake, miradi ya miaka miwili hii ni karibu bilioni 18. Kwa kweli amegusa karibu kila mahali, VETA sasa tunazungumza inajengwa Kiteto. Tumepata vituo vya afya viwili bilioni 1, Daraja la Sunya karibu milioni 800, shule shikizi madarasa karibu 57, shule za sekondari madarasa 44, mradi wa maji pale Kaloleni, digital x-ray milioni 900 kwa ajili ya kukarabati hospitali ya wilaya. Ambaye sasa sisi tuliomba na hii ni renovation ya Mkurugenzi aliomba kwamba tunajenga jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji na maabara. Sisi tulikataa kukarabati majengo yale na nashukuru TAMISEMI kwa sababu tumeomba na wametuambia, wametupa go ahead. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lniseme TAMISEMI walituambia ili kuweza kujenga majengo hayo sisi tunahitaji karibu bilioni moja na milioni 300 na wao wametupata mia 900 lakini sisi tukasema tutajenga kwa hiyo mia 900. Kwa hiyo, nitumie nafasi hii pia kumpongeza Mkurugenzi kwa renovation hiyo nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimpongeze Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Angellah, Naibu Waziri Dugange na Ndejembi, Katibu Mkuu, wote na timu nzima hii kwa kazi nzuri ambayo wanajaribu kufanya. Mheshimiwa Waziri kila wakati tukikuandikia, umekua mwepesi sana na timu yako nzuri sana. Nashukuru pia kwa ziara aliyoifanya Naibu Waziri Kiteto kwa kweli timu ya TAMISEMI mmejipanga vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru vile vile kwa pesa tuliozipata kwa ajili ya shule kongwe zile. Shule za Kijungu, Sunya, Ndosidosi, Kibaya na nashukuru kwa sababu tumeona mmetuongezea pesa tena kwa ajili ya shule hizi kongwe. Mheshimiwa Waziri tulikutana, ile idea yako ya kukutana na Wabunge wa Mikoa ilikuwa ni renovation nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na wewe unafahamu tarehe 12 Februari, tulikutana na timu ya Manyara na tukaleta maandishi yetu ya kujaribu kuonyesha miradi. Eneo kubwa ni TARURA, TARURA tulishakubaliana hapa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi iko bayana sana, tulisema ni lazima sasa TARURA iongezewe pesa kwa sababu ya mtandao wa barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ilani ya Chama cha Mapinduzi ilisema hivi na tuliahidi kwamba ni vyema sasa tuanze kuangalia ile formula ile kati ya TARURA na TANROADS kwa nia ya kuongezea TARURA pesa. Kwa mfano, kwa Kiteto pekee yake, mtandao wa barabara ni kilometa 1,291. Bajeti tunayoihitaji ni bilioni 11, lakini uhalisia tunapata bilioni mbili na milioni 800 haitoshi na siku ile Mheshimiwa Waziri unafahamu tulisema kama mtatuongezea sisi bilioni tatu walau tuwe tunapata bilioni 5.8 ama sita itatusaidia kuendelea kujenga mtandao huu wa barabara, ili wananchi waliopo vijijini wakapate kusafiri bila shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri ombi langu lipo pale pale, tunategemea kwa kweli hizi pesa ziongezeke. Na kwa kweli nimpongeze Mkurugenzi wa TARURA hata kwa sura simfahamu lakini nimemsumbua kwenye simu, Kiteto ilikua haina gari na sasa tumepata gari. Kwa kweli nampongeza sana. kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri mtuongeze pesa kwa ajili ya TARURA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine Mheshimiwa Waziri, alikuja Katibu Mkuu wa CCM Jimbo la Kiteto, ametuahidi kilometa 1 ya lami na taa za barabarani na maombi tumeshaleta. Taa za barabarani pale mjini ni karibu milioni 250 tu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri tunaendelea kumbushia, ambulance kwa ajili ya Engusero aliahidi Mheshimiwa Rais, Sunya gari lao lilipata ajali na hospitali ya wilaya. Kwa hiyo, kwenye zile ambulance mnazogawa Kiteto utupendelee. Kiteto ni kubwa kila siku nasema hapa, square kilometa 1,700. Mheshimiwa Waziri ukituongezea itatusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la walimu wanaojitolea; Mheshimiwa Waziri tunashukuru mmetangaza ajira, fuatilia tunataka walimu hawa wanaojitolea wapewe kipaumbele kwenye ajira. Kila mtu anapojitolea nia yake, kwanza ni suala kizalendo, kujitolea. Kwa hiyo, kwenye nafasi hizo kwa kweli uwachukue na inasadikika nchi hii sasa wapo walimu wanaojitolea karibu 70,000/80,000 hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wakianzisha mjadala wa kuwachukua hata kama ni kubadilisha sheria, kwamba vigezo ni merit, yes lakini mtu anayejitolea na yeye hicho ni kigezo ambacho ni muhimu sana, hawa watu wanafanya kazi nzuri sana. Kwa hiyo tunategemea kwamba tutaona vijana wengi wa Kiteto wanaojitolea wakipata ajira kwenye nafasi ambazo wametangaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Madiwani. Madiwani wetu wanafanya kazi kubwa sana. Wanasimamia miradi na nataka niseme kuna link kati ya fedha hizi zinazopotea labda na kwa sababu Madiwani hawako full time. Labda tuangalie huko mbele baadaye maslahi ikiongezeka na posho na stahiki kwa ajili ya Madiwani labda usimamizi utakuwa wa bora sana na pengine hizi fedha zinazopotea potea, haitatokea. Hebu waangaliwe sana Madiwani wanafanya kazi kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, liko suala la maboma ama miradi ile ambayo inafanywa na wananchi. Kiteto, wananchi wa Kiteto ni wachapa kazi sana. Kuna miradi mingi sana, kwa mfano zahanati tu peke yake karibu miradi 14 ipo kwenye lenta, wananchi wale wamefanya kazi kubwa sana. Kwa mfano, Zambia, Mbigiri, Mbeli, Taigo, Chapakazi, Engusero, Sidan, Logoet, Chekanao, Olduvai na mengine mengi. Zahanati zao ziko kwenye lenta. Tulikaa hapa mwaka jana, tukasema tujenge vituo vya tarafa, Kiteto bado nadai vituo vitatu vya tarafa. Tarafa ya Makame, Dosidosi na Kibaya. Tulisema tukipeleka huduma hizi kwenye tarafa itasaidia sasa zahanati tunazozijenga walau tutakuwa tumepeleka huduma karibu na wananchi. Kwa hiyo, kwa kweli tusikubali hili Bunge liishe hatajamalizana na habari ya vituo vya tarafa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli Mheshimiwa Waziri akatafute fedha. Hili halina mjadala hata kidogo, nataka vituo vitatu vya tarafa na tulishapitisha hapa. Haiwezekani watu wengine wanaendelea kujenga za kata wakati sisi wengine tunazungumza habari ya tarafa hapa and I am serious, very serious about this, kwa kweli. This is not negotiable, tumeshakubaliana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya majengo haya, Kiteto hospitali yetu ikipata tena majengo ya maternity, dharura (emergency), RCH na jengo la X-Ray ile mpya ambayo tunaitumia sasa, itasaidia kuweka Wilaya ya Kiteto kwenye hadhi ya Hospitali ya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la watumishi. Kuna Mkurugenzi yuko pale Same. Unajua siyo kila wakati lazima tukutane hapa tuna-complain kuhusu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Olelekaita, muda wako umekwisha.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkurugenzi wangu anachapa kazi sana abaki na aendelee kumaliza majengo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ahsanteni sana na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi, kwanza ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa afya njema na tuko hapa leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili tumpongeze Mheshimiwa Rais Mama Samia kwa kuja na ubunifu wa EPC + Finance. Nilizungumza mwaka jana hapa kuhusu barabara hizi za Kongwa – Kiteto na Simanjiro na kwa kweli nimpongeze Profesa Mbarawa - Waziri wa Ujenzi, Engineer Kasekenya – Naibu Waziri Ujenzi, Mheshimiwa Mwakibete- Naibu Waziri Uchukuzi, Makatibu Wakuu na timu nzima kwa kazi kubwa ambayo kwa kweli mmefanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka nilizungumza hapa ilikuwa ni tarehe 17 Mei, 2021 nikawa nazungumza habari ya barabara hizi za Kongwa – Kiteto – Simanjiro mpaka Arusha, lakini nimezungumza habari ya barabara kutoka Kibirashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Chemba mpaka Singida. Leo jioni hii Mheshimiwa Waziri kwa kweli wananchi wa Kiteto wamefarijika sana. Nimesoma bajeti yako hapa na hotuba hapa ukurasa wa 11, kwamba Barabara ya Handeni – Kibirashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Orboloti – Talai – Chemba - Kwamtoro mpaka Singida, kilometa 460 ipo kwenye mpango wa bajeti. Kwa kweli, nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri na wananchi wa Kiteto kwa kweli wamefarijika sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili barabara ya kutoka Kongwa – Kibaya – Simanjiro mpaka Arusha vilevile naona hapa kwenye hizi barabara hizi kilometa 2,000 zinazojengwa kwa mpango huu wa EPC + Finance. Kwa kweli tumefarijika sana na hii kwa kweli itafungua sana siyo tu maendeleo kwenye Majimbo haya lakini uchumi kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzuri wa barabara hii ya Tanga mpaka Singida kupitia Kiteto kwa kuwa tumeshafanya maamuzi kama nchi kujenga bomba hili la mafuta kutoka Hoima – Uganda mpaka Chongoleani – Tanga, barabara hii itasaidia sana kufungua uchumi na itakuwa inaendana na bomba la mafuta. Kwa hiyo, kwa kweli big up huu ni mradi ambao kwa kweli uta- complement vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ya Kongwa – Kibaya hizi barabara mbili hizi mimi naita ni barabara za vijijini. Kwangu tu Kiteto peke yake inapita zaidi ya vijiji 20, na kwa kweli Kiteto kutoka sasa kilometa nne za lami za pale Mjini ambazo hata taa hazina mpaka karibu kilometa 300 za lami baada ya hizi barabara zote mbili kujengwa, kwa kweli itafungua uchumi mkubwa sana.

Mheshimiwa Waziri huu mpango mpya wa EPC + Finance karibu sasa tutaitia majina ya watoto kule Majimboni EPC + Finance kwa sababu kila wakati tumekuwa tunasema kwenye mikutano ya hadhara, barabara zetu zitajengwa kwa EPC + Finance. Kwa hiyo, labda mtafute Kiswahili nzuri ya EPC + Finance kwa sababu ni kitu kizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hizi kwa umuhimu wake, kilimo, mifugo na usafiri kwa wananchi ambao wanapitiwa na barabara hizi kwa kweli itaondoa changamoto ya muda mrefu sana ambayo kwa kweli wananchi wamekuwa nayo. Kwa hiyo, kwa kweli kwa Kiteto simu leo zimekuwa nyingi sana kutoka Kiteto huko baada ya bajeti hii kusomwa na kwamba wananchi wale wamesikia barabara zao. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri nakushukuru sana na Mwenyezi Mungu awabariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili tunasubiri sana kama ulivyosema hapa kwamba sasa tunachosubiri ni kutiwa saini kwa ujenzi wa barabara hizi na vizuri uemesema ni kabla ya Juni mwaka huu. Kwa hiyo, kwa kweli tunasubiria sana na hii tarehe kwa kweli mtufahamishe, hata baadhi ya wananchi wanataka kuja kabisa hata kuona mikataba hii ikisainiwa. Hii kwa kweli italeta maana kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoomba sasa kwa barabara hizi mbili kazi ambazo wananchi watakuwa na sifa nazo ni vema mkaongea na wakandarasi ili wananchi wanaotoka kwenye maeneo haya wakapate hizo kazi kwenye barabara hizi na mhakikishe kabisa kwamba wananchi wanalipwa. Kwa hivyo, kama wakandarasi kuna sifa za wananchi zipo huko basi na wananchi waweze kunufaika na tender za barabara hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie habari ya ATCL (Shirika la Ndege la Taifa). Mimi nadhani ni expensive sana ticket ya ndege ya ATCL ni ghali kidogo. Kwa hivyo, pengine ni vizuri mkaangalia namna kwa sababu Watanzania wanapenda kutumia ndege yao hii, imekuwa ni ghali kidogo. Jambo ambalo linasikitisha kidogo eti ni ukipiga simu saa mbili ya usiku wamelala! Sasa hiyo kwa kweli kwa nchi ambayo sasa imefunguka na tunataka tuanze kusafiri, inaeleweka kwa Uwanja wa Ndege wa Dodoma hakuna taa sawa, lakini kwa Arusha na Kilimanjaro na Dar es Salaam na Mwanza kwa kweli nashangaa sana kwa nini hawa ndiyo wanaenda huko, na simu ya customer care, sasa wakienda kulala na wao saa mbili kweli itakuwa Hapana! Lazima hilo tubadilishe kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru Mheshimiwa Waziri nimeona pia barabara ya Dongo – Sunya – Kijungu mmetengea bajeti kwenye hotuba yako na kwa kweli kubwa kwangu leo unajua nimeishiwa maneno, leo kwa mara ya kwanza baada ya kuona hizi barabara hizi mbili hizi, barabara hizi mbili ambazo tumezipigia kelele kwa muda mrefu sana kuona leo kwamba ziko kwenye mpango wa EPC + Finance na faida zake zinajulikana, for once nimekosa cha kusema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa tuwapitishie bajeti wakafanye hii kazi haraka sana. Ninakushukuru ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi ya kuanza kuchangia. Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na leo tuko hapa salama kabisa. Pia, tumpongeze Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuweka fedha nyingi sana kwenye Wizara hii ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Waziri, rafiki yangu Nape Nnauye na Naibu Waziri, Engineer Kundo, kwa kazi nzuri sana ambayo mnafanya na tukianzia na hafla ile ya kusaini mikataba kwa ajili ya minara karibu 158. Kwa kweli hongereni sana ile ilikuwa ni innovation nzuri sana na sisi tunaotoka vijijini mmetufurahisha sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wizara hii ni muhimu sana. Huko duniani sasa digital economy ni kitu muhimu sana na ndio dunia ya sasa inakokwenda. Pia, nilikuwa nasoma ripoti ya World Bank hapa tunaambiwa digital economy ina range between 14 to 16 percent ya GDP. Kwa hiyo, ni eneo zuri sana na lazima kwa kweli tuendeleze na tuweke pesa nyingi zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Katibu Mkuu na timu nzima ya wizara hii na hasa hasa Mkurugenzi wa UCSAF unajua sisi tunaotoka vijijini ni lazima tumsifie Mkurugenzi wa UCSAF, I think she is the best CEO in my opinion. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niliandika ripoti hapa 2021, Mheshimiwa Waziri, nilileta kata karibu 15 za Kiteto zilikuwa na shida ya mawasiliano lakini leo kwenye bajeti yako hapa nimefurahi sana. Nimesoma ukurasa wa 100 nimekuta kata 12 zipo kwenye minara hiyo. Kata za Laiseri vijiji vyote kata hiyo ilikuwa haina mnara hata mmoja leo naona hapa. Mheshimiwa Waziri, nakushukuru ulimtuma Mheshimiwa Naibu Waziri, alifika Kata hii ya Laiseri. Kwa hiyo, wananchi wa huko Kiteto wa Kata ya Laiseri, Lengatei, Loolera, Magungu, Namelock, Partimbo, Sunya, Loitepesi, Songambele, Peresa, Njoro, Dosidosi, Ndirigishi. Sasa, tutaachaje kusifia kwa namna hiyo? Honestly kata karibu 12 na vijiji zaidi ya 23. Mwenyezi Mungu awabariki sana na wananchi wa Kiteto kwa kweli watakuwa wamefarijika na bajeti hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, liko jambo hapa la wizi unaotokana na mitandao. Imekuwa ni janga kubwa kidogo na linawasumbua sana watanzania walio wengi. Ninakuomba sana Mheshimiwa Waziri, tuendelee kuongeza teknolojia ili wezi hawa na matapeli wa mitandao wasiwatapeli watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, tumekuwa unajua kwa mujibu wa Sheria kila mtu anatakiwa aripoti kosa na tumekuwa tuki–volunteer. Hawa matapeli wanaotupigia tumekuwa tunaripoti kwa makampuni ya simu. Ambacho hatupati ni feedback kutoka kwa makampuni ya simu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima mkampuni ya simu yatuambie kama wateja kwamba ile simu uliyoripoti na sisi tumefanya moja, mbili, tatu na tunaendelea. Hiyo itajenga customer care nzuri. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri, wewe waandikie makampuni ya simu hapa. Haiwezekani sisi turipoti halafu tena wakati mwingine wanasema kabisa kwa quality control tunarekodi hii simu yako tusikilize halafu tunaripoti hizi simu na hawatupi mrejesho. Wakifanya hivyo itasaidia kupunguza wizi huo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Mheshimiwa Waziri, vyombo vya habari. Vyombo vya habari ni sekta muhimu sana na kwa kweli nakumbuka incident yako moja wapo jana nilikuwa naangalia YouTube, vyombo vya habari vilifanya kazi nzuri sana. If it wasn’t wao sijui tukio lile lilikuwaje. Kwa hiyo, please wasaidie sana na mkae. Ni taaluma ambayo ni nzuri sana inatupatia habari na kupata habari ni jambo la kikatiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Mheshimiwa Waziri, alisema Mheshimiwa Rais, siku ile ya kusaini mikataba, kwa sababu ya Sheria hizi za manunuzi kutengeneza mlolongo ambao ni bureaucracy kubwa inachukua muda wakati fulani, tungependa minara hii ifike vijijini kwa haraka. Pia, Mheshimiwa Rais, alisema mwezi mkoja tu na ilikuwa tarehe 13 karibu wiki moja sasa hivi imekwishakatika. Sisi ambao tumefurahi kupata minara hii tunategemea baada ya mwezi mmoja vibali vile vinavyotakiwa viwe vimepatikana lakini lazima mlete Sheria ya Procurement tuangalie ipunguze hii bureaucracy.

Mheshimiwa Naibu Spika, haiwezekani tupate pesa halafu tuendelee kukaa miezi sita, nane kwa sababu ya kuleta vifaa. Tunataka wananchi wapate huduma hii kwa haraka sana. Nadhani kwa sababu tunazungumzia habari ya kidijitali na TEHAMA, nilifikiri wewe ungekuwa na regime tofauti kabisa. Yaani wewe lazima uende haraka zaidi kuliko wengine. Haiwezekani wewe uwe na sekta hii ambayo tunazungumza habari ya kidijitali halafu bado Procurement Law ile ambayo inachukua muda mrefu zaidi inafanya kama vile ni manual system.Vile vile, hata hapa Mheshimiwa Naibu Spika, amesema wewe umetumia muda mfupi sana hapa, hiyo ndio TEHAMA, ndio digital. Kwa hiyo, lazima ninyi muwezeshwe mwende haraka zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, nilizungumza mwaka 2021 na 2022, kuhusu Radio Tanzania kutokusikika Kiteto lakini vilevile nafarijika kwenye hotuba yako ya mwaka 2022 na hata safari hii nimeona Kiteto ukurasa wa 125 kwamba mtaongeza usikivu, watanzania wale wa Kiteto ni vema wakaanza kufuatilia redio yao ya Tanzania. Haiwezekani miaka 60 baada ya uhuru bado wana Kiteto hawapati taarifa kutoka redioTanzania. kwa hiyo, nakushukuru sana kwamba Kiteto sasa itafunguka.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Mheshimiwa Waziri, suala hili la mawasiliano, tulikuona ukienda Mlima Kilimanjaro kupandisha internet. Unajua wakati tunapandisha Mwenge wa Uhuru Mlima Kilimanjaro kulikuwa na quotation nzuri sana ya Baba wa Taifa. Sasa lazima tuwe na slogan sasa kwa kuwa Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu Afrika lazima tuwe na slogan ya kupandisha ile na mantiki yetu ni nini?

NAIBU SPIKA: Ahsante, ahsante.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda naunga mkono hoja na Mungu awabariki sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema na tuko hapa leo tuna afya nzuri sana. Pili, nimpongeze Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa filamu ya Royal Tour, filamu ya Royal Tour imefungua nchi yetu imetuongezea watalii wengi sana, tatu nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Ndugu Mchengerwa, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na timu nzima ya Maliasili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo machache sana leo na I think ndiyo wakati pekee nitaongea leo a bit calm, kuliko wakati mwingine wowote. Utalii na uhifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utalii ni sekta muhimu sana inaongezea nchi yetu mapato lakini inasaidia kufungua nchi yetu, kuna uhifadhi vilevile ambayo ndiyo conservation, sasa na mimi nafikiri Mheshimiwa Waziri utalii na uhifadhi ni vitu viwili tofauti. Uhifadhi ndiyo hard core ya uhifadhi lakini utalii ndiyo soft part, the business element, sasa hivi ni vitu viwili tofauti tukivichanganya sana pengine tutashindwa ku - appreciate tofauti zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini mtu anayelinda maeneo ambaye ni mtaalam wa wanyamapori, ambae atakuwa natuambia study za wanyamapori zikoje, atakuwa anapambana na majangili huyo huyo mtu ndiyo atuuzie kweli hifadhi zetu the business element? Mimi siamini hivyo. Mheshimiwa Waziri hebu angalia tengeneza timu zako, timu inayo - deal na watalii peke yake na timu ambayo inafanya mambo ya uhifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukifanya hivyo nadhani tutapata namna ya kufaidika vizuri zaidi. Wale ambao ni wahifadhi tena ambao ni Jeshi USU siku hizi, tena ndiyo kabisa wanatakiwa wao waanze kupambana na majangili, mimea vamizi, waandike vitabu, waandike articles waende kwenye scientific conferences, wajaribu kuuza nchi yetu kwa scientific element part ya conservation. Watu ambao watafanya kazi ya utalii ambayo ndiyo business element, lazima tuwe na timu ambayo ni tofauti kidogo ambayo ni sharp ni creative ni innovative, kwa sababu biashara tunashindana na wengine it is about competitiveness, lazima tuwe na timu nyingine, hebu mui–organize kidogo tunaweza tukanufaika zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefurahishwa sana na pengine ndiyo maana leo am very calm na kauli zako mbili ulizotoa baada ya kuteuliwa. Umesema wananchi ni wahifadhi namba moja, lakini ukasema vilevile watu wa hifadhi watapimwa kutokana na wanachosema wananchi juu yao. Mheshimiwa Waziri hizi kauli zote mbili ukishikilia unaweza ukawa the best Minister of our life tangu nchi hii ipate uhuru. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitizama mahusiano kati ya wananchi na wahifadhi wanyamapori maeneo ya hifadhi ni mbaya, Mheshimiwa Waziri Ilani ya Chama cha Mapinduzi nikupe tu comfort ukurasa wa 113 inazungumzia kwamba tulisema tutaimarisha mahusiano kati ya wahifadhi na maeneo ya hifadhi na wananchi na Ilani inasema kabisa hivi na ninukuu “kuimarisha mahusiano kati ya maeneo ya hifadhi na wananchi na kulinda mali za wananchi na wananchi wenyewe, vilevile kutoa elimu. Ili sekta ya Maliasili iwe endelevu ni lazima ijali haki na maslahi ya wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, ukienda na hizi mbili, kwa kweli utakuwa an exceptional Minister of our life nikuambie tu ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu mwingine Mheshimiwa Waziri, unajua kati ya maeneo ambayo bado tuna elements za kikoloni ni kwenye eneo hili la conservation. Nilikuwa naangalia Sheria ya Fauna Conservation ya mwaka 1951, nikakutana na kipengele ambacho kinatutesa mpaka leo, hiki cha forfeiture. Ku-forfeit magari, mifugo ya wananchi pale ambapo wanaingia kwenye hifadhi zetu. Kumbe nikagundua kwamba ilianza wakati ule wa ukoloni, forfeiture! Fauna Conservation, Section 53, utakutana nayo na bado ipo mpaka leo kwenye Sheria yetu ya Wanyamapori. Mheshimiwa Waziri lazima tu-decolonize hizi sheria na policies ambazo zinaendelea kutesa watu wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuingia kwenye hifadhi ni kosa, lakini isiwe sababu ya mtu kuwa maskini. Mimi na-subscribe na conservation ambayo, na kauli zako zina-support kwamba, conservation for people and by the people. Hiyo tukienda hivyo tutafanya vizuri sana kwa sababu, after all hifadhi for whose benefit?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani ni wananchi hawa wa Tanzania hawa wanufaika. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri ukienda hivyo tuangalie sheria hizi ambazo zina-colonize. Sasa kwa mfano siku hizi ng’ombe wakikamatwa watu wanafanya compound halafu una-charge laki moja kwa kichwa cha ng’ombe, which is fifty percent of the price. Sasa kama tukiamua kwenda kwa njia hiyo, basi tukiwa tunakamata magari on traffic offences kama gari lako ni Vits tuseme fifty percent ya bei ya hili gari tu¬-charge kama fine kama ndiyo tunataka kwenda huko, lakini mimi siamini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge lilishasema maximum fine na minimum fine, una-charge kwa kosa siyo kwa kichwa cha ng’ombe. Hapa nimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu alitoa maelekezo hapa kwamba, Wizara yenu mkapitie na mkaangalie sheria. Haiwezekani ng’ombe ni laki moja na nusu, halafu unataka kunichaji laki moja kama fine, siyo sawa! lakini Mheshimiwa Waziri kuna ng’ombe wengi sana wamekatwa kwenye maeneo haya, kuna watu wamekwenda wameshinda kesi Mahakamani, lakini mpaka leo wananchi hawa hawajapewa mifugo yao na wapo wengi sana. Hebu wewe tizama na uangalie vizuri sana na pengine ukae na timu yako tena mu-re-evaluate hii kushika ng’ombe kila wakati. Mtengeneze mahusiano, mkitengeneza mahusiano mimi nadhani hakutakuwa na matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naongea na Mheshimiwa Dkt. Mbunge wa Muleba nae ana shida hiyohiyo, wananchi wake wanahangaika kila mahali. Mimi nadhani Mheshimiwa Waziri tengeneza mahusiano haya, wananchi wakifurahi uhifadhi utaendelea na sote tutafurai. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakupongeza unajua wakati mwingine ukipata report za hawa wataalam wako wa maliasili na utalii, achana na hizo ripoti njoo field tena, tembea. Nenda kaongee na wananchi wale, tembelea maeneo yale, utanufaika zaidi kwa kuwasikia wananchi wanasema nini kama ulivyofanya Serengeti. Hiyo ilikuwa ni innovation kubwa na nzuri sana, Mheshimiwa Waziri ukiendelea hivyo itakuwa nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo jingine ni WMA. Mheshimiwa Waziri hii strategy ambayo umeianzisha na nikushukuru kwamba, juzi mmezindua strategy ya kuendesha WMA. Nami najua wewe kwako una WMA hata mimi nina WMA, wananchi hawa wamefanya mambo mengi sana na kutoa ardhi hizi ziwe kwenye WMA na wao sasa waanze kushindana na mbuga za wanyama na maeneo mengine yote yenye WMA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikuombe Mheshimiwa Waziri, hapa tuna Wabunge wengi sana wa WMA, tufanye mpango, tengeneza group la Wabunge wa WMA. Zile WMA zi-protect kutokana na wale investors ambao wengine wakorofi, wanawashitaki Mahakamani. Ukifanya hivyo nadhani sekta hii itafanya vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda naunga mkono hoja na ninakutakia kila la heri. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi na kwa sababu ya muda nitakuwa brief sana. Nimpongeze Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa aliyofanya kuongeza tija kwenye kilimo. Ya kwanza, tumeona bajeti imeongezeka sana, kutoka bilioni mia mbili karibu na tisini na kitu mpaka bilioni mia saba na hamsini na kitu. Hilo kwa kweli ni a right step in right direction. Nimpongeze pia Mheshimiwa Rais kwa kazi za alizofanya Dubai Expo, tumeona mikataba mingi imesainiwa ya kuongeza tija katika kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze pia Waziri wa Kilimo, ndugu yangu Mheshimiwa Bashe; Naibu Waziri, Mheshimiwa Mavunde; Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na timu nzima ya Kilimo kwa kazi kubwa wanayofanya. Kwa kweli tumeona a revival ya kilimo na tunategemea mengi sana zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiteto ni food basket na nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa sababu alitembelea Kiteto. Nilikuwa nasoma taarifa hapa lile ghala la Ngusero ambalo liko chini sana asilimia 16 na anajua kwa nini iko hapo kwa sababu ya mkandarasi aliyekuwepo, Mheshimiwa Waziri a-push ili tumalize hili ili wananchi wa Kiteto wakapate kuhifadhi mahindi. Kiteto ripoti zake ukizisoma ile post-harvest loss ni karibu 40%, kwa hiyo hii itatusaidia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana pia Mheshimiwa Waziri, wananchi wa Kiteto wamefarijika sana kwa kilo 25,000 alizogawa za mbegu ya alizeti. Big up kwake, wananchi kwa kweli wamefarijika sana. Nakushukuru vilevile kwa kazi inayoendelea sasa ya kuhamasisha watu kuhusu alizeti. Kwa kweli tumeshajiwekea mkakati kama Taifa kwamba ili tuweze kupata mafuta ya alizeti hapa nchini, ni lazima tupate mbegu nzuri na vilevile wananchi wa Kiteto wako tayari…

TAARIFA

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe taarifa mzungumzaji kwamba Mheshimiwa Waziri asithubutu kuruhusu GMO. Akiruhusu GMO ataua kilimo chetu kwa sababu tutategemea teknolojia ya kigeni, ni unyonyaji kwa wakulima na tutapoteza asili ya mimea. Kwa hiyo Waziri asiruhusu kabisa suala la GMO kwenye nchi yetu ya Tanzania. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ole-Lekaita, taarifa hiyo unaipokea?

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa sijaongelea mambo ya GMO, but I agree with her. Ni kweli alishasema Mheshimiwa Waziri hapa siku moja na biashara ya GMO ni biashara kubwa sana, ina issues nyingi sana, inahitaji mjadala mkubwa wa kitaifa, kwa hiyo nakubaliana naye sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nazungumza kuhusu Kiteto na jinsi wakulima wangu walivyo tayari kwa ajili ya kuzalisha mafuta na mbegu za alizeti. lakini wanachotaka ni kitu kimoja tu, Serikali iweke mkakati tujue price ya alizeti ili tuhamasike tujue kabisa projection ya prices mwakani zikoje ili wananchi waweze kuhamasika. Nadhani tukifanya hivyo itamshawishi kila mtu na ataingia kwenye kilimo hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana kwenye hotuba ya bajeti ya Mheshimiwa Waziri, ukurasa wa 130, walisema walikuwa na nia ya kuwawezesha vijana 400 katika mikoa tisa na Manyara ikiwemo. Nilipiga mahesabu ni karibu vijana 45 kila mkoa na ukipiga mahesabu ya wilaya zile Kiteto ilikuwa inapata vijana sita sio chini ya sita. Sasa nataka Waziri atujibu hili wameshalifanya kwa sababu sisi Kiteto hatujasikia popote, vijana wale sita ambao walitakiwa kuwawezesha kuwapa zana hizi, nataka nisikie kwenye hitimisho. Tusije tukakaa tunapitwa, kwa hiyo please, comment on this.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii inaongelea sana kuhusu umwagiliaji na ni kweli is a shame as a country kwamba projection ukiangalia data za umwagiliaji tuko chini sana, less than 2. 5 %...

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

TAARIFA

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumpa taarifa mzungumzaji kwamba pamoja na hao vijana ambao wamemtaka Mheshimiwa Waziri katika hitimisho lake aseme chochote, wako vijana kwa ushirikiano wa Tanzania na Israel kila mwaka kama 100 wanaenda Israel kujifunza mambo ya kilimo lakini wakirudi hapa wanabaki idle.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ole-Lelekaita, taarifa hiyo unaipokea?

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, napokea.

MWENYEKITI: Malizia, dakika moja.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kwa sababu ya muda naendelea kuzungumzia kuhusu suala la umwagiliaji. Ni kweli wameweka pesa nyingi kutoka bilioni 17 mpaka bilioni 51, fine, lakini tunapoteza maji mengi sana wakati wa mvua, tusipofanya hii, nadhani tungekuwa na like a rapid fund fulani ili mvua zinapotokeza tusipoteze maji kwa ajili ya umwagiliaji. Tukifanya hivyo tukawa quick itatusaidia tusipoteze maji mengi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda, niishie hapo lakini kwenye umwagiliaji vilevile kama tunataka kufanya vizuri zaidi, mashine zile zinazotusaidia kwa ajili ya umwagiliaji, Mheshimiwa Waziri apiganie ili kodi ziondoke ili wananchi wapate encouragement.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa kabisa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi. Kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Rais kwa Tuzo ambayo Azimio la Bunge leo limepitisha. Nilifurahi sana kilichoandikwa kwenye tuzo ile, nanukuu: “The First Female President in East Africa Region, the only Female President in Africa for 2022, for your dedicated services that proves the women ability.” Mheshimiwa Waziri nikupongeze sana, tunataka tuone the women ability kwenye Wizara hii ya Ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza pia Naibu Waziri, Wakili Msomi Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete. Combination of the women ability na Wakili, tunatarajia kwa kweli Wizara hii migogoro tunayoisikia kutoka kila mahali itapata majawabu. Kwa kweli niwatie moyo, haya mnayoyasikia kutoka huku, tunawaambia tu kwamba kazi iliyo mbele ni kubwa zaidi, but we will support you. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Dkt. Allan Kijazi, very humble na uzuri ametoka Wizara ya Maliasili na Utalii, na anajua kelele nyingi zilikuwa zinatoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa sababu ya migogoro mingi ambayo ipo. Kwa hiyo, sasa hii timu, with that experience, kwa kweli tunatarajia mengi zaidi na migogoro hii itapungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ilileta mapendekezo ya sheria tumepitisha mwaka jana, na kwa kweli wameleta maboresho makubwa sana kwenye sheria ile ya migogoro kwa kupunguza nguvu za Mabaraza ya Kata ili waweze tu kusuluhisha tu migogoro kwa sababu ilionekana walikuwa wanafanya ambavyo sivyo kisheria. Wao wabaki kusuluhisha halafu Mahakama zile za ardhi zenye watu ambao wana uelewa wa kisheria wafanye kazi nzuri zaidi. Kwa hiyo, natarajia hayo yatakuwa ni mapinduzi makubwa yenye kuleta harmony kwenye migogoro ambayo ipo sasa. Pia walibadilisha sheria na Bunge hili lilipitisha sheria kuruhusu Kiswahili kitumike. Hii itasaidia wananchi kufuatilia hukumu zao kwa Lugha nyepesi kabisa wanayoifahamu. Big up. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa lililozungumzwa hapa ni la migogoro. Ni kweli tuna migogoro mingi sana vijiji kwa vijiji, mipaka ya vijiji na Hifadhi za Taifa, wakati mwingine mikoa kwa mikoa kubwa sana, na tunashukuru sana. Ni kweli waliompongeza Mheshimiwa Lukuvi, kwa kweli tunatambua sana kazi yake aliyoifanya kubwa. Nakumbuka walikuja Mawaziri nane kule kwangu kule Kiteto Kijiji cha Arkyush kwa mgogoro ambao umedumu kwa miaka 20 kwa Pori la Mkungunero na vijiji. Kwa kweli inashangaza sana kwa sababu GN iko clear sana na Mheshimiwa Rais Hayati Mkapa alisaini mwaka 1996, lakini eti ramani ambayo inachorwa na Maliasili na Utalii ndiyo inasema ile ramani ina-extend kwenda Kiteto. It is a bit funny kwamba ramani eti GN iliyosainiwa na Rais zinapishana, lakini hii yote inatokea kwa sababu wale walichora ramani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Ardhi msiruhusu mtu yeyote nchi achore ramani yake. Sheria iko clear sana, ninyi ndio custodian wa ardhi nchi hii. Mkishatutawanyishia mkasema hii ni ya Kijiji, hii ni ya Hifadhi, hii ni general land, ninyi mnabaki kusimamia. Mwenye shida yoyote anakuja kwenu. Siyo mtu anataka ardhi ya Kijiji, anachora ramani mwenyewe, anapeleka GN mwenyewe, haiwezekani. Msiruhusu tena. Najua migogoro mingi mnayopata ninyi inasababishwa na watu wengine. Kwa hiyo, mkisimama firm ninyi ndiyo custodian wa ardhi nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Kifungu cha 181 cha Sheria ya Ardhi, inasema, leo tukitunga sheria nyingi nyingi kidogo, ikatokea mgongano wa sheria hizi, on lands’ matter Sheria ya Ardhi takes precedent on lands’ matter. Kwa hiyo, wakati mwingine sijui migogoro inatokea wapi? Inatosha kwa Waziri wa Ardhi kusema Hapana. Akishasema hapana definition inayotokana na Sheria ya Ardhi ndiyo inakwenda hivyo. Siyo Sheria ya Wanyamapori. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwingine kijiji kipo miaka 20, Wenyeviti wamechaguliwa miaka 20, TAMISEMI inatambua, ina CVL lakini kuna mabingwa wengine wanakuja wanatengeneza ramani wanaingiza kwenye vijiji halafu inaanza migogoro. Nadhani migogoro hiyo muihamishe kutoka field ije kwenye Ofisi zetu hapa. Waje kwenu mkae TAMISEMI, Ardhi na Maliasili. Kaeni mnyongane Ofisini huku, but don’t bring the confusion kwa wananchi, kwa sababu hakuna mwananchi anachora CVL ni Taasisi za Serikali wala hakuna Kijiji kinachojiandikisha chenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, this time Mheshimiwa Attorney General ambaye namheshimu sana, I think is the only man ambaye amekuwa DPP akaenda Judiciary na sasa Attorney General. Sometimes migogoro inazuka, unakwenda Mahakamani, unashindwa ku-enforce eti kwa sababu unakuta ng’ombe, bingwa mwingine kauza na kesi inaendelea Mahakamani, tusikubali. Jana Mheshimiwa Mbunge wa Morogoro Kusini aliongea vizuri sana na naomba niwashawishi Wabunge hapa; hapa tumeletwa na wavuvi, wakulima na wafugaji. Ikija issue inayomgusa mkulima, mfugaji na wavuvi tusimame, wala hakuna Mbunge hapa ambaye ana wafugaji peke yake kwenye Jimbo lake, wala hakuna mkulima ambaye eti ana wakulima peke yake kwenye Jimbo lake. Sisi wote ni viongozi tusimamie migogoro hii bila kuvuta upande wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nawapongeza wananchi wangu wa Kiteto. Kiteto imetulia sasa, lakini bado kuna vitu kidogo kidogo hivi; mara mfugaji ameingiza ng’ombe shambani, unaambiwa kuna mkulima ameingia kwenye maeneo ya kilimo. Hiyo ipo kidogo kidogo, lakini to be exact, imetulia. Nawapongeza sana wananchi wangu wa Kiteto. Nami nawaambia kupitia Bunge hili, mimi sina mtoto wa mgongoni na wa kifuani; wakulima, wafugaji wote wanaoishi Kiteto ni wa kwangu. Wote nawaomba mwendelee kutulia hivyo hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Ardhi, Mifugo na Wanyamapori, tulikuwa tunaongea hapa na yule Mbunge wa Morogoro Kusini, migogoro hii siyo ya kwenu peke yenu. Mkitengeneza maeneo hotspots yenye migogoro, mkatengeneza ma-champion Wabunge hapa Bungeni, tutasaidiana tuende tuelimishe wananchi wetu na migogoro hii itapungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesoma ripoti ya Kamati hapa na kwa kweli Wizara imekuja na very ambitious plan kwa kweli nzuri sana, wanataka kupima asilimia 50 ya Kijiji, lakini Tume ile ya Matumizi Bora ya Ardhi wana upungufu wa Shilingi bilioni tisa. Kwa kweli tuwasaidieni. Mheshimiwa Sillo rafiki yangu Kamati ya Bajeti hebu mtafute Shilingi bilioni 10 muwezeshe hii Tume ya Matumizi Bora ya Ardhi ili Vijiji vipimwe. Vijiji vikipimwa, migogoro itapungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwashawishi wote kwa kweli tupitishe bajeti hii ya Wizara hii wakafanye haya yote ili mwakani tukutane hapa wakati tuna furaha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nakushukuru sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwa bajeti yake ya kwanza ambayo ni nzuri sana. Nampongeza pia Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, mwananchi; Mheshimiwa Naibu Waziri, Bwana Shemeji; na timu yote ya Wizara hii ikiongozwa na Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Wataalam wote kwa kazi nzuri ambayo mmefanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti hii tunaipongeza kwa sababu ifuatayo: Moja, kuhusu kilimo. Kilimo fedha imeongezeka sana, shilingi bilioni 954. Ni ongezeko la Shilingi bilioni 660 ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2021. Pia bajeti hii imezungumza kuajiri vijana 3,000,000 wa kilimo na itatenga karibu hekta 8,500,000 kwa ajili ya umwagiliaji. Vile vile wanazungumza habari ya kuanzisha viwanda vya saa 24. Twenty-four hours a day na seven days in a week, hii itaongeza kasi ya ajira. Kwa hiyo, kwa kweli ni nzuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kuhusu mifugo, mmezungumka habari ya kuongeza bajeti ya mifuko kwa shilingi bilioni 40 zaidi. Pia kuhusu TASAF, kuanzisha dirisha maalum kwa ajili ya vijana wanaotokana na familia ambazo zimejiandikisha kwenye TASAF, itaongeza sana sana sana ari ya wananchi. Kwa kweli vijana hawa wamekuwa wanateseka sana, hawawezi ku-compete. Usipowawekea dirisha maalum la kwao kwa kweli hasingeweza ku-compete kupata mikopo ile. Kwa hiyo, big up. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye sekta ya mifugo mmezungumza habari ya kuanzisha incubation centers na kuajiri vijana 1,000 wawe na miradi ya kunenepesha, very nice. Ila nina angalizo vilevile baada ya pongezi zote hizo. Kuhusu tani za vyakula vya mifugo; Ilani ya Chama cha Mapinduzi Mheshimiwa Waziri wa fedha I hope unanisikiliza. Tulisema hivi ukurasa wa 52, tani za vyakula vya mifugo ni 8,000,000 kwa miaka mitano, lakini kwa trend sasa tumetoka 900,000 tukaenda milioni moja, na tani laki mbili, na sasa tunazungumza habari ya milioni mojam tani laki tatu na themanini. Kwa hiyo, tukiendelea kwenda na trend ya laki mbili, laki tatu hatutaweza kufikia tani milioni nane. Kwa hiyo, in average actually ilitakiwa kwa miaka mitano kuwe na average kila mwaka tuongeze tani 1,420,000. Kwa hiyo we are not doing so well. Kwa hiyo, tujaribu kuongeza bidii ili tufanye vizuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nimefurahi sana kuona VETA kuna fedha zimetafutwa kwa ajili ya VETA na Mheshimiwa Waziri mimi niliuliza swali la kwanza Bungeni hapa, namba 13 kuhusu Kiteto kutokuwa na VETA. Majibu niliyopata kutoka Wizara husika wanasema wanatambua Kiteto haina VETA, lakini itakuwa kwenye priority list. Wakileta zile lists zao la VETA 36, Kiteto isipokuwepo usi-approve huo mradi, kwa sababu majibu tuliyowapa wananchi ni kwamba lazima Kiteto iwepo, lakini kwa sababu mmesema mtajenga kwenye Wilaya zote ambazo hazina, Kiteto I am sure itakuwepo tena inatakiwa iwe namba moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo, naomba sasa nizungumzie kitu kinachoitwa carbon credits ambayo ndiyo msingi wa hotuba yangu leo. Carbon credit ni new source ya finance ambayo itaiongoezea nchi mapato zaidi. Kwa Afrika nzima, Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa na eneo kubwa lenye mapori, baada ya DRC na Angola. Kwa hiyo, potential ya carbon credit kwa Tanzania ni kubwa zaidi, na kuna study zimefanyika na natural conservancy zinaonesha kwamba tangu Tanzania mmeanzisha mradi wa Red Plus Project na Tanzania imekuwa pioneers, tumeanza kufanya vizuri na tumeanza kuvuna fedha zinazotokana na carbon credit. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukimwuliza Mheshimiwa Kakoso kule kwao, Mbunge wa Mbulu kule kwao na Kiteto vile vile, sisi tumeanza miradi ya carbon credit na kwa kweli inasaidia sana wananchi. Nilitoa mfano siku moja hapa kwamba Kiteto, internal revenue ni 2.2 billion, lakini sisi baada tu ya kuanzisha mradi wa carbon, vijiji vitano tu vinatengeneza one billion a year. Kwa hiyo, sasa tunge-utilize vile vijiji vyote, maana yake carbon credit ni new financing area ambayo ni lazima Wizara ya Fedha, Wizara ya Makamu wa Rais, Mazingira, na Wizara ya Viwanda na TRA lazima sasa mje strongly mtengeneze policy.

Mheshimiwa Naibu Spika, alipokwenda Rais wetu kwenye baadhi ya safari za Kimataifa alisema hivi, baadhi ya wawekezaji, yaani wawekezaji wanaokuja kwa wingi sana ni watu wanaokuja na miradi ya carbon credit. Kwa hiyo, mtegemee kupata watu wengi sana wa carbon credit. But it is a shame, we don’t have a law and we don’t have a policy. Hakuna mtu atakuja hapa bila kuwa na framework na legislation for certainty purposes. Kwa hiyo, ni lazima sasa muanze ku-speed.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Bunge hili, Mheshimiwa Mbunge wa Vunjo Dkt. Kimei aliuliza swali hapa la cardon credit, Mheshimiwa Mbunge wa Kilolo aliuliza vile vile, lakini majibu tunayoyapata hapa, tunaambiwa bado Serikali inatengeneza policy. Honestly! Six years, ten years down the line? Mheshimiwa Rais anawaleta watu sasa waje kwa ajili ya wawekezaji...

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Taarifa.

T A A R I F A

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika, sina nia ya kumvurugia mtitiriko Wakili Msomi, lakini naomba kumpatia taarifa kwamba kupitia mifuko mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi kama Adaptation Fund, Climate Fund na kadhalika, tungeweza kunufaika sana, lakini nchi yetu ina taasisi mbili tu ambazo zimekuwa accredited ambayo ni NEMC na CRDB na hizi fedha nyingi na grants, wala siyo mikopo. Kwa hiyo, naomba kumpa hiyo taarifa. Nchi kama Kenya ina taasisi 18, sisi tunazo mbili tu wakati hii ni fursa kubwa sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kisau.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na nakubaliana na mchango mzuri sana huo, sana! Kwamba hii biashara ya carbon credit siyo tu kwamba ni biashara as business per-se, lakini pia inaongezea nchi fursa za kupata climate change financing. Kwa hiyo, ni lazima tujikite zaidi kutokana na biashara hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, in fact, tunaambiwa tuna mapori between 48 to 50 million hectors nchi hii zipo protected. How much we get it for this forest? Ni rasilimali iliyopo, in fact watu wengine wanasema ni business for doing nothing. Yaani mapori yapo tu, which is good for climate na itakuletea mvua, acha kukatakata mapori, halafu utapata cardon financing. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi zinazoongoza sasa duniani on cardon financing na wanao-produce carbon, ya kwanza ni India; ya pili, Marekani; ya tatu, ni China; ya nne, Indonesia, Peru, Kenya, Brazil, Guatemala, Uganda and Zimbambwe. Zinazoongoza kununua, market ni United States, France, United Kingdom, German and Switzerland. Kwa hiyo, najua hii carbon financing ni new area hata Wabunge wengi hawafahamu. Naomba hata Bunge litafute mjadala wa siku moja ili Wabunge wafundishe Habari ya carbon financing. It is a new sources of funding ili tuje tupate mjadala, wataalam waitwe, waje watufundishe ili nchi sasa ianze kukimbia mbele zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Afrika kwa mfano, projects ambazo zimekuwa registered on carbon financing ni miradi karibu 234. Asia and Pacific 6,580; Europe and Central Asia 89; Latin America 1,139; Middle East ni 87 ambazo ni worth 190 billion USD, ni fedha nyingi sana. Tusiache Mheshimiwa Waziri hii ni gold ambayo imekaa ili tuweze kui-utilize.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya, nakushukuru sana, ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MHE. EDWARD K. OLELEKAITA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii na kama walivyosema wenzangu niwape pole sana Wabunge kwa msiba wa Mbunge mwenzetu Engineer Nditiye, tunamuombea Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema peponi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa muda ni mdogo sana naomba nichangie hoja hii kwa kusema hivi Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020/2025 imetaja Kiswahili mara 39 namna tunavyotaka kutumia Kiswahili kwa mustakabali wa Taifa letu. Ukurasa wa 17, 130, 167, 168, 184, 185, 186, 244, 246, 247, 268, 286,287 na 288. Ukisoma Ilani ya Chama cha Mapinduzi utaona Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alivyofafanua namna tunavyotaka kutumia Kiswahili, kwa Muswada huu utatusaidia kama Taifa kuanza kubadilisha sheria zetu kwa lugha ya Kiswahili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na nikinukuu tu kwa ruhusa yako ukurasa wa 167; “Kuongeza uwelewa wa wananchi kuhusu sheria mbalimbali kwa kutafsiri sheria 157 kutoka lugha kiingereza kwenda ya lugha ya Kiswahili.” Kwa hiyo, takwa hili la kubadilisha sheria kwenda Kiswahili ni kwa mujibu ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama walivyokwisha kutangulia wengine Kiswahili kwa Taifa letu inatambulisha Taifa, Kiswahili kimetumika katika ujenzi wa Taifa letu hata wakati tunatafuta uhuru Kiswahili kinaleta utamaduni wa Taifa letu. Kiswahili ni sawa sawa na uzalendo, ukombozi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiswahili ni tunu ya Taifa letu. Kwa hiyo, tumpongeze sana Mheshimiwa Rais ni wakati sasa wa muafaka tuanze kuzungumza Kiswahili kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tafiti nyingi zinaonesha nchi nyingi sana Finland, Ireland, Bangladesh, Malaysia, Hong Kong, Hong Kong ilifika mahala wakaanza kuandamana nchi nzima wanakataa kiingereza kisitumike kwa sababu waliokuwa wengi Hong Kong wanazungumza chinese sasa sisi tumeanza hata hata kabla ya Watanzania hawajaanza kuandamana. Lakini sababu nyingine kimsingi sana ya kisheria ni haki ya mtu kufahamu lugha ya mashitaka kwa kiingereza wanaita due process, huwezi kumshitaki mtu ukaleta hati ya mashitaka kwa lugha ya kigeni, haelewei.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nyingine kuna kitu kinaitwa kwa kisheria uhalali wa lugha inayotumia (legitimacy) Watanzania wengi wanaongea Kiswahili kuendelea kuwa na sheria zilizoandikwa kwa lugha za kigeni ni kukosesha legitimacy sheria zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiwa na lugha ya Kiswahili kwenye sheria zetu, kwanza inajenga uelewa, vilevile inaleta watu kuheshimu sheria kwa sababu wanafahamu sheria kwa Kiswahili, wanafahamu lugha tuliyoandikia sheria. Lakini ukileta sheria zilizoandikwa kwa lugha za kigeni tutakuwa tunawasumbua Watanzania wasipo fuata sheria kwa sababu lugha hiyo imeandikwa ni ya kigeni. Kwa hiyo inaleta obedience, inaleta respect kama unaelewa lugha hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Muswada ulio mbele ya Bunge umeandikwa kwa kiingereza na kanuni zetu zinachanganya by the way na hukumu zetu sasa kama alivyosema Mwenyekiti wa Kamati zimeshaanza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili, kwa hiyo mabadiliko ya sheria yatarahisisha sana kazi hii ya tafsiri ya sheria zetu ziende kwa lugha ya Kiswahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama walivyokwisha kusema wengine nchi zinazozungumza Kiswahili sasa ni Rwanda, Uganda, Burundi, South Sudan, sehemu ya Mawali, Somali, Zambia, Mzumbiji, DRC na Visiwa vya Comoro. Kwa hivyo Kiswahili tayari kina soko kubwa sana ni zaidi ya watu milioni mia mbili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya, nakushukuru sana na ninaunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 2) wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Nishukuru pia kwa kuwa mchangiaji wa kwanza kwa Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, lakini kabla ya yote niwashukuru sana Wabunge kupitia ule Mfuko wa Faraja kwa support waliyonipa nilipompoteza mzee wangu. Tuendelee kumuombea alale mahali pema peponi.

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mwenyekiti wa Kamati yetu ya Katiba na Sheria kwa umahiri mkubwa sana. Sisi ambao tunafanya kazi naye na Wajumbe wenzangu watakubaliana nami kwamba tuna-enjoy leadership yake nzuri sana. Vilevile niwapongeze Wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria; nikupongeze, sijui ulitumia nini kuitengeneza timu hii ya Katiba na Sheria, tuna-enjoy sana, it’s a very good team, inaongozwa na Mawakili maarufu sana kama Senior Counsel Tadayo, ana miaka karibu 40 ya practice. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile niwapongeze wadau waliokuja kwenye Kamati ya Katiba na Sheria. Kwa kweli tulijifunza mambo mengi sana kwa wadau wale. Alikuja kijana mmoja mwanasheria kutoka Tangible Initiative anaitwa Kulwa William Mduhu, very young, very brilliant. Tulijifunza mambo mengi sana kupitia kwake na wadau wengine waliokuja kwenye Kamati yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hii inasisitiza tu kama tulivyosema kwenye ripoti ya Kamati kwamba Serikali ihakikishe kwamba inawashirikisha wadau katika marekebisho ya sheria mbalimbali. Tunajifunza mambo mengi sana kutoka kwa wadau. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna mambo mawili au matatu hivi niweke mkazo kwenye ripoti yetu. Nimpongeze Attorney General, Wizara ya Katiba na Sheria na CPD kwa kweli kwa ushirikiano mkubwa waliotoa wakati wa majadiliano kati ya Kamati na timu ya Serikali. Kama alivyosema Mwenyekiti wetu, kati ya vitu ambavyo tulizungumza ambapo kwa kweli msingi wake tulikuwa tunaufahamu, frustration wanayopata Makatibu Wakuu pale ambapo bodi hazipo na amendment iliyokuwa inaletwa ilikuwa ni kujaribu kuongeza muda ili kazi zisikwame lakini baada ya majadiliano tukasema na ni msingi tu wa kisheria kwamba hatuwezi kuongeza muda kwa sababu itakuwa ina-conflict sasa kazi za bodi zikiendelea kufanywa na mtu mmoja for an unlimited time. Kwa hiyo, baada ya mashauriano wakaamua ku-withdraw; that is excellent. Kwa hiyo, nawapongeza sana kwa kukubaliana na Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya Sheria ya Mawakili ni fursa nzuri sana kwa Mawakili kwa kuwaruhusu Mawakili kwenda kwenye Mahakama za Mwanzo. Mwaka 2016 Bunge lilileta mapendekezo ya kuongeza pecuniary jurisdiction ya property, kusema sasa kwenye Mahakama za Mwanzo unaongeza thamani ya kesi ambazo zinaweza zikasikilizwa na Mahakama za Mwanzo na fear ya mawakili that time ni kama sasa mnawanyang’anya kazi kwa sababu hela nyingi sasa zinakwenda Primary Court na Mawakili hawaruhusiwi kwenda. Kwa hili, I am sure Mawakili watakuwa excited kwamba sasa wanakwenda kwenye Primary Courts, zile kazi ambazo zilikuwa zimefungwa by restriction of law sasa watakwenda, that is excellent.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba tunaleta huduma karibu na wananchi ili wapate fursa ya kusikilizwa na kupata uwakilishi wa Wakili kwenye Primary Courts, mapendekezo haya vilevile yanazungumzia kutengenezwa kwa Bodi hizi za Mikoa zinazo-discipline advocates ili ku- protect society from advocates lakini vilevile ku-protect advocates kwa kuleta process ya kusikiliza zile kesi na malalamiko ya mawakili.

Mheshimiwa Spika, lakini wakili akiwa na cheti chake tukafikiri decision ya kusema sasa huyu wakili hafai na kwamba cheti anyang’anywe isifanywe na Kamati za Kimkoa kwa sababu kwanza composition ya Kamati zile na ile ya Kitaifa ni tofauti. Quality ya watu walioko kwenye National Committees ni Attorney General, DPP na ukiangalia sasa na composition ya wale wa mikoa ambao ni Registrars tusifanye kwamba ni rahisi sana hivi vyeti vikaondolewa kwa sababu watu wamehangaika na kwa kweli lazima viwe protected ziendelee kufanya kazi nyingine hizi za usuluhishi na mwisho wa siku wananchi wawe protected ile kuondoa cheti ibaki kwenye National Committee. Kwa hiyo, I think it is an excellent provision.

Mheshimiwa Spika, suala la nidhamu ni lazima kwa kweli liwe controlled. Hakuna profession ambayo watu wanaweza wakafanya watakalo. Kwa hiyo, kuwa na hizo Disciplinary Committees zitasaidia sana kuondoa malalamiko kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, baada ya marekebisho haya kuna mambo mengi yatabadilika. Nilikuwa naangalia Cheti cha Wakili kikishatengenezwa huwa kinaandikwa hivi na ninaomba ninukuu, kinasema kwamba: “Is an Advocate of the High Court and before the Court’s subordinate thereto save for Primary Courts”

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tumesema Mawakili watakwenda kwenye Primary Courts, Wizara sasa iweke regulations in place ili vyeti vya mawakili from next year iondokane na hilo sharti ili lisilete mapingamizi ya kisheria baada ya sheria hii kupita kwa sababu atakuja mtu ana certificate of practice lakini imeandikwa is an advocate of the High Court and Court’s subordinate thereto save for primary courts. Kwa hiyo, naomba suala hilo lishughulikiwe ili lisilete mkanganyiko wa kisheria.

Mheshimiwa Spika, Kamati imesisitiza kwamba wakati mwingine sheria inatoa mamlaka kwa mamlaka za chini kutengeneza regulations fulani fulani na sisi tukasisitiza kabisa kwamba wakati mwingine hizi mamlaka za chini zijue kabisa kwamba jukumu la kutunga sheria ni la Bunge, kwa hiyo, ziwe very careful kuangalia sheria mama ili wasilete lawama kwa Bunge.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa naangalia pia Amendments ya Sheria ya The Land Disputes Courts ya kuruhusu sasa wale Wenyeviti wawe Public Servant na nilikuwa naongea na Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, kwamba Kiteto haina Mwenyekiti, akaniambia tatizo ni hili. Sasa baada ya amendments hizi, naamini Kiteto sasa na wilaya zingine itakuwa mandatory kuwa na hawa Wenyeviti.

Mheshimiwa Spika, nina kitu kidogo tu, siku hizi ukisoma sheria hiyo na inasema na hii sasa inapelekea sheria zetu, siku hizi kuna mjadala unaitwa making laws work for women and men ama gender sensitive legislation. Ukiangalia kifungu kile kinaendelea kusema Chairman, and so on, sasa isituletee mkanganyiko tukafikiri kwamba wanaostahili kuwa Wenyeviti ni wanaume peke yao. Kwa hiyo, hiyo ili tuangalie isije ikaleta nanii fulani hivi.

Mheshimiwa Spika, mabadiliko haya ya sheria yatawezesha mabadiliko makubwa sana na yataleta haki kwa wananchi na yatafanya wananchi wafurahie haki hizi ambazo zimeletwa na mabadiliko ya sheria.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, nashukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (Toleo la Kiingereza)
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Nimpongeze Waziri wa Fedha na Naibu wake na timu nzima kwa kuleta hotuba nzuri inayohusiana na The Finance Bill.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianzie kwenye Mabadiliko ya Sheria ya Kodi, section 23 ya Finance Bill ambayo watu wengine walikuwa wanazungumzia hii kodi hii ambayo ni two percent withheld kwa mazao yanayotokana na kilimo, mifugo na uvuvi. Nawapongeza Kamati ya Bajeti ambayo wameichambua sana na hata wao wameona. Kama alivyosema Mheshimiwa Waziri kwenye hotuba yake nia sio kumtoza mkulima ama mfugaji au mvuvi lakini sasa sheria haiko clear kum-protect mtu huyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu amendments zime-define a resident cooperation, pale anaponunua vitu kutoka kwa mtu anayeitwa a resident person. Sasa a resident person is not defined. Sasa isipoangaliwa vizuri inawezekana baadaye huyo resident person aka-include mkulima, mfugaji na mvuvi. Kwa hiyo, kwa jinsi mlivyo-define hiyo resident cooperation ni vizuri pia m-define a resident person huyu sasa ambaye anauza kama mlivyo-define vizuri kwamba resident cooperation hai-include SACCOS, AMCOS na vitu vingine. Nahofia tusije tukajikuta kwamba yule ambaye tulitaka kum-protect is not protected. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naangalia hotuba ya Mheshimiwa Waziri hapa, kuna paragraph ambayo is not clear kwenye hizi amendment na nia yake ilikuwa ni nzuri sana. Kuondoa sharti lile linalomlazimisha mlipa kodi ambaye anataka ku-object ile assessment la kulazimishwa kulipa one third kama alivyosema Mheshimiwa Waziri, ukurasa wa 13 wa hotuba yake. Sasa ukiangalia sasa Sheria ya Kodi, section 51 ambayo ndio inaleta sharti hilo haipo kwenye amendment.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni vizuri pengine muangalie kama nia ilikuwa ni kuondoa sharti lile kwa sababu nilielezea vizuri sana siku ile, ukasema ni kweli mtu anaweza aka-inflate ile tax. For example, one third of 30 billion is too much. Kwa hiyo, ni kweli kama sharti ilikuwa ni ku-relax hii, basi muangalie section 51 kwa sababu ndiyo inayozungumzia masharti hayo na haiko kwenye amendment. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia pia kwenye Kamati na Schedule of Amendment iliyoletwa na Serikali, kulikuwa na wazo la kumfanya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ku-audit mashirika ambayo Serikali ina more than 50 percent share na inaonekana Kamati na Serikali wamekubaliana. Hata hivyo, ukiangalia ile Finance Act definition iliyokuwa inatolewa kwa public authority imekuwa extended Zaidi, imekuwa more broaden ku-include vitu vingi sio share peke yake, kuna vitu vingi sana vimeongezwa pale ambavyo actually ina-justify sasa kwamba hata anaweza aka-audit yale ambayo hata kama Serikali haina 50 percent share.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kuna haja ya kufanya re-alignment kuangalia exactly intention ilikuwa ni nini. Kwa sababu unavyo-broaden definition ya public authority ku-include vitu vingine beyond ile 50 share, maana yake unakaribisha sasa intention ya ku-audit hata zile nyingine. Kuna Mheshimiwa Mbunge alisema hata pale tunapoweka dhamana kwa miradi hii ambayo tuna ubia na watu wengine regardless ya share it is good iwe-audited na I think hii amendment ilikuwa inajaribu ku-cover more broadly vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu nyingine ambayo nilitaka kugusia kidogo ni TARURA. Kuna hili suala la TARURA ambapo tunawasifu sana na hata mlivyoweka kwenye amendment ya kifungu kile ni nzuri sana. My own concern ni moja, unajua tulishasema hivi tunahitaji fedha nyingi sasa ziende TARURA, kwa hiyo, hatulindi ile 100 peke yake mnayoongeza kwenye mafuta, tunataka pia ku-revisit ile formula ya TANROADS na TARURA ambayo imekuwa ni 30 percent na 70 percent ambayo tulisema it is unfair.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Mbunge nilikuwa naongea naye akaniambia in fact kwa kuwa tuliwapa mzigo mkubwa sana TANROADS kwa sababu walikuwa na kazi ya kuunganisha mikoa mingi na hiyo kazi imepungua actually, imebaki tu sasa barabara ya Kiteto, Dodoma, Arusha, Tanga, Manyara na Kigoma na sehemu zingine chache sana. Kwa hiyo, it is high time na kwa kuwa Ilani yetu inazungumza kwamba tureje formula ile ya TANROADS na TARURA, hizi amendment tunavyoenda kuzifanya ni vizuri Mawaziri wale wakaja pia na formula sasa, sio tu ku-protect hii one hundred ambayo tunaweka kwenye mafuta lakini kuangalia sasa ile formula ya Mfuko wa TARURA na TANROADS ili Mfuko huu uwe na fedha nyingi zaidi ili barabara za vijijini ziendelee kuwa nyingi zaidi. Kwa hiyo, ni vizuri muangalie kwenye amendment hiyo ili fedha ziweze kupatikana zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ambacho nimekiona kuna amendment ambayo nia I think ilikuwa ni njema, pale mnaposema mnataka ku-defer 12 months kabla ya ku-impose ile restriction ya yale makampuni kuwa na saver. Section 64 mnasema kwamba amendment inayohusiana na primary saver na sub-section (8) na (10) zinakuwa deferred zianze kufanya kazi 12 months later.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, huko mbele tena section 71 mnataka kuleta offence kwa mtu ambaye ata-fail ku-maintain ile primary saver. Sasa kama una-defer hizi sub-sections tatu maana yake ni kwamba hata hii section 71(m) ambayo ina-impose offence kwa yule ambaye ata-fail kuweka ile primary data saver lazima pia iwe deferred. Otherwise mtaleta confusion mna-defer section zinazo-put obligation kwa mtu kuwa na hiyo primary data lakini yule ambaye hatakuwa nayo unataka kum-punish even before 12 months ambayo ulitaka ku-defer. I think it is a drafting issue, ni issue tu ya ku-realign ili ikae vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo machache sana, nakubaliana na amendments hizi, I think nia ni njema sana na imekubaliana na mawazo mengi sana ya Wabunge. Nakushukuru sana. (Makofi)
THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) (NO. 5) ACT, 2021
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza kabisa nimpongeze Mwenyekiti wa Kamati na Wajumbe wote. Pia nimshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali, CPD na Wizara ya Sheria.

Mheshimiwa Spika, nitachangia mambo machache sana. La kwanza labda ni-clarify hii issue ya Kikatiba.

Mheshimiwa Spika, Ibara hii inayozungumzwa ya 147(4), mimi sijui hata kwa nini watu wanajadili kwa sababu, sisi tunazungumza habari ya majeshi. Ibara hii Waheshimiwa wanazungumza hapa ni definition ya mwanajeshi ambayo ni vitu viwili tofauti. Kwa hiyo, nadhani hii iishie hapa, lakini kwa wanaotaka kujifunza zaidi wasome Ibara ya 151, definition ya neno Askari, wataelewa zaidi likitumika kuhusiana na jeshi. Naomba ninukuu:

“…likitumika kuhusiana na jeshi lolote, maana yake ni pamoja na askari yeyote ambaye kwa mujibu wa amri ya jeshi hilo ni mtu anayewajibika kinidhamu.”

Mheshimiwa Spika, hizi ni terminologies. Unajua watu wasifikiri kila kitu kilichoko kwenye Katiba unaweza ukasema is unconstitutional na nitakupa tu mfano huko mbele ili Wanasheria waweke hii sawasawa. Huwezi kusema sheria hii is unconstitutional kwa sababu haina rangi ya Katiba, tunafahamu hii rangi ya Katiba, si ndio?

Mheshimiwa Spika, huwezi ukasema sheria hii is unconstitutional kwa sababu haina page numbers pamoja na kwamba, Katiba ina page numbers. Kwa hiyo, hili tumezungumza habari ya jeshi, sasa watuambie kama ile ibara inazungumzia jeshi ama mwanajeshi? Sasa sisi hatuzungumzi habari ya definition ya mwanajeshi, hatuzungumzi. Hilo moja.

Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Mwinyi pale, sasa naogopa kusema Wakili Msomi Mwinyi. Alichosema ni kwamba…

SPIKA: Unaruhusiwa Mheshimiwa.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, sawa, kumbe naruhusiwa, nashukuru.

SPIKA: Kabisa. Nimeshaelimishwa kwamba, ni wasomi. (Kicheko)

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Ni kweli, unajua hizi ni lugha za Mawakili, ukim-address wakili mwenzako is a sign of respect, ilikuwa haina haja ya kusema kwamba, sisi tuna nanihii zaidi, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo tulichokuwa tunakisema kifungu wanachosema Waheshimiwa Wabunge ni mfano tu kwamba, mwanajeshi atoke kwa makundi haya, kwa mfano tu, lakini kama nilivyosema haizungumzii majeshi inamzungumzia mtu mmoja. Definition ya mtu anayeitwa mwanajeshi.

Mheshimiwa Spika, wakati tunajadiliana kwenye Kamati tuliona suala alilokuwa analizungumzia Mheshimiwa Londo. Hata sisi tunachokisema kwa sababu, sheria hii ni kweli imeongeza hiyo forced marriage na imeongeza kitu kinaitwa forced begging ambayo kwa tafsiri ya Kiswahili maana yake ni ndoa za lazima kwa maana ya forced marriage na kumlazimisha mtu kuishi kwa ombaomba.

Mheshimiwa Spika, maoni ya Kamati, tuliishauri Serikali ku-define baadaye haya maneno ili yasilete mkanganyiko wa tafsiri na sheria nyingine kwa sababu, tunajua jamii nyingi za Watanzania baadhi ya ndoa hizi bado ni arranged kati ya wazazi na lakini ikitafsiriwa vizuri tu baadaye kwenye kanuni haitaleta mkanganyiko huo. Kwa hiyo, hata sisi tuliona, lakini kwa kuwa hii sheria haiku-define basi maoni ya Kamati tumeomba Serikali baadaye iondoe huo mkanganyiko kwa sababu tunajua Sheria ya Ndoa inazungumzia aina ya ndoa hizo ambazo jamii zetu nyingi sana wakiwemo wa Kiteto kuna hiyo tafsiri ya ndoa.

Mheshimiwa Spika, pia tulikuwa tumeomba, huku kulazimishwa mtu kuwa ombaomba inaweza pia ikawa na tafsiri pana ya kisheria. Kwa hivyo, tuliomba pia, baadaye Serikali iweke kwa namna ambayo kwa sababu, unajua kimsingi mtoto akiwa mtaani leo ana wazazi, akikutwa na hali ile sasa ya ombaomba maana yake ni kwamba, wazazi wameshindwa kutimiza hiyo obligation. Sasa tukasema baadaye pia, Serikali ifafanue kwenye kanuni ili isiwe kila mtoto anayekutwa mtaani ionekane basi wazazi wake wana- fall kwenye hii trafficking, kwa sababu, wakati mwingine familia zetu ni tofauti tofauti, viwango vya hali ya kimaisha ya Watanzania wote haifanani. Kwa hivyo tulisema na Kamati iliona hilo na kuiomba Serikali kulifafanua kwenye regulations ili iondoe utata huo na kwa kuwa hii sheria hai-define haya maneno itawekwa vizuri sana kwenye kanuni.

Mheshimiwa Spika, kitu kingine tulichoona kwenye Kamati, ni kwamba, pengine bado kwenye sheria nyingi nyingi utakutana na hili neno department. Tumeona kwenye amendments zile bado inasema kwamba, pamoja na mabadiliko haya litaendelea kutumika neno hilo, kwa mujibu wa Kifungu kile cha 3 kwamba, nanii itaendelea kutumika kama idara.

Mheshimiwa Spika, inasema:

“The Department established under subsection (1) shall be a Force within the Ministry and in that capacity”.

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, kwa kuwa sasa intention ni kufanya jeshi liwe independent. Kwa hiyo, kuna haja sasa kuangalia baadaye hizi sheria nyingine ili isitokee confusion ya word department na jeshi kwa sababu, department ni small unit. Bado lugha ile ya kizamani wakati bado ilikuwa ni department ndani ya jeshi ili iwe in order, usitokee tena mkanganyiko.

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo tuliliona pia hilo kama Kamati, tukashauri kwamba, kwa kuwa, bado sheria nyingi including sheria hii ambayo inakuwa amended ya Police Force…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naungana na Kamati na naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 7) wa Mwaka 2021
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Nami niungane na waliokupongeza kwa kura nyingi sana za kishindo. Hiyo ni ishara ya kutosha kabisa kwamba Bunge lina imani nawe, nami nafarijika kwa sababu ni Mwalimu wangu. Nakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Muswada wa Marekebisho wa Sheria Mbalimbali (Na. 7) wa Mwaka 2021, (The written Laws Miscellaneous Amendments (No. 7), 2021); kwa kweli kama kuna wakati tunawapokea wadau wanaotoa maoni yao wakishangilia mapendekezo yanayoletwa na sheria ni wakati tunapokea wadau wakitoa maoni kwenye sheria hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Jaji Dkt. Feleshi, ni mtu mwenye experience ya kuwa DPP, amekuwa kwenye bench na sasa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ni Mbunge, what an experience! Kwa kweli sisi Wajumbe wa Kamati tulinufaika sana. Kwa hiyo, nampongeza sana na tuna imani kubwa sana naye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri wa Sheria, CPD na Watalaam wote. Kamati yetu ilinufaika sana wakati wa mjadala wa sheria hii. Kati ya mapendekezo yanayoletwa sheria hii, ni Ibara ya 22 inayoongeza Kifungu kinachozungumzia Sheria ya Mashtaka Kifungu Kidogo cha (2) kuleta kitu kinachoitwa amicus curiae.

Mheshimiwa Spika, amicus curiae, friend of the court ni practice nzuri sana. Kwa hiyo, kuletwa kwa mara ya kwanza sasa kwa Mahakama zetu kuanza kutumika kwenye kesi hizi za Jinai, kwa kweli ni progress kubwa sana ya sheria. Amicus curiae imekuwa inatumika wakati wa kesi hizi za Kikatiba zaidi, lakini sasa kuleta pia kwenye kesi za Jinai inaongeza ufanisi mkubwa zaidi. Kwa hiyo, ni innovation kubwa sana, nawapongeza sana.

Mheshimiwa Spika, kama alivyosema mzungumzaji aliyepita, kuna kitu kinaitwa nolle prosequi ambayo kwa kweli imewatesa Watanzania kwa muda mrefu sana. Mtanzania anakaa miaka saba, nane halafu anaachiwa halafu anakamatwa baada ya dakika mbili, halafu kesi inaanza upya, regardless miaka ambayo amekaa Mahakamani. Mapendekezo haya yanayoletwa na kifungu kidogo cha (3) itaweka break kidogo sasa ili madaraka haya yasitumike vibaya. Kwa hiyo, hii ni innovation kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama alivyokuwa anasema Mheshimiwa Rais wetu hapendi sana kesi zilizopo Mahakamani ambazo hazina ushahidi wa kutosha ziendelee kutesa Watanzania. Kwa hiyo, kwa kweli this is excellent! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, najua madaraka ya DPP yanakuwa regulated na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, article 59(b). Sheria msingi wake ilikuwa lazima iwe kwa nia njema ya kutenda haki, lakini nyingine ni kuzia matumizi mabaya ya taratibu za utoaji haki, nyingine kubwa zaidi ni maslahi ya Umma. Kwa hiyo, yote yakiwa exercised kifungu hiki kitaleta mapinduzi makubwa sana kwenye criminal justice system. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna kifungu cha 131 (a) cha kukataa kesi zifunguliwe wakati upelelezi haujakamilika. Imekuwa ni wimbo kwa prosecution. Kila wakati wanaleta kesi halafu wanaimba kusema upelelezi bado haujakamilika na Mahakama inafungwa na wale wengine wanafungwa, hawawezi hata ku-control proceedings. Kwa Kifungu hiki sasa, kitalazimisha Ofisi ya Mwendesha Mashtaka na wale wapelelezi kufanya upelelezi, ndipo wafungue kesi Mahakamani. Kwa hiyo, kwa kweli it is brilliant innovation. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni Sheria ya Economic and Organized Crimes Control Act ambapo zamani ama kabla ya sheria ilivyo sasa na Mawakili wengi wanafahamu; mfano, kesi thamani yake ni shilingi milioni kumi au zaidi ya milioni kumi kidogo. Ili huyo mtu apate dhamana, unakwenda Mahakama Kuu kupeleka maombi madogo kwa ajili ya dhamana kwa sababu Mahakama za chini hazina mamlaka.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hii ya kuongeza sasa thamani iwe ni shilingi 3,000,000/= kwa Mahakama za chini, itasaidia sana watu wasisumbuke. Kesi zikifunguliwa kwenye Mahakama za chini, chini ya shilingi milioni 300, generally ni 80% ya kesi zinazokwenda kwenye Mahakama zetu hizi. Kwa hiyo, dhamana zitakuwa zinatoka ili kuondokana na msongamano mkubwa wa kesi za Mahakamani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna Kifungu cha 39, Ibara ya 39 na 40 ambayo inapendekeza kuongeza kifungu kidogo cha
(6) na hii ni habari ya michezo, kwa Sheria hii inayoitwa The National Sports Council of Tanzania Act. Tunakumbuka Bunge hili lilipitisha The Finance Act na kusema 5% ya sports betting iende kwenye Mfuko wa Michezo, lakini isingewezekana sasa bila mabadiliko haya. Kwa sababu, mabadiliko haya yanaanzisha huo Mfuko sasa, ili pesa hizo ziende na kwa kweli, tufanye mapinduzi kwenye sekta ya michezo. Hii itawezesha hata tununue zile Video Assistant Referees, itaondoa malalamiko mengi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kesi ya jana tu ya Mbeya Kwanza, yale mabao mawili yale huku linakataliwa, haya yote yatakuwa solved kama tungekuwa na Video Assistant Referee. Itaondoa hizi mbeleko za kubebwabebwa. Kwa hivyo, hii kwa kweli itafanya tasnia ya michezo tuipende sana na tuendelee kushangilia bila pressure; bao mbili za jana zilikuwa zina changamoto kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naomba niwaombe Bunge liunge mkono. Kwa kweli, mapendekezo haya yataleta reform kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa, 2022
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi na mimi nitoe mawazo yangu kwa Muswada huu wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 1 wa mwaka 2022.

Mheshimiwa Spika, kwanza, ninampongeza sana Mwenyekiti wa Kamati yetu ya Katiba na Sheria kwa kuwasilisha vizuri sana mada hii. Vilevile niwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria kwa michango mizuri, na walitoa mawazo mazuri sana wakati tunajadili Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, ninaipongeza Serikali vilevile wakati wa mijadala na Kamati, kwa kweli wamechukua mawazo karibu yote ambayo yalikuwa yanasemwa na Kamati, hili ni jambo jema sana. Ninawashukuru pia wale ambao tuliwaalika waje watoe maoni yao na walikuja Tanganyika Law Society na wengine wengi, tulibahatika kama Kamati, tulinufaika sana na michango yao.

Mheshimiwa Spika, kama walivyosema Wabunge wengine, Muswada huu umekuja wakati muafaka kabisa, tayari sheria tuliyokuwa nayo, The Management Act 2015, ilikuwa inaleta mkanganyiko mkubwa wa namna Serikali inavyojiandaa kukabiliana na maafa. Niwapongeze Serikali kwa kujaribu kufanya case studies nyingi. Wameangalia Sheria ya Afrika Kusini, sheria ya India na maeneo mengine kwa ajili ya kuboresha Pamoja na international standards by the way.

Mheshimiwa Spika, concept moja nzuri sana kwenye Muswada huu ni concept inaitwa Afya Moja (One Health Concept). Ni concept ambayo ni jumuishi, kwa kuwa majanga ni mambo ambayo ni complicated kidogo inagusa karibu kila mahali, walivyokuja na approach hii ya One Health Concept (Afya Moja) imesaidia Muswada huu kutengeneza a holistic approach kwenye namna ya kukabiliana na maafa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, taarifa ya Kamati yetu ya January/February 2022 kulikuwa na wazo la Bunge la kuiomba Serikali kwamba wakati wa kuleta Muswada huu wahakikishe kwamba Waheshimiwa Wabunge na wao wanakuwa sehemu ya hizi Kamati za maafa. Nafarijika sana kwamba Serikali imelisikia hili katika Ibara ya 11(2) utakuta uwakilishi. Tena tuliwaambia uwakilishi kwa ngazi za wilaya na mikoa, lakini wao walivyotengeneza ile structure kutoka Taifa wamewaweka Wabunge hata kwenye level ya Kitaifa, big up. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika Ibara ya 11(2), Ibara ya 13, Ibara ya 17 na Ibara ya 22 ya Muswada huu, kwa hiyo utaona kabisa kuanzia ngazi ya Taifa, mkoa, wilaya mpaka na Madiwani wapo. Kwa sababu wakati wa mijadala ilikuwa ni kitu cha ajabu kidogo kwamba, maafa yanatokea halafu kuna watu wanakaa kujadili halafu Mbunge ambaye ni Mwakilishi wa wananchi yuko nje. Akiulizwa na wananchi nini kinaendelea anasema tusubiri Kamati na vikao vitoke. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri, this is a very good initiative, itatufanya na sisi sasa tuanze kushiriki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tena mmefanya vizuri kwa sababu mnajua kazi ya Bunge ni oversight, kwa hiyo hamjawaweka kwenye zile Kamati zinazofanya kazi, ni zile Kamati elekezi ili waweze kuendeleza lile jukumu lao la oversight. Big up. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna kitu kingine ambacho ni innovation nzuri sana, kuanzisha Mfuko huu wa Usimamizi wa Taifa, lakini kubwa kuliko yote ni kuruhusu sasa sheria iseme kwamba ni lazima Serikali itaweka pesa inayopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii ni initiative nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, ukisoma Sheria ambayo sasa itafutwa baada ya Sheria hii kupita, ilikuwa inazungumza habari ya kutafuta hela za misaada, donations na vitu kama hivyo, lakini sasa ni jukumu la nchi kuweka sehemu ya bajeti yake kwenye Mfuko huu. Hii ni innovation nzuri sana. Unajua hata kabla hujaongea na wengine wanaokuchangia lakini umeshaweka commitment ya kwako ya fedha inayopitishwa na Bunge, nadhani ni initiative nzuri sana. Big up. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kimsingi hata nchi nyingine – tutaangalia baadaye – in fact wamefika mahali wana-dictate kuweka percent fulani ya National Budget. Hiyo ni stage ya juu sana lakini ninyi mmeanza vizuri kwa kuruhusu Bunge hili lipitishe bajeti ya kuweka pesa kwenye Mfuko huu.

Mheshimiwa Spika, Muswada huu vilevile kilichonifurahisha sana ni kwamba imetajwa Red Cross hapa. Red Cross kwa kweli Wabunge wengi hapa ni mashahidi – wamekwenda kila Jimbo. Kiteto, Manyara, kila mahali, kuweza kutambua mchango wa Red Cross nchi hii na kuwajumuisha kwenye Kamati hizi ni innovation nzuri sana. Tunawaomba tu muendelee kuwapa support nzuri wanayoihitaji ili waweze kusaidiana na Serikali katika jukumu hili.

Mheshimiwa Spika, ukisoma Muswada huu vilevile utakutana na volunteers (watu wanaojitolea), kwa sheria kuthamini na kutaja role ya volunteers vilevile ni kitu kizuri sana, ita-encourage watu waendelee kujitolea kwenye masuala haya ya majanga. Tunachoomba tu Serikali, pamoja na kwamba maafa ni jambo ambalo kuna Kamati nyingi na kuna watu wengi wanaohusika, sisi tunachoomba tu ni kuangalia suala la urasimu, isije ikawa ile complication ya watu wengi kuwepo ikaleta urasimu katika kufanya vikao na of course budget wise, isije ika-inflate budgets unnecessarily kwa sababu tunavutana kutafuta pesa kwa ajili ya majanga haya.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, nashukuru na ninaunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa Mwaka 2023
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza nimpongeze Waziri wa Sheria na Attorney General na Kamati kwa wasilisho zuri linalohusu marekebisho ya Sheria Mbalimbali (The Written Laws Miscellaneous Amendment (No.2) Bill, 2023)

Mheshimiwa Spika, kama walivyosema Kamati Muswada huu unahusu sheria tano. Kwa kuanzia, nianze na Sehemu ya Tatu na ya Nne ya Muswada ambao ulikuwa unahusu sheria mbili za The Natural Wealth and Resources Permanent Sovereignty Act ambayo baada ya mashauriano na Ofisi ya Attorney General Serikali ilikuwa inataka kuibadilisha Kifungu cha 35, 36 na Ibara ya 37 na 38, lakini baada ya mashauriano na kuona mantiki, Serikali kupitia Attorney General waliomba ku–withdraw. Kwa kweli tuwapongeze hata wadau ambao walikuja mbele ya Kamati yetu, maoni yao mengi sana yalikuwa yanagusa sehemu ya hizi Sheria mbili, kwa hiyo tunawapongeza Serikali kwa busara hiyo kubwa kuhusu hizi sheria mbili.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na sababu nyingi, kuna kesi zinazoendelea mahakamani lakini pia kuna kanuni zetu za Bunge zinazotuzuia kuzungumzia masuala ambayo yapo mahakamani. Pamoja na hayo yote tunaishukuru Serikali kwa kuondoa sehemu hizi mbili za Muswada.

Mheshimiwa Spika, sehemu nyingine ni The Atomic Energy Act na hapa niipongeze Wizara ya Elimu kupitia Tume ile ya Tanzania Energy Commission, walialika Kamati tutembelee Arusha na tuone kituo chetu cha energy. Sijui Wabunge wangapi wanafahamu hii Tume ambayo inafanya kwa kweli kazi nzuri sana. Wanajaribu kuratibu haya masuala ya atomic na kwa kweli Wajumbe wa Kamati yetu waliotembelea, walijifunza mambo mengi sana. Madhara tunayopata kutokana na simu hizi, microwave na haya mambo yote ambayo yana radioactive elements, kwa kweli tulijifunza sana na tunaomba Tume hii iendelee kutoa elimu kwa Watanzania kupitia vyombo vya habari, ili waendelee kujifunza athari ambazo zinatokana na the atomic energy.

Mheshimiwa Spika, kama walivyosema Kamati mabadiliko haya ni kuwezesha Tume kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi. Kwa mfano, kuna Kifungu cha 10 kinachozungumzia The Atomic Energy Act. Kwanza ukisoma Kifungu cha 4 utaona mabadiliko yake ni kupunguza kiasi cha mionzi kwenye vitu mbalimbali na hii ni kuendana pia na obligations za kimataifa. Tunajua nchi yetu ni sehemu ya dunia na kuna Shirika la Kimataifa linaloitwa The International Atomic Agency, ambalo lina–regulate mambo ya atomic energy na ili sasa tuondokane na jukumu hili na ambalo mara kwa mara huwa linatoa miongozo ya namna nchi ambazo ni wanachama wanufaike. Msingi wake ni kuhakikisha tu usalama wa wale ambao wanafanya kazi kwenye vyombo hivi na Watanzania kwa ujumla wanakuwa hawapati madhara ambao yanatokana na radioactive elements.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 11 utaona vile vile vitu ambavyo vilikuwa vinapatikana kwa mfano sheria inasema hivi, viwango ambavyo vilikuwa viko – exempted kuna kitu kinaitwa becquerel. Becquerel ni jina la kisayansi ilikuwa inasema kati ya 74 mpaka 3,700. Sasa kwa mabadiliko haya ni kupunguza sasa kiasi hicho ili kuipa Tume hii mamlaka ya kupata kazi kubwa zaidi ya kuweza kuondoa, kushughulika na vile vitu ambavyo vina hiyo mionzi kuanzia becquerel moja na kumi na hii itaongezea kazi kubwa Tume, lakini kusudi la haya yote ni kulinda afya za Watanzania. Kwa hiyo tuipongeze Serikali kwa kuliona hili ili kulinda afya za Watanzania wasipate maradhi.

Mheshimiwa Spika, mabadiliko mengine ya Sheria hii ya Dar es Salaam Maritime Institute, vilevile kutokana na mabadiliko ya Sheria iliyofanywa na Bunge hili 2021 kuna mabadiliko kutoka NACTE sasa kwenda kwenye Institute nyingine ambayo imebadilika jina sasa inaitwa The National Council for Technical Education kwa kuongeza kitu kinachoitwa Technical Vocational Educational Training. Kwa hiyo mabadiliko hayo sasa yatawezesha Sheria hii na Chuo hiki kiendane sasa na mabadiliko ya sheria.

Mheshimiwa Spika, tukirudi vile vile kwenye The Atomic Energy Act, mtu alikuwa akikutwa na kosa kwa mfano, Tume hii ilikuwa na mamlaka ya kumpeleka huyu mtu mahakamani. Kwa hiyo kesi zinakuwa ni nyingi, lakini ilikuwa haina uwezo wa ku–sanction na kutoza fine wale ambao watakuwa wame–violate sheria. Kwa hiyo, mabadiliko hayo kama tutakavyoona kwenye kifungu cha 72 inaiwezesha Tume sasa kuwa na mamlaka mapana zaidi ya kuweza ku–compound kwa mtu ambaye atakuwa amekosea. Tume iwe na mamlaka hayo ya kutoza faini za haraka haraka bila kupeleka mahakamani. Hii itawezesha Tume kufanya kazi kwa wakati na bila kuchelewa.

Mheshimiwa Spika, vilevile utaona mabadiliko ya Sheria hii ta Tanzania Industrial Research na hii pia ni kuendana na mabadiliko ya uchumi duniani. Sasa tunajua uchumi siyo state controlling peke yake, kuna private sectors. Kwa hiyo sharti la sheria hii kabla ilikuwa ni kujaribu kuleta assumption kwamba ni Serikali peke yake inahusika na mambo ya industrial research, kwa hiyo naipongeza Serikali kwa kuliona hili mapema kabla halijaonekana kwamba ni barrier.

Mheshimiwa Spika, kimsingi sheria zetu hizi zingine za 2003, zingine za 1992, kutokana na mabadiliko ambayo yanaendelea kwenye sekta mbalimbali sheria zetu ili tufanye sasa ziendane na standards na miongozo mipya ambayo nchi yetu inapitia.

Mheshimiwa Spika, sharti la kushtaki, sheria ilikuwa inasema Mkurugenzi anaweza akampeleka mtu kwa mahakama ya Hakimu Mkazi peke yake na tunafahamu siyo kila mahali tuna Mahakama hizi za Makimu Mkazi ama Regional Magistrate. Sasa kuondoa takwa hilo na kusema kwamba Mkurugenzi huyu awe na mamlaka ya kuweza kumshtaki mtu huyo popote kwenye mahakama, iwe ni Mahakama ya Mwanzo au mahakama yoyote ambayo itakuwa kwenye eneo hilo. Nadhani itasaidia bodi hii kuwa effective zaidi na itafanya kazi yake kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Mheshimiwa Spika, baada ya hayo machache sana, naipongeza Kamati kwa kufanya kazi nzuri sana na napongeza Serikali na naunga mkono hoja. Ahsanteni kwa kunisikiliza. (Makofi)
The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3) Bill, 2023
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi na nimpongeze Attorney General kwa kuleta Muswada huu ambao lengo lake ni kubadilisha sheria mbili. Sheria ya Kanda Maalum ya Uwekezaji kwa ajili ya mauzo ya nje, Sura ya 373 na Sheria ya Kanda Maalum ya Kiuchumi, Sura 420.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge litakumbuka na niwapongeze Wanakamati wenzangu ambao wamechangia. Mtakumbuka kwamba Bunge hili lilipitisha sheria mpya kabisa baada ya mjadala mkubwa wa Wabunge kutaka tulete Tume mpya ya Mipango ya Nchi. Mtakumbuka Mwezi Juni, tulitunga sheria mpya na kwenye Sheria ile ya Mipango Kifungu cha 3 kinasema: “Tume itaundwa na Mheshimiwa Rais na itakuwa na wajumbe wafuatao; moja, ni Waziri mwenye dhamana ya masuala ya mipango na maendeleo ya Taifa”.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo baada ya Bunge kupitisha Sheria hii ya Tume ya Mipango, tayari kabisa tulijua kwamba kuna mabadiliko ya Serikali na tutakumbuka Mheshimiwa Rais tarehe 22 Juni, kupitia Gazeti la Serikali namba 407(b), Mheshimiwa Rais aliunda Wizara mpya ya Uwekezaji, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Mipango ambayo Mheshimiwa Profesa Kitila aliteuliwa kuwa Waziri wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya mabadiliko hayo ni process, Bunge kwa sababu ya kuwa na Wizara mpya ilibidi na sisi tubadilishe Kanuni za Bunge kupitia Kamati ya Bunge ya Kanuni kubadilisha Nyongeza ya Nane ili kupanga Wizara pale kwenye Kamati na Majukumu ya Kamati na Wizara zinazokwenda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo hata Bunge, sisi kupitia Kamati yetu tulibadilisha Kanuni za Bunge, Nyongeza ya Nane ambayo Bunge hili lilikasimu madaraka hayo kwa Kamati ya Kanuni ya Bunge. Kwa hiyo, baada ya process hiyo nyingine ya pili sasa, Mheshimiwa Attorney General ameleta sasa mabadiliko ya Sheria hizi mbili, the Export Processing Zone Act ili ku-realign shughuli za Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo mabadiliko haya ni madogo sana na haya-create nanii yoyote, ni definition tu ya Minister kutoka Minister responsible for Industries iende kwa Minister ambaye atakuwa responsible kwa mambo ya uwekezaji. Nimshukuru Mheshimiwa AG kwa sababu ni kama ameongeza innovation kubwa hapa kwa kutokum-define tena Waziri kwa cheo chake na kusema tu Waziri atakayehusika na mambo ya economic processing zone. Maana yake, logic yake ni kwamba ikitokea mabadiliko mengine ya realignment, basi huyo huyo Waziri atakayechaguliwa, ambaye atakuwa anasimimamia masuala ya export processing zones tayari kwenye instrument yake itakuwa inataja tu bila kueleta mabadiliko mengine ya sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, so this is an innovation, Mheshimiwa Attorney General, big up. Kwa hiyo, mtaona kama mabadiliko madogo haya ni kuwezesha tu realignment ya Serikali ili functioning ya Serikali iweze kwenda bila ku-create lacuna.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya processes zote hizo za kuanzia Sheria ya Tume ya Mipango na Uwekezaji, baada ya Waziri kuteuliwa na baada ya Kanuni za Bunge kubadilishwa kwa maana ya ku-realign, Kamati na Wizara na sasa tunahitimisha kwa kuleta mabadiliko haya sasa ya sheria ambayo itampa Profesa Kitila kazi ya kwenda kufanya field sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati iliona labda huko mbele na tulimwambia Mheshimiwa Attorney General kwa sababu ya sheria hii ambayo wana-amend ile composition ya wale watu wa Kamati, sisi tuliona huko mbele wakiona haita-create confusion si mbaya kama Katibu Mkuu wa Wizara hii mpya sasa atakuwa sehemu ya Kamati hiyo kwa ajili ya records. Of course, tunafahamu na tunajua logic kwa nini hata ile sheria ambayo tunabadilisha sasa, Katibu Mkuu wa hiyo Wizara hakuwepo, kwa sababu Katibu wa Bodi hii ni Director General anayehusika na mambo ya economic processing zones, kwa hiyo hakuna confusion yoyote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu mabadiliko haya ni madogo sana na nahitimisha kwa kifupi namna hiyo, naomba niwashawishi Wabunge tupitishe huu Muswada haraka sana ili wakaufanye kazi haraka sana. Ahsanteni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)