Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Juma Hamad Omar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ole

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Bajeti, tulipata nafasi ya kuchakata wasilisho zote hizi na kwa kweli tunakubaliana nao. Nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshushulikia masuala ya uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli wasilisho la Profesa Mkumba, Profesa Kitila Mkumbo. Mjina magumu.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Juma Hamad anaitwa Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo. Naomba endelea na mchango wako.

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa samahani kwa kukosea jina hilo. Ni wasilisho zuri sana limetupa hali ya uchumi, matarajio yetu na huko tunakokwenda. Ninasema tuna mtu ambaye alikuwa very brilliant katika mambo haya ya uchumi. Congrats Prof. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Mwigulu as usual, ni very ductile wakati wote amekuwa akikubaliana na hoja kwa hiyo amekuwa very ductile anakubaliana na hoja na ninafikiri tunafika mahala Kamati ya Bajeti tunamwelewa tu. Tunafika mahala tunakwenda vizuri na yeye. Kubwa zaidi nimpongeza Mheshimiwa Rais wetu kwa kuunda Tume ya Mipango, kwa kweli kama kuna jambo amelifanya na litatutoa hapa tulipo kwenda kwenye uchumi mwingine ni hilo. Sasa kwa maoni yangu, ili uweze kufanikiwa, ili nchi iweze kufanikiwa kiuchumi kuna mambo kadhaa lazima uyatekeleze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza iwe na sera sahihi za kifedha prudent, physical and monetary policies. Pili iwe na sera sahihi za kiuchumi lakini ikishirikisha watu binafsi au kampuni (Private public participation), la tatu iwe na prudent taxation policies na bila kuwa na prudent taxation policies utakuta kodi unayokusanya hasa kwa wakati wetu huu sasa ambao ndiyo wa mitandao wa TEHAMA unaweza ukakuta kwamba kodi ni ndogo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la nne uwe na wafanyakazi ambao ni bora na ninafikiri katika mwisho wa hotuba ya profesa Mkumbo amesema kwamba prime minister wa Singapore alifanikiwa kwa kuwa na wataalam na wafanyakazi ambao wana uwezo wa kufanya kazi. Katika kuona hii hali halisi nasema yote haya manne lakini yawe chini ya umbrella ya good governance. Without good governance yote haya hayawezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nikitoa mfano wa tiger economies ambazo zipo Asia na nikisema tiger economics nakusudia economy za nchi nne. Ambazo ni Singapore, Hong Kong, South Korea na Taiwan. Hizi nchi wakati tunapata uhuru miaka ya 1960’s zilikuwa na uchumi kama zetu. Baada ya kufanya major industrialization kwanzia Miaka ya 1950’s wali-invest sana katika industries na kwa kutumia watu wao ambao walikuwa ni bora sasa hivi kwa kweli ni nchi ambazo ni za kupigiwa mfano ulimwenguni. Kwa kweli ni more than first one. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano GDP per capital ya Singapore sasa hivi kama sikosei imefikia dolla 67,359. Nichi ya pili inafuatia Taiwan, GDP kwa miaka 2020/2022 ilifikia 61,371. Hong Kong, GDP per capital ni 49,000 na mwisho South Korea GDP per capital ni dolla 48,309, wakati sasa hivi katika Africa nchi yenye GDP kubwa ni Mauritius ambayo nafikiri kama sikosei imefikia dolla 9,005. Inafuatiwa na Botwasa ambayo imefikia 6,610, kwetu sisi kama sikosei tunakaribia dolla 1,200 hivii, Kenya wenzetu wapo mbele kidogo kama 2,080.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema hawa watu wamefanya kazi kubwa sana. Maendeleo yao ya kiuchumi ni makubwa na hii imetokana na kona zote hizi nne nilizosema lakini chini ya utawala bora wa kisheria. Sifa tumpe, wanasema mnyonge mnyongeni lakini sifa mpeni, tumpe mama yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana alipokuwa akichangia Mheshimiwa Reuben alisema mama ni kama vile alitutoa msituni, it is very true. Mama baada ya UVIKO ndiyo akaingia madarakani na alipokuja jambo la kwanza alilofanya ni ku-negotiate na IMF tukapata ule mkopo wa COVID ambao ni karibu shilingi trilioni 1 na bilioni 100. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili kama hiyo haitoshi, ame-negotiate na IMF na World Bank tukapata ile credit facility ya shilingi trilioni 2.2 yaani trilioni mbili na bilioni 200. Kama hiyo haitoshi, akaenda akaweka trilioni moja za kuwasaidia wakulima ili wakulima waweze kupata mikopo. Sasa, mama kafanya mengi sana na anaendelea kufanya mengi. Kwa hiyo tumpe sifa kubwa, tumpe maua yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015 ina kifungu ambacho huwa inataka ianzishwe fungu ya dharura. Kwa nini? Kwa sababu katika hizi tunasema vigezo tarajiwa, moja katika vigezo tarajiwa ni kwamba tutajitahidi kuhakikisha kuwa kuna utoshelevu wa chakula. Suala la pili, tutahakikisha tunahimili tabia ya nchi au tunashughulikia tabia ya nchi. Sasa hizi ni unforeseen emergences kama huna contingency hauwezi kuhimili vitu kama hivi ambavyo ni unforeseen. Sheria ya Bajeti ya hiyo Na. 11 ya mwaka 2015 kifungu cha 35(1) mpaka cha (4) kinazugumzia uwepo wa kuwa na contingency lakini na fund au sources za contingency zitakuwa vipi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda katika Kifungu cha 36(1-3) kinampa uwezo Waziri wa Fedha ku-administer au kuishughulikia hili suala la fungu la contingency. Jambo hilo halijafanyika na mimi ninasema Waziri wa Fedha pamoja na mazuri yako yote lazima tufike mahala tuwe na contingency kwa ajili ya unforeseen emergences na sheria yenyewe inampa Waziri wa Fedha atenge asilimia tano ya total budget ambayo sidhani kama Mheshimiwa Dkt. Mwigulu umefanya hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajua una fungu lako 21 lakini hili fungu la 21 ni fungu ambalo kuna mambo mengi. Kuna malipo ya wastaafu, majaji, sijui stahili za viongozi nakadhalika. Sasa tusichanganye mambo hayo na fungu la dharura. Fungu la dharura ni lazima liwepo kwa mujibu wa Sheria hii ya Bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, private sector ndiyo injini ya uchumi. Ninajua kwa mujibu wa takwimu tulizonazo, mikopo kwenda kwenye private sector imekuwa ikiongezeka.

MWENYEKITI: Mheshimiwa malizia mchango wako.

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano mwaka 2021/2022 mikopo kwa sekta binafsi ilikuwa asilimia 9.9, iliongezeka katika 2022/2023 imekuwa 10.3 lakini hii ni sehemu ndogo sana. Pesa hizi nyingi zipo maana yake private sector huwa hawakopi benki, Benki Kuu huwa haikopeshi private sector inakopa kwenye Benki za Biashara. Benki za Biashara zinaendelea kupata faida kubwa sana mpaka zinafika mahala zinaanza kuuza hati fungani kama tulivyotamkiwa. Kwa sababu ukishafika mahala hapo kwamba unainyima private sector mkopo, kwa kweli utakuwa huwasaidii kuendeleza uchumi na tumesema private sector ndiyo injini ya uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu private sector wao wanapewa mkopo kutoka Benki Kuu na Benki Kuu wana instrument mbili, Moja, wanapunguza ile wanaita SMR (statutory minimum reserve), na la pili wana discount rate ya landing wanayompa private sector. Sasa, kama Benki Kuu ndiyo anayefanya bank supervision ninashangaa kwa nini Benki Kuu hawasimamii hizi benki za biashara kuhakikisha kwamba nayo mikopo kwa private sector inakuwa na riba ndogo, sijui kama naeleweka hapo. Inakuwa na bei ndogo na vilevile kwa kiasi kikubwa zaidi ya asilimia 10.3 kama tunavyosema inakwenda kwa private sector. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukifanya hivi tutakuwa tumewasaidia private sector na tutakuwa tumewachachua katika kujenga uchumi. La mwisho…

MWENYEKITI: Mheshimiwa malizia sentensi mbili za mwisho.

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia kwa kusema hivi, tatizo si wigo wa kodi. Wigo wa kodi tunao wa kutosha maana ukienda ukiagiza kitu sijui lipa, income tax, sijui VAT. Wigo wa kodi ni mkubwa lakini problem kubwa ni kuwa tax payers tunaolipa kodi we are talking of population of 61 million lakini tax payers wanaolipa kodi ni 6.7 million. Ndiyo kusema ni asilimia 4.5 tu ndiyo wanaolipa kodi katika population yote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kenya wenzetu wana tax payers around 2.5 million lakini population yao ni around 19 kwa hiyo, they are talking of 13.2%. kwa hivyo tupo chini sana, wengi hatulipi kodi. Wengi ni watu tegemezi. Ukishafika hapo ndiyo unakuta mara nyingi mapato yanayotokana na kodi hayatoshi kuendesha Serikali.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Juma Hamad Omar.

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja. (Makofi)