Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Hon. Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Bajeti Kuu ya Serikali, lakini namshuru Mungu kwa afya na uhai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa saba wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri ametanabaisha kwamba lengo la Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni kujenga uchumi kukabiliana na umaskini pamoja na ukosefu wa ajira hasa kwa vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya umaskini kwenye Taifa letu bado ni kubwa mno, Watanzania bado wanaishi kwenye maisha ambayo wana umaskini uliokithiri. Kwa miaka 10 mfululizo takwimu zinatuonyesha kwamba hali ya umaskini wa mahitaji ya msingi umepungua kwa asilimia 1.8 tu, kuanzia mwaka 2012 umaskini ulikuwa kwa asilimia 28.2, lakini mwaka 2021 umaskini upo kwa asilimia 26.4 asilimia 1.8 tu, kasi ya kinyonga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wanajitahidi kupambana kujikwamua kwenye umaskini, lakini pamoja na jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba Watanzania wanajikwamua kwenye lindi la umaskini, bado utitiri wa kodi ni mzigo kwa Watanzania. Watanzania wanaishi kwa kusaidiana Wabunge kwenye simu zao wana meseji za wapiga kura wao wakiwaomba hela ya kula, wakiwaomba hela ya matibabu, wakiwaomba michango ya shuleni, majukumu ni mengi, tunatumia simu zetu kufanya miamala kusaidiana kama Watanzania kujikwamua kwenye lindi la umaskini, lakini tozo za miamala ya simu, tulizungumza Bunge lililopita tunazungumza tena sasa hivi, pamoja na kwamba zimeshuka lakini Mheshimiwa Waziri kuendelea kuhangaika na trilioni 1.2 kwa sababu makadirio ya makusanyo ya tozo za miamala ya simu mwaka Julai, 2021 ilikuwa ni kukusanya shilingi trilioni 1.2 tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka mwezi Machi, 2022 Serikali imekusanya bilioni 261 tu, sawasawa na asilimia 25.6. Wakati Serikali inapanga tunaamini walifanya utafiti na waliona miamala ni mingi, kilichotokea kwa kukusanya asilimia ndogo hizi ni watu kuacha kufanya miamala ya simu. Kwa hiyo watu wanalazimika kuendelea kubaki kwenye umaskini uliokithiri kwa sababu wanajiepusha na kufanya miamala, maana yake Serikali imekosa mapato na Watanzania bado ni maskini, wanahangaika hata pato la kuishi kwa siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ku-deal na trilioni moja wakati ina uwezo wa kutafuta pesa nyingine kwenye kodi nyingine kubwa ni kufikiri kimaskini. Tuna kesi za kodi mahakamani, ziko kwenye Mahakama ya Rufaa za Kodi, ziko takribani Sh.357,000,309,000,000 kwenye Mahakama za Kodi. Miaka mingi na muda mrefu sana tuna hizo pesa huko, bajeti ya Serikali ni trilioni 41, trilioni 41 kwenye pesa zilizopo kwenye Mahakama za Rufani za Kodi inaingia mara nane, tuna bajeti, tuna pesa za bajeti za miaka nane mfululizo Mahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Waziri anahitimisha naomba atujibu nini kinaendelea Mahakamani kwenye kesi ambazo sisi tunadai. Miongoni mwa pesa hizi kuna shilingi 5,000,594,000,000 ambayo Serikali iko kwenye negotiation na makampuni ya madini Barrick, Bulyanhulu, Pangea Minerals na AGB exploration ziko kwenye negotiation. Kwa hiyo Serikali imalize negotiation lakini watujibu hizi pesa nyingine tunazipata lini? Waache kufikiri kimaskini kuwatoza Watanzania trilioni 1.2, wakati wana trilioni 350 ziko mahakamani. Naomba majibu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, asilimia 10 ya halmashauri…

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Kuna taarifa Mheshimiwa Nusrat, Mheshimiwa Emmanuel Mwakasaka taarifa.

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge anayechangia kwamba kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo, anaomba yeye kwamba Bunge litoe taarifa za mahakamani, Bunge hili haliwezi kuingilia mashauri yaliyoko mahakamani, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nusrat Hanje, unaipokea hiyo taarifa.

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie asilimia kumi za halmashauri. Siipokei hiyo taarifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kufikiri kuenda kupunguza asilimia 10 za halmashauri ni kufikiri vitu vidogovidogo ambayo sio level yao, Mheshimiwa Waziri yeye ni wa level ya juu sana, hivi vitu vidogovidogo aachane navyo. Naamini hizi pesa kuna watu zinawasaidia, Mheshimiwa Waziri mwenyewe kuna vijana wake kule, wale wanakimbiakimbia kipindi cha kampeni hizi pesa zinawasaidia. Asitafute ugomvi na laana za Watanzania kwenye vitu vidogovidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na kujenga miundombinu ya masoko kwa wamachinga, lakini nataka nimwoneshe Waziri sehemu atakayopata pesa, aachane na hizi atapata laana za watu kwa hawa maskini zinawasaidia. Kuna kitu kinaitwa Mifuko ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi; mwaka 2020, Mifuko hii imetoa shilingi bilioni 894 kwa Watanzania wajasiliamali, mwaka 2021 imetoa shilingi bilioni 903, pesa nyingi. Hizi pesa wakachukue mwaka mmoja wasiwape wajasiriamali waende wakawajengee masoko, Waziri aachane na hela za halmashauri atapata laana bure. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, soko linalochukuliwa kama mfano, lililojengwa ni la Dodoma, limejengwa kwa bilioni saba na kama milioni mia 200 hivi. Ukichukuwa shilingi bilioni 900 ukagawanya halmashauri 114 Tanzania kila halmashauri itapata bilioni saba na milioni 900, Mheshimiwa Waziri anaiona hiyo hesabu, yeye ni msomi, hivi vitu vidogo asihangaike na watu, asilimia 10 kila Mbunge analia na hii aachane nayo, achukue hizi hela za mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi, aende akawajengee watu masoko. Hii hesabu niliyomwambia ni practical ni kitu ambacho practical kabisa kwa sababu Mifuko ni ya kwetu na halmashauri ni za kwetu. Tunajua sio halmashauri zote zinazohitaji soko kubwa kama hapa. Kwa hiyo tunaamini hii pesa itatumika na itabaki na Watanzania watatumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya tatu, elimu, ukurasa wa 50 wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri amezungumza kuhusu higher education for economic transformation. Sasa Mheshimiwa Waziri amezungumza kuhusiana na kujenga vyuo its well and good ni kitu kizuri, shida yangu iko sehemu moja, kwanza itambulike huu mradi ni mradi kati ya Serikali ya Tanzania na World Bank, una takribani shilingi milioni 425. Lengo ni kuhakikisha kwamba the project is design to revitalize and to expand the capacity of the universities to contribute to key areas for innovation economic development and labour market relevancy kwa kuhakikisha kwamba wanawajengea uwezo Vyuo Vikuu ku-train Walimu watafiti na watu wa maofisi, semi administrators wawe katika fully exponential, wawe ni watu ambao watasaidia nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hizi pesa ni nyingi mno pamoja na kujenga vyuo vikuu mimi shida yangu iko kwenye content labor market relevancy, ubainishaji bayana kati ya kinachotakiwa kwenye soko la ajira na kinachotolewa vyuo vikuu. Vyuo vyetu Tanzania vinajiendesha vyenyewe, kuna kitu kinaitwa Senate za vyuo, kina autonomy power, ni kitu ambacho kilipitishwa Kiserikali na ni well and good, lakini vyuo siku hizi vinajianzishia kozi ambazo sio hitaji ya soko la ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kozi inaitwa social protection katika Chuo cha IFM hata kwenye portal ya ajira ya Serikali haitambuliwi, lakini kuna kozi inaitwa bachelor of science in physics inatolewa UDOM Bachelor of Science in Mathematics, hakuna kwenye portal ya ajira. Watanzania wanajinyima wanasomesha watoto wao vyuo vikuu, wanaenda ku-apply kazi, hata portal ya ajira hazitambui hizo kozi. Naomba Serikali iingilie kati, ianzishe chombo ambacho kita-oversee mitaala ya vyuo vikuu kwa sababu hata kinachofanyiwa mapitio sasa hivi ni sera elimu ya msingi, awali na sekondari, vyuo vikuu vinajiendesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha hata zile Wakala za Serikali sasa hivi zinatoa elimu, kuna chuo kinaitwa ADEM kipo Bagamoyo, sio chuo actually ni agency, ni Wakala wa Serikali, lakini leo wanatoa diploma, lakini pia wamepeleka maombi wanataka waanzishe degree yaani kila mtu anajifanyia kiholela, hatuwezi kufika. Kianzishwe chombo ambacho kitaratibu mtaala wa vyuo vikuu ili kozi zinazoanzishwa ziendane na hitaji la soko la ajira, lakini na dira na mwelekeo wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya pili kwenye elimu ni mitaala. Sasa hivi Wizara ya Elimu inapitia mitaala lakini kinachofanyika ni kama mchezo wa kuigiza, linafanyika kongamano, watu wanapewa dakika mbilimbili watoe maoni, halafu kikosi kazi kinakusanya maoni, kinaenda kujifungia kichakate. Kwenye nchi hii hatujaanza leo kukusanya maoni ya kurekebisha mitaala mwaka 1981, Mzee Nyerere aliunda Makwetta Commission ya kwenda kupita mfumo wa elimu, wabobezi wasomi walikaa, wakachakata, wakaandika, wakapelekea Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 1992 Mzee Mwinyi aliunda National Task Force ya kwenye elimu, wakachakata, Wizara ya Elimu ilikaa pembeni ikaangalia, hiki kinachofanywa hapa tutarudi tuje kuambizana humu. Mzee Kikwete kuna Professor wangu, Mwalimu wangu wa Chuo Kikuu, Professor Kitila Mkumbo, Mheshimiwa Mbunge, ameandika ten years of Jakaya Kikwete Presidency, promises, achievement, and challenges, ameeleza aliyoyafanya Jakaya Kikwete kwenye elimu.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. NUSRAT S. HANJE: Tunaomba itengenezwe commission ya Rais ambayo itafanya mchakato wa kupitia sera tunachokifanya ni mchezo wa kuigiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa dakika moja…