Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

Hon. Furaha Ntengo Matondo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikushukuru kwa kuweza kunipatia nafasi na mimi kuweza kuchangia. Kwanza kabisa niweze kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya hasa kwa wananchi wa Tanzania. Niweze kuwapongeza Mawaziri wote, Manaibu Waziri, Wenyeviti wa Kamati, Makatibu Wakuu lakini pia na wajumbe wa Kamati kwa kazi kubwa waliyoifanya mpaka kutuletea leo hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ni-deal kwenye Ustawi na Maendeleo ya Jamii. Kuna mfuko ulioanzishwa wa Maendelo ya Wanawake. Mfuko huu ulianzishwa mahususi kabisa kwa ajili ya kumkwamua mwanamke kutoka katika hali moja na kwenda katika uchumi wa hali nyingine. Mpaka tunavyoongea hapa mfuko huo ulianzishwa kwa ajili ya riba nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanamke ambaye aweza kukopa kwa riba ya 4% inayomuwezesha kulipa na akalipa vizuri pasipokuwa na shaka pasipo kunyang’angwa mali na pasipokuwa na riba kichefuchefu ambazo zinawenda kumflisi. Kamati tumebaini huu mfuko hauwasadi wanawake wengi ni kwa sababu ya elimu ndogo ambayo imetolewa haijaenda kuwagusa wanawake wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali ione sasa kuna haja ya kutoa elimu kwa wanawake. Wanawake wote waweze kufahamu nia na lengo zuri la Serikali la mfuko huu ambao unakwenda kuwakwamua kwenye hali nzuri ya uchumi. Kamati pia tulibaini Wizara haina mkakati Madhubuti wa kuhakikisha fedha ambazo zimekopwa zinarudishwa kwa wakati ili wanawake wengine ambao hawajakopa waweze kupata mikopo hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitoa mfano kwenye halmashauri kuna fedha shilingi milioni 574 zinadaiwa. Mpaka leo bado hazijarejeshwa ili kuona kwamba hawa wanawake wegine ambao hawajapata mikopo waweze kupata. Kamati tumefuatilia hizi halmashauri ni halmashauri zenye uwezo na zinauwezo wa kulipa zile fedha. Niiombe Serikali sasa kuweza kufuatilia fedha hizi shilingi milioni 574 ziweze kutoka ili wanawake wengine waweze kujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kidogo kuhusu machinga. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kuhakisha vijana na machinga wanakwenda kuinuka kiuchumi. Serikal imetenga bajeti ya shilingi bilioni 18.5 kwa ajili ya machinga. Hii yote ni kwenda kumtoa machinga kwenye hali moja na kwenda kwenye hali nyingine. Rais wetu mpendwa kwa kuona hilo ametoa shilingi milioni 10 kila mkoa kujengewa ofisi za mamchinga. Kamati tuliondoka tukaenda mkoa wa Mbeya tukaona ofisi nzuri ambayo imejengwa ya machinga lakini mpaka ninavyoongea hivi ni mikoa minne tu ambayo imejenga ofisi za machinga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali kuweza kufuatilia nia nzuri na mapenzi mazito ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuona vijana wake wanainuka kiuchumi zile feddha shilingi milini 10 ambazo zimetoka zinakwenda kufanya kile ambacho kimekusudiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala zima la watoto wetu walemavu. Leo hii tukitoka tukaenda kwenye vijiji vetu hatujaona kwamba kuna ile kasi ya kuona kuna vitenda kazi ambavyo vinapelekwa kwa watoto wetu ili waweze kujitoa hapa na kwenda sehemu nyingine mfano shuleni. Watoto wetu wenye ulemavu hasa kipindi hiki cha mvua wamepata shida sana lakini wangekuwa wanavitu vya kuwatoa sehemu moja mfano wheel chair au viti mwendo vya kuwatoa sehemu moja na kwenda mpaka shule wasingeweza kukaa nyumbani. Niiombe Serikali iweze kuliangalia hili kwa mara nyingine kuona watoto wetu na vijana wetu wanaweza kusoma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajira zinatolewa kila siku lakini sijaona 3% ya watu wenye ulemavu. Tunaingia ofisini sijawaona walemavu walioajiriwa. Kama mama napata uchungu mkubwa kuona wale watoto wetu wamesoma lakini ajira zikitoka hatuwaoni kwamba wameingia na wenyewe kwenye ajira ambazo zimetangazwa. Kwa hiyo, niiombe Serikali kuweza kufuatilia 3% ili watoto wetu wenye ulemavu waweze kupata ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mfuko wa maendeleo ya vijana wa kukuza uchumi kwa vijana. Mfuko huu ulianzishwa kwa lengo la kuwainua vijana kuweza kujiajiri na kuajiriwa. Changamoto ya mfuko huu ni bajeti ndogo. Niiombe Serikali itenge fedha kwa ajili ya mfuko vijana. Vijana tulionao ni wengi ambao wanahitaji kuwezeshwa waweze kujiajiri na waweze kuajiriwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niiombe sana Serikali iweze kulichukua hili bajeti ambayo ni ndogo na vijana wetu ni wengi waweze kupata ajira. Vijana wetu waweze kuondokana na janga kubwa lililopo la umasikini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu napenda nizipongeze taasisi zifuatazo:- taasisi ya OSHA, NSSF, PSSSF na WCF kiukweli taasisi hizi zimekuwa zikifanya kazi nzuri. Sisi kama Kamati tunazipongeza taasisi hizi kwa kazi nzuri wanazozifanya. Tunaomba waendelee kuwekewa bajeti nzuri hizi kazi ziende kutendeka vizuri na wananchi wetu waweze kupata huduma, nashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)