Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge kuhusu Wakala wa Kimataifa wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (International Renewable Energy Agency - IRENA) na Azimio la Bunge kuhusu mapendekezo ya kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Taasisi ya Dawa ya Afrika wa Mwaka 2019 (Treaty for the Establishment of the African Medicine Agency - AMA)

Hon. Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Azimio la Bunge kuhusu Wakala wa Kimataifa wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (International Renewable Energy Agency - IRENA) na Azimio la Bunge kuhusu mapendekezo ya kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Taasisi ya Dawa ya Afrika wa Mwaka 2019 (Treaty for the Establishment of the African Medicine Agency - AMA)

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia. Kwa sababu ya muda na kwa sababu nilikuwa nimejiandaa sana na upande huu nitachangia eneo moja tu upande wa Mkataba wa Kuridhia Uanzishwaji wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niseme kwamba mimi ni mdau wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi; kwa hiyo kitendo cha Serikali yangu japokuwa ni baada ya miaka ya kumi na nne na wameishajiridhisha kwamba imetosha sasa wametuletea Bungeni ili kujadili na kuridhia. Jambo ambalo niko proud sana na nchi yangu kwa sababu ni kitu ambacho kina faida nyingi na mkataba huu watu wote wenye mkataba wameuona, una ibara ishirini. Kimsingi Ibara zote zimejielezea vizuri sana mambo yetu ya msingi, muundo uendeshaji na kila kitu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ni concern yangu iko kwenye miongoni mwa Ibara ambazo ziko humu ambazo kimsingi ni nzuri pia. Kwa sababu tunajua kuna mashaka, na nikubaliane na Wajumbe wa Kamati pia na wao pia wameeleza kwamba inawezekana tukawa tunaingia mkataba huu lakini pengine ikatuzuia kufanya shughuli zetu nyingine. Kwa hiyo kitu kizuri ni kwamba tunaweza kujitoa wakati wowote tutakapoona mambo hayaendi.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa sababu nilisema nini ni mdau wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi, nilisoma andiko moja la Tume ya Muhamo wa Nishati ya Ulimwengu energy transition commission (ETC) ambayo ilizungumzia kuhusiana na clean electrification kama primary route to decarbonization, hicho ni kinyaturu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tume hii imezungumzia namna ambavyo kuna umuhimu wa kuelekea kwenye nishati jadidifu au nishati safi ili kupunguza ongezeko kubwa la mabadiliko ya tabianchi ambalo lina athari kubwa kwa jamii yetu; kwa hiyo ni kitu cha msingi sana. Na wote tunafahamu kwamba mpaka sasa hivi nishati jadidifu tunayozungumza ambayo tunaenda kupata mitaji baada ya kuridhia mkataba huu inaenda kuongeza nguvu kwenye nishati jadidifu ambazo sasa hivi zinachangia kwenye gridi ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu kwamba mpaka sasa hivi gesi asilia ni asilimia 62.12, maji ni asilimia 32.33, mafuta ni asilimia 4.96 na tungamotoka asilimia 0.59. Kwa hiyo bado tunaona tunahitaji kuongeza nguvu kwenye nishati jadidifu, huu ndio uwezo wetu kwenye gridi ya Taifa. Kwa hiyo ninafurahi kwa sababu hata sisi watu wa Singida sasa kwa kupitia kuridhia mkataba huu tunavutia wawekezaji ili tupate mitaji ili twende tukaanzishe Miradi ya Umeme wa Upepo Singida na kwingineko, kama vile Tabora pamoja na nishati ya jua ambayo ni sehemu ya nishati jadidifu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia pale Songwe kuna joto ardhi, nilienda pale kutembea kwa ajili ya kukagua wakati ule nikiwa kwenye Kamati ya Nishati. Ukweli ni kwamba tuna-resource kubwa sana pale lakini hatuna mitaji ya kwenda kufanya uzalishaji kwa ajili ya kupata umeme unaotokana na nishati ya joto ardhi. Kwa hiyo mimi kwangu ni furaha kubwa na ni mafakio kwa sababu tunakwenda kuvutia uwekezaji ili tupate fedha kwa ajili ya kwenda kuanzisha project hizi za kuongeza nguvu kwenye gridi ya Taifa, kwenye nishati jadidifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia niko kwenye Kamati ya Elimu sasa hivi; tumeenda kukagua pale Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Nishati Jadidifu na training, training center cha ku-train pale Arusha ETC. Pale kuna uwekezaji mkubwa lakini bado hakuna infrastructure. Kwa hiyo kuridhia mkataba huu kutakuwa ni sehemu moja wapo katika kuelekea katika kutafuta mitaji kwa ajili ya kwenda kuwekeza miongoni mwa miradi ambayo inahitaji fedha ikiwemo mradi ule wa pale Arusha ambao ni kituo ambacho tunategemea kiwe center of excellence kwenye masuala ya nishati jadidifu, kwa hiyo kwangu mimi ni kitu kikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia niseme pamoja na kwamba tulikuwa hatujaridhia mkataba huu bado niko proud na nchi yangu kwa sababu tuliweza ku-establish mradi mkubwa kama Mwalimu Nyerere. Na hizi takwimu zitabarika muda si mrefu kwa sababu ujenzi kwenye Mwalimu Nyerere unaendelea na soon unafika asilimia mia, kwa hiyo story itabadilika sana, na ni lazima tukubali kwamba hatujachelewa; kama tuliweza kuanzisha project kubwa ile ambayo ni ya kwanza katika Afrika Mashariki na ya tatu kwa Afrika. Wakati tunatumia resources za ndani maana yake ni kwamba sisi tunatakiwa tujipige kifua mbele, kwamba tuliweza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ndiyo maana tunasema ni sehemu tunaenda kuongezea katika kuendelea kufanya investment ili tuendelee kuwa na upatikanaji wa umeme wa uhakika kwenye Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini bado ipo Mikataba ya Kimataifa ambayo nchi yetu ilikubali kiasi kuridhia, bado hatuja-ratify. Niwaombe sana Serikali muendelee kujiridhisha, pelekeni watalamu wapitie mikataba ile ambayo mingine ina faida kwenye nchi ili muilete tuijadili na kuipitisha katika Bunge hili Serikali yetu ipate manufaa na wananchi wapate manufaa kwenye mikataba hiyo ya Kimataifa, ahsante. (Makofi)