Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon. George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nikupongeze kwa kuwa Spika wa Mabunge yote Duniani, hongera sana Mheshimiwa Spika wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nimeanza kuona viwango vya Uspika wa Bunge la Dunia kwa namna ambavyo una-balance. Eeh, ni Rais wa Mabunge Duniani. Niwie radhi kwa kushusha kidogo. Wewe ni Rais wa Mabunge yote Duniani na viwango hivyo vimeanza kuonekana hapa namna ambavyo umekuwa referee mzuri leo katika hizi timu mbili na ndio raha ya Bunge. Bunge lina pande mbili lazima pande zote zipewe nafasi. Nakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inasimamia masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Katika misingi ya utawala bora vipo vyombo ambavyo vinatusaida kutekeleza majukumu yetu. Moja kati ya vyombo vinavyotusaidia katika kusimamia uwajibikaji wa matumizi ya fedha ni Ofisi ya CAG. Ofisi ya CAG ikishafanya kazi yake, vipo vyombo vingine vinavyokwenda kusimamia na kuangalia utekelezaji wa yale yaliyoonesha mashaka katika Ripoti ya CAG. Moja wapo katika vyombo hivyo ni PCCB ambayo inasimamiwa na Wizara yangu.

Mheshimiwa Spika, ninataka nikuhakikishie kwamba katika misingi ya utawala bora CAG amefanya kazi yake vizuri sana na ninawashukru sana Waheshimiwa Wabunge wote, kwa kupongeza Ripoti ya CAG na kama tukitaka compromise misingi ya utawala bora ni pale tutakapodharau Ripoti ya CAG. Tusidiriki hata mara moja kufanya hivyo tuendelee kushughulika na haya mapungufu kama tunavyofanya na hivi ndivyo mnavyotakiwa kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, isionekane hata mara moja kwamba sisi Mawaziri tunaposimama kutoa taarifa tunatetea wahalifu, hapana. Sisi Mawaziri tunatoa taarifa kwa maeneo ambayo tunadhani pengine wenzetu wanaweza wakawa hawana taarifa ili waweze kupata taarifa na wala hata mara moja si nia yetu kuwatetea wezi, wahujumu uchumi, hapana, hatufanyi hivyo. Serikali hiyo hapo huku ndani haipo hapa Tanzania, tumekuwa tukichukuliana hatua na nitakuonesha ushahidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa miaka mitatu kutoka 2021, 2022 mpaka Oktoba, 2023 PCCB kutokana na Ripoti za CAG imefungua kesi 1,790. Katika kesi hizo 1,790 kesi ambazo Serikali tumeshinda yaani watu wametiwa hatiani na hawa wamo humo na hao wote mnaozungumzia wapo humo, Wakurugenzi wapo humo, accountants, wapo watu mbalimbali ambao wameshughulikiwa. Katika kesi hizo kesi 965 wametiwa hatiani wapo magerezani na wengine wamefukuzwa kazi na hatua nyingine za kisheria. (Makofi)

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Haya Mheshimiwa Simbachawene kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere.

TAARIFA

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ninataka kumpa taarifa mzungumzaji kwamba, PCCB ambao wanaoshughulika na mambo ya kesi, hivi wale TAKUKURU wa Kilimanjaro ambao KADCO imekatalia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, hawajachukua hatua?

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, ametoa taarifa yake kwa namna ya swali kwa hivyo hulazimiki kujibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa hiyo mpaka sasa, kesi 965 Serikali imeshinda na kesi 621 zinaendelea, zipo katika ngazi mbalimbali. Kazi kubwa imefanyika kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais aliyepokea ripoti, kazi ilianza kufanyika kuanzia wakati ule.

Mheshimiwa Spika, tulibadilisha kanuni hapa, tukabadilisha sheria. Tukasema ripoti ya Serikali ya namna tunavyoripoti, tutakuwa tunaleta kabla, tulileta Bunge lililopita. Tumefanya hatua fulani kubwa na mpaka leo hii tunaendelea kutekeleza. Mathalani, katika fedha ambazo TAKUKURU imezirejesha, zilizokuwa zimepigwa, nitumie lugha hiyo hiyo inayotumika. Zilizokuwa zimepotea ni Sh.14,274,000,000 pesa za Kitanzania pamoja na dola 14,571.

Mheshimiwa Spika, la pili, mali zilizotaifishwa ambazo zilikuwa zimepatikana kwa njia hiyo ya mapato yasiyo halali ambazo tumezirejesha (tumezitaifisha) zina thamani ya Sh.2,051,000,000.

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Simbachawene kuna taarifa nyingine kutoka kwa Mheshimiwa Mpina.

TAARIFA

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, mchangiaji anaendelea vizuri lakini kwenye taarifa ya majumuisho ya majibu ya Serikali ambayo ina kurasa 1,111, hilo jambo analolizungumza na hatua anazozizungumza hazimo kwenye majibu ya Serikali.

SPIKA: Sawa. Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Waziri anaweza akasema ni kipindi gani, lakini ile taarifa mtakumbuka ililetwa hapa Bungeni mwezi Juni, nadhani Tarehe10. Kwa hivyo, kwa maelezo ya Waziri nilivyomsikiliza labda kama nimemsikia peke yangu, amesema tangu taarifa hiyo iletwe yapo mambo mengine yaliyofanyika katika hiyo miezi kuanzia Juni. Kama hivyo ndivyo, inawezekana yale majibu yalipokuja mwezi Juni mpaka sasa ndiyo hizi hatua anazozisema, lakini kama Bunge bado nafasi yetu ipo pale pale ya kuendelea kufuatilia utekelezaji wa haya ambayo Serikali inasema imeyafanya. Mheshimiwa Simbachawene.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ni kweli. Hii ni mpaka Oktoba yaani mpaka mwezi huu uliopita, ndiyo Serikali tumefanya hizi kazi zote. Kwa hiyo, kusema Serikali haijachukua hatua yoyote, nilitaka nitoe taarifa kwa Waheshimiwa Wabunge kwamba hatua zimechukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika, fedha tunazozungumzia za POS, mpaka sasa tuna kesi ya uhujumu uchumi kesi Namba ECC 32 ya Mwaka 2023 ambapo, watuhumiwa 16 wanaotuhumiwa kupoteza au kufanya ubadhirifu kwenye karibu shilingi 8.9 billion out of ile bilioni 11 waliyoisema kwenye mashine za POS.nnKatika fedha hiyo, 8.9 billion zote hizi watu wapo tasked na kesi zimefunguliwa na wapo mahakamani.

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Haya ahsante sana, kuna taarifa kutoka kwa… sasa Waheshimiwa mmesimama watatu wote mnataka kutoa taarifa kwa mchangiaji mmoja? Mheshimiwa George Kakunda.

TAARIFA

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, maneno ambayo ameyazungumza Mheshimiwa Waziri ni muhimu sana, lakini naomba nimpe taarifa kwamba, Maafisa Masuuli walipokuwa wanakuja kwenye Kamati, walikuwa wanakuja kujibu hoja ambazo wamekaa na CAG siku tatu zilizopita. Kwa hiyo, ni muhimu Serikali ikiri kwamba, bado kuna kazi kubwa ya kufanya ya kurekebisha mambo.

SPIKA: Mheshimiwa Simbachawene unaipokea taarifa hiyo?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, naipokea kwa sababu kazi hii ni endelevu. Hii kazi ni endelevu, tunashughulikia uhalifu. Waheshimiwa viongozi tuzungumzie mambo halisi, yaani tusitafute humu, hii kazi ni endelevu, inaendelea. Mimi ninavyozungumza, out of ile 11 billion, so far 8.9 billion tayari tumekwishazirejesha Serikalini. 5.2 billion zilizokuwa zimepotea kwenye POS Machine. Hii ni kutoka kwenye Halmashauri ya Ilala, Ilemela na nyingine nyingi zimerejeshwa kwa sababu ya kazi nzuri inayofanywa na TAKUKURU.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo…

SPIKA: Muda wako umekwisha. Sekunde 30 malizia.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nimalizie. Imeelezwa hapa kwamba watumishi wa Serikali hawajalipwa malimbikizo ya mishahara. Hivi ninavyozungumza mpaka mwezi Oktoba Serikali ya Awamu ya Sita imelipa watumishi 137, 599, fedha zenye thamani ya shilingi bilioni 235.16. Hizi fedha zipo kwenye halmashauri zetu, watumishi wetu wamelipwa.

Mheshimiwa Spika, nimetembelea mikoa minne tulivyomaliza Bunge, nimeenda ninakuta furaha waliyonayo watumishi wetu. Kwa hiyo, nimalizie. Watumishi wa nchi hii, pamoja na mapungufu yanayozungumzwa hapa, lakini wapo waliofanya vizuri na ndiyo maendeleo tunayoyaona. Hao wachache ambao wanafanya vibaya tutawashughulikia na sheria zipo na ndiyo maana ya utawala bora. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi