Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo

Hon. Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia katika Wizara hii ya Kilimo. Kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya kama vile lile alilolifanya hivi karibuni, watumishi wa umma wanashukuru sana kwa ongezeko la mishahara, lakini na kima cha chini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba bajeti iliyopita ya Kilimo, mwaka wa Fedha uliopita, nilisimama hapa nikasema sitampongeza Waziri mpaka pale atakapomaliza matatizo yaliyoko kwenye ushirika. Sasa kwa kuwa ameshaanza kumaliza matatizo yaliyoko kwenye ushirika, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri na wananchi wa Jimbo la Hai wanampongeza, si tu kwenye ushirika lakini kwenye mambo makubwa aliyoyafanya ndani ya Jimbo la Hai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hakika anaitendea haki Wizara hii, tukimsikilizam tukiona matendo yake na namna anavyoenenda anafanya vizuri sana, ashikilie hapo hapo, imani ambayo Mheshimiwa Rais amempa kwenye eneo hili ana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko afanye kazi hiyo, nampongeza sana. Nampongeza pia kwa kuwa ameamua kwenda kutengeneza common use facility pale Hai, tunamshukuru sana. Nimeona humu kwenye hotuba ametuwekea fedha kwenye skimu, tunamshukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia niseme hili, kwenye ushirika tuna matatizo makubwa sana. Tunamshukuru kati ya vyama 40 vilivyoko Siha na Hai vyama 20 ameanza navyo na kwenye vile vyama vyama viwili amefuta mikataba yao, namshukuru sana. Hii ilikuwa changamoto kubwa sana. Hata hivyo, nimwambie nampongeza kwamba, ameweza kuvuka hila za hawa watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaambie ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge, katika eneo ambalo lina matatizo katika nchi hii ni ushirika, lakini Mheshimiwa Waziri huyu ameweza kuruka hila zao. Kitendo cha kukubali na kuvunja mikataba ile najua ameruka hila za watu wa ushirika na ameungana na wananchi wa Jimbo la Hai, namshukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimwombe Mheshimiwa Waziri, yale mashamba ambayo tumevunja mikataba, sasa tunaanza utaratibu upya wa kutengeneza mikataba mipya yenye tija, ikiwemo na Shamba la Makoa. Lile Shamba la Makoa najua Waziri anavyosumbuliwa, ameshapewa barua lakini bado anahangaika mtaani. Nimwambie tu Mheshimiwa Waziri, yule mwekezaji pale amekaa miaka mingi, hakuna alichokifanya, ametutia hasara, tumeshaamua, ushirika wenyewe wamepiga kura wakasema aondoke, nimwombe Waziri, aondoke kweli kweli. Najua anapita huku na huku kwenda kwa viongozi wakubwa kubembeleza arudi, sisi watu wa Hai hatumtaki, labda kwa kifupi wamwambie tu kwamba hatumpendi kwa sababu amerudisha maendeleo yetu nyuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka sasa hivi, katika lile eneo tutafute mtu anayeweza kutufanyia biashara pale, sisi tulienda anafanya ufugaji pale, Halmashauri ya Wilaya ya Hai haipati chochote, haajiri pale kwetu, hatuna tunachonufaika nacho. Tulienda pale na Waziri wa Maliasili na Utalii akiwa na viongozi wake wakuu hakuna chochote, mikataba iliyoko pale ni ya hovyo, yule pale ni dalali. Kama tunataka mwekezaji, basi awe ni mwekezaji mwenye tija, aje pale kwa ajili ya kufanya biashara ambayo ina tija kwa Halmashauri ya Hai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Waziri pale tumeshatengeneza business plan ambayo itatusaidia. Pale kuna biashara ya utalii, biashara ya kuuza vitu vya utalii, lakini kuna kilimo mle ndani na bahati mbaya sana ameua kinu chetu cha kahawa pale, lakini bado anaendelea kung’ang’ana anataka kurudi na kuzunguka huku na huku, hatumtaki, pamoja na wapambe wake. Mheshimiwa Waziri ni kwa sababu tu amenipa hela nyingi, nilikuwa nimejiandaa kweli kumwonyesha vitu ambavyo anafanya visivyofaa pale, ila kwa sababu ametupa hela nyingi na yeye anatusikiliza narudisha hapa. Hata hivyo, ujumbe wetu, hatumtaki, tutatafuta utaratibu mwingine wa kupata mwekezaji tuendelee pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nizungumze hivi, hivi vyama vya ushirika vinapata shida lakini ipo Taasisi ya Uchunguzi na Ukaguzi, hawa watu wanatusaidia jambo gani? Wanakagua kitu gani? Niombe wapewe fedha ili wafanye kazi yao, waende wachunguze vyama hivi, wamefanya uchunguzi, Mheshimiwa Waziri kwenye taarifa yako unasema, kuna hati mbaya Tanzania nzima 1,729, wanachukua hatua gani? Kama kuna sheria ina upungufu, iletwe hapa ifanyiwe marekebisho ili tuwape meno, waweze kusimamia matatizo yaliyoko kwenye ushirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza watu wa Hai, ugomvi na ushirika umekwisha kabisa, viongozi wangu wa ushirika tunasikilizana, tunazungumza lugha moja sasa hivi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)