Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Hon. Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuweza kunipa fursa ya kuchangia pamoja na kwamba siko vizuri kiafya, lakini nitajitahidi kuchangia kwa kadri nitakavyoweza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nitakwenda kuainisha kwa nini natoa pongezi zangu kwa mwanamama huyu ambaye ni Rais wa kwanza wa kike Tanzania. Kwanza kabisa, sote tunajua mazingira yaliyotokea Tanzania ambapo tulipotelewa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Mheshimiwa Hayati Magufuli na akawa ameacha miradi mingi ya kimkakati ambapo wengi wetu walibeza labda nafikiri kwa sababu ya jinsia yake. Hata hivyo, mama ameweza kuendeleza miradi hii kwa ufanisi mkubwa sana pamoja na kwamba kuna kuyumba kwa uchumi duniani lakini Mama ameweza kuhakikisha kwamba miradi yote inaenda na kwa ufanisi mkubwa na haya ni maendeleo kwa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, sote tutakubaliana kwamba Mama amehakikisha kwamba analeta demokrasia nchini. Ameweka uhuru wa mtu kujieleza iwe anatoa mawazo chanya au mawazo hasi, bado kila Mtanzania yuko huru kuweza kutoa mawazo yake. Tumeona hata sisi wa vyama vya upinzani tumepewa nafasi hata ya kuweza kufanya mikutano ya hadhara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hayo tu, kwa mara ya kwanza Rais ambaye kwa wenzetu ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ameweza kuhudhuria Kongamano la Kitaifa la BAWACHA, la chama pinzani na wakati huo ilikuwa ni siku ya Kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani akaweza kuacha Chama chake akaenda. Kwa kweli hii inajenga confidence, sio tu kwa vyama vya upinzani lakini pia hata kwa wawekezaji. Vile vile, hata kwa mataifa mengine tumeona uhusiano umekuwa ni chanya sana. Kwa hiyo hii pia inaweza kujenga confidence na watu kuja kuendelea kuwekeza Tanzania na hivyo kuweza kuona maendeleo yanatamalaki. Kwa hiyo, nimeona lazima nimpe credit hii Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipitia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bajeti, kwa kweli naiunga mkono na naiomba Serikali iweze kuchukua mapendekezo yote ambayo yameainishwa kwenye taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bajeti. Siwezi kuyasema yote kwa sababu muda ni mchache, lakini tumeona yameainishwa kwamba hata utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2022/2023 ambapo tulitenga fedha trilioni 15.1 mpaka kufikia mwezi wa nne ambayo ni quarter ya tatu tayari zilikuwa zimeenda shilingi trilioni 11.5. Ina maana kwa fedha zilizotolewa kwenda kwenye matumizi ya maendeleo mpaka tunakwenda kumalizia ni rai yangu itakuwa pia imefikia kwenye zaidi ya asilimia 80 au 90 kwa sababu sasa hivi ni asilimia 76.5. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huko nyuma tulikuwa tukija ku–discuss hapa wakati wa bajeti unakuta hata asilimia 50 ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo haujafikia. Kwa hiyo, hii ni credit ya kuona kwamba Rais ana dhamira ya dhati ya ku-push maendeleo kwa wananchi. Pia unaweza ukaona hata kuna miradi mbalimbali ya kimkakati imeelekezwa kwenye elimu, afya, maji ambayo kwa kweli ni tangible na unaweza ukaona. Hata ukikaa ukawa unashawishi Watanzania watoe kodi wanatoa wakiona kuna vitu vinakuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanaweza wakakaa kama wanafanya analysis ya kina waka–compare utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka huu na miaka mingine ya nyuma, then watumie kama basis ya kuweza kushawishi Watanzania. Kwa kweli hii hata wale ambao wako responsible kuhakikisha kwamba wanatangaza yale mema yaliyofanyika you are not doing your job well. Wakifanya vizuri na kuainisha watajenga confidence kwa Watanzania waweze kulipa kodi, waweze kwenda kununua vitu au bidhaa na kuhakikisha kwamba they pay na kuomba risiti kwa sababu wanaona service delivering zinavyofanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona hata kwenye Sekta ya Afya, sasa hivi niko kwenye Kamati ya PAC, nimetembelea miradi tumekwenda Mtwara na kwingineko, unaona hizi hospitali za rufaa na vifaa vya kisasa ambavyo vimewekwa. Ukienda unaona kabisa kuna hospitali za mikoa zimejengwa, hospitali za wilaya zimekarabatiwa. Kwa hiyo, for the first time baada ya miaka sita tumeona ajira zimetolewa kwenye utumishi wa afya ingawa bado ni kidogo sana elfu nane mia tisa na kitu, it’s a credit, so we need to compliment this na kushawishi Watanzania waendelee kutoa kodi kwa kina. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda pia kwenye sekta ya elimu the same thing applied tunaona VETA kila wilaya zinajengwa. Haya ni maendeleo, ukiwekeza kwenye elimu ndio unaweza kwenye uchumi wa Taifa letu. Tumeona shule za sekondari za wanawake za sayansi. Tumeona pia kuna miradi mingi ya shule inajengwa huko na imepunguza hata adha ya wananchi kuchanga. Sasa haya yote ukieleza mwananchi ataona kweli nikinunua kitu kwa shilingi elfu kumi natakiwa nipewe risiti yangu ili ile kodi iende ikaendeleze maendeleo kule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana, watendaji wa Serikalini na Mawaziri, sell out these things ambazo zinafanyika ili watusaidie Watanzania waweze kutoa kodi. Hii kodi ambayo tunakusanya sasa hivi na tunajisifia TRA it is just a peanuts nawaambia. Tukiwekeza na tukaondoa mianya yote ambayo inapotea kwa TRA, watu wakalipa kodi kwa asilimia zote, tutapata hata trilioni 60. This is the second time I am saying this in this House. Malipo yanayopatikana kupitia TRA it’s just a peanut. Tuelimishe umma, tuzibe mianya ya utakatishaji wa fedha. Tuhakikishe kila Mtanzania au kila mtu anayefanya kazi Tanzania analipa kodi kwa uhalisia, tutampunguzia hata burden Mheshimiwa Rais kwenda kuomba nje. Tutapata fedha ndani ya nchi, tutawekeza kimkakati na tutaleta maendeleo and this is what we are seeking for.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye maji na umeme, mimi mpaka kule kijijini kwa Mzee Matiko tuna umeme na tuna maji. Ila sasa nitoe warning, zile takwimu wanazozitoa sasa hivi kwa mfano, wakisema maji vijijini asilimia 77 na mjini asilimia 88, ni kweli yamefika kwenye center. Sasa ni wajibu wa Serikali kwenda kuwekeza kuhakikisha kwamba wanasambaza maji, mtandao wake unafika kwa wananchi wote kwenye mitaa na vijiji vyote. Equally wanasambaza umeme unafika kwenye vitongoji na mitaa yote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mathalani kwa Mkoa wa Mara, ukipitia statistics inakwambia vijiji vyote vimepata umeme, lakini kuna vitongoji bado havijapata na wananchi hawana umeme. Kwa hiyo, tunafikaje hapa? Ni kwa kuhakikisha kodi zinapatikana kwa kina ili miradi hii iweze kusukumwa na wananchi waweze kupata umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, nihame kwa sababu muda ni mchache sana niende kwenye Magereza. Kuna siku niliongea hapa Mheshimiwa Waziri wa Fedha akaniita mimi ni balozi wa hawa Maaskari na kwa kweli nitaendelea kuwatetea. Askari wetu wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana. Mimi ni shahidi kwa sababu nimewahi kuishi huko, walinipeleka nikaishi huko. Kwa hiyo, nikawa naona vitu vingine ambavyo nimeviona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Askari Magereza wametumikia nchi zaidi ya miaka 26 na narudia hii tena na hata Mheshimiwa Rais alisema, unakuta Mtu anastaafu yuko kwenye Staff Surgent ni kwa sababu ya mazingira ambayo sio rafiki ya kuwahakikishia hawa Watanzania wanaojitoa wanapandishwa vyeo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kuna Askari Magereza anakaa zaidi ya miaka mitano wakati utaratibu unasema kila baada ya miaka mitatu wapandishwe cheo lakini unakuta anakaa zaidi ya miaka mitano hajapandishwa cheo bado yuko kwenye Staff Surgent, ameshatumikia zaidi ya miaka 26 anamaliza katika cheo hicho, kwa hiyo, tunaomba sana mhakikishe kwamba hao Askari Magereza wanapandishwa na Maaskari wengine wote wapandishwe vyeo kulingana na inavyotakiwa. Maaskari ikitokea mfungwa amekimbia anapigwa faini ya kutopandishwa cheo miaka mitatu, halafu anakatwa nusu mshahara mbaya zaidi huo mshahara unaokatwa unapelekwa sijui kwenye mfuko maalum wa Kamishna wa Magereza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua hii hela anayokatwa ya mshahara wake unaenda kwenye mfuko maalum wa Kamishna wa Magereza inakuwa accounted vipi? Naomba wakati Mheshimiwa Waziri unakuja hapa utueleze inakuwa accounted vipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia wanadai madeni kwa miaka mingi hawajalipwa, tunaomba walipwe madeni yao, pia muwatoe utumishi muwapeleke kwenye consolidated fund kama wengine, yaani hao Magereza mnawaonea sana, hata mishahara yao ni tofauti na Majeshi mengine ambayo yako kwenye Idara hiyohiyo ya Mambo ya Ndani, muweze ku-revisit muwatie moyo. Hawa watu wanakaa na wale watu tunaowapeleka kama Magaidi, hawa watu wanakaa na watu wa tabia mbalimbali lakini wanaangalia at a high risk, msipoangalia vizuri ndiyo wanaweza kuongeza vishawishi vya kufanya mambo mengine ambayo hayatakiwi katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kuweza kupandisha mapato tumeona upotevu. Mwenzetu alisema hapa kwamba waweze kutoa motisha, hizi EFD zinatolewa alisema waweze kukaa kwenye mambo ya simu, mimi nilikuwa na-suggest kama tutaweza tunaona hii kwa mfano ukipata risiti unakuta kuna wakati mwingine umewekewa token pale, labda siku nyingine ukienda ukalipa unakuta una laki moja na milioni moja na milioni mbili watu watakuwa wanashawishika kuomba risiti wakijua wanaweza wakabahatika wakapata hiyo token ambayo unakuta imeandikwa kwenye risiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine naomba sana soko la kimkakati la Lemagwi liweze kujengwa kule Tarime ambalo litasaidia, leo tumeona malori mengi yamerundikana kule Sirari, hili soko likijengwa na Mheshimiwa Bashe aliahidi hapa kwamba masoko ya kimkakati ambayo yako pembezoni kwenye maeneo yote yaweze kujengwa, litasaidia kuweza kuuza mazao yetu pale watu wa Kenya watakuja upande wa pili ina multiply effect, uchumi utabaki Tanzania. Tunaomba sana mnipe majibu hili soko linaenda kukamilika lini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni uwanja wa ndege katika kukuza utalii wetu. Mheshimiwa Rais ametangaza Royal Tour na tumeona kwamba Utalii walau umeongezeka lakini bado tuko chini sana, siwezi kupita takwimu nadhani muda umeenda. Kama vile tu baada ya Royal Tour ya Rais, utalii umeongezeka zaidi ya asilimia 190 kwa ndani na kwa watalii wa nje zaidi ya asilimia Hamsini na kitu na mapato yame-trip yameenda zaidi ya asilimia tisini na kitu huko, tunaomba muwekeze kuhakikisha kwamba kwanza mnavitambua vivutio vya utalii, mnavitangaza, mnaweka vivutio vya kikodi. Tanzania tulitakiwa tuwe na turn out ya kuchangia, yaani utalii uchangie kwenye Pato la Taifa kwa fedha nyingi sana, pia utatangaza vivutio vingi. Utalii ungekuwa ni moja ya kitu cha kutuingizia fedha za kigeni, tukiwekeza dola moja kwenye utalii tutavuna zaidi ya dola kumi na hatuta regret, tukifanya hivi tutarnda kuongeza mapato ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumeangalia kwenye kingine.. ooh my god! cha kumalizia sasa maana naona hata karatasi zangu nimezi-arrange zimeenda ndivyo sivyo.

MBUNGE FULANI: Unga mkono hoja.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, siwezi subiri. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeomba kujengewa uwanga wa ndege Mugumu uweze kukuza utalii lakini pia kuhakikisha kwamba barabara zinazopita kwenye mbuga zetu zile ambazo zinapita kuunganisha Mkoa na Mkoa ziweze kujengwa hata kwa lami nyepesi tuangalie na wenzetu wanafanyaje, ile barabara iliyopo pale siyo rafiki hata kwa utalii kuwa attracted. Kwa hiyo, tunaomba sana tukifanya haya mambo na tukatoa fedha za kutosha kwenye Mamlaka zote ambazo ziko chini ya Maliasili na Utalii tunaenda kukuza uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa ni fedha kuweza kupanga ardhi yetu. Ni aibu kwa kweli kwa Taifa letu kuona kwamba baada ya uhuru sasa hivi kwamba vijiji 2,600 tu ndiyo vimepimwa, zaidi ya vijiji 12,000 havijapimwa, tukipima ardhi yetu tutakuwa na mpango mzuri wa kujua mifugo inafugwa wapi, kilimo ni wapi, uvuvi ni wapi na tukiwekeza kwenye uvuvi nilikuwa nimesahau, naomba dakika mbili tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba dakika mbili tu. Sasa hivi eti sekta ya uvuvi inachangia trilioni 1.8 kwenye Pato la Taifa. Uvuvi ambapo tuna bahari, tuna maziwa, nilitaka kuyataja hapa lakini tu muda umeenda, tunachangia asilimia 1.8 kwa Pato la Taifa ambapo kwa mwaka uliopita tunasema ilileta zaidi ya trilioni tatu. Tukiwekeza kwa kina kwa vifaa vya kisasa uvuvi utaenda kuleta zaidi ya trilioni saba trilioni kumi na tutakuwa hatuna hata bajeti tegemezi. (Makofi)