Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, naomba nichangie hoja hii kwa kushauri yafuatayo; kwanza Wizara ifanye utafiti wa kutosha kubaini chanzo cha tembo kwa nini wameamua kuhamia kwenye maeneo ya binadamu, tuondoe dhana ya ushoroba kuwa ndio chanzo cha kadhia hii. Je, huko nyuma miaka minne iliyo pita shoroba hizi hazikuwepo? Mbona migogoro haikuwa mingi hivi? Kuja na majibu mepesi wakati watu wanauawa na tembo kila siku hakuisaidii Serikali. Tembo wamebadili tabia hawataki tena kukaa hifadhini na hata ulaji pia hawataki tena majani ya porini wanatamani mazao ya wakulima ndio maana tunasumbuana nao kila kukicha.

Mheshimiwa Spika, kufanyike utafiti kubaini hizo zinazoitwa shoroba ili kuzibaini na kujua idadi na kuona namna gani ya kuzilinda ili kila kwenye shoroba kuwe na kituo cha askari wa wanyamapori ili kulinda shoroba husika

Mheshimiwa Spika, ushirikishwaji wa wananchi kwenye uhifadhi ni mdogo sana na haulingani na nguvu zinazotumika kwani kufanya kazi ya uhifadhi kwa kutumia nguvu bila ushirikishwaji haiwezi kuleta matunda yanayotarajiwa. Hivyo basi Wizara ione namna ya kuelimisha jamii umuhimu wa hifadhi badala ya kupiga watu kila kukicha. Kitendo hiki kinakuza chuki baina ya wahifadhi na wanajamii.

Mheshimiwa Spika, watumishi wa Wizari hii walio wengi wanafanyakazi kwa mazoea na kukomoana ndio maana hata Waziri akija na malengo mazuri kwenye Wizara hii hawezi kukaa kwani atakuWa anakwaza maslahi yao binafsi na hivyo wanamhujumu makusudi na hatimae ataonekana hafai. Uwajibikaji wa pamoja kwenye Wizara hii ni msamiati mgumu sana na ndio maana migogoro haiishi ndani ya Wizara hii.