Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Haji Amour Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makunduchi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. HAJI AMOUR HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii, kwanza kabla ya yote nampongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Pili nakupongeza wewe kwa namna ya unavyoweza kufanyakazi zako pia na namna ya philosophy ambazo unazozitumia katika Bunge letu hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tatu nawapongeza, nampongeza Waziri pamoja na Naibu Waziri wa Wizara yetu hii ya Utalii pamoja na mambo ya natural resource mambo ya Maliasili na Utalii, lakini pamoja na yote, pamoja na kuwapongeza lakini pia nawapa pole. Kwa sababu asilimia kubwa ya Wabunge hapa wanawapongeza lakini wakati huo huo wanakuwa na kitu kama lawama kidogo na hasa kwa upande ule wa maliasili. Kwa hiyo, kwa upande ule kule mimi nawapa pole sana, kwa sababu hili jukumu la maliasili ni jukumu ambalo ni zito na kwa nini nazungumza kwamba ni suala zito? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya namna ambavyo ya uasili wake, na siku zote kitu ambacho ni cha asili maana yake siku zote kitakuwa na lawama na ulawama wa asili maana yake huja pale kwamba huna namna ya kuweza kubadilisha. Kwa sababu hapa katika Bunge letu hili utakuta kwamba Wabunge wengi wanalalamika juu ya tembo na mambo mengine kitu ambacho tembo kwa namna ya uasili wake inakuwa ni vigumu sana kuweza kubadilisha na huna namna. Naamini pengine nitakwambia kwamba muweze kukubaliana tu na hizo lawama mnazopewa kwa sababu ya ule uasili wa mambo yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili nadhani kwamba leo nijikite zaidi kwa upande wa utalii. Utalii wetu wa Tanzania ni utalii ambao ni wakimaumbile, kwa ufupi kwamba naweza kusema kwamba Tanzania hatujawa na ile vision ya moja kwa moja katika suala la utalii kwamba tunaelekea katika utalii wa aina gani?

Mheshimiwa Spika, utalii ni kitu ambacho ni kikubwa sana, na mimi kama ningekuwa natoa ushauri kwa namna ya ukubwa wa Wizara na namna ambavyo ilivyo kwamba Wizara ya Maliasili na Utalii maana yake mimi nigeliweza kushauri tu kwamba huu utalii kutokana na namna ambavyo uwekezaji wake pengine mimi ningeshauri Serikali pengine suala na maliasili likabaki na upande wake na utalii ukabaki upande wake, na kwasababu utalii kwa namna yoyote ile ni sekta ambayo inayojitegemea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukizungumzia suala la utalii. Utalii ndiyo unaojenga kila kitu, tukiangalia hasa katika masuala ya component za utalii, utalii maana yake umejigawa katika component karibu sita, kuna suala la vivutio vya utalii. Vivutio vya utalii maana yake vinajenga pamoja na hizo rasilimali ambazo ndiyo tunazozungumza za misitu pamoja na vitu vingine. Sasa huo wote ni utalii. Tukizungumzia suala la accessibility maana yake yale mambo ambayo ambayo yaliyokuwemo katika ile nchi, maana yake tukiangalia suala la fukwe na mambo mengine, haya yote maana yake tunazungumzia suala la utalii.

Mheshimiwa Spika, tukizungumzia suala la accommodation ambalo ni malazi ambayo nalo ni suala utalii. Tukizungumzia suala la amenity ambalo ni suala pengine la yale mahitaji yaliyomo katika nchi ni suala la kiutalii, pamoja tukizungumzia na activity zile shughuli zilizomo maana yake ni suala la tunazungumzia ni utalii. Sasa utalii ni kitu ambacho nachozungumza kwamba ni sekta moja ambayo ni muhimu sana na ndiyo ni sekta ambayo mama. Kwa sababu kwa nchi za wenzetu mara nyingi jina la utalii hutangulizwa mwanzo lakini sisi maana yake kwamba kama Tanzania tumetanguliza maliasili na utalii.

Mheshimiwa Spika, sasa maliasili na utalii lakini utakuta kwamba maliasili kwa upande wetu maana yake imebeba sehemu kubwa sana hasa katika masuala ya majadiliano, ukiangalia hata kwenye Bunge letu hili maana yake utalii unazungumzwa kama ni component ndogo sana. Wakati utalii ndiyo inayojenga hivyo vitu vingine, hata suala la utalii maana yake tukisema suala la utalii maana yake utalii unatakiwa iwe ni sekta mama, kwamba ni utalii ambao ni sekta ya Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale au Wizara ya Utalii na Maliasili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, utalii pengine mimi ningesema kwamba uwe unaanza mwanzo kisha baadaye ije maliasili, kwa sababu kwenye maliasili ni kitu ambacho kuna vivutio kule. Kwa sababu vivutio vile maana yake ndivyo vinavyoitengeneza hiyo sekta ya utalii katika masuala ya kibiashara, na biashara yetu maana yake tunategemea nini? Tunategemea hizo mbuga za wanyama, tunategemea nini? Tunategemea misitu, tunategemea nini? tunategemea hoteli, tunategemea nini? tunategemea fukwe, tunategemea nini? tunategemea kila aina utamaduni wetu maana yake yote, maana yake ni moja ya utalii hasa utalii maana yake tukiwa tunauweka katika sehemu ndogo itakuwa kidogo tunaupa nafasi ndogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, najua kwamba unaniangalia kwa sababu ya dakika cha msingi niunge hoja mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nasema ahsante sana kwa kuweza kunipa nafasi hii. (Makofi)