Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kumpongeza, Naibu Waziri na uongozi mzima wa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kazi nzuri ya kulinda wananchi na mali zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya changamoto ya Wizara ni kwa baadhi ya Wilaya kutokuwa na vituo vya polisi vyenye hadhi hasa katika makao makuu ya Wilaya kwa baadhi ya maeneo nchini mfano ni Wilaya ya Kilindi, Mkoani Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Mambo ya Ndani ametembela Wilayani kwangu na kujionea hali halisi ya ubovu, uchakavu na udogo wa kituo cha polisi. Naomba leo Mheshimiwa Waziri anieleze, je, ni lini Wizara itatujengea?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja, ahsante.