Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi hii ili na mimi niwe kati ya wachangiaji kwenye bajeti hii ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa natoa pongezi zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya. Na kipekee nimpongeze hasa kwa kuijali Wizara hii ambayo kufikia mei 15 alikuwa maewapatia asilimia 84.2 ya bajeti yote tuliyowapitishia mwaka jana, ambayo ni bilioni 175; lakini pia kwa namna ambavyo mwaka jana alifuta malimbukizo ya riba ya pango kwa ajili ya wale wadaiwa sugu. Kwa hili amewasaidia sana Mheshimiwa Waziri kusafisha dawati lenu ili sasa mnapoanza kusimamia jambo la makusanyo ya kodi muweze kwenda vizuri kwa kuwa yale madeni sugu Mheshimiwa Rais amewarahisishia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze kwa bajeti yenu yenye mwelekeo mzuri, wewe Mheshimiwa Waziri na Naibu wako, na tunawatakia kheri, tutakapo wapitishia mkatende yale ambayo mmeyasema kwenye bajeti yenu. Lakini pia nimpongeze Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Rukwa, dada yangu Rehema, anafanya kazi nzuri. Kwa muda mfupi ananipa ushirikiano mzuri na Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Rukwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi leo nina mambo mawili muhimu. Jambo la kwanza nitaongelea migogoro ya ardhi, na nitazungumzia specifically migogoro iliyopo ndani ya Jimbo langu la Kwera na pengine Mkoa wa Rukwa kwa ujumla. Mwaka jana katika bajeti hii tarehe 25 mei, nilisimama tena kwa uchungu mkubwa na nikaongea maneno makali sana juu ya mgogoro wa ardhi uliopo ndani ya Jimbo langu la Kwera, kwa maana ya mgogoro wa shamba lile la Malonje la Efatha. Lakini Mheshimiwa Waziri mama yangu, dada yangu, rafiki yangu jambo niliona mmelichukulia very lightly. Hamku-take very serious note kwa jambo lile kwa sababu hivi ninavyoongea hatujakaa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, si kwamba mimi napinga uwekezaji wala nina shida na mwekezaji, Hapana; lakini lazima tufike mwekezaji anapofanya kazi yeye afanye shughuli zake za uwekezaji kwa amani na wananchi wawe na amani. Sasa iliyopo jimboni kwangu ni shida kubwa, migogoro haiishi. Juzi nilikuepo jimboni wananchi wameandamana kwenye Ofisi za chama. Kwa sababu mwekezaji amewaandikia barua kwamba mashamba yote yale waliyolima mahindi hawatakiwi kuvuna mpaka waende kwake yeye. Wakati wamepanda wamepalilia wameweka mbole, wakati wa kuvuna umefika ndipo sasa mwekezaji anakwenda wakamlipe fedha. Na shida ni kwamba ninyi wenyewe Serikali kupitia hii Ofisi ya Ardhi mlileta confusion. Vijiji vilikuwa na mipaka yao na hati yao, kabisa, mkaja kumpa Mwekezaji sehemu ya vijiji, na wanakijiji wana sehemu ileile ya kwao. Kwa hiyo kuna mgongano hapa. Wanakijiji wanadai eneo hili ni la kwetu na mwekezaji anasema hili ni la kwangu kihalali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mgogoro unaenda miaka 13 dada yangu Mheshimiwa Waziri na mwishowe tunaonekana sasa kama wananchi ni wakorofi, wanatumia nguvu nyingi ya dola kuwapiga, kuwaumiza, issue sio kupiga mnaweza mkapiga sasa mgogoro huu ni vijiji 11. Kwangu kwenye Jimbo langu la Kwela ni vijiji vitatu kule kwa ndugu yangu Aeshi vijiji saba, vyote hivi kila muda wapo kwenye movement, maisha yao ya movement.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nikashauri kwamba Waziri aunde tume tuje tukae, tumalize mgogoro, imetosha sasa mambo ya kufukuzana, mwekezaji na pia nilishauri hapa Bungeni, sisi uwekezaji tunaupenda, lakini namna ya shamba lile kuwa idle ekari 23,000 kwenda 25,000 hakuna shughuli inayoendelea, mwekezaji amelihodhi liko idle na pengine kwa sababu ya migogoro pia anaweza kuwa naye hataki kuendeleza chochote. Sasa Serikali position yao ni nini kwenye jambo hili, sisi pale ngano ndio wanaongea, kila siku Waziri Mheshimiwa Bashe naye nilimwambia, anapiga kelele suala la ngano kuna vitu vingine Serikali tumeshindwa tu kufanya maamuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna shamba la hekta 25,000 la mwekezaji wa Shamba la Malonje Efatha liko arable. Tukiwekeza tu pale tutapata tani 175,000 mpaka tani 100,000 za ngano, Waziri ataenda kupunguza deficit hiyo anayopiga kelele hapa, lakini kama halmashauri sisi tutaenda kukusanya mapato kutokana na huo uzalishaji milioni 600, 700 mpaka bilioni moja, lakini katika jambo hili nashangaa kwa nini tunasitasita, sisi hatuna ugomvi, twendeni tukakae pale mezani, tukaondoe huu ugomvi unaoendelea wa muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi tu imetokea shida tena ugomvi umehama kwa wananchi umehamia tena kwa mwekezaji na Serikali kwa sababu wale wafanyakazi wamechukua trekta lenye harrow wameenda kulima barabara ya TARURA ya kilometa wakaivuruga tu wakailima vuruga. Kilometa 1.5 wanadaiwa wakatengeneze barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunatakiwa tukaweke standard kwamba wewe ni mwekezaji mipaka yako ni ipi, ulipewa shamba kwa madhumuni yapi, ndani ya muda gani utekeleze nini, wananchi mipaka yenu ni hii moja, mbili, tatu. Tuna-close jambo lile kila mtu anaishi kwa amani, kuliko kila mwaka nisimame Bungeni, nina hansard nilikuwa nasoma hapa, mpaka nasikitika walilichukulia very lightly. Madhara yake yanakuja, watauana, wananchi wataamua kum-sabotage mwekezaji na mwekezaji naye anatumia walinzi wake kuwapiga wananchi. Hatuwezi kuuishi kwenye nchi hii kwa namna hii ya kuviziana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Waziri kesho anapohitimisha hili jambo nimeliongea sana, nimwombe alichukulie very serious ili chama nacho kwenye Mkutano Mkuu wa Chama, Mwenyekiti wetu wa Chama Mama Silafu Maufi amesimama pale mbele ya Mheshimiwa Rais akaongelea jambo hili. Kwa hiyo hata Chama kwa Mkoa wa Rukwa wao nao wanapiga kelele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi Mbunge hata Mheshimiwa Aeshi nilikuwa naye hapa, japo yeye anaweza asipate nafasi ya kusema, wananchi wetu wanatutazama juu ya jambo hili. Twende tukakae party zote tulimalize ili tuje na conclusion mwekezaji abaki na amani yake na wananchi wabaki na salama yao ili tukajenge majimbo yetu, yakawe salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili kuna jambo ambalo lipo chini ya mikono ya Wizara, Gereza la Mollo, Gereza la Mollo nalo hivyo hivyo kama alivyokuwa anasema ndugu yangu Mheshimiwa Ndaisaba, wamekuja pale wamewakuta wananchi kijiji kipo wametwaa eneo, wakasema haya tunapitisha mpaka humu tunachukua gereza. Sasa nao huo mgogoro umechukua miaka mingi sasa, inaenda miaka 15, wananchi wanasema ni eneo letu Gereza la Mollo linasema ni eneo letu. Alitumwa wakati ule Mheshimiwa Kangi Lugola akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, akawaambia wananchi tulieni tutarudisha, ikawa ndio jumla mpaka leo. Sasa nawaomba, wao ndiyo waliopewa dhamana ya kusimamia ardhi, waende wakamalize migogoro ya aina hii tusi- entartain migogoro itakuja kusababisha maafa watu wakauana pasipo sababu. Mheshimiwa Rais kama nilivyosema anajali, anawapa bajeti wanaenda huko, waende na mwaka huu hawajaja na waliniahidi watakuja tena alipokuwepo Naibu hapa Ndugu yangu Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alisema hamna shaka nakuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi kule wanasikia, wanasema mbona Mbunge ulidanganywa. Tumeona pia timu ya Mawaziri Nane kwenye mashamba haya yenye vijiji 11 hawajaja. Nimwombe mama yangu Mheshimiwa Waziri jambo hili mwaka jana aliona niliongea kwa uchungu mkubwa na leo narudia, waje tumalize mgogoro, sisi nasi tunataka tupate mapato kulingana na shamba lile na mwekezaji aendelee na maisha yake, lakini haki ya wananchi itazamwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kumaliza jambo la mgogoro, niende jambo la pili la muhimu la kumshukuru tena Mheshimiwa Rais kwa kupandisha hadhi vijiji sita ndani ya jimbo langu kuwa Miji Midogo kwa maana ya Mpui, Kaengesa, Mtowisa, Muze, Ilemba na Kiliamatundu. Sasa vile vijiji vinahitaji kupangiliwa sawa viendane na standard ya kuwa miji midogo. Niombe waisaidie sasa Ofisi ya Ardhi Mkoa kuongeza vifaa vya upimaji, tuna kifaa tu ambacho seti ile ya upimaji pale mkoani tunatumia Kalambo, Nkasi na Sumbawanga DC. Watuongeze ili vijiji vyote hivi ambavyo vimeshakuwa ni miji midogo niliyoitaja waweze kupangilia miji yao na kupangiliwa kwa miji tu hakutakuwa kunaishia hapo, bali kutaingiza mapato ambayo yata-boost mapato ya halmashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana naunga mkono hoja. (Makofi)