Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru wewe kwa kinipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Makadirio na Mapato ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Pili nachukua fursa hii ya kumpongeza Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoongoza nchi yetu kwa umakini mkubwa sana. Nchi imetulia na maendeleo yanaonekana. Namuombea kila la kheri katika uongozi wake huu.

Mheshimiwa Spika, napennda kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii pamoja na wasaidizi wake wote kwa namna walivyotayarisha hotuba hii kwa ubora wa hali ya juu na hatimaye kuiwasilisha katika Bunge lako tukufu kwa ufasaha mkubwa.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo: -

Mheshimiwa Spika, nianze na mikopo ya wanafunzi; napenda kuipongeza Serikali yetu kwa namna inavyojitahidi kuwasaidia wanafunzi katika kuwawezesha kuendelea na masomo yao ya juu. Hili ni suala zuri sana hasa ukizingatia kuwa watoto wengi hali zao za kiuchumi ni ndogo. Ushauri wangu katika jambo hili ni kwamba Serikali izidi kuboresha mfuko huu wa mikopo ili wanafunzi wengi zaidi waweze kunufaika.

Mheshimiwa Spika, kuhusu vyuo vya VETA nchini; vyuo vya VETA ni vyuo muhimu sana katika kuwawezesha wanafunzi wetu kujijengea uwezo wa kuweza kujitegemea baada ya kumaliza mafunzo. Tatizo la ajira ni kubwa sana sio tu nchini mwetu bali ulimwengu mzima. Vyuo hivi vya VETA vinaweza kuwa ni suluhisho kubwa kwa tatizo la ajira nchini.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kuongeza bajeti ya kuviwezesha vyuo hivi kufanya vizuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, Elimu ya Watu Wazima ni jambo zuri sana. Jambo hili lilikuwepo katika miaka ya nyuma lakini hivi sasa inaonekana sasa hivi Serikali yetu imelegeza kidogo kuliendeleza suala hili.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kurejesha elimu ya watu wazima nchini kwa manufaa ya wananchi wetu ambao kwa namna moja au nyingine walikosa fursa ya kuweza kusoma.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.