Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mimi kama Mwenyekiti wangu wa Kamati na Wajumbe wenzangu wa Kamati na watu wote ambao wamepongeza jitihada ambazo zimefanywa na Kamati ya Mapitio ya Sera na Mitaala. Pia nimpongeze sana Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako ambaye alianza mchakato, lakini pia Mheshimiwa Profesa Adolf Mkenda, ambaye na yeye alipokea mchakato wa mapitio ya sera na mtaala, lakini kwa upekee sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sababu, yeye alionesha political will kama kiongozi wa nchi kwamba, kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mapitio ya mfumo wetu wa elimu kwa ajili ya kuendana na mazingira ya sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee sana nimpongeze Profesa Makenya Maboko kwa sababu, amefanya kazi iliyotukuka na viongozi wote, Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Wizara, mama yangu Profesa Carolyne Nombo, anatuheshimisha sana kama wanawake na tunaona kwamba, tukipewa nafasi tunaweza kufanya makubwa zaidi. Kwa hiyo, majina yao yataandikwa kwa wino wa dhahabu kwa sababu, hii document ambayo wameitengeneza ukweli ni kwamba, ni one of the outstanding documents kwenye East Africa, inawezekana hata Nchi za Kusini mwa Afrika na inawezekana Afrika kwa hii document iliyotengenezwa, ni one of the best, kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wamepitia na wataalam wamepitia. Nipongeze kwa sababu walijipa muda wa kukusanya maoni na hawakuchukua speed kubwa sana, kwenda harakaharaka, wali-take time waka-exhaust na wamefanya kazi kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda kabla sijaanza kuchangia nizungumze jambo moja kwa sababu, mapitio ya mtaala ya sasa hivi na sera tunasema falsafa ya sasa hivi ni self-reliance, elimu ya kujitegemea. Sasa labda kwa sababu Mheshimiwa Dkt. Chaya ni Mwalimu wangu chuo kikuu niseme tu kidogo kwamba, alichokizungumza kwamba, tuache VETA tusubiri walio-drop wameshindwa waende VETA, maana yake tunakuwa hatutekelezi lile lengo la kusema kwamba, tunatengeneza mfumo wa elimu ya kujitegemea. Tunataka wazazi na Watanzania wote waone kwamba, aliyepo VETA ni ameamua tu alternative pathway, amechagua kwenda huko, sio kwamba, hana uwezo na ninajua ndio dhamira ya kufanya marekebisho na mapitio kwa sababu, tunajenga ujuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee sana nipongeze mchakato uliofanyika kwa ku-integrate skills za karne ya 21. Study za karne ya 21 ambazo wamezi-integrate, japo nina mambo kadhaa ya kuzungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nipongeze kwa sababu, wame-integrate communication, tulikuwa tuna tatizo hilo, lakini pia wame-integrate collaboration, wame- integrate creativity na innovation, lakini critical thinking, tafakuri tunduizi na nimekuwa nikizungumza, lakini problem solving, utatuzi wa matatizo, digital literacy, ethics and patriotism. Wameamua kuzichukua kwa sababu ndio karne ya 21, labda niwaambie Waheshimiwa Wabunge dunia tunayoishi sasa hivi ni dunia soft, inahitaji watu ambao wanafikiri sana na wanatatua matatizo yanayowazunguka kwa sababu, matatizo yanakuja kila siku na yanahitaji akili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli kuna maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, lakini the only thing ambayo haiwezi kuwa replaced na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ni kufikiri. Kwa hiyo, ni lazima mfumo wetu wa elimu uendane na namna gani ambavyo tuna-feed hilo gap la fikira kwa sababu, mwanadamu pekee ndio Mungu amempa uwezo wa kufikiri. Sasa kama una mfumo wa elimu ambao mtoto anatumia muda mwingi darasani na mfumo huo haumwelekezi huyu mtoto kufikiri, kuanza kung’amua matatizo yanayoweza kujitokeza baadaye, maana yake mfumo wako wa elimu unakuwa redundant. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nipongeze kwa hilo, ila nina changamoto moja; wameeleza, ukiangalia kwenye tamko la sera ambalo linaenda kusababisha mitaala kutengenezwa, tamko 3.3.6. Wanasema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha mtaala unalenga kukuza stadi za karne ya 21 ambazo amezitaja hapo kwa mfumo wa kuchopeka, ku-integrate. Wasiwasi wangu ni hapo kwenye ku-integrate kwa sababu, unawezaje kupima kitu ambacho Umeki-integrate kwenye process? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu, hakuna utaratibu waliouweka kwenye kupima. Labda niseme hivi, wameeleza kwamba, anayeenda kutekeleza mtaala, tunajua anayeenda kutekeleza mtaala ni Mwalimu na anaenda kujenga umahiri kwa wanafunzi na anaenda kujenga hizi stadi za karne ya 21, lakini hata kwenye marekebisho ya elimu ya ualimu, Mwalimu hajawekewa somo la kujenga umahiri wa hizi stadi. Mtu ambaye unamtegemea akazijenge stadi hujamwekea somo la kuzijua na nina mashaka sana kwa sababu tunawajua Walimu wetu ambao tunao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hizi stadi, kwani leo tunakosa nini? Kwa sababu, hizi stadi tukienda, tukirudi kwenye Sera ya mwaka 2014, tukirudi kwenye competence based hiki ambacho tunakirekebisha leo, hizi zilikuwepo na zilikuwa kwenye mfumo huu huu. Hazikuwa zimeandikwa kama hivi, lakini zilikuwa kwenye mfumo huu wa kuchopeka, sasa badala ya kuchopeka kwa sababu, tukichopeka tutakuwa hatuna namna ya kuzipima. Kwanza anayeenda kutekeleza hajajengewa umahiri wa hicho kitu, lakini kuzipima hatutaweza kuzipima kwa watoto wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini sasa tusitafute namna ya kuzifanya ziwe kwenye namna kama mada au somo kwa sababu, tumeweka ile elimu ya historia ya Tanzania na maadili? Kwa nini isiwe huko ili sasa tufuatilie hatua kwa hatua ili tuweze kujua ni namna gani ambavyo tunaweza tukampima mtoto mwisho wa siku kwamba, tumefanikiwa kumfanya awe ni mtatuzi wa matatizo kwenye jamii kwa kiasi gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasikitika pia kwamba, kwenye hizi skills, skill ambayo ni muhimu sana ya self- awareness, kujitambua, haipo katika hizi skills, haijawekwa. Niwaambie tu Waheshimiwa Wabunge kujitambua ni pamoja na wewe binafsi, intra personal na inter personal skills ambazo zinamfanya mtu ajitambue kihisia yeye ni mtu gani na zitatusaidia pia ku-solve matatizo ya kimaadili kwenye jamii kwa sababu, inawezekana watoto wanaangalia vitu vingine ambavyo vinawafanya wasijitambue wao ni akina nani na ndio wanakua katika utaratibu huo. Kwa hiyo, skills kama self- awareness ni muhimu mno iwepo katika mfumo wetu wa hizi skills za karne ya 21.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, upimaji na tathmini. Niseme tu katika Rasimu ya Mtaala, Sura ya Nane, Kipengele cha 10, Wizara imezungumza na wameeleza gaps zilizokuwepo kwenye upimaji. Naunganisha na masuala ya hizi stadi za karne ya 21 kwa sababu hata upimaji wake haueleweki. Kwenye mfumo wa kawaida wa shule continuous assessment, upimaji endelevu, umepewa asilimia 30, halafu upimaji wa mwisho umepewa asilimia 70 kwenye mfumo wa kishule, lakini kwenye mfumo wa elimu ya ualimu ni fifty-fifty angalau, hamsini-hamsini, lakini kwenye inactivate, amali, wao wameenda mbali zaidi wana zaidi ya asilimia 70 na kuendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ni kweli kabisa mtihani wa mwisho unaweza kumtambua mtoto kwamba ana akili au hana? Kwa sababu, hiki kilichoandikwa sasa hivi sio kwamba, hakikuwepo. Tumefanya review sasa hivi tume-highlight na vizuri kabisa Serikali imeonesha kuna gaps, lakini ni kwamba tume-highlight tu. Ukweli ni kwamba, continuous assessment, upimaji endelevu wa ndani ya shule, Mwalimu na mwanafunzi ulikuwa haufanyiki. Yale matokeo mnaona tunafanya ranking leo tunalalamika tumeondoa ranking, lakini yale ni matokeo ya mwisho. Kuna factors nyingi zinaweza kusababisha mtoto afeli mtihani wa mwisho, lakini sio kwamba, hana uwezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuniambia kwamba, mtoto aliyefaulu standard seven, akafaulu kidato cha pili anakuja kufeli form four tena kwa zero, haiwezekani, kuna namna ambavyo huyu mtoto katika kujifunza kwake kuna vitu anajua. Kama lengo letu la elimu kama ninavyolielewa mimi ni kumjenga Mtanzania mwenye umahiri, anayeelewa, ambaye anaweza kuwa mwananchi ambaye atakuwa na mchango kwenye nchi, tunahitaji kuongeza asilimia za continuous assessment. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sio tu kuziongeza, tuzipime kiuhalisia kwa sababu, Mheshimiwa Waziri anajua kwa sababu yeye pia ni Mwalimu na wapo Walimu wanafahamu. Ukweli ni kwamba, hakuna namna ambavyo wanafuatilia, tunaambiwa tu huu ni mkusanyiko wa mitihani yako ambayo umefanya. Lengo la continuous assessment ninayozungumza mimi sio majaribio na mitihani, kama tunapima problem solving ni lazima tuwe tuna utaratibu wa kuwapima watoto kwenye matatizo yanayowazunguka katika mazingira yao pale pale shule. Kwa hiyo, ni ushirikiano wa Mwalimu na mwanafunzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama NECTA ni machinery ambayo ina full autonomy ya kwake, utaratibu wake wa jinsi ya ku-operate, itafutwe namna tunaweza tukai-integrate. Kwanza tuongeze asilimia ili tufike angalau 50 mpaka 60 au angalao fifty-fifty, lakini nzuri ikiwa 60 kwa sababu ya kitu ambacho tunategemea tukipate hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu muda umebaki kidogo nimalizie kuhusiana na lugha ya kufundishia. Kwanza niwapongeze Serikali wame-play neutral role, wame-play neutral ground kwa sababu wamesema kwamba, anayetaka kufundisha Kiswahili ataomba kibali na anayetaka kufundisha Kiingereza ataomba kibali, kwa hiyo, wamejaribu ku-play politics hapo, lakini tunajua, sitazungumza kwenye lugha ya Kiswahili sana, najua siku zote huwa nazungumza kwamba, ni muhimu sana tujifunze kwa lugha tunayoielewa, lakini hata hicho Kiingereza, mimi nimesoma HKL Form Six, tumesoma syntax, phonology, semantics, vitu ambavyo tunajua leo hapa hatuzungumzi syntax, hatuzungumzi phonology.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunafundishwa Kiingereza tufundishwe kama communication language, lugha ya kuwasiliana, kwa sababu, tunataka hawa watoto wakitoka wamejua wamegundua vitu vyao, wawe wana uvumbuzi, waweze ku-communicate, waende wafanye biashara bila kutafuta mkalimani, aendee nchi yoyote duniani. Kwa hiyo, kama tunakubaliana ni Kiswahili basi kiwe Kiswahili na kama tunakubaliana ni Kiingereza basi kiwe Kiingereza, watoto wasikutane na Kiingereza barabarani. Nazungumzia watoto wa Kantalamba huko, wasikutane na Kiingereza barabarani, waanze kutoka darasa la kwanza, kutoka awali, la kwanza, waende na Kiingereza. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri ni jukumu lake kujenga umahiri kwa Walimu ili wawe the best. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vitu vingi hapa tunaweza tukavizungumza, vingine najua tutaviandika huko, lakini cha mwisho kabisa, bajeti ya Wizara ya Elimu. Asilimia zaidi ya 64 ya bajeti ya Wizara ya Elimu yote inaenda kwenye mikopo. Tutafute solution ya kudumu ya ku-fund mikopo ya elimu ya juu kwa sababu, tunakosa pesa za kufanya vitu vingine kwenye Wizara, kwa mfano, kitu muhimu kama utafiti hatuna pesa za utafiti. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)