Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, naomba nianze mchango wangu kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti hii mchango wangu utaanza kwa maswali kadhaa kama ifuatayovyo: -

Je, ni lini Serikali itaendelea au kusogeza huduma za kibingwa na kihadhi kimataifa/accreditation kwa hospitali kubwa na za kanda? Mfano wa Nyanda za Juu Kusini mojawapo ya hospitali inayosaidia karibu mikoa nane iliyopo ukanda huu ni Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (Mbeya Zonal Referral Hospital -MZRH).

Pili ni hospitali iliyo katika lango kubwa la nchi nyingi zilizo katika SADC kama lango kuu kwa upande wa Kusini; tatu, ipo katika mkoa ambao una barabara kuu ya kufikia nchi nyingine kupitia border za Tunduma na Kyela. Hivyo muingiliano wa wageni kutoka nchi jirani ni fursa kubwa ya kuzalisha utalii wa kimatibabu (Medical Tourism).

Mheshimiwa Spika, ikiwa patahitajika hospitali kubwa ya kuanza nayo kihuduma kwa wageni wa nchi jirani basi itakuwa ni hii MZRH. Hivyo ni fahari mno ikiwa hospitali hii itapewa kuwa kitovu cha utalii wa kimatibabu. Utalii wa kimatibabu utawezesha nchi za jirani au wageni kuja kupata huduma mbalimbali za kimatibabu na huduma bingwa kwa wepesi na ubora (fast & quality services).

Mheshimiwa Spika, umuhimu wa utalii wa kimatibabu ni kuwezesha kukua kwa pato la ndani la Taifa kupitia fedha za kigeni ambazo zitaingia nchini kwa wageni wanaokuja kupata matibabu na hata kujifunza baadhi ya huduma za matibabu za kibingwa kutoka kwa wataalamu wageni.

Mheshimiwa Spika, utalii wa matibabu na kujifunza teknolojia za matibabu kupitia hospitali hii kutaleta fursa ya muunganiko wa kujifunza hata wengine nao wanafanyaje na hata kuvutia uanzishwaji wa makambi (medical camps), nchi nyingine kwa ajili ya kutanua wigo wa huduma za afya.

Mheshimiwa Spika, ipo haja kubwa kwa Serikali na wadau kuweza kuhakikisha hospitali zilizo katika lango la nchi jirani kuongezewa uwezo wa kupewa hadhi za kutoa huduma tambuzi kimataifa (international accredited) katika kufanya kazi na mashirika makubwa na taasisi kubwa za kimataifa.

Mheshimiwa Spika, kufanikiwa kwa hili kutasaidia sana kukuza hadhi za huduma, huduma za kibingwa kuvuka mipaka ya nchi na hata iwe zamu yetu sasa watu watoke nchi nyingine kuja kupata huduma kwetu kama ilivyo India ilivyojipa nafasi kimataifa kuwa na uwezo mkubwa wa kupokea wagonjwa na hata kutoa fursa za utalii matibabu.

Mheshimiwa Spika, kufanikiwa kwa MZRH kupata hadhi hii kutatanua wigo wa hospitali katika kuwa na uwezo mkubwa zaidi katika idara za maabara na ngazi zote za matibabu.

Mheshimiwa Spika, katika Nyanda za Juu Kusini basi mojawapo ya hospitali inayosaidia karibu mikoa nane iliyopo ukanda huu ni Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Mheshimiwa Spika, ahsante na naomba kuwasilisha.