Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya

Hon. Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mungu kwa kunipa kibali cha kusimama katika Bunge lako tukufu na pia nakushukuru kwa kunipatia nafasi ili niweze kuichangia katika Wizara hii ya Afya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze na kumpongeza Rais wetu kipenzi, Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea pesa nyingi katika Mkoa wetu wa Kagera na ndoto yake ya kupunguza vifo vya akinamama na watoto Tanzania inawezekana, hongera sana Mama yetu, tunazidi kukuombea afya kila iitwapo leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze Waziri wa Afya, dada yangu Ummy pamoja na Naibu wake Dkt. Mollel na Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Afya kwa kazi nzuri wanazozifanya, hakika wanatutendea haki. Sasa naomba nijielekeze kwenye mchango wangu, Mkoa wetu wa Kagera halmashauri sita, zimekamilisha ujenzi wa hospitali, Katoke Biharamulo, Bujinangoma Bukoba DC, Bulembo Misenyi, Karagwe, Kyerwa, Ngara Rusumo. Pia kuna vituo vya afya na zahanati zilizokamilika zinahitaji vifaa tiba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hizi hospitali zimekamilika, lakini vifaa tiba imekuwa ni changamoto kubwa sana, pamoja na wataalam wa afya ili ziweze kuanza kutoa huduma. Kwa hiyo, naomba Serikali yangu Tukufu iweze kuleta vifaa tiba vya kutosha katika hospitali hizi pamoja na wataalam ili kuweza kuwasaidia wananchi.

Mheshimiwa Spika, katika hospitali na vituo vilivyokamilika, tunahitaji ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya ili kuwezesha kutoa huduma Madaktari Bingwa kwa muda wa saa 24. Kwa mfano, mgonjwa pale anaweza akaja mama mjamzito anakuja kujifungua anafika pale kituoni daktari yuko mbali, lakini tukiwa tumejenga pale nyumba ina maana Daktari atakuwa pale masaa 24. Kwa hiyo vifo vitapungua havitakuwepo kabisa kwa mama wajawazito pia na watoto na wazee. Nilikuwa naomba hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mkoa wetu wa Kagera katika mipaka yetu kuna mapungufu makubwa ya namna ya kudhibiti magonjwa hatarishi. Tunaomba kujengewa majengo ya medical department, insulation na kadhalika ili huduma za afya katika mipaka yetu ya Mtukula, Chamchusi, Bugango, Msagamba, Igoma, Rusumo na Kabanga ili kudhibiti magonjwa hatarishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mkoa wetu wa Kagera uko katika mlipuko wa majanga mengi. Kwa hiyo tunahitaji kujengewa kituo cha ufuatiliaji wa matukio ya mlipuko, kwa mfano ebola, marburg, surua, polio na yellow fever pamoja Covid, kwa sababu tumepakana na mipaka na nchi zetu jirani. Kwa hiyo, tunaomba sana Serikali yetu iweze kutuangalia kwa jicho la huruma katika Mkoa wetu wa Kagera.

Mheshimiwa Spika, Mkoa wetu wa Kagera tuna visiwa 38, visiwa vitano tu ndio vina zahanati. Mama wajawazito visiwani hawana pa kujifungulia ili kunusuru uhai wao, tunaomba Serikali yetu itununulie ambulance boat ili kuwezesha dharura za matibabu kutoka kwenda visiwa vingine. Kwa mfano mgonjwa mwingine yuko mahututi ili kumtoa katika visiwa vile aje katika hospitali ya rufaa. Kwa hiyo, naomba sana kwa Waziri, dada yangu Ummy tupate hiyo ambulance boat ili kuweza kunusuru uhai wa wananchi wetu wa Kagera. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mkoa wetu wa Kagera umeanza upanuzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa kwa kubomoa majengo chakavu. Sasa hivi tumeanza kujenga maghorofa, tuliahidiwa kuletewa bilioni tatu ili kuweza kumalizia. Kwa hiyo, tunaomba hela ije kipindi hiki ili tuendelee na ujenzi wa OPD, wodi za watoto na wodi za wanawake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yangu ni hayo machache, naunga mkono hoja. (Makofi)