Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

Hon. Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, nami naomba nichukue fursa hii kukushukuru kwa kunipa fursa ya kusema kwenye bajeti hii ya Wizara ya Maji. Nimesimama kuunga mkono hoja, na pili, nimesimama kuchangia kidogo kwenye bajeti hii ya Wizara ya Maji inayoongozwa na Mheshimiwa Aweso.

Mheshimiwa Spika, nami nimshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, maana mwaka 2022 tulipata mitambo kwa ajili ya uchimbaji wa visima na mabwawa katika mikoa yetu. Kwa kuwa maji haya ni kwa ajili ya wanadamu, lakini pia maji haya ni kwa ajili ya mifugo na huduma nyingine ikiwemo kilimo, nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge baadhi ya waliochangia hapa leo, wakisisitiza kwamba, katika maeneo yenye mifugo na ikiwa kama uko mradi wa maji kwenye eneo lile, basi ni vizuri sana ule mradi wa maji uzingatie kutoa huduma kwa mifugo pia.

Mheshimiwa Spika, katika hili namshukuru sana mtu muungwana, mtu mzuri, mweledi, mchapakazi, Waziri Aweso na timu yake yote, kwa hakika tumekubaliana kwamba katika kila designing ya mradi wa maji pale unapopita kwenye eneo la mifugo, basi uzingatie sana kupatikana kwa namna ambayo utasaidia mifugo yetu kuhudumiwa na maji yale.

Mheshimwa Spika, nimemsikia hapa Mbunge wa Ngorongoro, Mheshimiwa Shangai, vilevile nimemsikia Mheshimiwa Shangazi, wamesisitiza sana. Mimi ninafahamu, kwa wadau wa mifugo, sisi wafugaji ni bora wakati mwingine tukose maji sisi wenyewe lakini mifugo yetu iweze kupata maji. Ndiyo maana ninamshukuru sana ndugu yangu, Comred Jumaa Aweso, kwa kuwa tumekubaliana kimsingi ya kwamba tunakwenda kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, nawaomba Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwenye kusisitiza juu ya jambo hili, ikiwa mtaona kama kuna wasiwasi juu ya ile designing, siyo tu kumfuata kaka yangu, Mheshimiwa Aweso, hata nami nishirikisheni ili kusudi niweze kusukuma kwa pamoja; mimi, yeye na timu zetu, ili wafugaji wetu waweze kupata maji. Maana sote tunafahamu ya kwamba mifugo ni utajiri, na ili iweze kukaa vizuri, ipate malisho na maji.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, nakushukuru sana. (Makofi)