Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

Hon. Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana wewe kwa kazi nzuri unazozifanya na kutusaidia sisi Wabunge wako lakini pia nimshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ambazo anazifanya kwenye Wizara ya Maji. Nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri na Naibu wake Pamoja na Makatibu Wakuu mmekuwa wasikivu sana. Kwa kweli tuwapongeze kwa dhati kabisa kutoka kwenye mioyo yetu.

Mheshimiwa Spika, lakini pia tumpongeze sana Engineer Clement Kavigelo anafanya kazi nzuri; ndiye anaye-design miradi mikubwa ya maji hapa nchini, anafanya kazi nzuri sana. Kuna siku moja Wabunge walisema kwamba Chifu wa TARURA anastahili tuzo na huyu kijana anastahili tuzo, anafanya kazi kubwa, nina Imani kila Mbunge amemgusa.

Mheshimiwa Spika, mimi nijikite pia kwenye miradi yangu. Nishukuru sana, Mheshimiwa Waziri amenipatia fedha kwenye Kata yangu ya Chona Kijiji cha Itumbili milioni 500, mradi wa maji unaendelea vizuri. lakini pia umenipa fedha 1,200,000,000 Kata ya Sabasabini, mradi wa maji unaendelea vizuri na wananchi wanakunywa maji.

Ombi langu, niendele kukuomba Mheshimiwa Waziri, kuna vijiji ambavyo vinazunguka maradi wa maji ambavyo vinahitaji kupatiwa maji. Kwa mfano Kijiji cha Bungungu kiko jirani na tenki la maji lakini hakina maji. Kuna Kijiji cha Lusonzo nacho kipo jirani na tenki la maji lakini hakina maji. Niendelee kukuomba Mheshimiwa Waziri kwamba wananchi hawa tuwasaidie. Hawa ni walinzi wa miradi yetu, tu sipowasaidia maji madhara yake nina imani Mheshimiwa Waziri wewe mwenyewe ni shahidi, yanaweza ikawa makubwa sana.

Mheshimiwa Spika, vilevile kuna Kata yangu ya Igwamanoni na kwenyewe kuna mradi wa milioni 450 umenipatia maji, wananchi wa Igwamanoni Pamoja na Ilamba wanakunywa. Lakini kuna vijiji vyake ambavyo havipati maji kabisa, viko pale. Kijiji changu cha Kipangu na Nyakashagala, Kitongo pamoja na Luhaga bado havijapatiwa maji. Sasa faida ya mradi huu wa maji bado haujawafikia wananchi kwenye kata kwa kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Spika, lakini kubwa sana, Mheshimiwa Waziri wewe mweyewe ni shahidi, hali ya Ushetu ni mbaya sana. Zaidi ya kata 11 mmepeleka magari ya kuchimba; nimpongeze sana Menaja wa RUWUSA Mkoa wa Shinyanga ndugu yangu Julieth, amepeleka magari yeye mwenyewe ni shahidi; lakini kinachokutana pale hakuna maji. Kata ya Ulowa ambayo ina wakazi zaidi ya 35,000 hakuna maji. Kuna Kata za Ubagwe, K Ulewe, Uyogo, Bukomela, Kinamapula, Mapamba, Ushetu pamoja na Chona ambako pia anatoka Mwenyekiti wangu wa Mkoa wa Chama Cha Mapinduzi, hakuna maji. Mheshimiwa Waziri hata kile kisima cha pump angalau tungelikuwa angalau na visima vya pump navyo hakuna kwa sababu maji hakuna kabisa. Kwa hiyo ningekuomba Mheshimiwa Waziri unapokuja kuhitimisha naomba nijue hatma ya wananchi wangu wa Jimbo la Ushetu.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze, juzi alinitumia wataalamu wake wa RUWASA pamoja na KASHIWASA wameenda ku-design mradi wa Ziwa Victoria ambapo umechelewa kwa muda mrefu kwa wananchi wa Ushetu. Ulitakiwa uwe umeshafika muda mrefu, niombe Mheshimiwa Waziri aandike historia kwa wananchi wa Ushetu; ni kilomita 20 tu kutoka Kahama Mjini. Pia kuna Kata ya Igunda pamoja na kata ya Ukune, hizo ni kilomita saba kwa wananchi wanaokunywa maji ya Ziwa Victoria wao hawana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ni kipindi ambacho kama Mbunge napata wakati mgumu sana, na Mheshimiwa Waziri ni Mbunge mwenzangu anajua hali. Majimbo sita ya Mkoa wa Shinyanga, Jimbo la Ushetu tu peke yake ambalo halina mradi wa Ziwa Victoria, kata 11 hata visima vya pump hakuna, vinateseka, vinahangaika. Mradi wa maji wa Nyamilangano kidogo kidogo uliozinduliwa na Mwenge mwaka jana, ambao ulitumia Zaidi ya milioni kama 700, kidogo inasaidia, ambao tunaomba na wenyewe upanuliwe sasa kwenye vijiji vinavyozuunguka Halmashauri ya Kata ya Nyamilangano, Makao Makuu ya Halmashauri ili kule ambako mji unaendelea kupanuka tuweze kupata.

Mheshimiwa Spika, lakini jingine Mheshimiwa Waziri niendelee kukusihi tu kwamba shida ya maji katika Jimbo la Ushetu ni maji ya mradi wa Ziwa Victoria. Najua umeweka upembuzi pale vijana wako wamefanya kazi;akini naogopa kushika shilingi kwa kazi nzuri unazozifanya naona aibu lakini naomba tu unapohitimisha nipate jambo la kufanya kwa wananchi wa Ushetu.

Mheshimiwa Spika, kingineā€¦

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungunzaji)