Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa fursa hii ya kuchangia katika Wizara hii muhimu Bajeti ya Wizara ya Maji.

Kwanza kabisa nimpongeze sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akiitupia jicho Wizara hii ya Maji, kwa kuipatia bajeti kila mwaka wa bajeti na imekuwa ikiongezeka kwa kweli nampongeza sana Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, pili nikupongeze wewe Waziri, Naibu Waziri wako na timu nzima ya menejimenti katika Wizara hii ya Maji kazi yenu mnayofanya ni kubwa na mmeonyesha uwezo kama vijana mnatoa chachu kubwa na jinsi mnavyoisimamia hii wizara nawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia niwapongeze watendaji wenu ndani ya Mkoa wa Rukwa nikianza na meneja wa RUWASA Mkoa ndugu yangu Boaz na DM wangu Maganga pamoja na ndugu yangu Mkurugenzi wa SUWASA ndugu yangu Nzowa. Wanafanya kazi nzuri na tunawaamini sana mna vijana wazuri ndani ya Mkoa ya Mkoa wa Rukwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hii kabla sijaenda kwenye hoja nianze moja moja hapa kwenye jambo la watumishi, watumishi ndani ya hasa RUWASA. Waheshimiwa Wabunge wengi wamesema kwenye Wizara yako hasa upande wa RUWASA ma–DM wengi na mahali pengine ma– RM wanakaimu zaidi ya miaka miwili, mitatu. Sasa brother kazi yako nikubwa na una wa–entrust watendaji hawa kwa mabilioni ya pesa kwenda kusimamia miradi ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa kuwakaimisha kwa muda mrefu hii ni jambo ambalo nakuomba waziri kaondoe hii dosari tunajua mmewafanyia probations ya kutosha zaidi ya miaka miwili, mitatu sasa kawa–confirm wawe proper wafanye kazi ya kusimamia Wizara yako na itaongeza ufanisi.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili; niliuliza swali ndani ya Bunge juu ya Miji midogo ya Laela na Mmpui hasa ukosefu wa maji hii miji inaisha tu kipindi cha masika baada ya hapo kunakuwa na shida kubwa ya maji. Hili jambo mmeji–commit kuanza kuchimba visima, lakini nikusisitizie kwa mji mdogo wa Laela solution narudia tena ni kutumia maji ya Mto Momba. Mmejipanga itahudumia karibia taarifa nzima ya Laela na ambayo hiyo mmejipanga kuanza upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Spika, naomba ulitupie jicho la pekee na ndugu yangu nakuamini nilikuletea wazo la kuchukua maji Kwela na sasa hivi ukaleta bilioni tano najua jambo la kumaliza tatizo la maji Mmpui na Laela liko ndani ya uwezo wako ndugu yangu Aweso ujawahi niangusha katika jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili; niongelee jambo la wakandarasi. Umejitahidi sana na Wizara hii mnapata fedha nyingi, lakini kuna shida kubwa ya wakandarasi hasa wazawa. Kumekuwa na tendency moja ya wakandarasi kuwa na tamaa, wanaomba tender mikoa mbalimbali na wanakuwa na tender nyingi ikifika hatua execution wanashindwa ku– perform kwenye mikataba.

Mheshimiwa Spika, takupa mfano katika Jimbo langu la Kwela kuna mradi mmoja wa Ngomeni na kijiji kinaitwa Mpembano, mkandarasi alipewa kufanya zabuni yenye thamani ya shilingi milioni 940. Cha ajabu huyu bwana alikuja kuripoti site tukampa advanced payment ya milioni 100 badaye aka-abandon site akapotea.

Mheshimiwa Spiia, nawashukuru sana watendaji wako wa Mkoa wakiongozwa na Boaz walili–cover ile advanced payments bond ya shilingi milioni 100. Lakini tayari ilitakiwa atupe mradi ule Desemba, 2022 naambiwa mko kwenye process ya ku–terminate mmechukua muda mrefu wananchi wa Ngomeni na wa Mpembano Kata ya Lusaka wanasubiri kupata maji.

Mheshimiwa Spika, mkandarasi huyu ametuchelesha zaidi ya mwaka na ninaomba uende stepu mbili zaidi mbele msiishie tu ku–terminate contract lazima watufanyie watulipe liquidated damage hizi ambazo wamesababisha kwa kutuchelewesha.

Mheshimiwa Spika, pili, muwafanyie debarment mwende PPRA muwafungie. Hatutaki kuwa na wakandarasi ambao wanakuja kutuchezea wanaomba kazi kumbe hawana uwezo. Lakini pia nina miradi mingine inayoendelea kuna mradi unaitwa Mkunda Group pale ndani ya jimbo langu huo unapeleka maji Kata ya Kaengesa Kijiji cha Kaengesa A na B na kwenda Kianda. Mkandarasi huyu ilitakiwa amalize kazi yake mwezi Aprili, lakini mpaka sasa hivi ajajenga lile tenki na kuna kazi kubwa ya ku–supply mabomba.

Mheshimiwa Spika, ningeomba shughuli hii ya mabomba mfanye nyie wenyewe RUWASA kwa kutumia force account huyu hawezi kufanya hii kazi la sivyo utakuja kukuta huo mradi nao unaleta shida. Hali kadhalika mradi wa Iremba mkandarasi ni hivyo hivyo bilioni 1.9 tumempa hiyo kazi, lakini shughuli yake pale ameshindwa ilitakiwa naye akabidhi mwezi wa tatu hajakamilisha na inaoneka, chukueni basi ile part iliyobaki mfanye kwa force account.

Mheshimiwa Spika, hali kadhalika na mradi mwingine wa Lura Chitete huo ni mradi ambao pia ni muhimu sana ambao mkandarasi wake. Nina wakandarasi hao watatu niliokupa. Kwa mfano yule mkandarasi Kobeki wa Kwela anafanya kazi nzuri ni mtanzania mzalendo wakandarasi kama wale ndiyo tunawahitaji, umeampa kazi ndani ya muda mfupi amefikisha asilimia 75 na atatukadhi mradi mkubwa wa bilioni tano.

Mheshimiwa Spika, nikuombe Mheshimiwa Waziri katika jambo hili kaufatilie kwa umakini uwafanye review siyo wakandarasi tu ndani ya Jimbo la Kwela wakandarasi nchi nzima kawafanyieni performance appraisal muone je hawa tunawapa msiwarundikie kazi nyingi mtakuta mnawapa kazi nyingi wengine hawana uwezo wanafurahia tu ku–apply kazi mnawapa.

Mheshimiwa Spika, vilevile jambo lingine la muhimu ni juu ya vitendea kazi halmashauri yangu kwa maana ya Jimbo la Kwela tuna jiografia ambayo ni ngumu na inachangamoto ya miundombinu. Niombe sasa gari lile mlilotupatia limechoka brothe, fanya utaratibu mtafutieni DM ambaye anafanya kazi nzuri aweze kutekeleza majumu yake vizuri na hatimaye asimamie miradi ya mabilioni ya pesa mnayo peleka ndani ya Jimbo la Kwela.

Mheshimiwa Spika, pia niongelee suala lingine muhimu la Ziwa ya Tanganyika kwa maana ya hii project. Ulifanya commitment kubwa hapa jana na ukachukua na ku–quote maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kwamba nia unayo na umejipanga na kujidhatiti, tunaomba sasa sisi tunatega sikio unapo wind up hotuba yako ya bajeti utuambie mpango kazi na mkakati ni upi juu ya kutoa maji Lake Tanganyika kwa Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kweli tulikuwa na mijadala kwa Wabunge wa ukanda juu ya wewe kukushikia shilingi tunakusubiri kwenye ku wind up commitment gani unakuja nayo juu ya mradi huu wa kutoa maji Ziwa Tanganyika? Sisi hatuna shida tupe tu picha ambayo na ramani nzuri inayotekelezeka ili tujue mpango kazi aliyotupa Waziri ndani ya Bunge ni mpango kazi unaotekelezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo ninaunga mkono hoja kwa asilimia mia. (Makofi)