Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

Hon. Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Bismillah Rahman Rahim, ahsante sana.

Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kuwa na hali ya uzima na afya lakini niwashukuru na Wabunge wenzangu pia kwa hali hii hapa nawaona bado wazima na wana afya zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kuanzia kwanza nimpongeze Baba yangu hapo Waziri wangu wa Maji pamoja na Naibu wake, wanafanya kazi kubwa sana, wanafanya kazi kubwa sana isiyo na kifani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru Rais, wangu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na yeye amefanya kazi kubwa katika Wizara hii ya Maji hakuna asiyeona na kila anayesimama hapa anampongeza Mheshimiwa Rais, kutokana na kazi aliyoifanya katika Wizara hii ya Maji. Kwa kweli huyu Mama ni mfano, Mwenyezi Mungu ampe hekima, busara, ampe imani azidi kuongoza vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuboresha huduma ya maji safi katika Jiji la Dodoma. Mimi ni mkazi wa Dodoma, nimejenga Manispaa ya Makulu, nina nyumba na nina Watoto pale nakaa nao katika kiji kile cha Mkalama. Nyumba yangu imeandikwa namba sita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kadhia hii ya maji katika kijiji changu pale ninachokaa, katika mtaa wangu ninaokaa; ni kadhia kubwa imeingia, na ilifika mpaka kutoa swali la nyongeza hapa na Mheshimiwa Waziri alijibu vizuri tu yakapungua kidogo lakini yameanza kasi tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maji ya Mkalama tyana kasi kubwa yanapasua mabomba, maji ya makalama yanapasua maomba yana kasi, na kasi ile yanapopasua yale mabomba basi wewe huna haja ya kutafuta fundi ukasema uende ukampeleke pale azibe mabomba yale, sheria ile watu wa maji kama wako huku juu sijui wamaipata wapi, huna ruhusa ya kwenda kuziba lile bomba, uache yamwagike mpaka waje wenyewe waje wazidi kuyafunga; maana wakija wanayafunga. Kama limepasuka karibu na wewe unakosa maji. Nina changia hili isiwe hii kasi ya maji katika mji wetu pale iwe tena yale maji yapungue kasi, Hapana, yawe na kasi lakini yapunguzwe kidogo angalau yaweze kuingia vizuri na tuyatumie watu wote katika mtaa ule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kadhia nyingine katika Chuo cha UDOM. Chuo cha UDOM mimi nipo hapa Mkalama, Chuo cha UDOM pale majasi unapanda juu, ndiko ninakofanyia mazoezi mie, kila siku asubuhi, ukipita njia ile basi unanikuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha UDOM hakina maji, watu wanahangaika, wanafunzi wanahangaika, walimu wanahangaika. Mheshimiwa Waziri hili suala analijua lakini mwanangu! Kwamba pale UDOM maji hayapatikani, mtoto akivuliwa nepi haiwezi kufuliwa maana maji hana, anafutwa na karatasi anavikwa nepi nyingine; wengine wanyonge, ni maskini hawana kitu. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri hili suala ulijue, kwamba kule UDOM maji hayapatikani

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Kuna taarifa Mheshimiwa Mwantumu, Mheshimiwa Neema Mgaya.

MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Muda wangu huo ukipungua atanipa yeye maana nina dakika nane tu hapa.

TAARIFA

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kutoa taarifa.

Ningependa kumpa taarifa mkwe wangu pale sisikitiki sana namuongezea kidogo kwenye hotuba yake ili iweze kukaa vizuri. Tatizo lililokuwepo UDOM, UDOM ni karibu na Mkalama anapokaa yeye lakini kuna tatizo la maji. Hili tatizo ni sawasawa na pale Mlimwa C, nje kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Waziri Mkuu anapata maji ya kutosha, hivi Mheshimiwa Aweso watendaji wako hawaoni kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu anagombanishwa na majirani zake? Hawaoni kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi inagombanishwa na wananchi wapiga kula wake?

Haiwezekani kwa Waziri Mkuu maji yapatikane ya uhakika halafu nje maji hayapatikani kwa uhakika na ukifika nyumba ya tatu maji yanatoka yaani nyumba hii maji yanatoka baada ya nyumba nne maji hayatoki.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Neema, tayari dakika mbili zimekwisha, Mheshimiwa Mwantumu unapokea hiyo taarifa? (Makofi)

MHE. MWANTUMU D. HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, muda wangu utanilindia usije ukaninyima kidogo, na hiyo taarifa aliyoitoa mama yangu hapo mimi naiunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, UDOM maji hayapatikani. ninakwenda kwenye mazoezi watoto wanasikitika, hawanijui kwamba mimi ni Mbunge wa Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wananiona mimi ni kama mama yao tu, lakini mie yale maneno wanayosema mimi naya-note leo ninayatoa hapa wakisikia watasema kumbe yule mama Mbunge? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasikitika hakuna maji kwa hiyo Mheshimiwa Waziri nakuomba chonde chonde fanya kazi muhimu ili maji yapatikane katika Chuo cha UDOM ili watoto wetu waweze kuyatumia maji ya UDOM. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala langu la tatu, kuna mpango hivi sasa wa wezi, wanaingia majumbani wanafungua mabomba tulisharushiwa mpaka kwenye mitandao. Likitoka bomba maji huna ruhusa ya kutoka ukitoka unapingwa nyundo kali unaanguka wanaingia ndani wanaiba hiyo ndio staili yao waliyokuja nayo majambazi sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naliomba hili nalo lichukuliwe nba litiliwe maanani. Serikali yangu ifanye kazi kwa hawa majangili wanaopita katika nyumba kwenda kutuhujumu ndani ya nyumba zetu; hili suala nalo lifanyiwe kazi; na Mlimwa C nalo Mheshimiwa Waziri uende ukalifanyie kazi maji yapatikane. Mheshimiwa Waziri Mkuu yeye apate maji atumie kwa vizuri na mama nyumbani lakini na wananchi wake waliokuweko pale wapate maji watumie na wao ili wapate kufanya kazi ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naunga mkono hoja asilimia 100, ahsante sana baba piga kazi big up. (Makofi)