Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

Hon. Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia katika hoja iliyoko mbele yetu ya Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama amabvyo msemo maarufu unavyosemwa, kwamba maji ni uhai kweli maji ni uhai, na kwa ajili ya ustawi wowote wa jamii ni lazima kuwepo na uhakika wa upatikanaji maji safi na salama. Suala la upatikanaji wa maji safi na salama mdau wa kwanza kuhakikisha wananchi wanapata maji ni Serikali, ihakikishe wananchi wanapata maji katika maeneo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama haitoshi kwenye baadhi ya maeneo, kama endapo Serikali kama inachelewa kupeleka huduma hii wananchi wanaamua wenyewe kujianzishia miradi yao kwa mujibu wa taratibu ili mradi wapate maji kwa ajili ya wa ustawi wa jamii yao. Miaka ya 1990 katika Wilaya ya Karatu kulikuwa kuna shida kubwa sana ya upoatikanaji wa maji. Ulipofika mwaka 1999 wananchi wa Karatu waliamua wenyewe, pamoja na viongozi wao wa wakati huo kujitafutia ufumbuzi kuhakikisha wanapata maji katika maeneo yao. Katika vijiji sita katika Mji Mdogo wa Wilaya ya Karatu, waliamua kuchangisha wenyewe fedha zao, kuchimba maji na kutafuta maji. Walihakikisha kwamba wanataka kupata uhakika wa maji. Ilipofika mwaka 2002 wananchi wa Karatu wakaanzisha mradi wa maji maarufu kwa jina la KAVIWASU. Ni mradi ambao ulikuwa umebeba na unatoa huduma katika vijiji sita ndani ya Mji wa Karatu. Wananchi hawa walihakikisha kwamba wanaendeleza mradi huu kwa fedha zao na kwa gharama zao wenyewe, na walisajili mardi huu kama bodi ya wadhamini chini ya vijiji hivyo sita.

Mheshimiwa Naibu Spika, ilipofika mwaka 2022 mradi huu ulitimiza miaka 20 kwa huku wananchi wakiendelea kujiendesha wenyewe kwa kuhakikisha wanasambaza maji, wanapata maji na mradi unaendelea kukua. Lakini mradi huu mara ya kwanza ulikuwa unatumia maji mtiririko, kwa maana ya maji ya msimu wa mvua, lakini baadaye wananchi wakajiongeza wakaanza kuchimba na visima virefu ili kuhakikisha upatikanaji wa maji wa uhakika kwenye maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu katika miaka 20 uliodumu kabla ya mwaka jana maamuzi yaliyofanyika ambayo nitayaeleza uliweza kuhakikisha ndani ya vjiji hivyo sita katika Mji wa Karatu asilimia 76.8 ya wananchi wanapata maji. Lakini kama haitoshi mtandao wa maji uliweza kufikia kilomita 478.4, na wananchi ambao wamejivutia maji majumbani walifika takriban kaya elfu tatu na zaidi. Vilevile mradi huu ulikuwa unazalisha lita milioni nne kwa saa, katika mji wa Karatu. walikuwa na ma-tank ya kuhifadhia maji 23, ma-tank ambayo yanakidhi lita tofauti tofauti kuanzia elfu thelathini na tano, elfu kumi na tano, elfu saba na kuendelea. Lakini walikuwa na visima virefu nane vya uhakika vya kuhakikisha maji yanapatikana mwaka mzima na wananchi katika vijiji hivi wanapata maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia walikuwa wana Public DP, yaani machoteo ya maji ya wananchi wa kawaida 128, na yote yalikuwa ni active na yanapatikana bila shida. Sasa shida ikaja mwaka jana, Mheshimiwa Waziri amekwenda Karatu amevunja mradi huu. Wananchi wa karatu wanauliza; kwa mafanikio haya ambayo wao wenyewe kwa fedha zao mradi huu umechangiwa na wananchi asilimia 100 hakuna hata shilingi 10 ya Serikali iliyokwenda pale; ni sababu zipi zilifanya Wizara Kwenda kuvunja mradi huu? Wananchi hawa walikuwa na tatizo la maji miaka yote hawakupata hata shilingi 10 kutoka Serikalini, wakaamua wenyewe kwa jitihada zao wakajiletea mradi wa maji, wakausajili kwa utaratibu unavyotakiwa, kwa nini Wizara mmeend akuvunja mradi huo wa wananchi?

Mheshimiwa Naibu spika, lakini kama haitoshi kuwepo miradi kama hii Karatu si ya kwanza, kuna miradi mingine ambayo imefanya vizuri sana katika Jimbo la Hai. Nilikuwa naongea na Mheshimiwa Mbunge pale asubuhi kuna mradi wa Uroki, Bomang’ombe, kuna mradi wa Losaa-Kia kuna mradi wa Machame kuna mradi wa Lyamungo. Miradi hii inafanana kabisa na mradi ule ule ulioko Karatu, na miradi hii na inafanya vizuri sana. Mheshimiwa Mbunge amenipa taarifa pale asubuhi miradi hii bado ipo kwa upande wa Hai.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tunataka kujua Karatu wamewafanya nini mkaenda kuvunja huu mradi? Na kama kulikuwa kuna shida kwa nini hamkukaa na wananchi, mkawafuata na mkapata maoni mkataka kujua? Mheshimiwa Waziri mmeenda na hoja nyepesi sana, mmesema mradi wa KAVIWASU ulikuwa unatoza maji ghali, mkaanziha mradi wa Serikali unaitwa KARUWASA mwaka 2014. Wakati mnaanzisha mradi wa KARUWASA, KAVIWASU ilikuwa inashida gani? Sisi wananchi tunajua kulikuwa hakuna shida, nyinyi mkaanzisha mradi mwingine wa Serikali ndani ya eneo lile lile ambalo wananchi walijipatia maji wenyewe. Huu mradi wa KARUWASA mliouanzisha Serikali ulikuwa unatoa huduma kwa asilimia 30 tu. Ilikuwa ina mtandao wa maji kilomita 58, ilikuwa inazalisha maji lita 1,000,000…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)