Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

Hon. Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuchangia hoja iliyoko mbele yetu ya Wizara Maji. Pia nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha uhai na afya njema kwa siku ya leo nakuweza kusimama kwenye Bunge lako hili Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimpongeze Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya maji na hususani Wilaya ya Nyang’hwale. Tumeendelea kupokea fedha nyingi sana kwenye sekta hii ya maji hongera sana Mama tuko pamoja wana Nyang’hwale 2025 zako ni za kumwagika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimshukuru Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa alivyofanya ziara yake Mwaka 2018 pale Wilayani kwetu Nyang’hwale na kuweza kuja kukuta mradi huu wa kichefuchefu Nyamtukuza aliweza kutoa maneno makali na maelekezo makali na mradi huo leo umeweza kukamilika. Ombi kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu tunamuomba sasa aje auzindue mradi huo ambao tayari umeishakamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimpongeze Waziri pamoja na Naibu Waziri, pamoja na Katibu Mkuu na wizara yote kwa ujumla. Kwa kazi nzuri ambazo wamezifanya na walizozifanya katika Jimbo la Nyang’hwale kwa kweli mradi huu ulikuwa ni kichefuchefu. Alikuja Mheshimiwa Waziri Mkuu akawa anasema Nyang’hwale Oyee wanamwambia maji, akaja Waziri Aweso akasema Nyang’hwale Oyee wanamwambia maji. Lakini leo hii tatizo la maji Wilaya ya Nyang’hwale tumelipunguza kwa kiwango kikubwa sana. Hongereni sana Waziri Aweso pamoja na Prisca pamoja na timu nzima ya Wizara ya Maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwapongeze ma–manager wangu hasa ma–manager wa RUWASA Mkoa wa Geita Jabir pamoja na Moses wa Wilaya Nyang’hwale kwa kazi nzuri ambazo wanazifanya tunashirikiana nao vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuunga mkono hoja, kwanini naunga mkono hoja? Kwa kweli tulikuwa nashida ya maji katika Wilaya ya Nyang’hwale kwa kipindi kikubwa sana. Mwaka 2020 tulikuwa na asilimia 39 tu ya upatikanaji wa maji lakini kufikia mwaka 2023 tumefikia asilimia 65 kwa kiwango kikubwa tunatoa pongezi kwa wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna vijiji 40 ambavyo tayari tumeishafikiwa na maji lakini vijiji vilikuwa ni 62 bado vijiji 22. Maji yaliyopatikana ni kupitia visima virefu na vifupi lakini pia kupitia Mradi wa Maji Nyamtukuza lakini kutoka Mahando – Ilogi kwakweli maji tumeyapata hongera sana Mheshimiwa Waziri wa Maji pamoja na Naibu Waziri lakini pia pongezi nyingi zimuendee Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maji yaliyopatikana kwa kupitia Bomba la Mangu – Ilogi ni vijiji 20 mpaka sasa hivi vinanufaika na bomba hilo lakini watu wanaonufaika na maji katika Wilaya ya Nyang’hwale ni watu 133,000 kati ya watu 207,000. Mradi wa Mahando – Ilogi ifikapo 2022/2023 ampapo tunaenda kumalizia baadhi ya vijiji vitakavyokuwa vinanufaika ni vijiji vifuatavyo ikiwemo Karumwa, Busengwa, Izinya, Kayenze, Bukwimba, Mundu, Mwamakiliga, Lugwa, Kafita, Mushimba, Ikangala, Kitongo, Kakola, Nyaudele, Bungombela, Bukungu, Bulangale, Igeka pamoja na Nyamtukuza vijiji hivi vitaendelea kunufaika baada ya kukamilisha Mradi huu wa Mangwi – Ilogi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo Bajeti yetu hii ya 2023/2024 tunatarajia kukamilisha baadhi ya vijiji vifuatavyo;

Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya vijiji vilivyokamilika Jimbo la Nyang’wale ama Wilaya ya Nyang’wale itakuwa imeshakamilisha na kumaliza kabisa tatizo la maji. Vijiji hivyo sitaki kuvitaja niseme kwa sababu ya muda. Tuna bilioni 15 ambazo tulitengewa kwa ajili ya mradi wa Nyamtukuza. Mpaka sasa hivi tumeshatumia bilioni 10.3, ina maana bado kuna bilioni nne na point. Mradi huo umekamilika, tunaziihitaji fedha hizo ziendelee kutolewa ili tutweze kusambaza maji kwenye vijiji ambavyo nilikuwa nataka kuvitaja.

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha hizo ni takribani bilioni nne na kitu. Lakini pia tulitengewa bilioni nne kwa ajili ya ujenzi wa tank la chujio. Tumeahirisha kujenga chujio hilo sasa hivi tunaziomba fedha hizo ziendelee kutolewa kwa ajili ya kusambaza mabomba kwenye vijiji vingine vilivyobaki. Kwa nini tumesitisha hilo zoezi la kujenga hilo tank, ni kwa sababu sasa hivi tunatumia maji ya kutoka Mangu Kwenda Ihugi, maji safi na salama, hivyo hatuhitaji tena kujenga tank. Tunaziomba fedha hizo zitoke ili tuweze kukamilisha vijiji vyote ambavyo vimebaki.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo machache naomba kuunga mkono hoja, lakini ombi langu la mwisho, nakuomba Mheshimiwa Waziri; kwa sababu mradi huo ulikuwa ni kichefuchefu na wewe, Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Waheshimiwa Mawaziri wengine walifika kwa ajili ya mradi huo. Ninakuomba sasa nikuombe uje uuzindue mradi huo. Mwambie Mheshimiwa Waziri Mkuu tunawasubiri kwa hamu mje muuzindue. Lakini pia fedha hiyo niliyoiomba iendelee kutolewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii.