Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

Hon. David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa fursa ya kunipa nichangie wizara hii, kwa sababu pia ni wizara yangu ya kwanza kuchangia. Moja nitumie nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, kwa hotuba yake nzuri lakini pia aina ya uwasilishaji ambao unavutia. Sisi sote tunafahamu kwenye maji yako mambo manne la kwanza tunajadili rasilimali, la pilli tunajadili uwezo wa kusambaza maji hayo, la tatu tunajadili hali ya maji taka na la nne tunajadili ubora wa maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kabla sijaanza huko, nitumie nafasi hii kumpongeza Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amefanya mapinduzi makubwa kwenye sekta hii ya maji na hapa imeelezwa mambo aliyoyafanya sitoweza kusoma moja moja. Lakini amekamilisha miradi 1373, amekamilisha miradi kwenye miji 80 inayokwenda kuhudumia watu 4,000,000 lakini zaidi ya yote ametusaidia miradi vichefuchefu ikiwemo kule kwangu Sawala Mufindi Miradi 157 kati ya 177, Mheshimiwa Waziri hongera sana kwa usimamizi wa jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumeona mchakato wa miradi Miji 28 ambayo na Mafinga, Makao Makuu ya Wilaya yetu ya Mufindi kwa Ndugu yangu Chumi unakwenda kuanza, hongereni sana Wizara. Lakini pia tumeona asilimia imefika asilimia 77 kwenye maji vijijini ambapo kimsingi ndiko ninakotoka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma ripoti water utility performance review report for the financial year ya mwaka 2021/2022 imejielekeza katika mambo mbalimbali kwa kina yameainishwa mle ndani. Naomba nisome kakipande kadogo sana anaesema during financial year... nitaitafsiri katika Mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 uzalishaji wa maji uliongezeka kwa asilimia 1.2 lakini in stored water production capacity uwezo ulikwenda mpaka asilimia 2.6 lakini upande wa pili mahitaji ya maji yaliongezeka mpaka kufika asilimia 9.8 kulinganisha na mwaka uliyopita.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa ndipo hoja zangu mbili zinapokwenda kuibuka.tunafahamu Taifa letu, tuna fursa nyingi ambazo tunazo na pengine kabla sikufika huko nimalizie kushukuru kwenye upande wa Jimbo langu. Mheshimiwa Waziri, sina deni na wewe nakushukuru sana wewe, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, watendaji hususani wa kinamama wale viongozi wangu meneja kwenye wilaya na mkoa kwa kazi kubwa ambayo mmenifanyia katika mwaka uliopita. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi yote niliyotamani kusema leo nitegemee niongee kwa bashasha nije na takwimu umenifilisi. Ninachokuombe kheri, naomba ukaitekeleze ikafanyike kwa ufanisi mwaka jana ulianza Mradi wa Igowole nilikuomba ufanye extension isiishie Mkalala, Ikwega na Igowole nimeona hapa unapeleka mpaka Itulituli, Kihanga, Mninga, Kisasa, Kidatu, Uvizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilieleza juu ya umuhimu wa Kata ya Mtambula nimeona umeiweka humu ndani kwenye maji mwaka huu. Nimezungumza kuhusu mradi wa vijiji vya Sambalamaziwa nimeviona humu ndani, japo sijaona Iramba na Kindegebasi nitaomba utuongezee hapo pamoja na Namkangu kule Idunda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa Malangali niliulizia sana mwaka jana leo Mheshimiwa Tendaga amezungumzia, nimeoa amuweka hapa leo pia, mradi wa Itika – Horo na Idete nimeona pia umeukumbuka. Kwa ujumla maeneo karibu yote ambayo tulikubaliana umeyaweka kwa hiyo, kama mchangiaji wa kwanza pia sishiki shilingi yako, nakuombea kheri ukatekeleze Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi langu kwako na Wizara yako, kuna changamoto kubwa sana na uchelewaji wa kuanza kwa miradi. Sisi Mikoa yetu mitatu tulikuwa na afisa manunuzi mmoja haiwezekani vijana wako wengi mtaani hawani kazi kwa nini mtu mmoja apewe jukumu la miradi yote hiyo? Lazima mkarekebishe hili mwaka wa fedha unaofuatia Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu ya pili kwa Mheshimiwa Waziri ni moja tu ni uanzishwaji wa Gridi ya Taifa ya Maji. Kabla sijasema hiyo nikuombe nendeni mkarekebishe Sera ya Maji ya 2002 imepitwa na wakati. Hatuwezi kutumia sera ya miaka 10 iliyopita, miaka 20 iliyopita wakati muda umepita ebu karekebisheni, tusaidieni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwenye hoja dhidi ya maji ya Taifa, Taifa letu lina bahati kubwa sana hapa umetuambia mvua zinanyesha kwa wastani milimita 1,000 kwenda mbele, hapa tumeelezwa tuna maji ya bahari, tuna Ziwa Victoria, tuna Tanganyika, tuna Nyasa. Katika Ziwa Victoria sisi kama moja ya watu wenye majority shares zaidi ya utilization kubwa inafanywa na wenzetu wa Kenya sisi tupo tunaangali. Mikoa jirani tunaambiwa hapa jana kwamba ina changamoto ya ukame na itakosa chakula.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanganyika sisi tuna majority share kwenye ziwa lile lakini tunao mradi mmoja tu maji nenda Nyasa maji yake yanafaa kwa kunywewa na mwanadamu hakuna mradi hata mmoja, acha maji ya mvua Mheshimiwa Waziri wakati umefika wa kutekeleza kuanzisha gridi ya maji tukusanye maji yote ya nchi hii yaingizwe ndani tuweke ma– pipe makubwa yasambaze maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bahati nzuri nchi yetu katika nchi zenye highest pick Afrika, Tanzania ni moja wapo tunakwama wapi? Umetueleza mahitaji ya maji kwa sasa ni takribani bilioni 60 lita za ujazo, ume–project miaka 20 ijayo 2035 tutakuwa na bilioni 80 na wakati huo capacity ya maji tulizonazo ni 126 bilioni. Je, hayo mahitaji 2035 tutapata wapi maji? lazima twende tukaanzishe gridi ya Taifa ya maji kama ilivyo gridi ya Taifa ya umeme ili tuweze kupata maji ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Bashe jana amekuja hapa na hoja ya irrigation, gridi ya Taifa ndiyo mkombo. Tutapata maji kwenye viwanda, tutapata maji ya kilimo, tutapata maji kwenye uvuvi, maji ya wanyama pori, maji ya kunywa na kadhalika Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo katika mambo takayoyazungumza ambayo nategemea mwisho wa siku…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, Ahsante Kengele ya pili.

MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, ninaunga mkono hoja. (Makofi)