Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi pia na mimi ya kuchangia, na nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri na wasaidizi wake kwa hotuba nzuri ambayo ameitoa. Lakini kwa kwenda haraka nipongeze pia juhudi kubwa ambazo zimekuwa zinafanyika hasa kwenye kukuza diplomasia ya uchumi kwa sababu kazi kubwa imefanyika, nyote ni mashahidi; Mheshimiwa Rais amezunguka huku na huku akijaribu kuvutia wawekezaji. Kwa hiyo pongezi kubwa ziende kwako Mheshimiwa Waziri kwa sababu iko chini ya wizara yako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipindi unahitimisha nilitaka kujua pia, miongoni mwa vitu ambavyo nilitaka nijue nisije, nikakushikia shilingi shemeji yangu. Tumeona mkisafiri huku na huku tuna register wakandarasi zinafanyiwa memorandum nyingi sana. Tunataka kujua, katika zile memorandum of understanding ambazo zimesainiwa ni kampuni ngapi zimesharipoti hapa na zimeshaanza kufanya biashara au zimeajiri Watanzania; muweze kutusaidia ili zile fedha ambazo mnakuwa mnazitamka kule at least tuone kwamba zimeshaanza kuingia nchini na zinafanya kazi, hilo moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya pili sehemu yetu kubwa ambayo ni Wizara ya Madini halijaribiwi kuongelewa kwa kirefu kabisa ni issue ya Liganga na Mchuchuma. Hili jambo tumeliongea kwa muda mrefu sana kama Kamati. Lakini nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri lakini pia Mheshimiwa Rais, kwa sababu kwa taarifa ambazo tunazo na hotuba ambayo imetolewa ulituahidi mwezi wa nne fedha itakuwa imetoka lakini huu ni mwezi wa tano; na kwenye hotuba yako uliyotoa ni kwamba tayari pesa ile bilioni 15.4 iko kwenye process nzuri, kwa hiyo wale wananchi wa Ludewa wanaenda kulipwa pesa yao na haitima ya matatizo haya ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu tunahakika yatamalizika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tunasema tunauhakika yatamalizika, Serikali haikuwa imefanya commitment yote ile pale ndiyo maana Kamati tulikuwa tunapiga kelele. Kwamba tunataka tuone mkono wa Serikali pia. Kwa sababu tunavyosema mkandarasi alikuja tukakubaliana hivi ilhali Serikali haijawekeza hata shilingi ilikuwa inakuwa ngumu kwetu. Ndiyo maana tukaomba kwamba basi hata fidia tulipe sisi kama Serikali, na baada ya hapo ndipo turudi nyuma tuanze kutafakari ni wapi tunaenda au ni nini tunafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa baada ya kulipa fidia kwa sababu tuna uhakikia ni bilioni 15.9 za walipa kodi wa Tanzania zitakuwa zimewekwa pale sidhani kama kutakuwa na kurudi nyuma. Ni lazima tuone majibu na tuone mradi huu mkubwa wa liganga na mchuchuma ukinyanyuka na hatimaye uweze kutupa matokeo yale ambayo tunayahitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeongea mara nyingi na nimekuwa najiuliza huyu bwana ambaye tulikuwa tumeingia naye mkataba nadhani niliwahi kutoa taarifa kwenye Kamati hawa watu kiongozi wao ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa group yao alinyongwa tarehe 09 Februari kwenye nchi yao, kwa makosa ya rushwa na kujihusisha na vikosi vya mafia na vurugu nyingine ambazo zilikuwa zinaendelea huko. Since then, kumekuwa na hali ya sintofahamu. Kwa sabau kula wakati tukiuliza Mheshimiwa Waziri tunambana sana na kweli sometimes alikuwa anatoa majibu lakini unaona alikuwa anafikia hatua unaona anajibu lakini inafikia stage hawezi kuendelea tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho kipo ni kimoja; mimi niombe tena, hata kama tunarudi kwenye meza ya majadiliano, maana kunakuwa na tetesi kwamba huyo mtu kuna Serikali inataka imchukue halafu yenyewe irudi kwenye meza badala yake. Lakini ukijaribu kuangalia huyu mtu kwenye makubaliano yetu alikuwa anakuja na Dola za Kimarekani milioni 600 halafu tunaunda kampuni ya ubia. Tukiunda kampuni ya ubia huyu mtu anaenda kukopa bilioni 2.4 dola kwa kutumia mtaji wa eneo llile ambalo tumempa na hati zetu. Na huyu mtu amekwamisha mradi huu kwa muda mrefu kwa sababu anadai vivutio vya ziada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa unajiuliza fedha yenyewe ni dola milioni 600 hujaja nayo, bado tunaunda kampuni ya ubia ya kukusaidia kukopa hutaki kwenda, pili unataka vivutio vya ziada ilhali hata shilingi hujaweka. Sasa mimi nimekuwa na wasiwasi sana; lakini Mheshimiwa Waziri nikawa najiuliza, maana kuna tetesi nyingine zipo, kwamba CEO wa hii kampuni ni mtanzania mwenzetu, hivyo ninaomba wakati una wind up utujibu. Huenda hii kampuni inasemekana ipo china kumbe ipo hapahapa, tunazungushana na wenzetu. Kwa hiyo nilikuwa naomba hili pia tupate majibu ili tuweze kuondoka hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo jingine ambalo limeongelewa na watu wengi sana hapa, na mimi sitaki kuwa mbali ya hili, ningependa niligusie pia. Issue ya utoaji wa Kampuni ya Tanga Cement ikichukuliwa na Twiga Cement. Mimi sina shida sana na issue ya take over lakini kwa sababu jambo hili limeleta taharuki, jambo hili limelalamikiwa na watu wengi sana; Mheshimiwa Waziri nikuombe, kwa busara. Jana Mheshimiwa Ulega hapa wakati anamaliza alisema jambo moja kwamba Mheshimiwa Rais asingependa aone manung’uniko na vurugu zile. Ndugu zangu wa Kigoma waliokuwa pale wakashangilia,
Mbunge mwenzangu wa Kigoma aliyekuwa hapa mbele yangu akaanza kupiga simu jimboni kwamba mambo yamemalizika nikasikia na wananchi wanashangilia kwenye TV. Maana yake ni kwamba jambo hili lilikuwa na shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusingependa twende na mambo ambayo yanatuletea shida. Mimi kwangu ukiniambia mtu anamiliki share hundred percent, kama antulipa kodi na ameajiri Watanzania its fine, acha amiliki. Kwa sababu at the end of the day hatutegemei kwamba kiwanda hiki cha Twiga kitashindwa ku-expand au Kiwanda cha Tanga kitashindwa ku-expand kwa sababu tu kina limit. Lakini tunachokisema, sheria yenu mliyojiwekea wenyewe ikoje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni Bunge hatuwezi kutunga sheria halafu tukakanyaga sheria sisi wenyewe, hapo ndipo utata unapokuja. Ndiyo maana tunaomba, kama kweli sheria ilitungwa na iko hivyo tuheshimu sheria tulizojitungia wenyewe, maana kama hatutazijali hizi sheria kesho zitatuletea shida hapa hilo ndilo tunaloliomba. Maana kweli FCC ipo chini ya Wizara, hii FCT ipo chini ya Wizara hii. Haiwezekani tukawa na taasisi mbili chini ya wizara moja zinasimamiwa na Waziri mmoja; huyu anasema hivi na huyu anasema hivi halafu sisi tukaamua ku-side na taasisi moja wapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima tukubali turudi nyuma kama kuna irregularities zilizofanyika wakati wa take over hii tuzifute tutangaze upya. Kukiwa open kila mmoja akaona tutaweza kwenda mbele. Maana ilisomwa habari hapa, kuna kampuni gani ambayo sijui imefutiwa usajiri, walisema ni Chalinze au whatever, nimesikia, kwamba ilifutiwa usajiri. Lakini kama ilikuwa na usajiri mpaka mwaka jana inafungua kesi mtawafikia BRELLA huko; lakini yenyewe bado ni sehemu ya ile kesi kwa sababu tayari walishakuwa na usajiri kipindi jambo linaanza na kama halipi, hakuna anaye mtetea asilipe. Na kama ana fedha huyu mtu mnasema kampuni ya mfukoni…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: … na kama ni kampuni ya mfukoni tayari mnasema ana fedha, hii fedha anaitoa wapi na ni kampuni ya mfukoni? Kwa hiyo ningependa tusiende sana kujiuliza huko kutaja kampuni au kufanya nini; tunachotaka tuone procedure yetu iko sawa ili tuweze….

MWENYEKITI: Mheshimiwa Engineer Ezra naomba upokee taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Msukuma.

TAARIFA

MHE. JOSEPH K. MSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru napenda kumpa taarifa mzungumzaji. Nilivyochangia mchana nilisema kampuni hii ni kampuni ya briefcase ambayo haijukani inakotokea. Sikutaka kwenda mbali kwa sababu muda wangu wa kuchangia ulikuwa mchache; lakini tunao ushahidi na uthibitisho ambao unaonesha kuwa kampuni hii ni hewa haijulikani ilikotoka address fake, kiwanda kiko kwenye plot Kinondoni na wenye kiwanda ninazo picha zao hapa ukitaka tukabidhi tukabidhi. Tuachana na hizo biashara ya matapeli Bungeni.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Ezra Chiwelesa unapokea taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Msukuma?

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napokea taarifa, maana kama kampuni ilisajiliwa na Serikali halafu tunaita ni kampuni fake, kwamba ni za kwenye briefcase means kampuni nyingi ziko hapa mnatuambia tuna makampuni yamesajiliwa kumbe hayapo basi Serikali irudi nyuma ikayaangalie kama yapo mengine yafutwe sawa na hiyo Kamapuni ya Chalinze ilivyofutwa. Napokea taarifa ya kaka yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa kumalizia, nime- experience kidogo na haya mambo, naomba ni share experience yangu. Nimefanya kazi Air Tanzania mwaka 2020, that time nilikuwa najihusisha kama cabbing crew. Kilichokuwa kinafanyika; hizi take over ni nzuri sometimes take over ni mbaya. Unakatiwa tiketi Air Tanzania ndani inasema Air Tanzania cover juu limeandikwa South African Airways. Kilichokuwa kinatokea ukishasoma kesho una haja ya kwenda Air Tanzania, si utakata moja kwa moja kwa msafirishaji mwenyewe?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo sometimes take over ni nzuri lakini intention ya yule anaye-take over unaijua? Huyu bwana Tanga anazalisha clinker kwa sehemu kubwa, Twiga Cement akishakaa na Tanga Cement wakaanza kushirikiana na shareholder ni mmoja huyu anahitaji material kutoka kwa mwenzake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, achana na mambo ya sukari ile ni miwa, huwezi kutoa muwa Kagera ukaupeleka Bukoba kwenda kuzalisha ukaupeleka Morogoro kwenda kuzalisha, hautakulipa. Huyu bwana akichukua clinker Tanga kwa bei ambayo wanajuana wao akaongeza tu bei ya transport, kwamba transportation cost yangu mimi kutoka Tanga kwenda Dar es salaam ni kadhaa maana yake production cost yake itakuwa kubwa, twiga pale. Production cost ikiwa kubwa ata-declare low profit aki-declare low profit maana yake kodi tutapata ndogo.

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kodi tukipata ndogo huku Tanga akapunguza production ya clinker maana yake huyu anaweza akafanya biashara tukapata kiwanda kipya kinazalisha lakini hatupati faida na kodi kwa Serikali.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ezra…

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ungeacha nimalizie tu.

MWENYEKITI:…naomba upokee taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Mhagama.

TAARIFA

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimuongezee taarifa Mheshimiwa Engineer Ezra kwamba Teknolojia ya Twiga ni ya viwango vya juu sana ukilinganisha na teknolojia ya Tanga Cement maana yake nini? Maana yake uwezekano wa Tanga Cement na asset zilizopo pale Tanga Cement pamoja na resources zilizopo pale zikawa zinatumika kusafirishwa zaidi kwenda kuzalisha Dar es salaam kuliko kuendeleza kiwanda cha Tanga.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chiwelesa unaipokea taarifa?

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nipokea na unilindie muda kidogo kuna jambo nilikuwa namalizia. Kwa hiyo ninachosema ni kwamba, tunaweza tukaendelea na production ya cement Tanga, its fine, itaendelea kuwepo pale, lakini wakazalisha kwa kiwango kidogo halafu Dar es salaam wakaongeza huku waki-declare kwamba cost of production kwa Dar es salaam ni kubwa kwa sababu watakuwa wanaunua raw material pale. Kiwanda kile kitazalisha less tutakiua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Wabunge wa Kanda ya Ziwa cement tunayotumia kwa sehemu kubwa ni cement ya Simba. Leo hata mkisema kwamba cement inazunguka nchi nzima leo tunaona mfuko 24,000, cement ukiitoa Mtwara ukaifikisha Biharamulo utauza mfuko kwa shilingi ngapi? Cost of production ni ileile transportation cost itakuwa kubwa; ndiyo maana kama hilio jambo tunalisema hapa Serikali itusikilize.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo hata ya Liganga na mambo mengine Waheshimiwa Wabunge walipata nafasi ya kusema, sasa msiposikiliza tuangalie mbele siyo leo take over ya leo ni nzuri kwa sababu amekaa na fulani ameongea lakini baada ya miaka mitano miaka kumi miaka 20 tunaoongea sisi hatutakuwepo, hata Wabunge tunaoongea humu ndani ya bunge labda watakuwa wamebaki asilimia 30 au 20, sasa where are we going baadaye? Turudi hapa tena kubadilisha sheria? Turudi hapa kulaumiana? Ni bora tunapowashauri leo msikilize kuliko kusubiri mambo yaharibike baada ya miaka 10 miaka 20 warudi hapa watu kuja kubadilisha sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yangu ni hayo nashukuru kwa nafasi na ninaunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)