Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Katani Ahmadi Katani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tandahimba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kukushukuru sana. Nitakuwa na mambo mawili tu; moja hili ambalo mzungumzaji aliyemaliza kuchangia amezungumza, lakini la pili pia linahusiana na hili hili tunalolisema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yetu ya Maendeleo ya Jamii, tunao Maafisa Ustawi wa Jamii wako mtaani kule, leo kumetokea changamoto hii kubwa ya tatizo, hili janga la kitaifa, maana hili limeshakuwa janga la kitaifa. Vile vile tuna wanafunzi waliohitimu elimu ya ustawi wa jamii na ni wataalam wamezagaa mtaani. Hivi vitendo vinavyozungumzwa mchangiaji amezungumza vizuri sana na Mwenyekiti umeshauri tuzungumze kwa stara. Haya mambo ni ya mtambuka, kuna haya tunayoyaona kwa macho, yapo tusiyoyaona kwa macho na yanafanywa majumbani kwetu. Ndiyo maana mchangiaji akashauri hapa ikiwezekana maana utaratibu wa Jeshini watu wakienda wanapimwa. Vile vile na sisi ni wawakilishi wa wananchi lazima tupimwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ni wawakilishi wa wananchi na ni lazima tuwe kioo cha jamii. Sasa hatuwezi kuwa kioo cha jamii kuna watu wanakuja hapa kumbe wanashughulikiwa, itakuwa sio sawa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye jambo hili Mama Masaburi alikuwa anachangia pale, akawa ananukuu vitabu vya Mungu…

MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Katani, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Kunti Majala.

T A A R I F A

MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Napenda kumpa tu taarifa Mheshimiwa Katani kwamba suala la Wabunge sisi kupimwa naamini halishindikani na Bunge limekuwa na tabia ya kutuletea Madaktari kwa ajili ya ku-check afya zetu. Sasa naamini wiki ijayo kuanzia Jumatatu litafanyika hilo, Wabunge wote wataletwa Madaktari hapa tutaanza kupimwa. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Katani, taarifa unaipokea?

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea taarifa hiyo na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Afya yupo, nikuombe sana dada yangu kwenye jambo hili tuwe serious.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Katani kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Musukuma.

T A A R I F A

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Hili jambo nampa taarifa mzungumzaji kwamba tunalichukulia kama mzaha na Watanzania wanaangalia Bunge live. Tukizungumza mambo ya ufisadi watu tuna- concetrate kusikiliza, sasa tukizungumza suala la Wasenge linakuwa kama ni utani. Hata hiyo, nampa taarifa mzungumzaji kwamba nchi yetu imepitia majaribio mengi sana. Tulikuwa na jaribio la Kibiti na Lindi, Serikali ilishughulika likaisha, tumepata la Corona, Serikali imeshughulika limeisha wala hatukujadili humu, tuliwaachia wataalam, tumepata janga juzi la mwisho la panya road, leo hawapo. Sasa hili lina ugumu gani kulimaliza kimya kimya kuliko kulileta Bungeni? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Katani, taarifa unaipokea?

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa naipokea, lakini nadhani anatoa maelekezo kwa Waziri Mkuu, ninavyohisi wala hanipi mimi taarifa hiyo, maana anasema washughulikie huko Serikali. Sasa kwa sababu mimi sio Serikali mimi ni upande wa Bunge, sisi tunatunga Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema dada yangu Mheshimiwa Ummy yupo hapa na naamini tunavyo vifaa vya kutosha. Kunti ameshauri jambo jema sana, tusisubiri subiri hapa wamezungumza mambo ya supu ya mbwa inanywewa ikiwa ya moto. Hili jambo tusisubiri subiri, Mama kama wataalamu wapo waje hata kesho shughuli ianze.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Katani endelea, muda umekwenda.

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mama Masaburi pale kumbe vitabu vya dini hivi viko sawasawa sana. Mama alikuwa anakumbusha kitabu cha Lutu ambacho na sisi kwenye Quran ipo. Sura ya 11, surat Hud ukienda aya ya 82 watu wa Lutu walishatolewa hukumu ya kuuawa, walawiti wale nchi ilipinduliwa kukawa na vitu kama mawe kwenye Quran.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kuna hadithi hapa sahihi kabisa ya Mtume Muhammad (S.A.W) “Raawu Imam Abu Dawud an ibn Abbas qala; qala Rasulu Allah, Swala- Allah Alayh Wasallam, idhaa raaytum man yaf-al amara kaumi Luutwi faktulu fa’ila walmafuula bih.” Imepokewa na Imamu Abu Daud kutoka kwa Ibn Abbas amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa sisi Waislamu ni hadithi sahihi; mtakayemkuta anafanya kitendo cha watu wa Lutwi, ulawiti, kuingiliana kinyume na utaratibu, vitabu vyote kila kiungo cha mwanadamu kimetengenezwa kwa ajili ya kazi maalum. Binadamu sisi tumekuwa wanyama unakwenda kufanya jambo kwenye sehemu ambayo ya kutolea uchafu wa mwanadamu. Hii ni dhambi, watu hawa wameamuliwa kuuawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama Bunge tunayo nafasi kubwa, tunaogopa nini? Ndio misaada inayosemwa? Yaani Taifa liangamie kwa kuogopa misaada ya wafadhili? Wanaoleta hizi taasisi za watu wa kufanya mambo ya hovyo wapo mtaani. Watu hawa tutunge sheria hapa. Uganda wamefanya mfano pale miaka 10 sisi tusisite. Sheria zilikwishatungwa toka mwanzo, alete sheria hapa Waziri mwenye dhamana tupitishe sheria hapa. Ili watu wakome ni kunyongwa tu. Tukisema wanyongwe tu, hakuna mtu atachezea chezea, hakuna mtu atacheza huu mchezo na hata majumbani huku ndio maana tukasema tupimane hapa, wanaume kwa wanawake tupimane. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo kama Bunge lazima tuone kwamba tuko serious, Taifa haliwezi kupotea hivi. Hii ni nguvu kazi, tusipoanza sisi kwenda kuwaambia wananchi huko wapime itakuwa shida. Ilikuja corona hapa ilikuwa ni lazima, huwezi kusafiri bila kupima corona na sisi Wabunge huwezi kuingia ndani kama hukupima, tutapima wote hapa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetoa aya nzuri sana, kila kiungo kina matumizi yake, sio wanaume tu hata wanawake wanaoshughulikiwa huko na wenyewe wapimwe tu, maana kila kitu kimewekwa kwa uhalali wake, ndio maana nikasema mlangoni pale dada yangu Mheshimiwa Ummy alete wataalam na wakiletwa wataalam ili tuingie humu kila mtu atapima.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Katani, ahsante sana muda wako umeisha.

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)