Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kabla siajaanza kuchangia naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu, ambaye amenipa kibali cha kuweza kusimama hapa katika Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudie kumshukuru Mungu, kwa sababu kabla sijaanza kazi hii ya ubunge tulikula kiapo kwa kutumia Biblia na wenzangu Waislam, ndugu zangu walitumia Quran Tukufu. Kwa hiyo tunapokwenda kufanya kazi kwa kumtumia Mwenyezi Mungu, twende kufanya kazi kwa kumheshimu na kumwogopa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii pia kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayoifanya yeye na wasaidizi wake Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri wote, Watendaji wote wa Serikali pamoja na Wabunge, wamefanya kazi kubwa sana kwa kuhakikisha kazi na maendeleo yanaendelea katika nchi yetu. Mheshimiwa Rais, aliahidi kwamba atafanya kazi na slogan yake ni “Kazi Iendelee” baada ya kurithi kazi aliyoiacha marehemu Dkt. John Magufuli. Mheshimiwa Rais, aliahidi ukweli na amefanya kazi, amepambana sana, tumetembelea miradi mingi, tumeona mambo makubwa yanayofanyika, Mama amefanya kazi kubwa sana tena ya kijasiri. Waheshimiwa Wabunge na Waheshimiwa wananchi, tunaomba tumuunge mkono Mheshimiwa Rais, ana nia njema sana katika nchi hii. Tumpe nguvu, tumwombee kwa Mwenyezi Mungu, aweze kutimiza ahadi zake alizoahidi kwa wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, amani na usalama katika ngazi ya familia. Suala la maadili na malezi ya watoto wetu yanashabihiana na amani na usalama katika ngazi ya familia. Sisi wazazi na walezi tulitetereka katika kulea watoto, tumeachia wadada wa kazi kulea watoto, tumeachia watoto majirani kutunza watoto sisi tunahangaika na kutafuta pesa. Matokeo yake watoto wamejilea wenyewe, watoto wetu wamebakwa, watoto wamelatiwa, watoto wamejifunza tabia tofauti kinyume na maadili, sasa tunalia, tufanye nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile mfumo wa elimu yetu hauko sawa katika kulea watoto au kufundisha watoto kuanzia ngazi ya shule za awali. Serikali iwekeze kwenye shule za awali kwa kuweka walezi wazuri ambao watamtengeneza mtoto, huyu mtoto ambaye anakuja kuwa kiongozi katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tukumbuke kisa cha Sodoma na Gomora. Naomba kunukuu hii Sodoma na Gomora kitabu cha Biblia utasoma mwanzo 19, mstari wa 23
– 26 inasema, nanukuu: “Jua lilipokuwa limechomoza juu ya nchi ya Lutu alipoingia Sowayi ndipo bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa bwana, akaangusha miji hiyo ya bonde lote na wote waliokaa katika miji hiyo na yote yaliyomea katika nchi ile lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake akawa nguzo ya chumvi.” mwisho wa kunukuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna wake wengi wa Lutu katika nchi hii ambao wanataka tugeuke nguzo ya chumvi ambao wanatetea suala la ushoga, lakini tunasema alipo shoga kuna basha, lakini wanaoonekana wengi hapa ni mashoga, mabasha wako wapi? Basha huwezi kumtambua kirahisi na mabasha ndiyo wenye pesa. Namuunga mkono dada yangu Dkt. Thea anasema waasiwe, tunasema kabla hajaasiwa na kukuhumiwa kwanza wachapwe viboko hadharani, kama nilivyoona kule Wahindi na kama nilivyo waona Waganda na wale Wamasai walivyo mchapa yule mtu aliyewasaliti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo nawakumbusha tena kuna habari za gharika kuu, uwasi wa mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu alinyesha mvua siku 40 usiku na mchana akaifuta ile nchi yote chini ya uongozi wa Nabii wake Nuhu. Hiki kitu kinachoongelewa siyo mzaha, tumeongelea miradi mingi inafanyika katika nchi hii, matrilioni ya fedha yanatumika katika nchi hii, tuna madini, tuna maziwa, tuna bahari, tuna rasilimali nyingi katika nchi hii. Nchi hii ilipendelewa na Mwenyezi Mungu, lakini tuwekeze kwa watoto waadilifu. Haya tunayosema kuna majizi, wala rushwa, yote inatokana na ukosefu wa malezi tangu mtoto mdogo. Mtoto mdogo kuanzia kuzaliwa mpaka miaka sita anaiga kila kitu. Ukimtengeneza ataiga kitu kizuri, usipomtengeneza ataiga kitu kibaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, twende Serikali tukawekeze kwenye malezi ya watoto. China wamewekeza kwenye malezi ya watoto wao, Singapore wamewekeza kwenye malezi, kuna nchi zimejifungia kutengeneza kizazi kitakachoweza kushika nchi. Tunaweza kukataa ndoa za jinsia moja maana yake unakataa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, zaeni mkaongezeke, watu wanazuia watu wasizaliane, wingi wa watu ni tishio, China wako wengi wanatisha dunia, India inatisha dunia kwa sababu ya wingi wa watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuja kudanganywa na uzazi wa mpango. Ule ni uongo wa kutuzuia tusizae ili tuendelee kuwa dhaifu. Ahadi ya Mwenyezi Mungu, ni kuzaa, utazaaje unatengeneza wanaume kuwa wanawake? Sisi wanawake ambao tunashika mimba miezi tisa unaambiwa umezaa mtoto gani? Wa kiume, zamani ulikuwa unaulizwa umezaa mtoto gani? Mwanajeshi, leo unaenda kutoa litoto linakuwa nyoronyoro, litoto langu kama lile mimi naweza kulipoteza tu, siwezi kuona vitu vya namna hiyo, haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siwezi kuwa na mtoto msenge halafu bado namchekeachekea, nitahama hata kama mji, kama nipo Dar es Salaam nitahama, siwezi kukaa na mtoto msenge. Tunaongea kwa lugha laini laini inakera sana, inanikera, inaniudhi na nawapongeza Viongozi wa Dini wameongelea kwa nguvu sana. Nampongeza Waziri Nape nimemwona juzi ameongea, lakini kila Mbunge sauti yako ni sauti ya Mungu, usiposema utahukumiwa na Mwenyezi Mungu, utakuwa umemsaliti Mwenyezi Mungu, kuungana na wale watu wa Sodoma na Gomora. Hatuwezi kufanya kazi kubwa katika kuendeleza nchi hii tukaanza kufumbia macho masuala haya. (Makofi)

MHE. ISSA J. MTEMVU: Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Issa J. Mtemvu, taarifa.

TAARIFA

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mzungumzaji anaendelea kuzungumza vizuri. Kwenye eneo la maadili hilo nilitaka nimkumbushe tu, si tu wazazi kule nyumbani, si tu Serikali kutengeneza mifumo ambayo itatuwezesha kujifungia ndani na kutengeneza msingi mzuri wa malezi kwa Watoto, lakini inasemekana hata ndani ya Bunge kuna hao unaowazungumza, hata ndani ya Bunge inasemekana, kwa hiyo Mheshimiwa Mwenyekiti, sina uhakika yanasemwa tu kwa hiyo ndiyo maana tunapata ugumu wa kulea.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Issa unachangia hiyo taarifa na kuzungumza. Mheshimiwa Janeth Masaburi, taarifa unaipokea?

MHE. JANETH M. MASABURI: Hii taarifa naipokea. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea kwa sababu nitakuwa mwongo mbele za Mwenyezi Mungu. Wenye tabia hiyo waache, tunawajua, wengine viongozi, hatutaki kusema sana, tunamwogopa Mungu si mwanadamu, haya ya dunia ni ya kupita tu. Leo niko hapa kwenye hiki kiti kesho sipo na kesho nipo labda nimekufa, lakini Mungu apewe sifa yake, Mungu ahidimiwe Mungu ndiye mwenye kutukuzwa na Mungu ndiye mwenye kuogopwa. Sisi wanadamu siyo kitu, tuko duniani kesho tunapita lakini kizazi lazima tukiendeleze kwa sababu ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutasifia ndiyo lakini kwa nini watu wanafanya hivyo na hizo NGO kubwa naona zina…

MWENYEKITI: Mheshimiwa ahsante sana, muda wako umekwisha, tunakushukuru sana. (Makofi)

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)