Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante. Kwanza sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu pamoja na kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa Hotuba yake nzuri, ilikuwa ndefu lakini tumemwelewa dhima na dhamira yake aliyoikusudia kwa Tanzania na kwa Bunge zima. Vile vile sina budi kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Mama Samia, kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kuiletea maendeleo Tanzania pamoja na Mheshimiwa Hussein Mwinyi Rais wa Zanzibar, kwa kazi nzuri kwa kushirikiana bega kwa bega na Mama Samia, kwa kuifanyia kazi Tanzania na Zanzibar kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 27, Serikali ilizungumzia jinsi Mahakama zetu zilivyoongeza watendaji ambao Majaji wa Mahakama ya Rufaa, Mahakimu na baadhi ya viongozi wengine kwa kuweza kufanya kazi kwa weledi katika Mahakama zetu, lakini kwa kweli utendaji bado uko chini, siyo wa kiwango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wameongezwa lakini kazi iko vile vile as usual, kwa sababu umewekwa pale kama Hakimu, wamewekwa pale kama Majaji Wakuu lakini kazi wanazozifanya na watendaji wao haziridhishi raia, raia bado wanapiga kelele, Mahakama hazitendi haki, mahakama zinakawia kufanya shughuli zake na mwisho hata hayo magereza yetu pia yameambukizwa kwamba nayo yanafanya kazi chini ya kiwango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija ukurasa wa 86, hii ambayo inazungumzia shughuli za Muungano, imesema kwamba kulinda, kuenzi na kudumisha Muungano wetu. Hili ni kusudio kubwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikishirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nasema hivyo kwa sababu nilimwona Mama, Mheshimiwa Dkt. Samia kipindi kile alichopewa pesa za UVIKO, alikasimu akaleta Zanzibar na huu ndiyo mtazamo mwema wa Muuungano kwa sababu zilikuja Zanzibar zimetenda kazi katika Sekta za Jamii, Sekta za Afya, Sekta za Elimu na Sekta za Maji. Sasa hapa moja kwa moja unaona kwamba Muungano wetu unafanya kazi pande zote mbili. Kinachopatikana huku na huku kinapelekwa, Mwenyezi Mungu ambariki Mheshimiwa Rais, wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri ya jinsi anavyotuangalia raia yake kwa pande zote mbili za Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja katika ukurasa wa 84, unaozungumzia ukatili wa watoto. Mheshimiwa Waziri Mkuu, alisema kwamba kuna mikoa nane ambayo imeunda Madawati ya Ulinzi na Usalama ambayo madawati hayo yako 1,993. Nasema hivi, haya madawati ni kidogo kwa mikoa nane madawati yawe kwa Tanzania nzima, hali imebadilika sasa hivi Tanzania, tunasikia mambo yanavyokwenda, tunasikia watoto wetu wanavyodhalilika, tunasikia watu wanavyopenyapenya wa kutaka jinsia moja, sasa hii dawati ikiwepo itatoa elimu nzuri na watoto watakuwa rahisi kwenda kuwa–face kule na kuweza kuzungumza. Nasema hivi kwa sababu tatizo lililopo sasa hivi ulezi tumeuachia Serikali, wenyewe wazazi kila mmoja yuko busy anatafuta maisha na kwa vyovyote Serikali haiwezi kulea mtoto, mtoto alelewe na wazazi wake kwa kushirikiana na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Zanzibar na Tanzania Bara zote zinahitaji kuangaliwa kwa jicho pana, kwa sababu hili jambo lipo sehemu zote za Tanzania na tunatakiwa tuungane ili kulipiga vita. Unajua ushoga si jambo zuri, bora akuharibikie mtoto mwanamke unajua ataolewa, atastirika, lakini akikuharibikia mtoto mwanaume kwishinei, kaisha, hawezi kitu. Taifa litakuwa limeharibikiwa, mzazi kaharibikiwa na yeye mwenyewe kaharibikiwa, ina maana hawa madada poa na makaka poa Tanzania wawe hawana nafasi. Maana kama hatukukazana hii aibu haitokuwa kwa yule mtendwa na mtenda, itakuwa aibu kwa Taifa letu. Tupige kelele, tupaze sauti, twende na sheria, tuwe na uwajibikaji kwa vitendo Serikali tuwajibike kwa vitendo siyo kupiga kelele, tukipiga kelele hili jambo mtu anaona ahaa si wanasema tu, lakini kama tutakuja kwa vitendo hili jambo litakoma. Tanzania bila ya ushoga inawezekana, tujikaze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija ukurasa wa 83 haya ya 199, hili linazungumzia kuhusu sheria ziwe za Kiswahili, tuzitafsiri, siyo mbaya kwa sababu hii itatatua migogoro kwa wananchi. Baadhi ya wananchi hawazifahamu hizi sheria kwa Kiingereza na hili si gumu kwa sababu wenzetu Baraza la Wawakilishi Zanzibar wanalifanya. Ya Kiingereza iwepo na ya Kiswahili iwepo na nashukuru Dkt. Samia Hassan Suhuhu, kalibariki hili lifanyike na katika maelezo ya Waziri Mkuu kalisema, sasa naomba hili jambo lifanyike ili nasi ile dhamira iliyokuwa imekusudiwa itekelezwe na mambo yetu yote waweze kukaa sawa na tuweze kufanikiwa. (MakofI)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haya machache, naunga mkono hoja. (Makofi)