Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuimarisha demokrasia nchini na kukuza diplomasia ya uchumi

Hon. Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Azimio la Bunge la kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuimarisha demokrasia nchini na kukuza diplomasia ya uchumi

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuchangia kwenye hoja hii ya kumpongeza Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Engineer Chiwelesa kwa kuleta hoja hii, mimi Mbunge wa Jimbo la Makete nina kila sababu za kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais, kuna hoja kadha wa kadha ambazo unaweza ukamzungumzia Mheshimiwa Rais kwa yale ambayo ameyafanya mengi.

Mheshimiwa Spika, kwanza ukiangalia kwenye sekta kwa mfano ya utalii, wakati dunia ina-suffocate kutokana na suala la Covid na watalii kupungua, Tanzania tumeweza ku-excel kwa kuongeza idadi ya watalii wengi kutokana na juhudi za Mheshimiwa Rais programu ya Royal Tour.

Mheshimiwa Spika, kwa idadi ya watalii tu, tumetoka kutoka 900,000 tumeenda 1,500,000 kwa kipindi hiki cha mwaka 2021 kuja mwaka huu. Haya yote ni matunda ya Mheshimiwa Rais. Ukienda kwenye suala la makusanyo ya fedha kwenye utalii, tumetoka dola milioni 1,300,000, tumeenda dola 2,500,000 ndani ya muda mfupi sana ambao Mheshimiwa Rais amefanya. Kwa hiyo, mimi kama Wabunge wengine, ninampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi ambazo amezifanya.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia kwenye suala la miradi ya maendeleo, kuna miradi mikubwa ambayo tunaendelea nayo kama SGR, ununuzi wa ndege na ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere. Ni miradi ambayo certificate zina-mature mara kwa mara na zinatakiwa zilipwe. Hata hivyo, at the same time ukienda kwenye Halmashauri, miradi mingi inaendelea na fedha zinashuka kwa kiwango ambacho wakati mwingine ule haijawahi kushuka. Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais anafanya kazi ngumu, anafanya kazi nzuri, anastahili sana kupongezwa.

Mheshimiwa Spika, nawaomba Watanzania ambao wanatufuatilia, wafahamu kabisa kwamba Mheshimiwa Rais anachohitaji sasa ni kutiwa moyo tu. Haya mambo anayoyafanya, ukienda kwenye Halmashauri, Wakurugenzi, miradi ilivyokuwa ni mingi, madarasa yanavyojengwa, kwenye Mataifa mengine tunaona wanavyolia. Nenda kwenye suala la inflation rate kwa maana ya mfumuko wa bei, Taifa letu na Mataifa mengine yote yaliyoko kwenye Afrika Mashariki, Tanzania inafanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii yote ni kwa sababu Mheshimiwa Rais ameweza ku-maintain uchumi wa Taifa letu kwa kiwango kikubwa sana. Kilo moja leo hapa Tanzania, ndiyo, ni kweli vitu vimepanda bei, lakini la kujiuliza, na sehemu nyingine zipo kama Mataifa ya jirani yanayoendelea huko, sisi tuko chini sana kwenye suala la mfumuko wa bei. Pia bado Mheshimiwa Rais anatoa ruzuku kwenye mafuta, anatoa ruzuku kwenye mbolea, lakini bado wanafunzi wa vyuo vikuu anahangaika aweze kuwaongezea mikopo. Hii yote ni kwamba Mheshimiwa Samia anafanya kazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kazi nzuri ambazo anafanya Mheshimiwa Rais ikiwemo pia maridhiano haya ya kisiasa, na hata sasa ukiangalia anaendelea kuunda timu kwa ajili ya kuboresha diplomasia ya uchumi kwenye Wizara ya Mambo ya Nje, ameunda kikosi kazi chini ya Balozi Yahya Simba ili waangalie tathmini ya utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje ili kuendelea kuboresha diplomasia yetu ya uchumi kupitia Wizara ya Mambo ya Nje. Ni jitihada za kweli za Mheshimiwa Rais anaendelea kuhakikisha Taifa letu linazidi kufunguka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kwa haya anayoyafanya, maridhiano ya vyama vya siasa kwenye Taifa letu na demokrasia, hata vyama vingine viweze kuiga ambacho Mheshimiwa Rais anafanya. Mheshimiwa Rais anatengeneza maridhiano. Hata wao kwenye vyama vyao, tuwaombe wawe na maridhiano kwa sababu Taifa hili tumeamua kusamehe yote yaliyopita, tumeamua kuanza ukurasa upya. Hata wao wawe na ukurasa mpya kwa sababu kama wameridhia kuchukua ruzuku kutoka Serikalini kutokana na idadi ya Wabunge na idadi ya kura, basi waridhie hata kuwasamehe hawa ndugu zetu ambao pia walikuwa na changamoto hizo. Kwa sababu ruzuku hiyo imetokana na wao wanayoichukua. Sasa huwezi ukatambua ruzuku, lakini usiwatambue Wabunge ambao tuko nao humu ndani.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba tu, hata maridhiano hayo yaendelee kufanyika kwenye maeneo mengine. Jitihada za Mheshimiwa Rais ziguse kila mtu, na wao kwenye vyama vyao viweze kuwagusa.

Mheshimiwa Spika, mimi sina mambo mengi sana, lakini kwa niaba ya wananchi wa Makete, kwa kweli miradi ya maendeleo tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais amefanya kazi kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)