Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuimarisha demokrasia nchini na kukuza diplomasia ya uchumi

Hon. Tabasamu Hamisi Hussein Mwagao

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sengerema

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Azimio la Bunge la kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuimarisha demokrasia nchini na kukuza diplomasia ya uchumi

MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na mimi kunipa nafasi ya kuchangia hoja hii. Nataka kuwaeleza Watanzania kwamba kazi kubwa aliyoifanya Mheshimiwa Rais Samia anazo sifa zote za kupongezwa kama binadamu. Binadamu katika asili akifanya vizuri akasifiwa basi anamshukuru Mwenyezi Mungu, kwa hiyo kwa hatua hii hatujafanya kosa lolote leo ndani ya Bunge hili kupeleka maono yetu na kuyasema yaliyopo katika vifua vyetu nafsi zetu ziweze kuridhika, kazi alizozifanya Mheshimiwa Rais ni kubwa sana katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na kazi anazozifanya Mheshimiwa Rais za usiku na mchana kwa ajili ya kuja kuhakikisha ustawi wa Taifa hili, Mheshimiwa Rais anajitahidi kuweka hali ya hewa katika nchi hii iwe salama. Pamoja na kuweka hali ya hewa kuwa salama katika nchi hii, yapo pia matatizo makubwa sana ya utawala bora sehemu kubwa sana ya utawala bora, kutumia hii dhana ya utawala bora watu wanapata nafasi kubwa sana ya kumrudisha Mheshimiwa Rais nyuma, katika jambo hili ni kwamba tunatakiwa kuwa makini sana wasaidizi wake hasa Bunge ni wasaidizi namba moja kwa kazi anazozifanya Mheshimiwa Rais katika kumuunga mkono.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya CAG imepokelewa na kikanuni inatakiwa ije hapa ndani baada ya siku Saba, haya yote Mheshimiwa Rais aliyoyasema wakati anapokea taarifa ile alikuwa katika saumu, alichukia akiwa amefunga, sasa nasi tunatakiwa tuchukie huku tumefunga tuko ndani ya saumu. Hii siyo dhambi na wala hatutatengua saumu zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bajeti iliyokuwa imepitishwa hapa haikuwa na fungu la wezi, naomba nirudie, tulipitisha bajeti pesa ziende kwenye shughuli za maendeleo hakukuwa na fungu la wezi. Sasa fungu la wezi linatokea kila taarifa ya CAG. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo Mama amepokea taarifa ya pili ya CAG na akaonesha ujasiri kusema hadharani amekerwa na akatumia lugha ambayo siyo ya staha ndani ya mwezi wa Ramadhani. Mimi mwenyewe siku hiyo wakati anatumia ile lugha nilichukia zaidi yake sina nafasi tu, ngoma iletwe Bungeni hapa halafu tuoneshe hali ya hewa kwamba tunamuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa dhati, tumechoka na wizi.

Mheshimiwa Spika, tulitegemea kabisa pamoja na mambo mazuri yanayofanyika huko wataalamu wetu wanafanya kazi lakini wako Wataalam ambao siyo wazalendo, wako Viongozi wenzetu ambao siyo wazalendo, taarifa hii kwa sababu haijawa dhahiri lakini tukiipitia ripoti ya CAG safari hii tunaomba dakika 20 kuchangia ili tutoe adabu isije ikajirudia tena. Kanuni ziko kwako leo tunamsifia Mheshimiwa Rais tunataka tukusifie na wewe safari hii utuwekee hii taarifa tuinyambue sawasawa, uingie kwenye historia kuzuia wezi katika nchi hii. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana naunga mkono hoja. (Makofi)