Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana kwa nafasi ya kuchangia, lakini pia nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa wasilisho zuri na ushirikiano mzuri ambao amekuwa anautoa kwetu.

Mimi na declare kwamba ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji; ndiyo maana nampongeza waziri kwa sababu tangu ameingia kwenye Wizara hii kwa kweli amejitaji kwa kiasi kikubwa kutoa ushirikiano kwa Kamati, lakini pia kuyapokea mawazo ya Wabunge na ushauri ambao tumekuwa tunautoa. Kwa hiyo, tumshukuru sana yeye na msaidizi wake na Katibu Mkuu na wengine wote ambao wanahusika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi leo nitajikita kwenye jambo moja tu, suala la mafuta ya kula ndiyo nitakaloliongelea tu kwa leo, maana masuala ya Liganga na Mchuchuma nimeongea sana hapa mpaka nikafikia stage ya kuchumba chima (kuchimba chuma), kwa hiyo leo naomba niiache twende kwenye suala la mafuta ya kula. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, jana tumesimama hapa kwa jambo la dhalura tukijadili suala la mafuta ya petrol, diesel na mafuta ya taa. Lakini tukirudi huko mtaani suala la mafuta ya kula bado ni kero kubwa na ni mzigo mkubwa kwa Watanzania, bei zime-shoot sana almost more than 100% increment ukilinganisha na wakati uliopita.

Sasa nikirejea katika Ilani ya CCM, ilani yetu inasema ambayo tunaitekeleza kwamba tuhamasishe ujenzi wa viwanda lakini viwanda ambavyo vitaajiri watu wengi na watu wengi wakitoka katika kilimo, mifugo na uvuvi. Lakini Mpango wetu wa Tatu wa Maendeleo unasema kwamba ni ujenzi wa uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu. Sasa tukirejea huko kote nimekuwa nikipitia baadhi ya papers, nina journal hapa ambayo imeandikwa na Bwana Mgeni Nampenda wa Department of Trade and Investment College of Economic and Business Study, Sokoine University; inauliza Can Sub-Saharan Africa become food safe sufficient? Analyzing the market demand for sunflower edible oil in Tanzania. Lakini ikaja nyingine ninayo hapa ambayo nimekuwa nazipitia investment analysis of sunflower farming and prospect of raising household income in Iramba District Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimechukulia hizi case study mbili nikajaribu kupitia demand yetu ya mafuta, katika kupitia ni kwamba tumekuwa tuna annual demand ya almost tani 570,000 kwa mwaka. Uwezo wetu wa ndani wa kuzalisha ni tani 205,000 kwa record ambazo nimekuwa nazipata. Kwa hiyo, tumekuwa na shortage ya takriban tani 365 na almost more that 90 something percent tunaagiza haya mafuta kutoka Malaysia na spending yetu ilikuwa ni zaidi ya bilioni 443 tukiagiza haya mafuta.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ukijaribu kuangalia si kusema Watanzania hawataki kuweka viwanda vya kuzalisha mafuta haya ya alizeti, viwanda vipo lakini shida kubwa imekuwa ni upatikanaji wa alizeti yenyewe ambayo inabidi ikamuliwe ili iweze kutengeza mafuta. Sasa baada ya kupitia kwa muda mrefu nikijaribu kusoma huku na huku, nimejaribu kuangalia demand, ukijaribu kufuata Ripoti ya Shirika la Chakula Duniani - FAO; average yield ya sunflower per hectare ni kilo 979 ukilima hekta moja unaweza ukapata kilo 979.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile kilo moja ya mafuta inayo ujazo wa lita 1.1 na kwa hekta moja tunaweza kuvuna lita zaidi ya 700. Sasa ukijaribu kuangalia ile demand yetu ya takribani tani 365,000 ambazo zimepungua, tunajikuta kwamba tunahitaji takribani lita 401,500,000 ili tuweze ku- cover lile gap. Sasa hizi lita 401,500,000 tukijaribu kuangalia uzito wa mbegu ya alizeti ambayo tunahitaji ili kuweza kuzikamua ni takribani tani 287,196. Tukirudi nyuma huku kwenye hii ambayo nimeisema kuhusu kuzalisha tunajikuta kwamba ili tuweze kupata mbegu hizi tani 289,196 tunahitaji tuwe na hekta 290,000 average. Sasa hekta 290,000 tukirudi hata kwenye maandiko ya dini nilikuwa najaribu ku-refer hapa mimi ni Mkristo, Mathayo 6:20-21 unasema; “Jiwekeeni hazina Mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuharibu wala wezi hawaingii maana pale ilipo hazina yako ndipo pia utakapokuwa moyo wako.” (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nianze kuchangia, tunapopanga kufanya maendeleo ya viwanda ni lazima tuelewe, huwezi kumwambia mtu leo tumeshaongelea hapa tani zaidi ya 290,000 inabidi zilimwe alizeti. Unamwambia mtu aliyekaa Dar es Salaam abebe shilingi bilioni 50 akazifiche Biharamulo au kwenye mapori kule yeye kakaa kule, hazina iko kule moyo hautakuwepo. Desire ya mfanyabiashara yeyote yule ni apate profit anapowekeza sehemu kwa hiyo, kama hili jambo hatutalichukua kama Serikali hakuna anayeweza kuwekeza huku. Kwa sababu tunahitaji mbegu za alizeti ili tukamue mafuta. Sasa tunachoweza kukifanya hapa, baada ya kuangalia hizi mbegu tani hizi zinaweza zikazalishwa kwa fedha kiasi gani ni almost shilingi bilioni 190. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tukiweza kuibeba hii kitu kama Serikali tuka-invest almost shillings 200 billion, tunao vijana wengi sana ambao hawana ajira kwa sababu tani 190,000 ni kwamba hii nchi tutailima alizeti karibu kila sehemu. Sio tunazunguka hapa mapori yote yameshikiliwa na TFS, kila unapozunguka ni mapori, tunapozunguka ni mapori. Sasa ifikie hatua Serikali ibebe jukumu la kulima. Ikishabeba jukumu la kulima kwa kuwaweka vijana wakazunguka vijana wamemaliza form four, imagine lile darasa lenye wanafunzi 100 wanaofaulu ni nusu, nusu wanabaki tunawapeleka wapi wale vijana? Tubebe JKT, tuwape maeneo, tuwape fedha, wabebe vijana wa Kitanzania, tukalime haya mapori tukishamaliza kulima, mavuno yatakayopatikana kama tunavyofanya kwenye NFRA wakati wa mahindi yakahifadhiwe pale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mtu mwenye kiwanda sasa anayeweza kuhamasishwa akajenge kiwanda cha shilingi milioni 200, shilingi milioni 300, shilingi milioni 400, shilingi milioni
500 hata sisi Wabunge tutaweza kufanya. Yule mtu ataondoka atakwenda atanunua mbegu kwenye ghala la Serikali, atasaga kwa muda wake kila mwezi anaweza kufanya. Kwa sababu kilimo cha alizeti ni zao la miezi minne tu sasa hata wenye viwanda wanapata shida. Maana mimi wakulima wamelima miezi minne hii, mimi natakiwa nifanye production mwaka mzima kinachonitokea ni nini, inabidi ninunue alizeti ya kusaga mwaka mzima ila benki wanani- charge for something that I am just keeping it in my stock.

Kwa hiyo, tungeweza kufanya hiki kitu kikafanywa na Serikali, Serikali ni sawa na inavyotuuzia mahindi ihifadhi alizeti wenye viwanda watakuwa wanakwenda wananunua, in monthly consumption two months, three months or wherever, waweze kuzalisha mafuta. Tutakapokuwa tumebeba hawa vijana tukawaweka after four months wanarudi mtaani wameshajifunza kilimo, lakini pia na wao wamepata fedha watakwenda hata wao wataanzisha kilimo. Kesho na kesho kutwa tunakuwa kwenye position hata ya kuwalisha majirani zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maana nimekuwa najiuliza what if Malaysia kesho watasema hawatuuzii sisi wanapeleka Marekani? Maana yake hapa hatutakuwa na mafuta. Huwezi kuendesha nchi kwa kutegemea mtu mwingine akuletee mafuta more than 90 something percent. (Makofi)

Kwa hiyo, tuweze kuiona hii kama focus mpya Serikali iichukue sawa na tulivyo-approve shilingi bilioni 50 hapa mwaka jana tukapeleka kwenye mahindi, hebu tuone hii ili Waziri huyu anapohangaika na watu wenye viwanda kuja kuwekeza hapa mbegu za alizeti wazikute.

Mimi ninakuhakikishia kama tutalifanya hili kwa study ambazo nimezifanya kama tutalifanya hili in two or three years, nakuhakikishia hatutakuwa na shida ya mafuta ya kula hapa tunaweza tukaanza kuwalisha na majirani zetu. Kwa sababu maeneo tunayo kinachohitajika ni nia tu, tukiweza kuweka nia chini tutatoka hapa tulipo tutasogea mbele zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu shida ya mafuta ya kula ni kubwa, wananchi mitaani wanalalamika yanazidi kupanda, sasa hatutegemei baada ya hapa yataelekea wapi. Kwa sababu as long as anai-control mtu mwingine hatuna ubavu nayo tutakwenda kununua ndio maana umeona idea inayokuja sasa hivi tunakuja na kuondoa duty tunataka duty irudi zero kwenye importation ya mafuta ya kula, maana yake ni nini, tunaleta tu mafuta ili tule tuishi Taifa halitapata faida yoyote kwa sababu mafuta yanazalishwa na Malaysia watatuletea hapa with zero duty, nchi haipati chochote kile ila tunachofanya tunaji-sustain ili tuweze kuendelea kuishi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuyasema haya mimi nimesema naongelea mafuta ya kula tu leo, ili kuwahi kengele na muda naomba niishie hapa, naunga mkono hoja, ahsante. (Makofi)